Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Wanaweza mbona...
Mwenyewe ni kibonge na nina mpango wa kupanda! Ila watu tuloko nao wanakata tamaa kila leo!

😂😂😂jitahidini mfike
 
Nakupongeza tena Heaven On Earth, kupitia uzi huu:
Nimefanya mazoezi ya maandalizi na wewe,
Nimepanda na wewe,
Nimeona jamaa aliyefariki akishushwa sambamba na mkewe katika majonzi,
Nimechoka na wewe,
Nimelia na wewe,
Nimekata tamaa na wewe lakini nikajifariji na wewe na nikasonga mbele na wewe,
Nikawaona wavuta bangi wakitupita kwa kasi na badae mmoja wao akathibitisha kutangulia si kufika, akarudishwa duniani,
Kila ulipochoka, akili yangu ilikupa moyo, "twende HOE bila wewe siwezifika kileleni" ulikubali kwa machozi ya uchovu,
Nilisonga na wewe,
Simu yako iliishia chaji, nilihuzunika kwa kuwa hata kama tukisonga pamoja sitaona tena taswira nzuri ya safari yetu,
Nikawasikia ma-guide wakishauriana juu ya kuendelea ama kutoendelea na safari, nikaiona hatari ya kifo mbele yetu, nikasikitika.

Ukungu ulipozidi kule juu kiasi cha kutomuona aliyeko mbele yako, nilipatwa na hofu labda utapotea na kuporomokea upande wa Kenya,
Lakini nilikuwa na wewe,
Picha ya mwisho ambayo barafu imeziba maandishi ya kibao cha Uhuru Peak, ilinitia simanzi kubwa kwa hali ya hewa, nikajaribu kujifananisha na wewe kwa kujidumbukiza kwenye freezer ya butcher, lakini ukasema barafu niiwazayo mimi ni "cha mtoto"...

Hata hivyo, kwa jinsi ulivyotiririka kwa ustadi mkubwa, sikutamani muishie hapo na safari ya kurudi duniani ianze...

Nilitamani safari iendelee, mzuka wa simulizi yako uliniaminisha kuwa baada ya Uhuru Peak, Heaven on Earth would be taking me to the next peak... And probably it could be real Heaven like her name... Can't wait for the next episode.

Pongezi kwa guide wako Fredy kwa kukufikisha kileleni, iwe funzo kwa wanawake wengine wote kuwa, mwanaume kumfikisha mwanamke kileleni haijawai kuwa kazi rahisi, yaitaji uvumilivu na kushikamana.

Hongera sana HOE.
Ngoja nielekee You tube kujazilizia elimu hii tamu.

LOL... Umenifanya nicheke saana, Thank you kwa kunifatilia na kusoma mwanzo hadi mwisho
Nitamalizia safari ya kurudi chini muda si mrefu.
 
Niwe tu mkweli, story hii nimeisoma kwa ajili tu ya kutaka kuona picha mbalimbali za msimuliaji, hasa baada ya hii picha hapa chini.

16bc00a84e515adb383cf530a5c579ce.jpg


Muda wote nilitaka kuona picha picha picha, then story ikawa tamu nikajikuta navutiwa na masimulizi.

Heaven on Earth asante sana, nimeona kuna mahali umesema 2020 una plan ya kwenda, please am making my own arrangements kuhakikisha naungana na ninyi kwenye hiyo safari.

I know how to reach you.

Happy New Year.
 
Jamani Jamii Forums kumbe tuna warembo wazuri hivi,nashukuru siku hiyo ulipokuwa unapanda nilikufanyia usaili pale main ofisi,kumbe ndio wewe Heaven on Earth,japo umeficha sura nimekufahamu,uko too blessed
 
Heaven on Earth ,
..HONGERA sana.

..umezungumzia BARIDI kali kadiri mlivyokuwa mkipanda mlima.

..Je, hiyo ni mara yako ya kwanza kukutana na baridi kali.

..Umewahi kuishi ktk nchi zenye baridi kama Canada, Usa, au nchi yoyote ya bara ulaya?

..Je, kuna tofauti kubwa kati ya baridi ya majira ya winter na baridi ya wakati wa kupanda mlima Kilimanjaro?


MKUU umeuliza maswali ya msingi sana. Najua Heaven on Earth atakuja kujibu hapa, lakini kwa uelewa wangu, ile hali ya kule juu haiwezi kufanana na nchi yeyote kwa sababu moja kubwa. Hali ya mwinuko juu ya usawa wa bahari. Hiyo peke yake, inafanya kiwango cha Oxygen kuwa kidogo na kuleta hali ya kupumua kwa shida. Baridi la kule maji mnayobeba mgongoni yanaganda, inafika wakati ni nyuzi hasi 15 na kushuka chini Zaidi. Kuna nchi zinaweza kuwa na hali ya baridi Zaidi kuliko huko Uhuru Peak lakini mwinuko wake hauleti shida kwenye mfumo wa upumuaji. Hiyo ndio tofauti kubwa.

Kumbuka mnafika mahali ambapo mvua ikinyesha haiwahusu, inashughulika na walio chini yenu, nyie mpo juu yake.
Mengine wataongezea wataalam na mainjinia watakapokuja kusoma hii unayotaka kusikia hii hahahahahahaaa.
 
Jamani Jamii Forums kumbe tuna warembo wazuri hivi,nashukuru siku hiyo ulipokuwa unapanda nilikufanyia usaili pale main ofisi,kumbe ndio wewe Heaven on Earth,japo umeficha sura nimekufahamu,uko too blessed
Siku hizi urembo sio kitu kwenye uhalisia wa maisha yetu hapa. Mwanamke akikosa akili huku akiwa mrembo ni sawa na nguruwe aliyevishwa hereni. Akili zinazotakiwa sio za darasani hata kuweza kumshawishi mwanaume akakuoa ni akili pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiishia Kibo maana yake ni kwamba utakuwa umeishia njiani,Kibo ni kituo cha miwsho kabla ya kuanza safari ya kuelekea Uhuru Peak kwa Njia ya Marangu na huwezi kupata cheti kutoka Tanapa.

Mgeni ananza kupata cheti kuanzia Gillmans Point,Stella Point na baadaye Uhuru Peak
 
😂😂😂madame mie naon wanaOpanda wengi ni maportable..hv wanene wanaweza kweli?yaan bado sijashawishika ..maana nikama safari ya jehanum jaman
Yaani we acha tu.
Ila Heaven on Earth kaniambia wanene tunapanda tu...kikubwa ni kufanya medical check up na Dr. atakwambia kama upande au lah!!
Hv ndio ghafla nafika katikati, lile baridi mafuta yanaganda kwenye moyo, nashindwa kuendelea na safari....wale wagumu wataweza kunibeba kweli....
Dahh!!!
 
Coldril sio dawa nzuri kwa mazingira ya kule ina mchanganyiko wa dawa ambao unaweza ukakuletea usingizi ukawa kama umelewa itakuwa ni hatari kwako na zaidi unaweza ukashindwa kupumua vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yap.
Hiyo inaleta usingizi ndio....ila naweza fanya njia gani mbadala ili nami niwe katika hali nzuri bila mafua?
Maana mimi nina allergy na baridi vibaya sana.
Yaani mvua tu ikinidondokea....napata mafua.
Maji ya baridi yakigusa tu ngozi...ni balaa
 
Angeulizwa akiwa mlimani angesema siwezi thubutu kufanya huu upuuzi tena. Ni majibu niliyoyatoa mimi
Ila kwa sasa natamani hata kesho niambiwe anza maandalizi ya Kilimanjaro hiking
Pole na Hongera sana mdada Heaven on Earth , nafikiri hii itakua moja ya post bora ya 2018 sijawahi kuhamasika kupanda licha ya kuwa na ndugu alikua anafanya.kazi pale marangu lango la.kuingia kupanda mlima me nikaishia pale waterfalls lakin kwa jinsi ulivyosimulia nimeshwishika sana mdada anapanda mlima mimi nashindwa hata kujaribu ingekua vizuri kama ungekua umechukua video ungeitengenezea TV show nzuri na utafute kituo bora cha TV urushe kipindi maana TBC hamna anaetaka kuangalia hata kama wanaonyesha.
SWALI : Je toka umapanda umeshawahi.kufikiria kupanda tena na kama ndio ilikutumia muda gani kufikiri kupanda tena?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom