Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Huwezi ndugu coz kulala tu kwenye huwezi kujinyoosha, unajikunja ili upate joto, halafu nguo za kulalia zinabana fulani hivi mfano zetu zilikuwa zinaitwa thermos, ukivaa hizo nguo then shuka ni kama mfuko hivi, unaingia zako kwenye hilo shuka....unajikunja kuutafuta usingizi

Salute to those porters.....niliwashangaa wale watu lkn pia nilimshangaa Mungu..... kwenye jiwe la kubusu sisi tunawaza tutapitaje manake ukiteleza kidogo tu wanakusahau lakini wao wanapita utadhani wanapita kwenye barabara tena na mizigo kichwani au mgongoni na mkifika kituoni mnakuta wameshafunga matent, kila mtu bag lake limeshawekwa kwenye tent lake, wameshaivisha chakula, meza zimeshaandaliwa and they are so kind and humble. Nilisikitikaga sana kusikia zile kampuni zinawalipa ujira mdogo sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Basi mi nilijua hilo baridi ndo linahamasisha kunjunjana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Congratulations kwako Heaven on Earth ujasiri mkubwa sana,despite machache uliyopitia yaliyokuweka katika wakati ngumu remember"we never promised good way,always rough" Niko inspired kitambo sana,mpaka nikapata fursa ya kwenda bure kabisa but majukumu was on my toe,I couldn't take a step to anywhere. But I will,mwakani,naanza kutunza kububu cha MT.KLM. Thank you strong lady
 
Nakupongeza tena Heaven On Earth, kupitia uzi huu:
Nimefanya mazoezi ya maandalizi na wewe,
Nimepanda na wewe,
Nimeona jamaa aliyefariki akishushwa sambamba na mkewe katika majonzi,
Nimechoka na wewe,
Nimelia na wewe,
Nimekata tamaa na wewe lakini nikajifariji na wewe na nikasonga mbele na wewe,
Nikawaona wavuta bangi wakitupita kwa kasi na badae mmoja wao akathibitisha kutangulia si kufika, akarudishwa duniani,
Kila ulipochoka, akili yangu ilikupa moyo, "twende HOE bila wewe siwezifika kileleni" ulikubali kwa machozi ya uchovu,
Nilisonga na wewe,
Simu yako iliishia chaji, nilihuzunika kwa kuwa hata kama tukisonga pamoja sitaona tena taswira nzuri ya safari yetu,
Nikawasikia ma-guide wakishauriana juu ya kuendelea ama kutoendelea na safari, nikaiona hatari ya kifo mbele yetu, nikasikitika.

Ukungu ulipozidi kule juu kiasi cha kutomuona aliyeko mbele yako, nilipatwa na hofu labda utapotea na kuporomokea upande wa Kenya,
Lakini nilikuwa na wewe,
Picha ya mwisho ambayo barafu imeziba maandishi ya kibao cha Uhuru Peak, ilinitia simanzi kubwa kwa hali ya hewa, nikajaribu kujifananisha na wewe kwa kujidumbukiza kwenye freezer ya butcher, lakini ukasema barafu niiwazayo mimi ni "cha mtoto"...

Hata hivyo, kwa jinsi ulivyotiririka kwa ustadi mkubwa, sikutamani muishie hapo na safari ya kurudi duniani ianze...

Nilitamani safari iendelee, mzuka wa simulizi yako uliniaminisha kuwa baada ya Uhuru Peak, Heaven on Earth would be taking me to the next peak... And probably it could be real Heaven like her name... Can't wait for the next episode.

Pongezi kwa guide wako Fredy kwa kukufikisha kileleni, iwe funzo kwa wanawake wengine wote kuwa, mwanaume kumfikisha mwanamke kileleni haijawai kuwa kazi rahisi, yaitaji uvumilivu na kushikamana.

Hongera sana HOE.
Ngoja nielekee You tube kujazilizia elimu hii tamu.
 
STELLA POINT.
e43ceb86210e16086d81156551c61482.jpg


Nilivyofika Gilmans nilipata some sort ya relief.. Na kwa mimi nafikiria Gilmans was the hardest part. Watu wengi huwa wanaishia hapo anakosa nguvu ya kuendelea mbele. Wote katika group yetu tulipumzika then tukaanza safari ya kuelekea Stelle.

Njiani kulikua na barafu saana.. The wind is blowing hatari.. tulikua tunatembea juu ya barafu.. Problem nyingine ni kwamba tulikua hatuwezi kuonana kutokana na ukungu..Mtu yuko hatua tatu mbele ila huwezi kumuona kwasababu kuna ukungu wa kufa mtu. To be honest ilikua inatisha..

Shida inakuja kuwa hewa inakua ndogo saana. Nikaanza kuona hali tete kabla hatujafika...baada ya Masaa kadhaa tukafika Stella... Pale Kibaoni tukapiga picha haraka ili tuendelee mbele.

f88521fdd08c07bd253e06eb7726140c.jpg




Sim yangu haikuweza kuwaka.. We only took group photos

8539d6d4096127f29fe7bbc33369ec6e.jpg



UHURU PEAK.


Baada ya pale tukaanza kuitafuta Uhuru..Ambayo ni kama 30mints.. hizi dakika kuzitamka hapa unaona chache ila ukiwa kule juu ni kama mwaka...Yaani hali ya hewa ilikua mbaya saana. Nilikua nime sha give up nimechoka na nilikua sijielewi yaani natembea tu.. Sielewi kitu. Niliambiwa nilipata Hallucination..

Kuna baba mmoja mwanzoni niliwaambia kuwa yeye kapanda mara 18 ila alisema katika kipindi choote alichopanda hakuwahi kukutana na hali tuliyokutana nayo sisi kule juu. Storm inayopiga ni ya hatari..... Upepo unapiga mnakimbilia katika jiwe kubwa ili atleast upepo upungue kidogo ndio tuendelee mbele. Jamani nilikua kama naiona jehanam. It was life and death experience kule juu. Upepo ukivuma ukija hivi uso wote unafunikwa na barafu... Nilikuja kuambiwa baadae kuwa storm tuliyokutana nayo huko juu haijawahi kutokea for decades

Tukaanza kupotezana hapo.. Guide mkuu akasisitiza hali ni mbaya turudi tusiendelee mbele..kiongozi wetu anasema haiwezekani.. Mimi nilikua sielewi kitu siwezi kuongea nawatizama tu.... hata haya mengine nilikuja kuhadithiwa Yeye alikua anasisitiza hakuna mtu anarudi.... Yaani hapo hadi ulitokea ugomvi kati yetu na guide mkuu anaetuongoza. Storm ni ya hatari inapuliza mpaka unasikia jiwe kubwa linatikisika hapo nawaza hili jiwe si linaweza kubiringita hapa then litudondokee ndio iwe bye bye


I reached Uhuru Peak.. kufika summit was one of the best experiences of my life. The summit view was absolutely stunning and I don’t think any words could really give a justice... Unapaswa ushuhudie mwenyewe mtu asikuhadithie. Yaani nilisahau hata ile dhoruba tuliyokutana nayo...

Niliona mazoezi na jitihada zangu zimezaa matunda mwisho wa siku, I felt a sense of achievement kwa kutimiza kile ambacho nilijiwekea kwamba i want to STAND ON THE ROOF OF AFRICA. Nakumbuka nililia saana.... Nikiwa summit na pia wakati wa kurudi ni machozi ya furaha na relief. Mind you sisi hatukuchuka hata dakika pale juu tuligeuza muda ule ule kutokana na hali ya hewa.


4d30f6deb3d8dd89ae4b96c4086403f6.jpg


Group yetu wote hatukufanikiwa kukigusa kibao wala kupiga picha katika kile kibao.. Hii ni kutokana na barafu nyingi. Wote tulikubaliana as long as tumefika Peak hiyo inatosha... It was sad thing kutokupiga picha pale lakini pia ukifikiri ulikotoka na pale tulipofika unaona IT was okay

Nikipokea certificate yangu

daa9cf6211f80256f29dd4d894cd559b.jpg


Ukumbusho wa cheti.

f351a28485629dae51e0af9feaf946f6.jpg


Next post ya mwisho nitamalizia kushuka.
I can feel you. I did half and it was like hell. Congrats.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom