Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Kiasi gani mlitumia ktk safari nzima?
Garama nililipa 400$ kwa trip ukijumlisha na tip ili range 600$ kwa staff Porter at least 5$ per day kuna chef 10$ kuna guide 30$ kwa siku so mnajumlisha alafu unagawa kwa idadi yenu (tourist) maana kiukweli bila hawa jamaa hufiki mahali
Salute to the Porter's and all mountain staff hawa watu ni wanaume na nusu

Nb; nimejaribu kutoa ufafanuzi wa tip maana wanadai hawana salary za maana wanaishi kwa tip so ni kama desturi ila hata wewe ukiona kazi wanayo piga utaelewa
 
Aisee mm Moshi napapenda San nataka safari niende Kili Marathon
 
Garama nililipa 400$ kwa trip ukijumlisha na tip ili range 600$ kwa staff Porter at least 5$ per day kuna chef 10$ kuna guide 30$ kwa siku so mnajumlisha alafu unagawa kwa idadi yenu (tourist) maana kiukweli bila hawa jamaa hufiki mahali
Salute to the Porter's and all mountain staff hawa watu ni wanaume na nusu

Nb; nimejaribu kutoa ufafanuzi wa tip maana wanadai hawana salary za maana wanaishi kwa tip so ni kama desturi ila hata wewe ukiona kazi wanayo piga utaelewa
Twendeni
 
Garama nililipa 400$ kwa trip ukijumlisha na tip ili range 600$ kwa staff Porter at least 5$ per day kuna chef 10$ kuna guide 30$ kwa siku so mnajumlisha alafu unagawa kwa idadi yenu (tourist) maana kiukweli bila hawa jamaa hufiki mahali
Salute to the Porter's and all mountain staff hawa watu ni wanaume na nusu

Nb; nimejaribu kutoa ufafanuzi wa tip maana wanadai hawana salary za maana wanaishi kwa tip so ni kama desturi ila hata wewe ukiona kazi wanayo piga utaelewa
Inshallah, my cousin and I are scheduled to go Dec 28- Jan 2. I have been training and I am praying my body iniruhusu nifike mwisho. Otherwise, all this gear tumenunua, let a lone pesa za kupanda will be a real waste!!!
 
SAFARI YA KIBO.

5a39fad92fe0b860539a404fb8f9f622.jpg


Siku iliyofata ilikua ni tunaodoka Horombo kwenda Kibo... Nilikua mzima kabisa.. Kila asubuhi na jioni tulikua tunafanyiwa check up. Nilikua salama. Safari ya Horombo hadi Kibo ilikua ndefuuu saaana.Sikumbuki masaa mangapi tulitumia.

Nilikua niko na Fred pia.. He was so helpful.. Njiani tulikua tunapishana wengine wanakwenda wengine wanarudi.. Wazungu ndio wengi sana.. huko utaambiwa wish you luck.. Pole pole.. Pia nilikua naulizia hali ya huko wanatuambia its very windy & Cold.. Wengine anakwambia point aliyofika.. Hii yote tulikua tunadadisi ili kujua ninachoenda kukabiliana nacho huko mbeleni. Nilikua natembea pole pole.. ila pia speed ya mtu automatically inapungua tu.

Kulikua na upepo saana. Ilivyofika mchana tulikua tunahitajika kula sehem ya kula ilikua ni kwenye Mapango ya mawe.. hiyo ndio sehem atleast mnaweza kukaa mkala chakula na upepo ukapiga kidogoo.. Upepo unavuma haswaa. Jua lilikua linawaka saana tu ila upepo ndio hatari.

Kuelekea Kibo kuna point ambayo ndio mwisho maji yanapopatikana. Huko mbele ni kama jangwani hakuna maji. Kwahiyo hata porters ilikua inawalazim kubeba maj kutoka hiyo sehem hadi Kibo camp. Dum la lita 20 ya maji ndio mtu anabeba. Ni kazi nzito saaana.Mimi tu nilikua na ka back pack ila hoi ila yeye ndio maisha yake ya kila siku hayo. Kubebelea maji kupeleka Camp.

HABARI YA KIFO..

Tukiwa bado masaa machache kufika camp kuna mtu akawa kabebwa katika stretcher anashushwa chini.. huku filimbi inapuliza.. wote tukasogea pembeni kupisha. Alikua ni mwanaume mtu mzima mzungu.. kalala chali huku Mke/partenr wake alikua akilia saana nakumbuka maneno niliyoyasikia hadi leo “Ooh my God..Nitafanya nini mimi.. Nitaeleza nini katika familia yetu Maisha yangu bila yeye yatakua ya namna gani” nimefanya kunukuu kiswahili

Analia kishenzi.. Mwili wote ukapata ganzi.. I was schocked.. nikasimama huku nimepigwa na butwaa..Tulivyofika camp tuliambiwa kuwa alifika summit vizuri alivyorudi akalala kabla hajaendelea na safari ya kurudi Horombo so mauti ilimkuta usingizini. Imagine unapanda mlima salama then mauti yanakufika baadae..

Huo muda wakati wanashuka na stetcher akili yangu inawaza kuwa huyu mtu aliyelala anashushwa chini akiwa maiti naweza kuwa mimi.. naweza kuwa mimi ndio nashushwa chini kama maiti.. nakuja kupanda Mlima then nafia huku.. hivi niendelee ama nirudi tu nilikotoka I cant risk my life kama hivi.. Nadhani kila mtu alikua anafikiri yake na kilichotuumiza ni namna yule mama alivyokua analia.. Lilikua tukio la kusikitisha Saana.

Watu wanaweza kuogopa ukisikia hivyoo.. Kama ana mpango wa kwenda akaahitosha lol.. Safari ikaendelea hadi Kibo.. Kibo ni camp kuko busy saana.. Jamani kuna upepo saaana pale Camp.. Ila ukiingia bwenini kuna joto.. Nilikua nawawazia wale wanaolala katika tent nje.. Mimi tu nilikua ndani ila nilikua nasikia hivyo hao wa nje je? Vyoo pia si safi maybe kutokana na kutokua na maji..

Mtu mmoja katika kikundi chetu anapata shida kufika Kibo.. Alifika njiani nae akashindwa kutembea hali yake ikawa mbaya.. Alibebwa juu juu hadi maana alishindwa kutembea kabisa... Na yeye ndio tulikua na wasi wasi nae saana kama angefika akiwa haumwi.

Tuna masaa machache ya kupumzika kabla ya kuanza kupanda Mlima. Saa 6 usiku ndio Safari itaanza

Naenda kuleeee kileleni [emoji4]


1e4b57f88fbaa7f5071f6234d5e45cb9.jpg


Huyu mtoto ana miaka 10 alitokea SA.. wakiwa na Trek4Mandela.. Sijui alifika summit

1659e050ed47d9aae8fcd9741fa10165.jpg


Hii ndio sehem ya mwisho maji kupatikana

fb4082a14402e62a0786908a5e18d88e.jpg


Angalia hao porters

c347751072ae8b7ac44d5b216c81dae0.jpg


e7a1be1ead060058f678e2ab411d2978.jpg


Huyu baba kapanda Mlima mara 18 na siku zote alifika kileleni
cf04cf91cf6d364bffcf48953a4f356a.jpg


Hiko kitanda cha pembeni juu kabisa ndio nililala hapo.. Chini kulikua na mdada mzungu anatapika kishenzi..

4fe4ba885b7b3b2101e99f1c0d788559.jpg


Mandhari ya KIBO

f812dcd0ea12517e859d013166f0921d.jpg


Sehem ya kupumzika

438448f24dab6db9fc860a0d5c9a7ad8.jpg


Kulikua na baridi nje.. Hiko choo nilienda kuingia ndani.. Ushawahi kuona unakaa chooni na unaona ndio sehem nzuri kabisaa kuliko nje

f706f46ae3d08f281b5a3431cf16fe1b.jpg



SUMMIT NIGHT.


KUELEKEA GILMAN'S POINT

824dbcf3bbf8f2526bbd3ae7b07acce4.jpg




Mlima Kilimanjaro haupandwi mchana wala asubuhi ni mnapanda usiku.. yaani ile Mid night ndio safari ya kupanda inaanza. Mimi nakumbuka tulihimizwa kula haraka na kwenda kulala mapema. By Saa 5 sharp tunaamshwa... yaani nilijiona hata sijalala hata kidogo then muda huo.

Hapa unashauriwa kupanda Mlima na clean clothes kuanzia chupi hadi socks.. sijajua ni kwanini. Wakati naamka yule mzungu alielala chini ya kitanda changu wao ndio walikua wanaondoka. So naamka kivivu naanza kubadili nguo kuna baridi so nilikua naona kama mateso fulani cos inabidi nichojoe nguo zooote. Sim yangu ilikua full charged na nilikua na power bank maana nilitaka kupiga as many pictures as possible.

Katika group yetu mtu mmoja anashindwa kupanda Mlima.. Yeye aliishia Kibo hata alivyopimwa ikaonekana oxygen kwake itakua shida so bora abaki.. Na huko juu ndio kuna mgandamizo mkubwa wa hewa. Nikamuonea huruma. Huyu ni yule aliebebwa pia hadi kufika Kibo maana alishindwa kutembea.

Saa 7 kamili ndio tunaanza safari...Hii ni kosa kubwa tulifanya la kuchelewa kuondoka nadhani tulikua group kubwa la watu wengi kuchelea kutoka. lazima uwe na head tochi hio inakusaidia kuona usiku cos kuna mawe saana.. Chupa ya hot water..tulipangwa katika msururu mmoja.. Tukasisitizwa kutembea katika line bila kuachana wala kutoka katika mstari.. Wale ma Guide ndio walikua pembeni. Tukapiga sala ya pamoja pale then safari ikaanza.

Taratibu ule mstari ukaanza kuachia.. wengine wakaanza kubaki nyuma.. wengine katikati.. wengine mbele.. Mimi hapo mwanzo nilikua fresh.. yaani mambo mswano naona Uhuru ile inafikika fasta tu... Wale porters wanaimba nyimbo za kutuhamasisha kupanda Mlima.. Yaani wale jamaa wanafanya kazi kubwa saana. Mimi ile hali niliyokua nayo hata kunyanyua mdomo nilikua siwezi..

Kwa mbali unaziona tochi tu kwa juu yako.. I’m like I wish mimi ndio ningekua kule juu ama yatokee maajabu nipae hadi kule juu lakini ilikua haiwezekani ni lazima upande wewe mwenyewe.. Njia ya kuelekea Gilmans ni zig zag yaani mnakua mnazunguka na hii inachangia pia kuchoka na kutumia muda mwingiiii... kuna mawe mengi na makubwa pia so walikua wanasisitiza kuwa makini.

Nikaanza kuchoka.. Speed yangu ikawa ndoogo.. Nahema kwa shida kama mbwa alietoka kukimbia mbio ndefu halafu vile anakua anatoa ulimi wake nje kuhema ndio nilikua mimi... Muda mwingine ilinibidi kufungua mdomo ili kuweza kutoa na kuingiza hewa. There is very thin layer huko juu.... Mtu mwingine hali yake inabadilika inabidi arudishwe chini haraka sana. Na kunakua na team kazi yao ni kurudisha watu.. Akaanza kulia hataki kurudi.. She is like I came all the way then nirudie hapa SIRUDI.. nyie niacheni niendeelee.... wakifanya vipimo vyao wanaona hii ngoma ikipanda zaidi ya hapo ni atarudishwa akiwa mahututi ama kifo.. walitumuia Muda kum convince ndio akakubali. Wale ma Guide pia hawataki kuchukua risk za namna hiyo..Uruhusu mtu aende juu then akafie huko..... Kwenye 21 tukabaki 19

Nilikua sizungumzi na mtu ni macho tu ndio yanaongea. Yaani ukinitizama usoni unaweza kujua hata nini kinaendelea katika mind yangu... nikawa nawashangaa hata wale wengine wanapata wapi nguvu za kuimba... Tunatembea then kidogo mnasimama kupumzika.. Nilikua nakasirika tukipumzika kidogo hao tunaambiwa tunyanyuke tuendelee na safari. Kwasababu Mimi katika group ya watu 8 let say nakuwa mwishoni wenyewe wako mbeleni so wakati wao washapumzika mimi ndio nafika...Muda wa kupumzika unakua hautoshi.

Nilikua na usingizi wa kufa mtu yaani pamoja na lile baridi nilikua nikifumba macho huku tunatembea naona kabisa usingizii huo unanipitia... Guides walitusisitiza tujitahidi tusifumbe macho.. The thing is unaweza kupitiwa na usingizi then ikawa moja kwa moja. Kwa mara ya kwanza katika maisha niliona usiku ni mrefu... yaani hakukuchi kufike asubuhi

Kuna muda nikasimama nikaangalia chini nilikotoka naona Taa zinamulika yaani unaona kabisa mjini.. Nikaanza kujiuliza hivi mimi why did I come here?? Ili iweje?? Sasa hivi si ningekua nimelala sehem nzuri badala yake niko mlimani huku.. ningekua nakula vizuri badala yake nimekuja huku. Nikaanza kumuonea wivu yule tulimuacha KIBO. Nikaona si bora ningebakia zangu kibo nipumzike.. nilale weeee. Nikaona yeye kubaki was the best decision ever.


Kwenda Gilmans sio mchezo jamani.. na mnatembea usiku kwa usiku kuanzia saa 7.. ngoma ikagonga saa 10 mtu unatembea tu na haujui unafika saa ngapi..unaambiwa in one hour utakua Gilmans.. lisaa linapita hufiki..Naanza kukata tamaa... Nguvu ya ku Give up ikawa inakuja..Nikaona to hell with all these.. Ngoja tu nipoteze pambano nirudi zangu Kibo.. Then upande mwingine nafikiria hivi mimi I came all the way nije kukata tamaa hapa what if ni kipande kichache kimebakia then nitakua nimefika..

Asubuhi kunakucha na kupambazuka hatujafika Gilmas.. Fred mwanzoni nilikua nae lakini baadae kuna mtu katika group akawa hali yake sio nzuro ikabidi nimuache nae ili aje nae juu taratibu..

Kisa cha Bangi

Tukiwa njian tunaenda kuna hao wazungu tulikua nao sambamba.. Kuna sehem wakafika katika mawe makubwa kupumzika wakawa wanavuta sasa kaka mmoja (Alex nimpe hilo jina) tulikua nae group yetu wakamwambia you wanna try.. It helps a-lot.. Alex kihere here akajoin bila kujua hao wazungu ni wazoefu wa hizo mambo.... sisi hao tukaendelea mdogo mdogo.. Baada ya muda tukawaona hao wanakuja na wapo mwendo mkali kidogo zaidi ya wakwetu.. Na Alex alikua nao so akatuacha sisi akawajoin hao wazungu..

Nakumbuka kimoyo moyo nikasema ningejua ningejaribu hata puff moja mbona jamaa yetu kawa na nguvu.. So wakatupita.. Muda si muda nikashangaa Alex anarudishwa chini mzobe mzobe kabebelewa hali imekua tete hajiwezi.. Tukashtuka labda tushampoteza huko tukaambiwa he is okay ila he cant breathe well wanamrudisha huko chini akatafutiwa stretcher likamshusha. Baadae alivyokuka kutuhadithia nilicheka sana kumbe wenzake ni wazoefu wa zile mambo anasema alichungulia mlango wa kifo

Mida ya saa mbili kasoro nadhani ndio naingia Gilmas.. Sisi tumefika Gilmans kuna group nyingine walikua washafika Uhuru peak wanarudi chini.. Tulichelewa sana kufika Sikuamini aisee Nikawa naona kama muujiza fulani.. Tulivyofika tu wakatuwahi na maji moto. Jua liko vizuri ila the thing is baridi unaisikia hadi katika mifupa.

Nikiwa Gilmans

29ebfa60118c2c475ae9132664cd7062.jpg



Japo sim yangu ilikua full charge ukiwa juu ikazima kabisa kwamba battery empty. the last picture I took with my phone


40c7062c34b9a820756b5e9342e2d9c6.jpg



Tulikua tunatembea namna hiyo

10d184e1216887a442a07b5e2fe05ea5.jpg



Hapa ukiwa maeneo umya Juu Gilmas ukiangalia tulikotoka kule chini

4c00e27f62e7db0468d8e1ff7db5dc6d.jpg



3c45e6688ea9cb7a5b206c08aed9e104.jpg
Mna bahati sana, wakati napanda, ile tumefika tuu kibo, ikaanza kuangika snow ya nguvu pamoja na mvua kubwa sana, siku ya summit barafu tulianza kuikanyaga nje ya vibanda vya kibo hadi kileleni ni barafu tupu. Binafsi nilipata changamoto ya kuumwa kichwa na kutapika, ilikuwa nikila chochote kile natapika, kuna wazungu nilikuwa nao room moja wakawa wananicheka tuu. Ila nilikomaa na kupanda ya mlima bila ya kula hadi níkatoboa maana sunrise ilinikuta nishafika uhuru peak
 
Mna bahati sana, wakati napanda, ile tumefika tuu kibo, ikaanza kuangika snow ya nguvu pamoja na mvua kubwa sana, siku ya summit barafu tulianza kuikanyaga nje ya vibanda vya kibo hadi kileleni ni barafu tupu. Binafsi nilipata changamoto ya kuumwa kichwa na kutapika, ilikuwa nikila chochote kile natapika, kuna wazungu nilikuwa nao room moja wakawa wananicheka tuu. Ila nilikomaa na kupanda ya mlima bila ya kula hadi níkatoboa maana sunrise ilinikuta nishafika uhuru peak
Hongera sana mkuu.
 
Inshallah, my cousin and I are scheduled to go Dec 28- Jan 2. I have been training and I am praying my body iniruhusu nifike mwisho. Otherwise, all this gear tumenunua, let a lone pesa za kupanda will be a real waste!!!
How was the challenge?
 
Inshallah, my cousin and I are scheduled to go Dec 28- Jan 2. I have been training and I am praying my body iniruhusu nifike mwisho. Otherwise, all this gear tumenunua, let a lone pesa za kupanda will be a real waste!!!
Tupe feedback
 
Inshallah, my cousin and I are scheduled to go Dec 28- Jan 2. I have been training and I am praying my body iniruhusu nifike mwisho. Otherwise, all this gear tumenunua, let a lone pesa za kupanda will be a real waste!!!
Ni gharama sana kununua vifaa, zaidi kuna vifaa ukishatumia kupandia mlima huwezi vitumia tena, ni bora ukakodisha tuu, kampuni niliyopata kwa gharama ya chini ya milioni moja walinipa vifaa, fee za KINAPA, chakula na usafiri wa kunitoa mjini na kunirudisha.
 
Kiukweli kabisa hamasa ya kupanda mlima Kilimanjaro niliipata baada ya kusoma thread hii. Na nilijihapiza lazima nije kupanda mlima bahati nzuri siku niliyoenda kileleni ilikuwa ni tarehe 01/01/2021 (siku ya mwaka). Changamoto za kupanda mlima zipo cha muhimu ni kuwa na nia utafika kileleni, ila ukiwa mfuata mkungo utaishia njiani.
 
Back
Top Bottom