Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Ha ahaa ahaaaa ...

Wewe endelea kukojolea sufuria la msosi tu[emoji23][emoji23][emoji23]
Narudia tena kwa jinsi story ilivyo nisisimua wallah nahisi nimesha panda na mie ule mlima hivyo basi sihitaji kwenda kupanda maana najua hata gilman sifiki nitakata upepo nikufe bure hapa tuu kutembea km 3 nahisi kunya akuu mkwende wenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unafanyiwa checkup ya mammbo mengi sana kuona kama utahimili hali ya hewa inayobadilika badilika kadri mnavyosogea juu.
Cha kushangaza, watoto wadogo wa umri kati ya 12-14 wanapanda bila kupata dhoruba kama ilivyo kwa watu wazima,...

Dhambi nazo zinatuongezea mizigo hahahahahahhaha
😂😂😂😂😂😂nimecheka kifala sana,eti dhambi duh.
 
Congratulations kwako Heaven on Earth ujasiri mkubwa sana,despite machache uliyopitia yaliyokuweka katika wakati ngumu remember"we never promised good way,always rough" Niko inspired kitambo sana,mpaka nikapata fursa ya kwenda bure kabisa but majukumu was on my toe,I couldn't take a step to anywhere. But I will,mwakani,naanza kutunza kububu cha MT.KLM. Thank you strong lady
Maseratiiiii
 
sasa inakuaje watoto wapande bila miili yao kusumbua sana? Au sie viungo na miili tumeshaifanyisha sana majukumu na kazi mileage zimeenda sana? Unataka kwenda kupanda?
Nadhani watu wazima tumekwepa mishale mingi😂😂😂watoto bado sana tena 12-14 bado sana hao.Inshallah mwakani nitapanda,nimeanza kutunza kibubu leo.
 
Nakupongeza tena Heaven On Earth, kupitia uzi huu:
Nimefanya mazoezi ya maandalizi na wewe,
Nimepanda na wewe,
Nimeona jamaa aliyefariki akishushwa sambamba na mkewe katika majonzi,
Nimechoka na wewe,
Nimelia na wewe,
Nimekata tamaa na wewe lakini nikajifariji na wewe na nikasonga mbele na wewe,
Nikawaona wavuta bangi wakitupita kwa kasi na badae mmoja wao akathibitisha kutangulia si kufika, akarudishwa duniani,
Kila ulipochoka, akili yangu ilikupa moyo, "twende HOE bila wewe siwezifika kileleni" ulikubali kwa machozi ya uchovu,
Nilisonga na wewe,
Simu yako iliishia chaji, nilihuzunika kwa kuwa hata kama tukisonga pamoja sitaona tena taswira nzuri ya safari yetu,
Nikawasikia ma-guide wakishauriana juu ya kuendelea ama kutoendelea na safari, nikaiona hatari ya kifo mbele yetu, nikasikitika.

Ukungu ulipozidi kule juu kiasi cha kutomuona aliyeko mbele yako, nilipatwa na hofu labda utapotea na kuporomokea upande wa Kenya,
Lakini nilikuwa na wewe,
Picha ya mwisho ambayo barafu imeziba maandishi ya kibao cha Uhuru Peak, ilinitia simanzi kubwa kwa hali ya hewa, nikajaribu kujifananisha na wewe kwa kujidumbukiza kwenye freezer ya butcher, lakini ukasema barafu niiwazayo mimi ni "cha mtoto"...

Hata hivyo, kwa jinsi ulivyotiririka kwa ustadi mkubwa, sikutamani muishie hapo na safari ya kurudi duniani ianze...

Nilitamani safari iendelee, mzuka wa simulizi yako uliniaminisha kuwa baada ya Uhuru Peak, Heaven on Earth would be taking me to the next peak... And probably it could be real Heaven like her name... Can't wait for the next episode.

Pongezi kwa guide wako Fredy kwa kukufikisha kileleni, iwe funzo kwa wanawake wengine wote kuwa, mwanaume kumfikisha mwanamke kileleni haijawai kuwa kazi rahisi, yaitaji uvumilivu na kushikamana.

Hongera sana HOE.
Ngoja nielekee You tube kujazilizia elimu hii tamu.
Salute, kwa summary uko vizuri sana...
Karibu sana Kilimanjaro
 
Mkuu Monk, kinachowasaidia watoto ni wastani wa kiwango cha haemoglobin zao ni nyingi ukilinganisha na wastani kwa watu wazima.

Haemoglobin inahusika sana hasa katika upumuaji uchukuaji wa hewa ya oksijen. Kwa hiyo mtu mwenye kiwango kidogo cha haemoglobin mfano mwenye upungufu wa damu atapata shida sana kule ndio maana HOE amesema lazima ufanyiwe check up, so watoto kiwango chao haemoglobin kinachopatikana katika chembe nyekundu za damu kinawasaidia sana.
sasa inakuaje watoto wapande bila miili yao kusumbua sana? Au sie viungo na miili tumeshaifanyisha sana majukumu na kazi mileage zimeenda sana? Unataka kwenda kupanda?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Natamani kupanda sema mafua na joints za miguu.
Kama baridi la kwetu Magamba Lushoto linanilaza kitandani wiki na mafua juu, je nitaweza kwea Mlima Kilimanjaro?
kiwatengu naweza beba coldril kwa ajili ya kukata ukali wa mafua au siruhusiwi kunywa dawa nikiwa katikati ya safari?
Duuh... Inamaana unamafua kwa mwaka mzima?
Ukiwa na mafua hutaweza kupanda.
 
Sijajua hawa wanaodaiwa kuvunja rekodi ya kupanda mlima Kilimanjaro kwa kutumia saa 5 ni nani anahakiki huo muda?

Kwa uzoefu wangu wa kupanda mlima Kilimanjaro hapa tunadanganyana mchana peupeeee.

hebu jiulize ambaye hujapanda mlima huo,inawezekanaje mtu atumie saa 5 katika safari ambayo tunatumia siku sita hadi saba kuupanda mlima?


Niia ya Marangu ni siku 6


1.Marangu Gate to Mandara Hut,day one

2.Mandara Hut to Horombo Hut,day two,hapa Horombo ukifika unapumzika siku mbili na utaenda eneo la Zebra Rock umbali wa KM3 kwa ajili ya kuzoea hali ya hewa kabla ya siku ya tatu kuanza safari ya Kutoka Horombo Hut kwenda Kibo Hut.

Safari ya kwenda Uhuru inaanza usiku pale Kibo Hut,muda wa kuondoka unategemeana na maelekezo ya waongozaji wageni ambao bila hawa jamaa kwa kweli huwezi hata kufika Horombo,jamaa ni wazuri sana kwa hamasa hata kama unataka kuishia njiani wanauwezo wa kukupeleka Uhuru kutokana na hamasa yao
 
Back
Top Bottom