Nakupongeza tena Heaven On Earth, kupitia uzi huu:
Nimefanya mazoezi ya maandalizi na wewe,
Nimepanda na wewe,
Nimeona jamaa aliyefariki akishushwa sambamba na mkewe katika majonzi,
Nimechoka na wewe,
Nimelia na wewe,
Nimekata tamaa na wewe lakini nikajifariji na wewe na nikasonga mbele na wewe,
Nikawaona wavuta bangi wakitupita kwa kasi na badae mmoja wao akathibitisha kutangulia si kufika, akarudishwa duniani,
Kila ulipochoka, akili yangu ilikupa moyo, "twende HOE bila wewe siwezifika kileleni" ulikubali kwa machozi ya uchovu,
Nilisonga na wewe,
Simu yako iliishia chaji, nilihuzunika kwa kuwa hata kama tukisonga pamoja sitaona tena taswira nzuri ya safari yetu,
Nikawasikia ma-guide wakishauriana juu ya kuendelea ama kutoendelea na safari, nikaiona hatari ya kifo mbele yetu, nikasikitika.
Ukungu ulipozidi kule juu kiasi cha kutomuona aliyeko mbele yako, nilipatwa na hofu labda utapotea na kuporomokea upande wa Kenya,
Lakini nilikuwa na wewe,
Picha ya mwisho ambayo barafu imeziba maandishi ya kibao cha Uhuru Peak, ilinitia simanzi kubwa kwa hali ya hewa, nikajaribu kujifananisha na wewe kwa kujidumbukiza kwenye freezer ya butcher, lakini ukasema barafu niiwazayo mimi ni "cha mtoto"...
Hata hivyo, kwa jinsi ulivyotiririka kwa ustadi mkubwa, sikutamani muishie hapo na safari ya kurudi duniani ianze...
Nilitamani safari iendelee, mzuka wa simulizi yako uliniaminisha kuwa baada ya Uhuru Peak, Heaven on Earth would be taking me to the next peak... And probably it could be real Heaven like her name... Can't wait for the next episode.
Pongezi kwa guide wako Fredy kwa kukufikisha kileleni, iwe funzo kwa wanawake wengine wote kuwa, mwanaume kumfikisha mwanamke kileleni haijawai kuwa kazi rahisi, yaitaji uvumilivu na kushikamana.
Hongera sana HOE.
Ngoja nielekee You tube kujazilizia elimu hii tamu.