SaidAlly
JF-Expert Member
- Jan 22, 2011
- 2,328
- 2,228
Safi sana kwa tafsiri nzuri. Pia mpangilio wa kuandika huwa unanivutia kusoma.Kuna mengi ya kujifunza kutoka simulizi ya HOE ila kuna kubwa nimelitafakari kuhusu mhusika Fredy kama personal guide.
Sisi wote katika maisha yetu tuna nafasi moja au zaidi kuwa guide aidha ya kumuongoza mtu au kundi kufikia kilele cha mafanikio au kilele cha kutimiza malengo.
Tunawahitaji watu ma guide au porter ambao ni wema kama Fredy wanaoweza kututia moyo na kutuhurumia kipindi tunapambana kufika hatua fulani katika maisha yetu.
Licha ya kuwahitaji akina Fredy kama ma guide ila pia tunao wajibu wa sisi pia kuwa na moyo kama wa Fredy ili kuwawezesha na kuwasaidia wafike kileleni.( tuwafanyie wengine vile tungependa na sisi tufanyiwe)
Na watu kama Fredy/guide ni lazima tuwape heshima zao kwa kutambua thamani na umuhimu wao katika maisha yetu( jambo ambalo HOE amelifanya kwa kutambua na kumpa credit guide)
Tujiulize na kutafakari sote, je mimi na wewe tumewasaidia na kuwawezesha wangapi katika mambo tunayoyajua au tuliofanikiwa kuwafikisha wengine kilele cha mafanikio?
Tunahitaji kuwa kama Fredy katika vipindi vya maisha yetu na pia tunahitaji kujifunza kwa HOE kwa kutambua na kueleza umuhimu wa watu kama Fredy.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app