Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

-Ningependa kujua kuna njia ngapi(Routes) za kufika Kilele cha mlima kilimanjaro?-(
Marangu
Rongai
Machame
Lemosho
Umbwe)

-Mwanzoni tulifundishwa Kibo na Mawenzi ndio vilele vya mlima kilimanjaro ila kwenye hii thread nimeona vilele zaidi ya 10 na kingine naambiwa Uhuru peak,Je Uhuru ndio Kibo au Mawenzi? Vilele vipo viwili mawenzi ambacho hakipandwi kina miamba nachani ndo caldera na Kibo...katika kibo ukipanda kuna vituo kwa njia ya marangu kuna stella point,gilmans point,then unafika juu kabisa uhuru peak

-Inachukua siku ngapi kwa kupanda hadi kufika kilele cha mlima k/njaro? Kwa Routes zote.(kuanzia siku5 hadi 7 kwenda na kurudi inategemea na ulipopandia)

-Tupeni faida/changamoto za routes zote za kufika kwenye peaks.kila route inachangamoto zake ukisoma mada humu watu wamejaribu elezea

-Gharama za kufika huko either personal au kutumia agents.(kuanzia laki5 hadi 1.5 inategemea idadi ya watu mliopo)

-Vitu gani vya kuzingatia ukitaka kwenda huko gears/facilities.(mountain boots,mountain clothers,head gear ,sungrasses mhm sana koz ukiiangalia barafu bila mawani unapata temporary blindness)

-Hali ya kiafya,je inatakiwa uwe katika situation gani ya kiafya ili usipate makandokando ya kufika peak,maana wamezungumzia afya general iwe nzuri,kwahiyo watu wenye HIV,pressure,kisukari etc hawewezi kuruhusiwa kwenda?Kikubwa usiwe na matatizo yoyote kwe mfumo wa kupumua...hata mtoto wa miaka 10 anapanda.mfano ni kama ukiwa unakimbia huku umefumba pua ile feeling ndo inakua mda wote kule juu
Wengine watazidi kujazilizia
Thanks sana mkuu.
 
Heaven Sent

Naomba nikiri kwa mara ya kwanza kuwa huu kwangu ndio umekua uzi bora kabisa wa kufungia mwaka,tangu jana sibanduki hapa na umeniinspire kiasi cha kuweka dhamira kuwa mwaka huu 2019 lazima nianze tizi nitapanda mlima loleza na mlima mbeya kama maandalizi ya kupanda kilimanjaro kabla ya mwaka huu kuisha,nimekupenda sana dada yangu.

Ubarikiwe sana Heaven Sent.

Kwenye maisha ukiwa na dhamira hakuna kinachoshindikana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni heaven on earth sio heaven sent
Heaven Sent

Naomba nikiri kwa mara ya kwanza kuwa huu kwangu ndio umekua uzi bora kabisa wa kufungia mwaka,tangu jana sibanduki hapa na umeniinspire kiasi cha kuweka dhamira kuwa mwaka huu 2019 lazima nianze tizi nitapanda mlima loleza na mlima mbeya kama maandalizi ya kupanda kilimanjaro kabla ya mwaka huu kuisha,nimekupenda sana dada yangu.

Ubarikiwe sana Heaven Sent.

Kwenye maisha ukiwa na dhamira hakuna kinachoshindikana.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HOROMBO.

5b9b773c85ba173c3a61848751efa146.jpg


Katika vituo vyote sehem niliyoipenda zaidi kukaa ni horombo. Ilituchukua masaa karibu 9/10 kufika HOROMBO. Ni sehem iliyo changamka.. kama kijiji fulani hivi..katika safari yetu Kuna vituo vya kupumzika.. Na pia kuna sehem huko huko barabarani ni stop kwa ajili ya Lunch... Kuna upepo na baridi sana yaani kuliko kukaa nje mtu unaenda chooni upepo usikupige. Vyoo ni Safi na vimejengwa vizuri.

nakumbuka nikiwa nakaribia kibao cha Horombo I was excited kwamba nimefika after a long walk, nikaanza kutembea haraka huku nashangilia na kupiga mayowe, haikuchukua hata sekunde kadhaa hali yangu ikabadilika I couldn’t walk, mapigo ya moyo hayakua sawa kutembea nikashindwa, kihere here chote kikaishia hapo.. ikabidi nipumzike chini na waanze kuniangalia hali yangu. baada ya dakika kadhaa hali yangu ilivyokua sawa ndio nikafika hapo. Yaani usicheze na mambo ya altitude..

Complication..

Ilipofika usiku nikaanza kujisikia vibaya... Yaani sijielewi elewi hali yangu sio nzuri, nikaenda kupima oxygen na vitu vingine wakanambia niko safi tu laba uoga na mawazo. Na kweli I was scared. Nikaingia kulala mapema nikashtuka kama saa 7 USIKU, MAPIGO YANGU ya moyo yanapiga kwa kasi ya ajabu, siwezi kuhema vizuri, nikiangalia pembeni naona kama kila mtu kalala, nikalaani kitendo cha kushtuka mida hiyo nikihesabu muda naona hadi kukuche its like forever. Na nikawa naogopa pia kulala usingizi what if hivi ninavyoshindwa ku breathe ndio nipitilize moja kwa moja.

Sim hazitoki... hakuna mtandao..The only thing nilifanya ni kusikiza music tu mpaka kunakucha. Nimesikiza album za Maher Zain hapoo wee.. Asubuhi tunavyohadithiana kumbe kila mtu anasema I couldn’t sleep last night..





Sent from my iPhone using JamiiForums

View ya Horombo jioni utaona mlima unaonekana kwambalii
eb09577086d34256d89f5ed7753968ab.jpg



Kuelekea Horombo.. Mvua ilikua inayesha muda huo.. ndio maana full kujifunika
ed299501727a66b26ceeb7f8e45f97c8.jpg



Hawa porters.. Imagine hii ndio maisha yao ya kila siku.. wadada tuwe na huruma [emoji23]
43ddc7a5d575fb3e0232efa1b502b968.jpg


Picha ya kwanza baada ya kuweza kutembea na kufika kibaoni[emoji23][emoji23]

a214bb2f38fc77b729224f8bfe21cefd.jpg


Baada ya kupata joto..

b390627c55eb4e7f9398dc5f64a1d03d.jpg


Lunch point hiyo sehem kuna upepo hatari. Mr Peter huyo rasta yeye kazi yake ilikua kuhakikisha tunapata msosi. He is a very nice guy.. anajua kazi yake.. Sijapata kuona aisee

5896567e1c96d7c4065684ffdcb8a586.jpg
18a0cabeec5b7293383222e9e4b6f093.jpg


SAFARI YA ZEBRA ROCKS - ACCLIMATIZATION DAY

078fa31d626341b788a6ee01e95ef626.jpg


Hapa tunakaa one day kwa ajili ya Acclimatization. Sijui kiswahili wanasemaje. Ukipita njia ya Marangu lazima uwe na siku moja ya kukaa hapo ili kuzoea hali ya hewa ya mlimani.. hii pia wanasema inaongeza chance ya kufika summit

Asubuhi nikawa fresh sio kama yule mtu nilikua naumwa usiku. Tangu tuanze safari hii ndio siku naingia kuoga.. Kuna baridi saana yaani maji yanatoka katika bomba ila yanaganda na kuwa barafu.. ila niliona bora kuoga. Kama huogi unajisafisha na wet wipes ama wet towels na kubadili nguo tu.


NAKUMBUKA ilikua birthday wa mmoja wa crew yetu wale ma guide walifanya suprise ya cake, wakaimba nyimbo zao fresh saana, mimi mwenyewe nikawa mmoja wa waimbaji baada ya breakfast mood ikawa zero kabisaa, nikaenda kuongea na guide mkuu akanambia nisiwe na wasi wasi I will be okay. machozi yakaanza kunilenga lenga Mim nikaona kama hanitendei haki ataniambiaje niko sawa wakati mimi namwambia naumwa.

DIAMOX:Hizi ni dawa tulishauriwa kununua zinasaidia kama mtu ukipata altitude sickness na mimi kwa vile nilivyokua najisikia nikazinywa kwa mara ya kwanza.

I was so emotional and sensitive..nikapanda juu tunakolaa nikaanza kulia, ila nalia sitak mtu ajue kama nalia.. Ilivyoanza safari ya Zebra Rock nikawa wa mwisho kabisa kutoka hapo niko na FRED.. Mtu akiniongelesha ndio nahisi nipaze sauti nilieee .. Nilitembea kidogo then nikakaa katika jiwe nikaanza kulia.. Fred na porter mwingine wamesimama pembeni yangu kimya wananiacha tu nilie.. Nikaliaaa weee hapo nikawa nalia kwa sauti... hiyo point pia kuna network nikaomba simu nipige.. Nikawaza kumpigia Baby huo muda hatukua vizuri I was like what if asipokee au apokee asiniambie maneno ya kunifariji ninayotaka. Sikumpigia. I called kiwatengu maana yeye ndio alikua kama guide wangu mkubwa katika safari hii. Alipopokea tu sim aka notice kuwa nalia.. Akaanza kunishauriii wee akanipa moyoo... Ikanisaidia kiasi chake.

Tulienda Zebra rocks na kurudi Horombo. Ni kama 4500m kufika. Kufika kule nikawa poa kabisa kama sio yule niliekua nalia huko chini.. nikajumuika na watu na pia nikapanga mawe kule. Ukitembea Zebra Rocks pembezoni watu wamepanga Mawe na hawashauri kupangua hayo mawe if you want unaweza kupanga ya kwako.

One thing nili notice watu wengi tulikua tunapata emotional break down bila sababu ya msingi.. sio mimi tu nilililia kuwa wengine pia.. na kila mtu alikua na namna alivyo i handle.




Sent from my iPhone using JamiiForums

a4aca4a91708c93f92530680389d139a.jpg


Nikiwa na Fred.. He is such a nice guy sijapata kuona.. Mtu mwema sana

0dc38baa36bc40e3bbc503a1fb7491ba.jpg


Kunaitwa Zebra Rocks kutokana na hiyo mistari kama pundamilia..

7e13c1fdf131cd175b50a39fd98ae600.jpg


Hiko kilima hapo nyuma ni Mawenzi

8a56c6b733c81c0c50bb931585493815.jpg


Okay

8ee8ab5002b515215590686241ab9737.jpg



Sent from my iPhone using JamiiForums
i know this pictures[emoji41][emoji41][emoji41]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera sana mdada umefanya vyema sana zaidi umezidi kunipa moyo wa kukwea huo mlima japo binafsi nimeshajaribu sana kuwasihi jamaa zangu tupeane kampani twende ila wanakataa naamini ipo siku nitapanda, aidha nizidi kukupongeza kwa kazi nzuri uliyofanya na ya kututia moyo pia kwa usimulizi wako murua. Stay blessed

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona uvivu kuendelea kuandika..

Mniombee ndugu zangu in JP voice. [emoji23]


Sent from my iPhone using JamiiForums
Mi nishakuombea uendelee, umesimulia vizuri sana, napenda story za aina hii na kutalii, mi niliwahi kupanda mara moja ila visa yetu ilikuwa inaishia mandara hut

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom