Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Heaven on Earth
Hongera sana my dear, umenifanya nizidi kuamini na mimi naweza kuukwea mlima! Kama wewe mwembamba umeweza hata mie kibonge nitaweza zaidi!
Yaani hongera mnoo!
Unaweza sana, kujipanga tu physically, mengine yanawezekana! Maana kama ni mabadiliko ya hali ya hewa kila mtu yanampata awe kibonge au mwembamba.

Huu lazma tuukwee[emoji41]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wamenifurahisha walivyoweka utaratibu wa kutoa vyeti.

Kwamba huo ni mtihani,unatakiwa uufaulu kwa namna yoyote ile,vinginevyo personally hata wewe unajihisi kuwa disapointed kabisa.ndio maana dada yetu alikuwa analia na kuona walioshindwa au kufariki kabisa lakini yumo tu[emoji23][emoji23][emoji23].

Kwakweli tz inapendesha na kushangaza,kwa kupitia hii journey to the top.kazi kwao hao tz safari wa tbc wanatakiwa wachukue documentary basement mpaka huko juu na kueleza uhalisia,but kama kawaida yetu subiri vituko.
 
Utamu wa huu uzi balaah!!

hapa sijamaliza kuusoma,nimeishia hapo getini marangu ulipokuwa unaangalia picha za watu mbali mbali walipanda mlima na kuweka rekodi

Natafakari kidogo uyo aliepanda kwa 5hrs only,daaah!! huyu alikua na mapafu gani aisee? au alikua anapanda kwa kukimbia?, au ndo alipanda non stop mpaka kileleni? hahahahaa bila shaka uyu atakua alipanda kwa kutumia Toyo.....very interesting
 
Nimesoma baadhi ya comments wamesema kuna sehemu route ya Machame pamekaa vibaya njia nyembamba sana halafu kuna steep slope na njia nyembamba,kwahiyo kupita hiyo sehemu inabidi ulikumbatie jiwe halafu unapita polepole sasa hapo ndio kupita kuna kasheshe mda mwingi unapotea hapo.
Pasikutishe mkuu hamna hatari kubwa sana ya kutisha, porter hapo zinapita na mzigo mnene bila tatizo sembuse we mwenye ka backpack kako tu na fimbo pakushinde? Kikubwa wakati mwingine ni kuwa makini na porter aliyeko mbele yako kwani ikitokea bahati mbaya mzigo wake ukateleza ukuguse kuna uwezekano nawe ukaenda korongoni...
 
MKUU umeuliza maswali ya msingi sana. Najua Heaven on Earth atakuja kujibu hapa, lakini kwa uelewa wangu, ile hali ya kule juu haiwezi kufanana na nchi yeyote kwa sababu moja kubwa. Hali ya mwinuko juu ya usawa wa bahari. Hiyo peke yake, inafanya kiwango cha Oxygen kuwa kidogo na kuleta hali ya kupumua kwa shida. Baridi la kule maji yana mnayobeba mgongoni yanaganda, inafika wakati ni nyuzi hasi 15 na kushuka chini Zaidi. Kuna nchi zinaweza kuwa na hali ya baridi Zaidi kuliko huko Uhuru Peak lakini mwinuko wake hauleti shida kwenye mfumo wa upumuaji. Hiyo ndio tofauti kubwa.

Kumbuka mnafika mahali ambapo mvua ikinyesha haiwahusu, inashughulika na walio chini yenu, nyie mpo juu yake.
Mengine wataongezea wataalam na mainjinia watakapokuja kusoma hii unayotaka kusikia hii hahahahahahaaa.
Ha ha hii ya mvua imenifanya nicheke mkuu, mnakua juu ya mvua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom