Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Asante kwa simulizi nzuri....you seem to be a good writer.
Hongera sana kwa kufika "rooftop" ya Africa. Baada ya kusoma imeamsha ari yangu ya kutaka kupanda.
Karibu mwakani kushiriki Killy Marathon....
 
Kwangu mie huu ni uzi bora, huchoki kusoma. Mie siwezi kupanda umri umeenda sana.nilishindwa hata kupanda mapango ya KOLO. Naona ningeishia marangu getini.HONGERA SANA.
 
Baridi ya K'njaro si baridi hizi tumezoea za mwezi wa sita/saba...

Normally mwili unapokuwa subjected kwenye freezing temps kuna vitu vingi sana vinakuwa inactive including hamu ya mapenzi...

Kwa walioishi nchi/ukanda wa dunia unaopitia msimu wa baridi kali wanaweza wakawa mashahidi namna ambavyo mwili unavyokuwa kama mfu ukiwa kwenye baridi...
Heaven on Earth kwenye baridi huwa si mzuka wa genye kupanda unakua speed 20

Vipi wewe umekaa kwenye ile mibarafu muda wote ule,hukuwa na mzuka kabisa

Hamnaga mahali umefika ukaona hapa angekuepo bebe angenikunjua mpk,maana panashawishi?

AU ukiwa kule ubongo haukumbuki upande wa pili wa shilingi kabisa,unawaza kifo tu?
 
Nitakupa kifua changu six pack uegemee ukielemewa na nakuahidi mhelemeo ukikuzidi nitatafuta kichaka ambacho hakuna atakaetuona ili nikufanyie diagnosis ya mapafu. Ha ha ha Billie doctor wa mapenzi nipo.
Woow!! I'd love it, tupange twende mie nnavopenda maadvencha eehehehee ila nikianza kukata pumzi ujiandae kunibeba si ujajua uzee tena heheheheee.

Kasinde Mahaba.
 
Nitakupa kifua changu six pack uegemee ukielemewa na nakuahidi mhelemeo ukikuzidi nitatafuta kichaka ambacho hakuna atakaetuona ili nikufanyie diagnosis ya mapafu. Ha ha ha Billie doctor wa mapenzi nipo.

Toobaah.... Raha iliyojee kukwea mlima na dokta wa Mahaba....

Naanzaje kukataa sasa... Sina ujanja huo eeheheheeee.
 
Hiyo hamu hata haipo... Mimi sikuwazia kabisa mambo ya kugegedana.

Halafu kupanda sio mazoezi saaana na stamina pia ya mwili kuhimili mabadiliko ya hali ya hewa. Si waona yule mwarabu fighter hajafika kileleni na ubaunsa wake wote
Kumbe mpwa we we ni kipotable çha ukweli, yaani ni bebable kabisa.
 
1.Dada yangu hujasema mlitumia siku ngapi kufika juu.
2.Kuna pale mahali kwa mbele kidogo ya uhuru peak kuna lile shimo la volcano hamkuonyeshwa?
Sasa ushangae mfano mimi natoka mkoa wa Kilimanjaro asubuhi unaamka umefunga taulo unapiga mswaki unachungulia juu unaona dheluji ya mlima lakini hujawahi panda mlima sababu unaona kitu cha kawaida penye miti hakuna wajenzi.
You are so courageous woman kama umeolewa your husband must be lucky keep it up ni inbox
 
Hongera dear, Umenitamanisha kwakweli japo pia umenitisha sana, natamani kwenda. Nkipata group na nkajua gharama nitaenda
 
SAFARI YA KUSHUKA MLIMA..

71e42ea7ef4312fde77d882c8c3243de.jpg

Kule juu hatukuchukua muda tulianza kurudi kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya.. Nilikua nimechoka saaaaana. Tukatembea weee hadi tukafika Gilmans. Uzuri wa kushuka ni unaenda straight hakuna mambo ya kusema upite zig zag mle mle katika njia unapita tu.

Nilivyofika Gilmans nikaanza kushindwa kutembea miguu ikagoma kabisa..nikitembea dakika moja nyingi naishiwa nguvu nasimama au nakaa. Huo muda Fred alikua ameshashuka chini kwani yule mwenzetu niliemuacha nae aliishia Stella so alimrudisha chini. This time nikawa ma guide mmoja mtu mzima anaitwa Moses no comment on him but... Nikamkumbukaje Fred hapa angekua ananibembeleza [emoji23]

Nikaanza kulia.. kushuka ni rahisi ila mimi nilikua nimeishiwa nguvu. Kuna muda nilikua nakuangali kule juu najiuliza hivi mimi niliwezaje kupanda juu halafu hapo najisemea hata unipe bilion moja hunirudishi huko juu mimi...

mzee Moses ananisisitiza nijitahidi nishuke ananiambia Kibo ni pale tunafika sasa hivi wewe jitahidi..Na kweli naona vibanda vilee najipa moyo mwenyewe nanyamaza then naendelea kutembea.. Nikitembea kidogo nachoka nakaa tena naanza kulia. It was a mixed feeling... halafu pia nilikua nimeikumbuka familia yangu.... Tukipishana na watu wananipa pole kama zote.... Nikaishiwa nguvu siwezi kutembea mwenyewe so akawa ananishikilia ndio naweza kutembea.... Tumeshikizana wee Kufika sehem I couldn’t walk at all yaani hata kusimama mwenyewe nikawa siwezi... Hata nikijaribu vipi nashindwa.... ilikuja stretcher kunibeba na kunirudisha Kibo.

Wakati tunaelekea Kibo nilishangaa porters wengi wanapanda kuelekea mlimani. Nikawa najiuliza hawa jua lote hili ndio wanaenda kupanda Mlima nikauliza akanambia wanaenda kupokea watu wanaotoka mlimani. Wengine ndio hao wanarudi na hali kama ya kwangu.

Ukifika Kibo yaani wanakuhudumia vizuri hapo.. Nikapewa chai.. mara soup ya moto.. Tukaambiwa tupumzike kidogo tukiamka tunaanza safari ya Horombo. Ngoma hailali. Nikamuwazia yule mzungu aliefariki.. Nikasema silali wala nini nitakaa macho hadi hiyo time ya kurudi Horombo.. Nisije kufia usingizini. Ila Chezea usingizi na uchovu nilikuja kushtuka naamshwa nikale.. I wish niweke picha moja niliyopigwa wakati nimelala... I was half dead.. chakaram.

ku pack vitu was a headache.. Na ilitupasa tufanye haraka maana hizo domitories kuna wageni wengine walikua wamefika so inabidi waingie.. Saa 8/9 tunaaza safari ya kurudi Horombo.. Usingizi ulinisaidia sana huku nilikua poa njiani tunapiga story kwa saaana na wala sikua na uchovu mkubwa sana.. Rohoni kwangu najisikia safiii. Horombo nawahi kufika mapema kushinda hata wale wengine..Kuna baadhi ya watu walienda kuoga mimi sikuoga wala nini.. Nilisema hadi nifike mjini.. I want hot shower nikae hata lisaa bafuni.

Horombo tunalala then kesho asubuhi inaanza safari ya kurudi Marangu getini. Kabla hatujaondoka hapo Horombo tuliimbiwa nyimbo nadhani kama ni utamaduni fulani.. Nili enjoy saana zile nyimbo.. tukacheza pale.. Mimi na wenzangu 3 tulirudi Marangu getini na ambulance. Asubuhi ile Guide kama kuna mtu katika watu wake hayuko vizuri kuna gari linakuwepo for emergency kuwarudisha getini.. So wengine wanatangulia kwa miguu sisi tunabakia kusubiri gari...

Katika Ambulance kuna waarabu fulani ambao niliwakumbuka vizuri wakati wa kupanda kuanzia Mandara tulikua wote benet.. nao wanarudi kwa ambulance na mchina mmoja. Wale waarabu wa 4 they told us kwamba only 1 of them was able to reach the peak.. huyo mwanaume wale wadada hawakufika.... Mmoja wao alikua anatapika saana... alikua analalamika kuumwa... walituambia wametokea UAE.. Kurudi na gari was another experience..

Ile asubuh tulipoamka Horombo ndio tulianza kushangaana sura zetu [emoji23][emoji23] ni pua zimebabuka... ngozi haiko sawa.. ukimuangalia mwenzako unaweza kujiona wewe una afadhali na mwenzako nae akikuangalia anajiona yeye ana afadhali.. Sisi ndio tunakua wa kwanza kufika tunasubiria wenzetu waliokuja.

Final Goodbye na Porters

Tunapata wasaa wa kuagana na crew ya Origin pale Marangu getini maana baada ya hapo tulikua tunaenda hotelini na wengi wao wasingeweza kuja kule.. It was very sad. Its only few days we stayed in Kili but the bond we had shared with those people was so strong... Watu walilia saana...

Tip tulichangishana tangu mwanzo elfu 75 each.. na mwanzo tulipanga kila mtu achangie laki wengine wakaona laki nyingi tufanye 75... Maana tayari tulishalipia fedha.... ila baada ya kupanda mlima na kuona kazi wale watu wamefanya we all thought kwama 75 haikua pesa.. It was nothing compared na service walitotupatia kule juu. Ile pesa waligawana katika group. Sisi hatukutaka kila mtu ampe tip mtu mkononi kivyake.. maana kuna mtu wa jikoni yeye humuoni unashangaa tu chakula mezani.. kuna mtu anaebeba bag yako humuoni ila muda wote ukifika point fulani unaletewa bag liko salama. So kuna wengine hatu interact nao ila tunapata service yao. Wao wenyewe walijua waligawana vipi ile pesa.

Nilichukua mawasiliano na Fred.. Alinambia hataweza kuja hotelini.. na mpaka kesho kutwa huwa tunawasiliana ingawa most of the time anakua hapatikaniki yuko mlimani.. Nilimpatia tip yake personal tofauti na ile ya group na pia vifaa vingi nilivyonunua kwa ajili ya kupanda mlima nilimuachia.. Alishukuru sana. Pia alinambia ataenda kusomea mambo ya u guide kuna chuo huko.. Kwasababu yeye ni porter na ili uwe guide inabidi upate cheti... So kitu ambacho nimepanga ni kumsaidia part ndogo ya ada.. Mimi sio tajiri maisha yangu ya kuunga unga but what he did kwangu ni wema na utu wa hali ya juu. He was extremely caring. Very understanding.... Maybe that is the only way I can repay him.. Mara kibao huwa namwambia yeye ni mtu poa saana.

Tunarudi Hotelini.. Hiyo ndio siku kulikula misosi tunayopendelea.. It was a celebration evening.. Hiyo siku nilitumia karibu saa nzima kuoga.. maji ya motoooo... I was so relieved... Jioni tukagawiwa certificates wenye kunywa bia ndio walizinywa hapo na pia nilipata nafasi ya kuonana na kiwatengu kwa mara ya kwanza na nitumie nafasi hii kumshukuru kwa ushauri wake na moyo wa kunisaidia mpaka nikafanikisha safari yangu Kilimanjaro.

Wengi wetu tulipata na ganzi katika mikono siku zile za mwanzoni lakini baadae iliishia taratibu.

We came back to DSM safely with a lot of great memories. Climbing Mt Kilimanjaro to the peak is something that I will hold close into my heart. My trip was very eventful and joyous, I met new people who were very generous and down to earth like Fred.. they took care of me as if I were their own child/sister, I came across various obstacles, I strived for the best and most importantly I achieved my goal. It’s unreal how we became so attached with guides/porters in such a short period of time. I journeyed through pain, laughter, suffering, dirtiness and Mr Peters famous porridge and soup.(ambayo ilikua huwezi kukwepa kunywa)

I had the greatest moments and created incredible memories which will remain in my mind and heart forever. As they say nothing comes easy and it’s true, It wasn’t easy at all but I did it... One thing I learned is to appreciate everything this life offers.

I thank God for protecting me all the time, My Mother for her support.. My group mate who not only made the trip funny but also easy,.....Mr Emmanuel & Origin Team for for this wonderful journey[emoji92]

My family & Friends made this for Us..

