Simulizi ya ujasusi: Do not shout (Usipige kelele)

Simulizi ya ujasusi: Do not shout (Usipige kelele)

DO NOT SHOUT
(usipige kelele)
Season 2
Sehemu ya.........01
Mtunzi Saul David
WhatsApp: 0756862047


ILIPOISHIA
Mazungumzo haya yaliyoibua maswali mengi kwenye kichwa cha Yusto aliyekuwa mlangoni anawasikiliza, akawa haelewi ni nini kinaendelea.
"Caren, kwani wewe ni nani?"
Yusto alijiuliza swali ambalo hakuwa na majibu yake, lakini tayari alishaanza kuhisi kitu.
JE, NINI KITAFUATA.?
SASA ENDELEA...
Mazungumzo ya John na mama yake madam Jane yalionekana kutokuwa na manufaa yoyote kwa john, hakuwa amepata kile alichokuwa akikitafuta lakini tayari alihisi kuwa kuna jambo mama yake analificha. Alihisi kuna Siri nzito iliyokuwa imejificha kati ya mama yake na mama yake Yusto, akatamani kujua. Baada ya kutoka ndani ya ofisi ya mama yake John alipiga tena simu kwa kijana wake wa kazi Abdullah.

"Vipi anaendeleaje huyo mwenzio aliyepigwa risasi"
"Kwa sasa yupo vizuri bosi tayari tumesha muhudumia"
" Okay, sasa sikia, fuatilia hakikisha Kama kweli Yusto na mama yake wamekufa kwenye ule mripuko Kisha utanipa taarifa mimi narudi chuoni kupumzika" Alisema John
[emoji294][emoji294][emoji294]
Muda mfupi tu baada ya John kutoka ndani ya ofisi ya mama yake mara aliingia mtu mwingine ambaye ndiye aliekuwa amepewa kazi na madam Jane ya kufuatilia taarifa za yule mwanamke kichaa Zubeba.

"Enhe nambie imekuwaje" madam Jane alianzisha mazungumzo baada ya kusalimiana na yule mtu.

"Bosi nimemfuatia Zubeba yupo na alikua anashinda kwenye lile jalala jirani na soko la matunda Huwe.
lakini kuna taarifa nimepata kuwa kuna watu walifika wakamkamata kwa nguvu wakamuingiza ndani ya gari na kuondoka nae leo, hatujajua ni akina nani wala walipompeleka bado tunaendelea kufuatilia"

Hizi zilikua ni taarifa ambazo kwa kiasi zilimfanya madam Jane kuamini kile alichokuwa akihisi ni sahihi.

" Sitaki John ajue chochote kabla sijalipa kisasi changu kwa baba yake, naomba mtafute Zubeda popote alipo na ikibidi muueni"

"Lakini bosi yule mwanamke si ni kichaa tu, wasiwasi wako nini?"
"Vichaa wengi huwa hawapotezi kumbukumbu za mambo muhimu yaliyotokea kwenye maisha yao, nilifanya makosa kumuacha hai, tayari John ameanza kuulizia taarifa zake lolote linaweza kutokea, alafu tangu lini ukaniuliza maswali nikikupa kazi?" Madam Jane aliuliza kwa ukali kidogo

"Samahani bosi, kwa hiyo nitumie njia gani kumuua, au niwatumie vijana wako"

"Hili jambo linatakiwa kwenda kimya kimya sana kwa sababu nahisi John anaweza akawa anahusika au anafuatilia pia, nitafutie kijana mmoja makini mwenyewe uwezo mkubwa kule kambini afanye hii kazi" alisema madam Jane.

"Aah sawa bosi yupo binti mmoja makini sana anaweza kuifanya hii kazi vizuri lakini tayari yupo kwenye ile misheni ya kuchafua sifa ya chuo cha mark moon"

"Ni nani huyo?"
"Diana kwa Sasa tunamwita CAREN"

"Ooh Caren kale ka binti kazuri tuliko kachukua Burundi na mama yake tulimpeleka India kutibiwa bila shaka"
"Eeh huyo huyo, Sasa hivi yule mwanamke ni mashine ya kazi yuko vizuri sana atatusaidia"
"Lakini Mimi siamini wanawake, hebu tafuta mwingine"
"Bosi mimi pia huwa siamini wanawake lakini Caren ni mtu na nusu, anaweza sana kazi yule binti"

"Okay! muite basi Sasa hivi nionane naye"
Alisema madam Jane.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Yusto akiwa bado yuko pale mlangoni aliendelea kusikiliza mazungumzo kati ya Revocatus na yule msichana. Baada ya kumaliza mazungumzo hayo Revo alielekea moja moja kwenye chumba alichokuwepo Yusto.
Yusto baada ya kuona hivyo alikimbia na kwenda kujitupa kitandani akatulia kimya Kama vile bado hajaamka. Revocatus aliingia akamtazama kwa muda, akagundua kuwa drip ya maji ilikuwa imechomolewa, akatabasamu.

"Naona umeamka, haya inuka twende ukamuone mama yako" alisema Revo kisha akaanza kutembea kuondoka.

Yusto aliendelea kujituliza kimya lakini mwisho akafumbua macho akamtazama Revocatus ambaye tayari alishafika mlangoni, akageuka nyuma.

"oy twende basi" alisema Revo
Taratibu yusto aliinuka pale kitandani kisha akaanza kumfuata Revo huku mara kadhaa akimuangalia kwa macho ya kuibia ibia. Walianza kutembea wakiwa wamefuatana wakikatisha vyumba kadhaa ndani ya jengo hilo lililojengwa kwa muundo wa ajabu sana.

"Najua unamaswali mengi sana unatamani kuniuliza, usijali Caren atakueleza kila kitu. Muhimu kujua kwa sasa ni kwamba Mimi sio mume wa Caren kama unavyozani wala Caren hana mtoto Kama ulivyoambiwa na Sophia, kulikuwa na sababu ya sisi kufanya vile" alisema Revo kiasi cha kumfanya Yusto amtazame sana.

Mwisho waliingia ndani ya chumba kimoja kilichokuwa na vitanda viwili ndani yake, kimoja upande wa kushoto na kingine kulia.
Upande mmoja alilala Caren na upande mwingine alilala Zubeba mama mlezi wa Yusto.
Hali ya mama yake Yusto ndio ilionekana kuwa mbaya zaidi, alikuwa amewekewa mashine maalum inayomsaidia kupumua. Yusto na Revo walifika na kusimama katikati yao.

"Mama....Caren" Yusto aliita akionyesha kuwa na wasiwasi zaidi hasa na mama yake aliekuwa anapumulia mashine.

"Usijali wote wawili watapona" alisema Revo kisha akamgeukia Yusto na kumshika begani.

"Sikiliza Yusto, Caren amejitoa sana kwa ajili yako ameweka rehani kila kitu chake kwanzia kazi hadi ndugu zake kwa ajili mapenzi yake kwako, anafanya hivyo kwa sababu anakupenda sana na kukuamini. Kama nilivyo kwambia siwezi kusema kila kitu lakini naomba nikupe onyo, ukifanya jambo lolote la kipuuzi ukahatarisha usalama wa Caren, nitakupasua mwenyewe kwa mikono yangu"
Alisema Revocatus Kisha akageuka na kuondoka, akamuacha Yusto mle ndani akiwa amesimama na kutulia kimya akiyatafakari maelezo ya Revo yaliyoonekana kuwa na maana zaidi ya moja. Akawa anawatazama Caren na mama yake kwa zamu.
Hawa walikuwa ni wanawake muhimu sana kwenye maisha yake aliwapenda pengine kuliko kitu kingine chochote.

Yusto aliendelea kusimama akiyatafakari maelezo ya Revo hali akitamani kujua zaidi ni kwa nini Caren anafanya yote yale, ni vitu gani alivyoviweka rehani kwa ajili yake? kwa nini alidanganya akijifanya mke wa mtu na mama wa mtoto? ni nini kinaendelea? Hivi ni baadhi kati ya vitu vingi ambavyo Yusto alitamani kuvijua kutoka kwa Caren.

Taratibu alisogea na kupiga magoti pembeni ya kitanda alicholala Caren.
Akawa anaitazama sura nzuri ya mwanamke huyo ambae alikuwa ni mrembo haswa. Alisahau kabisa kama walikuwa kwenye ugomvi mkubwa masaa kadhaa yaliyopita.

" Caren, siwezi kujizuia kuacha kukupenda, moyo wangu unagoma kabisa kuwa mbali na wewe, siwezi, sijui ukiamka utaniambia nini mama, naogopa. Lakini sijali hata kukiwa na sababu mia moja zakukuacha nitatafuta sababu moja tu ya kuendelea kuwa na wewe Caren wangu, nakupenda, nakupenda sana Caren"
Yusto alikuwa akiongea kwa hisia kali huku akiwa ameung'ang'ania mkono wa Caren. Mapigo yake ya moyo yalikuwa yakienda mbio, machozi yalikuwa jirani kabisa kumtoka akajikuta anashindwa kuhimili, taratibu akasimama na kuanza kuondoka.
"Yustoo"
Akiwa amefika mlango ni kama alisikia sauti imemuita, akasimama ghafula huku akijiuliza amesikia vibaya au ni kweli ameitwa.

Taratibu akageuka,
Yusto hakuamini pale alipomuona Caren akiwa amefumbua macho yake anamtazama.
Caren alikuwa amerejewa na fahamu zake tangu mda mrefu lakini aliyafumba macho yake Kama vile bado hajazinduka, maneno yote aliyozungumza Yusto aliyasikia, akajikuta anaumia na kupata faraja kwa wakati mmoja.

"Ca.. Caren" Yusto aliita,
Caren akiwa na sura ya huzuni alinyoosha mikono yake akimtaka Yusto aje kumkumbatia.

JE, NINI KITAFUTA
Nini hatima ya wawili hawa wanaopendana ?
Vipi kama madam jane atampa Caren kazi ya kumuua mama mlezi wa Yusto?
Nini kitatokea?
Harakati za John zitaishia wapi?

ENDELEA KUFUATILIA SIMULIZI HII YA KUSISIMUA.

Season 2 na season 3 ya mwisho zote zipo tayari njoo WhatsApp
0756862047
 
𝗗𝗢 𝗡𝗢𝗧 𝗦𝗛𝗢𝗨𝗧
(𝘂𝘀𝗶𝗽𝗶𝗴𝗲 𝗸𝗲𝗹𝗲𝗹𝗲)
𝗦𝗲𝗮𝘀𝗼𝗻 2
Sehemu...........2
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
Caren alikuwa amerejewa na fahamu zake tangu mda mrefu lakini aliyafumba macho yake Kama vile bado hajazinduka, maneno yote aliyozungumza Yusto aliyasikia, akajikuta anaumia na kupata faraja kwa wakati mmoja.

"Ca.. Caren" Yusto aliita,
huku Caren nae akiwa na sura ya huzuni alinyoosha mikono yake akimtaka Yusto aje kumkumbatia.

JE, NINI KITAFUTA?

𝘀𝗮𝘀𝗮 𝗲𝗻𝗱𝗲𝗹𝗲𝗮...
Yusto alisogea akamkumbatia Caren kwa nguvu. Kila mmoja alionekana kummiss mwenzake kwa kiasi kikubwa baada ya kupita kwenye kipindi kigumu, tangu kule Arena hoteli, kuumia kwa Sophia na kutekwa kwa mama mlezi wa Yusto.
Huu ulikuwa ni mfurulizo wa matukio uliowafanya wawili hao kuwa katika wakati mgumu mno.
****

Zilikuwa zimepita dakika kadhaa mpaka sasa, kwa kiasi Caren alionekana kutulia hakuwa akilia tena.

"Huyu ni mama yako mzazi" hatimae Caren alifungua kinywa kuzungumza baada ya ukimya wa muda mrefu.
"Hapana, lakini ndie mama pekee nilienae hapa duniani, yeye ndio alienilie tangu nikiwa mdogo kabisa, bahati mbaya aliugua kichaa nikiwa bado mgodo na hajawahi nambie wazazi wangu harisi"
"Kwa hiyo hujui Kama wako hai au wamekufa"

"Imani yangu inaniambia wameshakufa, ni mda mrefu sana umepita Kama wangekuwepo wangeshajitoka"

"Polee Yusto"

"Asante, nilishapona mda Caren" alisema Yusto huku akigeuka na kumtazama Caren usoni kisha akageuka kumtazama mama yake ambae bado alikuwa hajarejesha fahamu zake.

"Usijali atakuwa sawa, ukiwa hapa atapata huduma zote muhimu"

Alisema Caren kauli iliyomfanya Yusto ageuke tena na kumtazama, Kisha akamuuliza swali.
"Kwa nini ulikuja Caren, ulijuaje Mimi niko kule bandari ya uhuru?"

Caren alitulia kwa muda kisha akafungua droo ya kitanda na kutoa simu kubwa ya Yusto.

"Niliiona video uliotumiwa na John alipomteka mama yako kwenye hii simu yako, mimi ndio chanzo so nilikuwa na kila sababu ya kuja kukusaidia, namjua John akili yake yule ni mwenda wazimu ona sasa alitaka kuwauwa wewe na mama" alieleza Caren huku akimkabidhi Yusto simu yake.

"Caren"
"Beeh"
"Tell me everything Caren, nini kinaendelea nahitaji kujua kila kitu please, wewe ni nani hasa"

Kimya kilitawala Caren akawa anawaza wapi pa kuanzia.

"Yusto"
"Yes mama"
"Kwanza nataka ujue kwamba nakupenda, nakupenda sio kidogo, sana tu"
"Yes, hilo nalijua hata kabla hujaniambia, lakini kwa nini haya yote wewe na huyu jamaa Revocatus mkoje, hapa ni wapi, mnafanya kazi gani"

"Yusto, Nitakwambia kila kitu, hii ni siri ambayo sikutamani uijue lakini imebidi nikwambie, nakuamini kwa sababu tayari umekua sehemu ya maisha yangu.."

Caren alitulia kwa muda Kisha akaendelea...
"...Mimi na hawa wenzangu unaowaona hapa tuko pamojaa tangu tukiwa wadogo, sisi ni maagent wa siri ambao tuko chini ya tajiri mmoja ambae anatumiwa na serikali pale inaposhindwa jambo fulani basi huwa wanamwambia bosi wetu na bosi wetu anatutumia sisi kufanya upelelezi au kufanya tukio fulani"
Caren alieleza kwa ufupi lakini ulikuwa ni ufafanuzi ulioshiba.
***
Hivi ndivyo Caren na wenzake walivyokuwa wanajua kuwa kazi zote wanazopewa na Madam Jane zilikuwa ni chini ya serikali ikiwemo ile ya kumuangusha kiuchumi tajiri mark moon. Madam Jane aliwadanganya kuwa ni mpango maalum na wa siri wa serikali lakini kumbe haikuwa hivyo ilikuwa ni chuki yake binafsi na kisasi kizito alichonacho dhidi ya mark Moon.
***
"Hiyo ndio kazi ulioichagua Caren"
Aliuliza Yusto.

"Ndio ni kazi ambayo naipenda pia, mbali na hilo pia hawa watu wamenisaidia sana mimi na familia yangu bila wao sidhani kama hata mimi na wewe tungekutana leo, nawaheshimu sana"

Kimya kilitawala kwa muda huku Yusto akijaribu kuyatafakari maelezo ya Caren.

" Kwa hiyo pale chuoni wewe unafanya nini, upo kikazi pia?" Yusto aliuliza swali ambalo jibu lake likikuwa ni kutangaza vita rasmi kati yake na Caren kwani Caren alikua ni agent wa Siri wa madam Jane na Yusto alikuwa ni mlizi wa siri katika chuo cha mark moon.

Kabla Caren hajazungumza lolote mara ghafula mlango ukafunguliwa akaingia Revocatus hali akionekana mwenye wasiwasi, Caren na Yusto waliligundua hilo.

"Kuna nini Revo" aliuliza Caren
"Dharula, kuna simu yako ya dharula Caren nashukuru umeamka"
Alisema Revocatus.

Caren alikurupuka pale kitandani akasimama, kisha akatoka haraka haraka wakiongozana na Revo, wala hakumuaga Yusto.

Yusto alibaki katika hali ya mshangao asielewe kinachoendelea, tayari taarifa za Caren kuwa agent wa siri zilikuwa zinamchanganya bado alihitaji maelezo zaidi lakini ndio hivyo Caren anakuwa bize ghafula.
Alibaki mle chumbani akiendelea kumtazama mama yake aliekuwa bado kitandani hajitambui.
****

"Vipi umemwambia Yusto kila kitu"
"Ee ndiyo japo sio kwa upana wake"
"Kwa hiyo anajua kuwa hata pale chuoni upo kikazi"
"Hebu tusikilize kwanza simu Revo hifadhi maswali yako kwanza utaniuliza baadae"

Haya yalikuwa ni maongezi kati ya Caren na Revocatus ambao baadae walifika kwenye Kona moja ndani ya nyumba hiyo kulipokuwa na simu ya mezani.
Revocatus aliinyanyua ile simu akabonyeza vitufe kadhaa na kuiweka sikioni.

"Ndio Revocatus nazungumza..sawa...sawa"
Alizungumza Revo kisha akageuka na kumtazama Caren, akampa simu.

Caren aliipokea kisha akaiweka sikioni.

"Hallo Diana naongea...ndio....sawa"
Caren aliongea kwa sekunde chache Kisha simu ikakatwa.

"Vipi" aliuliza Revo kwa bashasha.
"Ni oda" alijibu Caren huku akionekana kutafakari jambo.

"Oda, oda gani tena si tuko na kazi ya mark Moon kwa Sasa"
"Ndiyo lakini kasema nisitishe kwanza, hii ni VIP oda"
"VIP?"
"Ndiyo ni VIP"
"Kwa hiyo unakwenda kuonana na madam Jane"
"Ndiyo sijajua hata ni kazi gani, naogopa"

"Noo usijali unajua hadi bosi mkubwa amekwita basi umeaminika sana hongera Caren"
"Asante baadae basi"
"Haya powa... lakini vipi"
"Vipi nini"
"Yusto"
"Ooh mungu angu, nimesahau kabisa, atarudi chuoni mama ake abaki hapa please kuwa makini hakikisha anakuwa salama"
"Sawa".
*****

DAKIKA 45 BAADAE...
Gari aina ya Noah lilipaki nje ya chuo cha mark moon, Yusto aliekuwa amefungwa kitambaa cheusi usoni tangu safari inaanza aliambiwa akifungue, akafanya hivyo.

"Basi masomo mema Yusto,tutakuwa tunawasiliana usijali kuhusu mama yako atakuwa salama" alisema Revocatus ambae ndie alikuwa dereva wa gari hilo.

"Asante, nashukuru" alisema Yusto Kisha akashuka kwenye gari.
Revocatus aliondoka na gari yake taratibu huku Yusto akimsindikiza kwa macho, hakuelewa ni wapi wametoka wala lile jengo walilokuwepo liko upande gani.

ITAENDELEA...
 
𝗕𝗔𝗞𝗜 𝗡𝗔 𝗠𝗜𝗠𝗜
(Stay with me)
𝗦𝗲𝗮𝘀𝗼𝗻 2

Sehemu ya..........3
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA ....
Revocatus aliondoka na gari yake taratibu huku Yusto akimsindikiza kwa macho, hakuelewa ni wapi wametoka wala lile jengo walilokuwepo liko upande gani.

SASA ENDELEA...
Yusto hakujali sana, moyoni alikua na amani kabisa akiamini mama yake yuko kwenye mikono salama, alimwani sana Caren pasipo kujua kuwa Caren ameenda kuonana na madam Jane ambaye pengine angempa kazi ambayo itahatarisha usalama wa mama yake.

Yusto alielekea moja kwa moja chumbani kwake akaoga na kubadili nguo zake haraka kisha akatoka kwenda hospitali kumuona Sophia rafiki yake kipenzi alielazwa baada ya kujeruhiwa vikali na Caren.
Hakuwa na taarifa zozote kuhusu hali ya Sophia kubadilika ghafula akaongezewa damu na Caren Kisha kufanyiwa upasuaji wa dharula, Yusto hakuwa na habari hiyo kabisa.

Wakati anatoka chumbani kwake mara anakutana na rafiki yake Frank, wote wakiwa ni walinzi wa Siri chuoni hapo.

"Wewe Yusto, mungu wangu umerudi, enhe ulienda wapi mwanangu?" Frank aliuliza maswali mfurulizo.

"Nilikua nje mara moja, vipi kuna usalama?" Yusto alijibu kwa kifupi, hakutaka kuweka wazi kile kilichotokea.

"Unahabari kuwa Sophia kafanyiwa oparesheni, oparesheni kubwa ya kichwa, aliumia sana, damu ilivujia kwenye ubongo"
Alisema Frank kauli iliyomfanya Yusto apatwe na mshituko akatoe macho kwa mshangao.
[emoji294][emoji294][emoji294]

HOSPITALI...
John alikua amekaa kitandani pembeni ya Sophia huku wakionekana kuwa kwenye mazungumzo. Yalikua yamepita masaa kadhaa tangu Sophia alipofanyiwa upasuaji na sasa alikua amezinduka japo hali yake haikua imeimarika sana.
Baada ya John kutoka kuonana na mama yake alipata habari za kuumia kwa Sophia hivyo alienda moja kwa moja kumuona mpenzi wake huyo ambaye hawakuwa kwenye maelewano mazuri wakati huo.

"Nimesika tena unamtaka Caren?" aliuliza Sophia huku akimtazama John kwa macho ya dharau
"Unamaana gani kuuliza swali kama hilo mda huu, subiri upone kwanza" John alijibu.
"Siku zote huwa hautaki kuulizwa maswali kama hayo kwa sababu unazijua tabia zako chafu. Yusto na Caren wanaonekana kupendana sana laiti ungejua kilichotokea kati yao Jana usinge amini kuwa hawa watu bado wataendelea kuwa pamoja"

"Kwa hiyo umekata tamaa, humpendi tena Yusto wako?" John aliuliza kwa kejeli.
"Siwezi kuacha kumpenda, lakini itafika wakati nitazoea tu, mbona nilikubali kuwa na wewe na angalia bado nampenda"
"Kwa hiyo ukanifanya mimi kipozeo si ndio?"
"Hebu kwenda, mwanaume malaya Kama nini, si bora hata ungekuwa hicho kipozeo" Alisema Sophia lakini wakati huo John alionekana yuko mbali ki mawazo.

Aliwaza nini kitatokea Kama Yusto na mama yake wamekufa kwenye ule mripuko kule bandarini. Kuna wakati alitamani iwe hivyo kwani sasa angepata nafasi ya kuwa na Caren pasipo pingamizi lolote, alifanya yote hayo kwa sababu tu ya kumtaka Caren kimapenzi.

Wakati akiwaza hayo mara simu yake iliita, alipoitazama namba ya mpigaji alikuwa ni kijana wake Abdullah aliyemtuma kwenda kuhakiki kama Yusto na mama yake wamekufa.

John aliinuka pale kitandani akamuacha Sophia na kutoka nje akasimama kwenye korido moja ndefu kisha akapokea simu ile.

"Ee Abdullah nipe ripoti"
"Bosi hawa watu watakua waligawanyika vipande vipande kutokana na ule mripuko "
"Kwa nini? wewe umejuaje?"

"Niko hapa eneo la tukio bosi, naangalia polisi bado wako hapa, wanakusanya tu mabaki ya miili za hao watu"

"Lakini si ulisema kuna mwenzenu mmoja alibaki hapo vipi yakawa ndio mabaki yake"
"Hapana bosi, eneo tulilomuacha ni tofauti kabisa na eneo wanapokusanya haya mabaki ya binadamu"

"Kwa hiyo unataka kusema Yusto na mama yake wamekufa?"
"Ndiyo bosi bila Shaka"
Alisema Abdullah,,,,
"Hallo...hallo....hallo bosi ...haloo"
Abdullah alikua akiita upande wa pili lakini kukawa kimya ghafula, John alikua hajibu chochote.

Upande wa pili John alionekana akiwa ameduwaa na simu yake ikiwa bado sikioni, alichokua akiambiwa kwenye simu kilikua ni tofauti kabisa na kile alichokuwa anakiona wakati huo.
Yusto alikuwa amesimama mbele yake umbali wa hatua kadhaa kutoka alipokuwa.
John hakua ametegemea kumuona yusto wakati huo wala Yusto naye hakuwa ametegemea kumkuta John hospitalini hapo.
Walisimama kwa sekunde kadhaa huku kila mmoja akimtazama mwenzake kwa macho makali.
Yusto alikuwa na hasira isiyo na mfano, mtu aliyesababisha yeye na mama yake kunusurika kufa Sasa alikua amesimama mbele yake.
John naye akiwa amehakikishiwa kuwa adui yake amekufa lakini anashangaa kumuona amesimama mbele yake tena akionekana mwenye afya tele.
Ndugu hawa wawili mtu na kaka yake walitazamana kwa macho makali huku kila mmoja akidhihirisha chuki kubwa aliyokuwanayo dhidi ya mwenzake
[emoji294][emoji294][emoji294]
Upande wa pili Caren aliwasili Kwenye jengo kubwa la kifahari lililokuwa limejegwa katikati ya jiji. Jengo ambalo ndipo ilikuwepo ofisi ya bosi wake, mama mwenye pesa zake yaani Madam Jane.

Caren alipokelewa na kijana mmoja ambaye alikwisha andaliwa tayari, akamuongoza moja kwa moja hadi kwenye mlango wa kuingia katikati ofisi kuu ya madam Jane.

Alibisha hodi kisha mlango ukafunguliwa na mwanaume mmoja ambae yeye alikua anatoka, sura ya mwanaume huyo haikuwa ngeni machoni kwa Caren mara kadhaa alikua akimuona pindi alipokua kambini na wenzake.

"Karibu Diana karibu, ingia bosi yupo ndani anakusubiri" alisema yule mtu kisha akaondoka zake.

Caren alitikisa kichwa kukubali kisha akanyonga kitasa, akapiga hatua kuingia ndani.

Naam uso kwa uso Caren akagonganisha macho na Madam Jane ambae ki uharisia alipaswa kumuheshimu kama mama mkwe kwani mama huyo ndiye alikua mama mzazi wa Yusto lakini kwa bahati mbaya hakuna aliyelijua hilo si Caren wala si madam Jane mwenyewe.

"Ni kitambo hatujaonana Diana a.k.a Caren, karibu uketi"alisema Madam Jane huku akitabasamu, akamuonyesha Caren eneo la kukaa.
Ilikuwa ni nadra sana kumuona madam Jane, Caren hakuwa anakumbuka alimuona wapi na lini kwa mara ya mwisho, ni watu wachache sana ambao ndio walikuwa na uwezo wa kukutana naye mara kwa mara.
Hata mwanae John kuna wakati alikua akipata wakati mgumu kumuona mama yake, kuna kipindi alimaliza hata wiki moja hawajaonana.

Caren aliinamisha kichwa chake chini kwa heshima kubwa kisha akasogea mahali alipoelekezwa akakaa.

Akiwa bado ameinamisha kichwa chake chini, alitupa macho mezani na hapo ndipo akaiona picha ya mama mlezi wa Yusto aliyemuacha kule kambi ndogo akiwa amepoteza fahamu.

Moya wa Caren ulipiga
Paaa!!
Hakujua ni kwa nini picha ya mama mlezi wa Yusto iko pale, imefikaje na kwa sababu zipi?

"Vipi unamjua huyo?" Madam Jane aliuliza baada ya kuona ni Kama Caren ameshtuka.

Caren alitulia kwa sekunde kadhaa akiwa hajui ajibu nini, akijibu ndiyo huenda kukawa na maswali mengi zaidi ya hapo. Akisema hapana pengine Madam Jane anajua kila kitu kuhusu kuwepo kwa yule mama kambini kwao na ndio maana amemuita kumuliza.
Aliendelea kubaki katika hali ya utata asijue ajibu nini.

"Careen"
"Ndio bosi"
"Are you there?"(uko hapa)
" Ndio bosi"
"Ooh!! come on, usiwe muoga basi, unajua kwanzia leo Mimi na wewe tutakuwa marafiki, nimekuita hapa kwa kazi maalum, Leo utazijua Siri zangu nyingi ambazo ni wachache sana wanazijua, kuanzia Leo utakuwa mtu wangu wa karibu kwa hiyo usiniogope sawa" alisema madam Jane.
[emoji294][emoji294][emoji294]

YUSTO NA JOHN HOSPITALI...
Ndugu hawa wawili mtu na kaka yake walitazamana kwa macho makali huku kila mmoja akidhihirisha chuki kubwa aliyokuwanayo dhidi ya mwenzake. Yusto akiwa bado amesimama mlangoni mara akapita nesi mmoja akiwa anasukuma toroli la vifaa vya kutolea huduma kwa wagonjwa.

"Habari kaka usisimame mlangoni mapokezi pale eleza shida yako watakusaidia" alisema yule nesi Kisha akaendelea na safari yake akawa anaelekea upande ule alipo simama John.

Yusto hakujibu chochote badala yake akawa anatazama vifaa vilivyomo kwenye toroli la yule nesi.

Akiwa bado na hasira Yusto alikimbia kwa kasi hadi pale alipokuwepo yule nesi, akainama na kukwapua mkasi kutoka kwenye lile toroli, Kisha akaendelea kukimbia kumuelekea John.
"Wee Kaka...mungu wangu, unafanya nini!!" Yule nesi alipiga kelele ni Kama alijua kuwa Yusto anataka kufanya jambo la hatari.

Ilikuwa hivyo kwa John pia alielewa ni namna gani Yusto alikua na hasira dhidi yake, akawa amejiweka tayari kukabiliana naye.
Kufumba na kufumbua tayari Yusto alikua amefika na kusimama mbele yake, akainua mkono wake wa kulia juu ule alioshikilia mkasi tayari kumchoma John shingoni.
Lakini John alikua ameiona hatari hiyo naye akainua mkono wake akamzuia kwa nguvu.
Yusto alikua amedhamilia haswaa kufanya kile alichotaka kufanya, baada ya kuona John amekinga mkono wake kumzuia, aliuachia ule mkasi ukawa kama unadondoka chini lakini ulipofika usawa Fulani mara akaudaka na mkono wake wa kushoto kisha bila kupepesa macho akauzamisha kwa nguvu kwenye tumbo la John.

"Mmmmnnh" John aliguna kwa maumivu makali aliyoyapata.

" Mamaaaaa...." Yule nesi alipiga kelele kwa Mara ya pili , kelele zilizosikika karibu kila kona ya hospitali hiyo.

"Vipi unajisikiaje, inauma eeeh, hivyo ndivyo nilivyoumia baada ya wewe kumgusa mama yangu, hili ni onyo tu usimguse wala kukaribia tena mama yangu, nitakuua" alisema Yusto huku akimtazama John kwa macho makali kisha akauchomoa ule mkasi na kuuweka mfukoni, akaondoka zake.
Sekunde chache tayari watu walifika eneo lile wakitaka kujua kinachoendelea.

"Vipi kuna nini?"
"We kijana shida nini?"
"Ooh mungu wangu damu?"
"Tuone nini shida?"
Yalikua ni maswali kutoka kwa watu tofauti tofauti waliofika eneo hilo.

Yule nesi alikua amekaa chini akitetemeka kwa hofu hakuwa na uwezo wa kueleza chochote kwa wakati ule.

"Ni ajali tu naomba msaada" John alidanganya huku akiwa amekandamiza mkono wake kwenye eneo la jeraha kuzuia damu isiendelee kutoka.

Mwisho walifika wahudumu wakamchua na kundoka naye kwa ajili ya kumpa huduma ya kwanza.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Wakati akiendelea kushonwa kidonda chake John alikua ametulia kimya huku kifua chake kikiwa kimebebe hasira nzito, akawa anawaza ni vipi atamkabili tena yusto na kumuadabisha.
Kwa heshima aliyokuwanayo John chuoni hapo, ama kwa hakika Yusto alikua amevuka mipaka.

"Kaka kwani umefanya nini mbona uko kimya tu hutuambii, inaonekana pia unahasira sana" daktari wa kike aliekuwa akimshona aliuliza tena swali

"Nimesema ni ajari, unataka kusikia nini tena, hebu fanya kazi yako bana"
John alijibu kwa jeuri Kama ilivyokuwa kawaida yake.
******

Upande wa pili Yusto alionekana akiwa wodini amekaa pembeni ya kitanda alicholazwa Sophia,
Uso wake ulikuwa umekunjamana kwa hasira huku akionekana kuzama kwenye dimbwi la mawazo.

Tangu aingie ndani ya chumba hicho hakuwa amefungua mdomo wake kuzungumza lolote

"Una nini Yusto mbona hivyo, mikono yako ina damu umefika hapa husemi chochote umekaa tu, shida nini lakini"
Sophia aliuliza kwa kulalamika.
Yusto akawa kimya wala hakujibu chochote
*****

Je, nini kitafuata?
Madam Jane ataweka wazi Siri zake kwa Caren?
Caren atafanya nini?
Vipi kuhusu sakata la John na Yusto?

ITAENDELEA...
Simulizi hii inapatikana yote kwa tsh 1000 tu.
 
𝗗𝗢 𝗡𝗢𝗧 𝗦𝗛𝗢𝗨𝗧
𝘂𝘀𝗶𝗽𝗶𝗴𝗲 𝗸𝗲𝗹𝗲𝗹𝗲
𝗦𝗲𝗮𝘀𝗼𝗻 2

Sehemu ya.........04

Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862017

ILIPOISHIA....
Caren aliendelea kubaki katika hali ya utata asijue ajibu nini.
"Careen"
"Ndio bosi"
"Are you there?"(uko hapa)
" Ndio bosi"
"Ooh come on, usiwe muoga basi, unajua kwanzia leo Mimi na wewe tutakuwa marafiki, nimekuita hapa kwa kazi maalum, Leo utazijua Siri zangu nyingi ambazo ni wachache sana wanazijua, kuanzia Leo utakuwa mtu wangu wa karibu kwa hiyo usiniogope sawa" alisema madam Jane.
*****
Je, nini kitafuata?
Madam Jane ataweka wazi Siri zake kwa Caren?
Caren atafanya nini?
Vipi kuhusu sakata la John na Yusto?

