Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Sijajua hawa wanaodaiwa kuvunja rekodi ya kupanda mlima Kilimanjaro kwa kutumia saa 5 ni nani anahakiki huo muda?

Kwa uzoefu wangu wa kupanda mlima Kilimanjaro hapa tunadanganyana mchana peupeeee.

hebu jiulize ambaye hujapanda mlima huo,inawezekanaje mtu atumie saa 5 katika safari ambayo tunatumia siku sita hadi saba kuupanda mlima?

Niia ya Marangu ni siku 6

1.Marangu Gate to Mandara Hut,day one

2.Mandara Hut to Horombo Hut,day two,hapa Horombo ukifika unapumzika siku mbili na utaenda eneo la Zebra Rock umbali wa KM3 kwa ajili ya kuzoea hali ya hewa kabla ya siku ya tatu kuanza safari ya Kutoka Horombo Hut kwenda Kibo Hut.

Safari ya kwenda Uhuru inaanza usiku pale Kibo Hut,muda wa kuondoka unategemeana na maelekezo ya waongozaji wageni ambao bila hawa jamaa kwa kweli huwezi hata kufika Horombo,jamaa ni wazuri sana kwa hamasa hata kama unataka kuishia njiani wanauwezo wa kukupeleka Uhuru kutokana na hamasa yao

Google Mount Kilimanjaro record climbing
 
Mkuu kucha za vidole vya miguu ziling'ookaje? ulikuwa umevaa kandambili au? manake kabla ya kupanda mlima Kilimanjaro ni lazima ufanye preparation ya vitu vifuatavyo:
1.Viatu vigumu (Boots) lakini viwe vyepesi ili kukusaidia kutembea bila kuchoka.
2.Soksi pair 4 ndefu safi na nzito.
3.Mycotta powder.
4 Gloves safi zenye sufi ndani.
5.Jacket au pullover zito.
6.Boshori lile kofia la sweta linalofunika kichwa na kuacha sehemu ya macho tu.
7.Miwani nyeusi kupunguza mng'ao wa theluji.
7.Climbing stick
8.Kibuyu au chupa ya maji.
9.Back pack kwa ajili ya kuhifadhi vitu vidogo vidogo kama glucose,biscuits,juice n.k.
Hayo ndio mahitajio ya msingi unayotakiwa kuconsider kabla ya kuanza safari ya kupanda mlima.

Sent using Jamii Forums mobile app
Swali langu huko Mlimani hakuna wanyama wakali au nyoka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salute, kwa summary uko vizuri sana...
Karibu sana Kilimanjaro

Asante mkuu, sio mgeni sana hapo ila mara yangu ya kwanza kuuona mlima huo kwa kutokea Moshi mjini nilishangaa sana kwa nini dude hilo liliitwa "mlima" kama ilivyo kwa milima mingine tuionayo sehemu nyinginezo za nchi,lile ni dude lisiloelezeka kirahisi kwa mtu ambaye hajawahi kuliona, ni zaidi ya mlima. Na kwa uzi huu, lazima niupande mwaka huu.
 
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
Big up. Karibu sana
 
Wakuu naomba maelezo kidogo ,wadau wanasema kipindi kizuri kupanda huo Mlima ni kuanzia Julai .
Hiyo Julai huku kwetu bonde la Kilombero ndiyo kuna baridi kali usiku.
Sasa huko kwenye uwanda wa juu si unalifuata hukohuko ?

Kiwatengu na Wazoefu wengine , ni kwanini hicho kipindi Julai hadi Desemba ni kizuri?
 
Asante mkuu, sio mgeni sana hapo ila mara yangu ya kwanza kuuona mlima huo kwa kutokea Moshi mjini nilishangaa sana kwa nini dude hilo liliitwa "mlima" kama ilivyo kwa milima mingine tuionayo sehemu nyinginezo za nchi,lile ni dude lisiloelezeka kirahisi kwa mtu ambaye hajawahi kuliona, ni zaidi ya mlima. Na kwa uzi huu, lazima niupande mwaka huu.

[emoji23][emoji23][emoji23]kwa wageni ile kofia inazingua sana,huoni mlima chini umeanzia wapi bali unaona tu uko juu ya mawingu,na kofia nyeupe juu zaidi.

Unaweza dhani unaelea juu.
 
Back
Top Bottom