80a1aea0e82016378de52fa15f5dd06e.jpg

The Team behind our success

28135f6fadaf143b68a13658755970bf.jpg

Going back to Horombo

8c6fd52e073b6e6758d8a5cbbf46ecb0.jpg

Last picture @ Kibo

bd15f5493f3ad6121c40f423cd68be42.jpg

I bought so many things pale Marangu Getini ikiwemo hii T shirt na i dedicate kwa wote ambao wanasema hawawezi kupanda Mlima

6ea49fb4301c3a3c19cbfaa139eae9f8.jpg

THE END
safi sana, nimesoma najiona kama niko napanda
 
MY JOURNEY TO THE ROOF OF AFRICA

Kabla ya mwaka kuisha napenda ku share na nyie experience yangu ya kupanda mlima Kilimanjaro nitaambatanisha baadhi ya picha na video za safari yangu yote. Kama kuna watu wamewahi kupanda Mlima Kilimanjaro wanaweza ku share pia uzoefu wao.

Kampuni niliyotumia inaitwa Origin Trails.. Kundi letu tulikua 21, Njia niliyotumia ni MARANGU.. Cost ilikua ni 560$ hii ili include kila kituu.. kuanzia usafiri Dar-Moshi Dar, chakula, hoteli.. vifaa.. fees za getini... personal guides... etc etc.. gharama zinapungua kutokana na huduma unayohitaji..

c449ae42b836bcda5f243c52a04c237b.jpg

MAANDALIZI YA SAFARI.

Baada ya ku confirm ushiriki wangu kupanda Mlima Kilimanjaro. Jambo la kwanza nilifanya Medical check up.. nikawa 100% fit kupanda mlima na hadi kufika kileleni... Nikaanza mazoezi nakimbia uwanja nazunguka mara 7-10. Mazoezi ya kupandisha ngazi wanaojua jengo la UHURU HEIGHTS.. Nimepanda na kushuka hizo ngazi saana.. Pia tulikua tunafanya SEA CLIFF WALK haya yalikua matembezi kutoka Upanga hadi Sea cliff kwenda na kurudi kila jumamosi Kwa mwezi mara mbili. Kim beach kigamboni kutembea katika michanga Etc etc.

Pia nilijisajili na kitengo cha Flying Doctors Africa wako chini ya Amref.. wanatoa huduma ya helicopter kwa ajili ya ku rescue mlimani incase of emergency. Kusema ukweli nilikua muoga saana kwa sababu ya stories unazosikia so ilikua ni tahadhari maana ilikua ndio first time kupanda mlima.. & you never know nini kitatokea huko juu milimani. Fee ni 50$ kwa mtu mzima.

Nilisoma kila habari kuhusu kilimajaro na kupanda Mlima.. vifo vinavyotokea.. risk ukiwa mlimani..

KUPANDA MLIMA ULUGURU:Uluguru height ni kama 8600ft na hii ilikua ni moja ya majaribio kabla ya kupanda Mlima... Uluguru was the easiest tulienda Ijumaa.. Jumamosi tukapanda Mlima... Jumapili tukarudi Dar.. Mandhari ya Uluguru ni bomba sana...Kuna memories nyingi ila mojawapo ni kuoga alfajiri katika water falls...... Jambo ambalo sikupenda Uluguru ni hali ya choo pale.. Nilibanwa haja kubwa ila mzigo wangu niliubana hadi nilivyorudi town maana kushusha gogo porini nilikua siwezi. I wonder kwanini SUA hawarekebishi.

Tent tulizotumia kulala
181393d9af06585dd377fcf76f9b607e.jpg

Hii ndio camp kunaitwa Morning Site..tulikofikia.. humo kuna chata za watu wengi

e388057a293813c80ee7f191631c286c.jpg

The View
16bc00a84e515adb383cf530a5c579ce.jpg

3f673959c9f79e081a5f7c6109e53c62.jpg

Nitaendelea Next post.

SAFARI YA MOSHI

Tunaingia Moshi usiku saa 2... Tunapokelewa na wenyeji.. wakarim kishenzi.. wale ma guide sijui walidhani tumetoka nchi gani hatuju kiswahili kumbe ni wabongo tu.. Nimesahau jina la hotel kiwatengu anaweza kunikumbusha. Pale hotelini kulikua na wazungu kibao.. wengi wakiwa wametoka mlimani wakipongezana dinner.. wines na kupeana vyeti... Nikawa nawatizama kwamba can I do this?? unaona watu wanachechemea miguu, sura hazitamaniki wamebabuka, hapo ni bonge la mtu wengi wako hoi.ile usiku tukafanyiwa training na rescue team ya ile kampuni.. tukapewa maelekezo yote muhim.. Asubuhi Safari ya Mlimani.

SAFARI YA MARANGU.

Alfajiri tunaamka.. Mimi pamoja na kununua vifaa vya mlimani lakini still nilikua nahitaji kodi baadhi ya vifaa kama Hiking boot, balaclava, walking stick.. sleeping bag.. na hizi ni zile zenye joooto maana huko juu tushaambiwa kuna baridi la kufa mtu.

Saa 3 asubuhi tunaanza safari ya Marangu. Si umbali mrefu. usajili getini tunamaliza saa 9. miezi ni High season kuna watu kutoka nchi mbali mbali wanakua wamekuja kupanda mlima.!kulikua na nyomi la kufa mtu. Jambo nililopenda Marangu getini kuna ramani ya njia unayotimia kufika kileleni na pia kuna picha za record za watu mbali mbali walifanikiwa kupanda mlima kwa muda mchache, kuna mmoja alipanda kwa 5hrs.. huyu najiuliza hadi leo alifanyaje fanyaje .. Masaa 5 hadi kileleni its not a joke

Marangu Getini hapo.

3e60d5fda7033b8ca1a8b1013a96d1f3.jpg
96e92c82d02ef15bdf21e69ee621c59f.jpg

Fuatilia next post.. huko ndio kwenye mziki

Safari ya Mandara.

f75e778e28a5a00dfe275f01fe7babc5.jpg

Hii ndio ilikua point yangu ya kwanza baada ya kutoka getini. Nilikua na personal porter anaitwa FREDY. Mwenyewe alinipokea bag na kijitambulisha vizuri kwangu. Ukiwa na personal guide ina maana yeye atakua na wewe bega kwa bega.. atakubebea back pack.. achana na wale guide wa group.

Tulianza kwa story akanielezea safari zake milimani.. yeye keshapanda mara 6 hadi Uhuru peak.. I was excited..mwanzo story zilikolea baadae zikakata ule uchovu.
Tunavyopanda tulikua tunakutana na makundi ya watu wanarudi na wengi walikua wanatuambia “pole pole” nadhani huu ndio msemo maarufu ukifuatiwa na “Jambo”.
Nilianza kuchoka jinsi masaa yanavyokwenda.. Nikawa kama siwezi kupumua vizuri muda mwingi Fred alikua ananisitiza kunywa maji...

Kuna muda wenzangu walikua mbele.. baada ya kupumzika nikasema hebu nikae hili kundi sitaki kubaki nyuma... Enhee bana kumbe kasi yao haiendani na mimi.. ila kutembea hata dakika 5 nyingi.. nikaona kama roho inataka kutoka mapigo ya moyo yanaenda mbio hatari roho kama yataka kuchomoka.. joto likanipanda.. Fred as usual akaniambia pumzika. Nikakaa chini vua sweta nikanywa maji.. baada ya muda ndio nikarudi hali ya kawaida.. Nilishaanza kupanick kuwa nakufa sasa. maana hapo si tulishaambiwa watu wanakufa huko sana na kila mtu unamwbia unaenda Kupanda Mlima unakuwa na doubt.. Mimi nikajua mama yangu hapa na mimi ndio bye bye

Akanishauri kuwa kila mtu ana speed yake so i should keep same speed maana tunazidi kupanda juu.. hali ya hewa ni ya mgandamizo.. Tunaingia Mandara saa 2/3 usiku. i was excited kwamba after a long walk kuna sehem tumefika tupumzike. Kitu cha kwanza ni ku register majina.. kulikua na baridi hatari mikono ilikua na ganzi hata kuandika nilishindwa waliiandikia jina nikaweka sign tu.

Tukaonyeswha dormitories nikatafuta kitanda changu cha chini..

c282b3eeccab55a3f072cfe19f3a018c.jpg

yaani kuna bariiidi hatari nikajifunika sleeping bag nikajilaza.. nina hasira kishenzi.. ukiuliza hasira za nini sijui..
Usingizi ukanipitia baada ya muda kidogo mtu akaja kuniamsha kwa ajili ya dinner yaani nilichukia nikaona sijawahi kukutana na mtu mbaya na katili duniani kama huyo alieniamsha kula.. Na hapo tunasisitizwa kwamba ni lazima ule kama unataka kufika juu.. Kufika kileleni nataka ila kama hali ndio hii NO WAY

Nikaanza kulia ndani ya sleeping bag... lia kishenzi.. Makamasi na machozi yanatiririka tu ila nalia kimya kimya watu wasinisikie. mtu unaweza kushangaa kama ni the same person niliyekuwa nashangilia muda mchache uliopita.. Nikawa najiuliza hivi nimekuja kufanya nini huku?? Baridi lote hili tena nikale huko nje.... nikaja kuamshwa tena hapo wenzangu hawawezi kula hadi watu wote watimie.. Nimefika dinning sijataka kuongea na mtu.. wakinichekesha najilazimisha kucheka. Huo muda Akili inawaza mambo kibao.

Chakula chenyewe nakutana na vegetable soup.. macaroni.. ndio siyapendi kudadadeki.. mikate.. chai... Chakula ni kizuri ila hamu ya kula sikua nayo hata kidogo.. Duh nakula then straight in bed sisemeshani na mtu. Na mtandao ni hakuna so no whatsup. Instagram wala JF.

Hii ni asubuhi.. tunajiandaa kwenda Horombo

57e4798f9e4bd7a8400770fcc660ae35.jpg

Huko ni njiani tu...
Daaa,hongera sana yaani nimekuwa very emotional wakati nasoma hili bandiko,utafikiri ni mimi,hongera mkuu
 
Hivi humo njiani hamna wezi na vibaka?, kwanini kusiwe na helicopter zinazofika hadi Uhuru peak? Huko juu Uhuru peak kwanini kusijengwe hotel moja matata sana yenye vifaa maalumu vya joto?
Haitakuwa kupanda mlima sasa
 
SAFARI YA KUSHUKA MLIMA..

71e42ea7ef4312fde77d882c8c3243de.jpg

Kule juu hatukuchukua muda tulianza kurudi kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya.. Nilikua nimechoka saaaaana. Tukatembea weee hadi tukafika Gilmans. Uzuri wa kushuka ni unaenda straight hakuna mambo ya kusema upite zig zag mle mle katika njia unapita tu.

Nilivyofika Gilmans nikaanza kushindwa kutembea miguu ikagoma kabisa..nikitembea dakika moja nyingi naishiwa nguvu nasimama au nakaa. Huo muda Fred alikua ameshashuka chini kwani yule mwenzetu niliemuacha nae aliishia Stella so alimrudisha chini. This time nikawa ma guide mmoja mtu mzima anaitwa Moses no comment on him but... Nikamkumbukaje Fred hapa angekua ananibembeleza [emoji23]

Nikaanza kulia.. kushuka ni rahisi ila mimi nilikua nimeishiwa nguvu. Kuna muda nilikua nakuangali kule juu najiuliza hivi mimi niliwezaje kupanda juu halafu hapo najisemea hata unipe bilion moja hunirudishi huko juu mimi...

mzee Moses ananisisitiza nijitahidi nishuke ananiambia Kibo ni pale tunafika sasa hivi wewe jitahidi..Na kweli naona vibanda vilee najipa moyo mwenyewe nanyamaza then naendelea kutembea.. Nikitembea kidogo nachoka nakaa tena naanza kulia. It was a mixed feeling... halafu pia nilikua nimeikumbuka familia yangu.... Tukipishana na watu wananipa pole kama zote.... Nikaishiwa nguvu siwezi kutembea mwenyewe so akawa ananishikilia ndio naweza kutembea.... Tumeshikizana wee Kufika sehem I couldn’t walk at all yaani hata kusimama mwenyewe nikawa siwezi... Hata nikijaribu vipi nashindwa.... ilikuja stretcher kunibeba na kunirudisha Kibo.

Wakati tunaelekea Kibo nilishangaa porters wengi wanapanda kuelekea mlimani. Nikawa najiuliza hawa jua lote hili ndio wanaenda kupanda Mlima nikauliza akanambia wanaenda kupokea watu wanaotoka mlimani. Wengine ndio hao wanarudi na hali kama ya kwangu.

