Umslopagaas
Member
- Nov 13, 2016
- 47
- 112
Sijajua hawa wanaodaiwa kuvunja rekodi ya kupanda mlima Kilimanjaro kwa kutumia saa 5 ni nani anahakiki huo muda?
Kwa uzoefu wangu wa kupanda mlima Kilimanjaro hapa tunadanganyana mchana peupeeee.
hebu jiulize ambaye hujapanda mlima huo,inawezekanaje mtu atumie saa 5 katika safari ambayo tunatumia siku sita hadi saba kuupanda mlima?
Niia ya Marangu ni siku 6
1.Marangu Gate to Mandara Hut,day one
2.Mandara Hut to Horombo Hut,day two,hapa Horombo ukifika unapumzika siku mbili na utaenda eneo la Zebra Rock umbali wa KM3 kwa ajili ya kuzoea hali ya hewa kabla ya siku ya tatu kuanza safari ya Kutoka Horombo Hut kwenda Kibo Hut.
Safari ya kwenda Uhuru inaanza usiku pale Kibo Hut,muda wa kuondoka unategemeana na maelekezo ya waongozaji wageni ambao bila hawa jamaa kwa kweli huwezi hata kufika Horombo,jamaa ni wazuri sana kwa hamasa hata kama unataka kuishia njiani wanauwezo wa kukupeleka Uhuru kutokana na hamasa yao
Google Mount Kilimanjaro record climbing