MKUU umeuliza maswali ya msingi sana. Najua
Heaven on Earth atakuja kujibu hapa, lakini kwa uelewa wangu, ile hali ya kule juu haiwezi kufanana na nchi yeyote kwa sababu moja kubwa. Hali ya mwinuko juu ya usawa wa bahari. Hiyo peke yake, inafanya kiwango cha Oxygen kuwa kidogo na kuleta hali ya kupumua kwa shida. Baridi la kule maji yana mnayobeba mgongoni yanaganda, inafika wakati ni nyuzi hasi 15 na kushuka chini Zaidi. Kuna nchi zinaweza kuwa na hali ya baridi Zaidi kuliko huko Uhuru Peak lakini mwinuko wake hauleti shida kwenye mfumo wa upumuaji. Hiyo ndio tofauti kubwa.
Kumbuka mnafika mahali ambapo mvua ikinyesha haiwahusu, inashughulika na walio chini yenu, nyie mpo juu yake.
Mengine wataongezea wataalam na mainjinia watakapokuja kusoma hii unayotaka kusikia hii hahahahahahaaa.