Ukifika Kibo yaani wanakuhudumia vizuri hapo.. Nikapewa chai.. mara soup ya moto.. Tukaambiwa tupumzike kidogo tukiamka tunaanza safari ya Horombo. Ngoma hailali. Nikamuwazia yule mzungu aliefariki.. Nikasema silali wala nini nitakaa macho hadi hiyo time ya kurudi Horombo.. Nisije kufia usingizini. Ila Chezea usingizi na uchovu nilikuja kushtuka naamshwa nikale.. I wish niweke picha moja niliyopigwa wakati nimelala... I was half dead.. chakaram.

ku pack vitu was a headache.. Na ilitupasa tufanye haraka maana hizo domitories kuna wageni wengine walikua wamefika so inabidi waingie.. Saa 8/9 tunaaza safari ya kurudi Horombo.. Usingizi ulinisaidia sana huku nilikua poa njiani tunapiga story kwa saaana na wala sikua na uchovu mkubwa sana.. Rohoni kwangu najisikia safiii. Horombo nawahi kufika mapema kushinda hata wale wengine..Kuna baadhi ya watu walienda kuoga mimi sikuoga wala nini.. Nilisema hadi nifike mjini.. I want hot shower nikae hata lisaa bafuni.

Horombo tunalala then kesho asubuhi inaanza safari ya kurudi Marangu getini. Kabla hatujaondoka hapo Horombo tuliimbiwa nyimbo nadhani kama ni utamaduni fulani.. Nili enjoy saana zile nyimbo.. tukacheza pale.. Mimi na wenzangu 3 tulirudi Marangu getini na ambulance. Asubuhi ile Guide kama kuna mtu katika watu wake hayuko vizuri kuna gari linakuwepo for emergency kuwarudisha getini.. So wengine wanatangulia kwa miguu sisi tunabakia kusubiri gari...

Katika Ambulance kuna waarabu fulani ambao niliwakumbuka vizuri wakati wa kupanda kuanzia Mandara tulikua wote benet.. nao wanarudi kwa ambulance na mchina mmoja. Wale waarabu wa 4 they told us kwamba only 1 of them was able to reach the peak.. huyo mwanaume wale wadada hawakufika.... Mmoja wao alikua anatapika saana... alikua analalamika kuumwa... walituambia wametokea UAE.. Kurudi na gari was another experience..

Ile asubuh tulipoamka Horombo ndio tulianza kushangaana sura zetu [emoji23][emoji23] ni pua zimebabuka... ngozi haiko sawa.. ukimuangalia mwenzako unaweza kujiona wewe una afadhali na mwenzako nae akikuangalia anajiona yeye ana afadhali.. Sisi ndio tunakua wa kwanza kufika tunasubiria wenzetu waliokuja.

Final Goodbye na Porters

Tunapata wasaa wa kuagana na crew ya Origin pale Marangu getini maana baada ya hapo tulikua tunaenda hotelini na wengi wao wasingeweza kuja kule.. It was very sad. Its only few days we stayed in Kili but the bond we had shared with those people was so strong... Watu walilia saana...

Tip tulichangishana tangu mwanzo elfu 75 each.. na mwanzo tulipanga kila mtu achangie laki wengine wakaona laki nyingi tufanye 75... Maana tayari tulishalipia fedha.... ila baada ya kupanda mlima na kuona kazi wale watu wamefanya we all thought kwama 75 haikua pesa.. It was nothing compared na service walitotupatia kule juu. Ile pesa waligawana katika group. Sisi hatukutaka kila mtu ampe tip mtu mkononi kivyake.. maana kuna mtu wa jikoni yeye humuoni unashangaa tu chakula mezani.. kuna mtu anaebeba bag yako humuoni ila muda wote ukifika point fulani unaletewa bag liko salama. So kuna wengine hatu interact nao ila tunapata service yao. Wao wenyewe walijua waligawana vipi ile pesa.

Nilichukua mawasiliano na Fred.. Alinambia hataweza kuja hotelini.. na mpaka kesho kutwa huwa tunawasiliana ingawa most of the time anakua hapatikaniki yuko mlimani.. Nilimpatia tip yake personal tofauti na ile ya group na pia vifaa vingi nilivyonunua kwa ajili ya kupanda mlima nilimuachia.. Alishukuru sana. Pia alinambia ataenda kusomea mambo ya u guide kuna chuo huko.. Kwasababu yeye ni porter na ili uwe guide inabidi upate cheti... So kitu ambacho nimepanga ni kumsaidia part ndogo ya ada.. Mimi sio tajiri maisha yangu ya kuunga unga but what he did kwangu ni wema na utu wa hali ya juu. He was extremely caring. Very understanding.... Maybe that is the only way I can repay him.. Mara kibao huwa namwambia yeye ni mtu poa saana.

Tunarudi Hotelini.. Hiyo ndio siku kulikula misosi tunayopendelea.. It was a celebration evening.. Hiyo siku nilitumia karibu saa nzima kuoga.. maji ya motoooo... I was so relieved... Jioni tukagawiwa certificates wenye kunywa bia ndio walizinywa hapo na pia nilipata nafasi ya kuonana na kiwatengu kwa mara ya kwanza na nitumie nafasi hii kumshukuru kwa ushauri wake na moyo wa kunisaidia mpaka nikafanikisha safari yangu Kilimanjaro.

Wengi wetu tulipata na ganzi katika mikono siku zile za mwanzoni lakini baadae iliishia taratibu.

We came back to DSM safely with a lot of great memories. Climbing Mt Kilimanjaro to the peak is something that I will hold close into my heart. My trip was very eventful and joyous, I met new people who were very generous and down to earth like Fred.. they took care of me as if I were their own child/sister, I came across various obstacles, I strived for the best and most importantly I achieved my goal. It’s unreal how we became so attached with guides/porters in such a short period of time. I journeyed through pain, laughter, suffering, dirtiness and Mr Peters famous porridge and soup.(ambayo ilikua huwezi kukwepa kunywa)

I had the greatest moments and created incredible memories which will remain in my mind and heart forever. As they say nothing comes easy and it’s true, It wasn’t easy at all but I did it... One thing I learned is to appreciate everything this life offers.

I thank God for protecting me all the time, My Mother for her support.. My group mate who not only made the trip funny but also easy,.....Mr Emmanuel & Origin Team for for this wonderful journey[emoji92]

My family & Friends made this for Us..

80a1aea0e82016378de52fa15f5dd06e.jpg

The Team behind our success

28135f6fadaf143b68a13658755970bf.jpg

Going back to Horombo

8c6fd52e073b6e6758d8a5cbbf46ecb0.jpg

Last picture @ Kibo

bd15f5493f3ad6121c40f423cd68be42.jpg

I bought so many things pale Marangu Getini ikiwemo hii T shirt na i dedicate kwa wote ambao wanasema hawawezi kupanda Mlima

6ea49fb4301c3a3c19cbfaa139eae9f8.jpg

THE END
Very inspiring, what a good writer you are! I climbed it when I was in secondary school in early 80s!
 
Hongera kwa darasa hasa kwa wale ambao hawajapanda mlima Kilmanjaro,kwa kuusikia mlima kilimanjaro unaweza ukaona ni kazi rahisi sana kuupanda huo mlima lakini kuna changamoto nyingi sana ambazo zinaweza kuchangia mtu asipande na kikubwa ni kwenye huduma ya uokoani ambayo kwa kweli Tanapa hawajawekeza vya kutosha.

Kazi kubwa ipo kuanzia Kibo Hut kwa wanaotumia njia ya Marangu,ukiweza kufika Gilmans point unakuwa na uwezekano mkubwa wa kufika Uhuru Peak maana hicho kigongo ni mwisho wa matatizo,kuna haja ya kila mtanzania kwa kile alichojaaliwa aweze kupanda japo mara moja kila baada ya miaka mitatu .

Ni aibu kubwa mzungu anakuuliza umewahi kupanda mlima Kilimanjaro ukamjibu sijawahi,hii ni aibu sana kwa kweli.
 
Asante jitahidi me niliwahi panda mlima meru kabla na cho ni kiama lol ila kupanda milima ni kumbukumbu nzuri sana maishani
Hongera sana kwa kuweza kupanda huo mlima mwenzio nikiamkaga asubuhi nikiona lile libarafu najiona nimeshaupanda halafu umepitia njia ngumu machame uko vizuri
 
Back
Top Bottom