Kasiano Muyenzi
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 13,858
- 22,729
Mount kilimanjaro sio hifadhi ya wachaga natamka rasmi mimi jiwe😀😀😀
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Wanaweza mbona...
Mwenyewe ni kibonge na nina mpango wa kupanda! Ila watu tuloko nao wanakata tamaa kila leo!
Nakupongeza tena Heaven On Earth, kupitia uzi huu:
Nimefanya mazoezi ya maandalizi na wewe,
Nimepanda na wewe,
Nimeona jamaa aliyefariki akishushwa sambamba na mkewe katika majonzi,
Nimechoka na wewe,
Nimelia na wewe,
Nimekata tamaa na wewe lakini nikajifariji na wewe na nikasonga mbele na wewe,
Nikawaona wavuta bangi wakitupita kwa kasi na badae mmoja wao akathibitisha kutangulia si kufika, akarudishwa duniani,
Kila ulipochoka, akili yangu ilikupa moyo, "twende HOE bila wewe siwezifika kileleni" ulikubali kwa machozi ya uchovu,
Nilisonga na wewe,
Simu yako iliishia chaji, nilihuzunika kwa kuwa hata kama tukisonga pamoja sitaona tena taswira nzuri ya safari yetu,
Nikawasikia ma-guide wakishauriana juu ya kuendelea ama kutoendelea na safari, nikaiona hatari ya kifo mbele yetu, nikasikitika.
Ukungu ulipozidi kule juu kiasi cha kutomuona aliyeko mbele yako, nilipatwa na hofu labda utapotea na kuporomokea upande wa Kenya,
Lakini nilikuwa na wewe,
Picha ya mwisho ambayo barafu imeziba maandishi ya kibao cha Uhuru Peak, ilinitia simanzi kubwa kwa hali ya hewa, nikajaribu kujifananisha na wewe kwa kujidumbukiza kwenye freezer ya butcher, lakini ukasema barafu niiwazayo mimi ni "cha mtoto"...
Hata hivyo, kwa jinsi ulivyotiririka kwa ustadi mkubwa, sikutamani muishie hapo na safari ya kurudi duniani ianze...
Nilitamani safari iendelee, mzuka wa simulizi yako uliniaminisha kuwa baada ya Uhuru Peak, Heaven on Earth would be taking me to the next peak... And probably it could be real Heaven like her name... Can't wait for the next episode.
Pongezi kwa guide wako Fredy kwa kukufikisha kileleni, iwe funzo kwa wanawake wengine wote kuwa, mwanaume kumfikisha mwanamke kileleni haijawai kuwa kazi rahisi, yaitaji uvumilivu na kushikamana.
Hongera sana HOE.
Ngoja nielekee You tube kujazilizia elimu hii tamu.
Heaven on Earth ,
..HONGERA sana.
..umezungumzia BARIDI kali kadiri mlivyokuwa mkipanda mlima.
..Je, hiyo ni mara yako ya kwanza kukutana na baridi kali.
..Umewahi kuishi ktk nchi zenye baridi kama Canada, Usa, au nchi yoyote ya bara ulaya?
..Je, kuna tofauti kubwa kati ya baridi ya majira ya winter na baridi ya wakati wa kupanda mlima Kilimanjaro?
Hujamsoma sentensi ya mwisho kuhusu FredLOL... Umenifanya nicheke saana, Thank you kwa kunifatilia na kusoma mwanzo hadi mwisho
Nitamalizia safari ya kurudi chini muda si mrefu.
Siku hizi urembo sio kitu kwenye uhalisia wa maisha yetu hapa. Mwanamke akikosa akili huku akiwa mrembo ni sawa na nguruwe aliyevishwa hereni. Akili zinazotakiwa sio za darasani hata kuweza kumshawishi mwanaume akakuoa ni akili pia.Jamani Jamii Forums kumbe tuna warembo wazuri hivi,nashukuru siku hiyo ulipokuwa unapanda nilikufanyia usaili pale main ofisi,kumbe ndio wewe Heaven on Earth,japo umeficha sura nimekufahamu,uko too blessed
Yaani we acha tu.😂😂😂madame mie naon wanaOpanda wengi ni maportable..hv wanene wanaweza kweli?yaan bado sijashawishika ..maana nikama safari ya jehanum jaman
Yap.Coldril sio dawa nzuri kwa mazingira ya kule ina mchanganyiko wa dawa ambao unaweza ukakuletea usingizi ukawa kama umelewa itakuwa ni hatari kwako na zaidi unaweza ukashindwa kupumua vizuri.
Sent using Jamii Forums mobile app
Uhuru nilifika mkuu.Ok,nimekusoma mkuu.Vipi lakini ulifanikiwa kufika Uhuru peak au uliishia pale Hans mayor?
Sent using Jamii Forums mobile app
Pole na Hongera sana mdada Heaven on Earth , nafikiri hii itakua moja ya post bora ya 2018 sijawahi kuhamasika kupanda licha ya kuwa na ndugu alikua anafanya.kazi pale marangu lango la.kuingia kupanda mlima me nikaishia pale waterfalls lakin kwa jinsi ulivyosimulia nimeshwishika sana mdada anapanda mlima mimi nashindwa hata kujaribu ingekua vizuri kama ungekua umechukua video ungeitengenezea TV show nzuri na utafute kituo bora cha TV urushe kipindi maana TBC hamna anaetaka kuangalia hata kama wanaonyesha.
SWALI : Je toka umapanda umeshawahi.kufikiria kupanda tena na kama ndio ilikutumia muda gani kufikiri kupanda tena?
Ni kweli, changamoto ya ratiba ndo penye utata! Ila acha tuone. Mimi kufikia 2020 lazma niwe nimeukwea huo mlima.Hilo nalo linawezekana kulingana na ratiba ya mtu!
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122] kulala crater ulitumia route ya muda mrefu kidogo