SAFARI YA KUSHUKA MLIMA..
Kule juu hatukuchukua muda tulianza kurudi kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya.. Nilikua nimechoka saaaaana. Tukatembea weee hadi tukafika Gilmans. Uzuri wa kushuka ni unaenda straight hakuna mambo ya kusema upite zig zag mle mle katika njia unapita tu.
Nilivyofika Gilmans nikaanza kushindwa kutembea miguu ikagoma kabisa..nikitembea dakika moja nyingi naishiwa nguvu nasimama au nakaa. Huo muda Fred alikua ameshashuka chini kwani yule mwenzetu niliemuacha nae aliishia Stella so alimrudisha chini. This time nikawa ma guide mmoja mtu mzima anaitwa Moses no comment on him but... Nikamkumbukaje Fred hapa angekua ananibembeleza [emoji23]
Nikaanza kulia.. kushuka ni rahisi ila mimi nilikua nimeishiwa nguvu. Kuna muda nilikua nakuangali kule juu najiuliza hivi mimi niliwezaje kupanda juu halafu hapo najisemea hata unipe bilion moja hunirudishi huko juu mimi...
mzee Moses ananisisitiza nijitahidi nishuke ananiambia Kibo ni pale tunafika sasa hivi wewe jitahidi..Na kweli naona vibanda vilee najipa moyo mwenyewe nanyamaza then naendelea kutembea.. Nikitembea kidogo nachoka nakaa tena naanza kulia. It was a mixed feeling... halafu pia nilikua nimeikumbuka familia yangu.... Tukipishana na watu wananipa pole kama zote.... Nikaishiwa nguvu siwezi kutembea mwenyewe so akawa ananishikilia ndio naweza kutembea.... Tumeshikizana wee Kufika sehem I couldn’t walk at all yaani hata kusimama mwenyewe nikawa siwezi... Hata nikijaribu vipi nashindwa.... ilikuja stretcher kunibeba na kunirudisha Kibo.
Wakati tunaelekea Kibo nilishangaa porters wengi wanapanda kuelekea mlimani. Nikawa najiuliza hawa jua lote hili ndio wanaenda kupanda Mlima nikauliza akanambia wanaenda kupokea watu wanaotoka mlimani. Wengine ndio hao wanarudi na hali kama ya kwangu.
Ukifika Kibo yaani wanakuhudumia vizuri hapo.. Nikapewa chai.. mara soup ya moto.. Tukaambiwa tupumzike kidogo tukiamka tunaanza safari ya Horombo. Ngoma hailali. Nikamuwazia yule mzungu aliefariki.. Nikasema silali wala nini nitakaa macho hadi hiyo time ya kurudi Horombo.. Nisije kufia usingizini. Ila Chezea usingizi na uchovu nilikuja kushtuka naamshwa nikale.. I wish niweke picha moja niliyopigwa wakati nimelala... I was half dead.. chakaram.
ku pack vitu was a headache.. Na ilitupasa tufanye haraka maana hizo domitories kuna wageni wengine walikua wamefika so inabidi waingie.. Saa 8/9 tunaaza safari ya kurudi Horombo.. Usingizi ulinisaidia sana huku nilikua poa njiani tunapiga story kwa saaana na wala sikua na uchovu mkubwa sana.. Rohoni kwangu najisikia safiii. Horombo nawahi kufika mapema kushinda hata wale wengine..Kuna baadhi ya watu walienda kuoga mimi sikuoga wala nini.. Nilisema hadi nifike mjini.. I want hot shower nikae hata lisaa bafuni.
Horombo tunalala then kesho asubuhi inaanza safari ya kurudi Marangu getini. Kabla hatujaondoka hapo Horombo tuliimbiwa nyimbo nadhani kama ni utamaduni fulani.. Nili enjoy saana zile nyimbo.. tukacheza pale.. Mimi na wenzangu 3 tulirudi Marangu getini na ambulance. Asubuhi ile Guide kama kuna mtu katika watu wake hayuko vizuri kuna gari linakuwepo for emergency kuwarudisha getini.. So wengine wanatangulia kwa miguu sisi tunabakia kusubiri gari...
Katika Ambulance kuna waarabu fulani ambao niliwakumbuka vizuri wakati wa kupanda kuanzia Mandara tulikua wote benet.. nao wanarudi kwa ambulance na mchina mmoja. Wale waarabu wa 4 they told us kwamba only 1 of them was able to reach the peak.. huyo mwanaume wale wadada hawakufika.... Mmoja wao alikua anatapika saana... alikua analalamika kuumwa... walituambia wametokea UAE.. Kurudi na gari was another experience..
Ile asubuh tulipoamka Horombo ndio tulianza kushangaana sura zetu [emoji23][emoji23] ni pua zimebabuka... ngozi haiko sawa.. ukimuangalia mwenzako unaweza kujiona wewe una afadhali na mwenzako nae akikuangalia anajiona yeye ana afadhali.. Sisi ndio tunakua wa kwanza kufika tunasubiria wenzetu waliokuja.
Final Goodbye na Porters
Tunapata wasaa wa kuagana na crew ya Origin pale Marangu getini maana baada ya hapo tulikua tunaenda hotelini na wengi wao wasingeweza kuja kule.. It was very sad. Its only few days we stayed in Kili but the bond we had shared with those people was so strong... Watu walilia saana...
Tip tulichangishana tangu mwanzo elfu 75 each.. na mwanzo tulipanga kila mtu achangie laki wengine wakaona laki nyingi tufanye 75... Maana tayari tulishalipia fedha.... ila baada ya kupanda mlima na kuona kazi wale watu wamefanya we all thought kwama 75 haikua pesa.. It was nothing compared na service walitotupatia kule juu. Ile pesa waligawana katika group. Sisi hatukutaka kila mtu ampe tip mtu mkononi kivyake.. maana kuna mtu wa jikoni yeye humuoni unashangaa tu chakula mezani.. kuna mtu anaebeba bag yako humuoni ila muda wote ukifika point fulani unaletewa bag liko salama. So kuna wengine hatu interact nao ila tunapata service yao. Wao wenyewe walijua waligawana vipi ile pesa.
Nilichukua mawasiliano na Fred.. Alinambia hataweza kuja hotelini.. na mpaka kesho kutwa huwa tunawasiliana ingawa most of the time anakua hapatikaniki yuko mlimani.. Nilimpatia tip yake personal tofauti na ile ya group na pia vifaa vingi nilivyonunua kwa ajili ya kupanda mlima nilimuachia.. Alishukuru sana. Pia alinambia ataenda kusomea mambo ya u guide kuna chuo huko.. Kwasababu yeye ni porter na ili uwe guide inabidi upate cheti... So kitu ambacho nimepanga ni kumsaidia part ndogo ya ada.. Mimi sio tajiri maisha yangu ya kuunga unga but what he did kwangu ni wema na utu wa hali ya juu. He was extremely caring. Very understanding.... Maybe that is the only way I can repay him.. Mara kibao huwa namwambia yeye ni mtu poa saana.
Tunarudi Hotelini.. Hiyo ndio siku kulikula misosi tunayopendelea.. It was a celebration evening.. Hiyo siku nilitumia karibu saa nzima kuoga.. maji ya motoooo... I was so relieved... Jioni tukagawiwa certificates wenye kunywa bia ndio walizinywa hapo na pia nilipata nafasi ya kuonana na
kiwatengu kwa mara ya kwanza na nitumie nafasi hii kumshukuru kwa ushauri wake na moyo wa kunisaidia mpaka nikafanikisha safari yangu Kilimanjaro.
Wengi wetu tulipata na ganzi katika mikono siku zile za mwanzoni lakini baadae iliishia taratibu.
We came back to DSM safely with a lot of great memories. Climbing Mt Kilimanjaro to the peak is something that I will hold close into my heart. My trip was very eventful and joyous, I met new people who were very generous and down to earth like Fred.. they took care of me as if I were their own child/sister, I came across various obstacles, I strived for the best and most importantly I achieved my goal. It’s unreal how we became so attached with guides/porters in such a short period of time. I journeyed through pain, laughter, suffering, dirtiness and Mr Peters famous porridge and soup.(ambayo ilikua huwezi kukwepa kunywa)
I had the greatest moments and created incredible memories which will remain in my mind and heart forever. As they say nothing comes easy and it’s true, It wasn’t easy at all but I did it... One thing I learned is to appreciate everything this life offers.
I thank God for protecting me all the time, My Mother for her support.. My group mate who not only made the trip funny but also easy,.....Mr Emmanuel & Origin Team for for this wonderful journey[emoji92]
My family & Friends made this for Us..
The Team behind our success
Going back to Horombo
Last picture @ Kibo
I bought so many things pale Marangu Getini ikiwemo hii T shirt na i dedicate kwa wote ambao wanasema hawawezi kupanda Mlima
THE END