SASA ENDELEA....
"Caren" madam Jane aliita
"Ndiyo bosi"
"Unajua nimewalea wewe na wenzako tangu mkiwa wadogo kabisa hadi umri huo mliofikia, nimefanya jitihada kuwalinda kwa kila namna ninyi na familia zenu ili tu kuhakikisha mnaishi maisha ya furaha pasipo vikwazo vyovyote"

"Naelewa bosi, binafsi sina cha kukulipa madam, umenisaidia sana mimi na familia yangu, mama yangu alikua mgojwa sana nikawa nimekata tamaa nasubiri siku mungu akiamua kumchukua lakini wewe ulikuja kama miujiza ukatusaidia, asante sana madam jane"

"Usijali ilikua ni lazima nifanye kila kitu kuhakikisha wewe na wenzako mnakuwa sawa ki mwili na kiakili ili na ninyi mfanye kazi zangu kwa ufasaha"

"Asante bosi, nambie chochote nitafanya"

"Caren, Kama mimi nilivyokulinda wewe na familia yako kwa miaka yote safari hii ni zamu yako wewe kunilinda mimi"

Madam Jane alitulia kwa muda akanywa glasi moja ya maji Kisha akaendelea kuongea huku caren akiwa makini kusikiliza kazi atakayopewa.

"Kuna mtu anajua Siri zangu nyingi sana, siku akifungua mdomo kuzungumza nitaharibikiwa kila kitu, si Mimi tu hata ninyi mtapoteza ramani ya maisha yenu sitoweza kuwahudumia tena, nataka umdhibiti huyo mtu kabla hajafanya hivyo"

"Niko tayari bosi niambie ni nani natakiwa kumdhibiti vipi?''

"Ni mama mmoja hivi anaitwa Zubeda, nataka umuue"

Alisema Madam Jane kauli iliyomfanya Caren atoe macho kwa mshangao.

"Mbona unashangaa Caren,unaogopa? hujawahi kuua?"

"Ha..hapana bosi sijawahi"

"Ooh shit! , sawa lakini naamini unaweza kuua, tafadhali fanya hivyo kwa ajili yangu na kwa ajili yako pia, huyu mtu anaweza kutuharibia kila kitu, uko tayari kuona tuharibikiwe Caren? "
Aliuliza madam Jane, Caren akabaki kimya.

"Lakini madam nakumbuka ulisema wewe unafanya kazi chini ya serikali, kitengo chako ni cha Siri, kazi zote unazotupa ni kwa ajili ya serikali kama hii ya kuangusha biashara za Mark moon, vipi kuhusu hii kazi unayotaka kunipa? huyu mtu anajua siri zako au siri za serikali? na je ni serikali ndio inatuagiza tumuue?"

"Caren acha maswali ambayo sio ya msingi, sikiliza Kama huyu mwanamke ataendelea kuwa hai akatoa Siri zangu hata hiyo serikali haitonipa kazi tena, Sasa naongea Kama bosi wako fanya kazi nikiyokuagiza sawa" madam Jane alifoka, Ilibidi Caren awe mpole.

"Hiyo picha ya huyo mama mezani hapo ndio picha ya huyo mtu anaetakiwa kuuwawa, ni kichaa huwa anashinda pale soko la matunda hue, lakini nimesikia kuna watu walimteka hivi karibu fuatilia ujue ni akina nani kisha ufanye kazi yako"
Hii ilikua ni kauli nyingine iliyomfanya Caren kuwa katika hali ya kuduwaa zaidi.Hakujua mwanamke anaezungumziwa alikuwa ni mama yake Yusto kumbe ndiye Zubeda mwenyewe.
Kwa kifupi hii ilimaanisha kuwa Caren anatakiwa kumuua mama mkwe wake yaani mama wa mpenzi wake Yusto mama ambaye kwa sasa yupo mikononi mwake ndani ya Kambi yao ndogo. Moyo ulizidi kumdunda Caren na kujikuta yuko njia panda asielewe cha kufanya.

"Utaongezewa pesa kwenye account yako ukihitaji zaidi utasema, naomba ufanye kazi hii kwa nguvu zako zote Caren tunakutegemea na tunakwamini, siku tatu zitakutosha kabisa, habari njema nyingine ni kwamba....."
Alisema madam Jane, akainuka kwenye kiti chake akamsogerea Caren Kisha akainama na kumnong'oneza.

"Mama na mdogo wako watasafiri kutoka India kurudi Tanzania siku tatu zijazo, matibabu yote yamekamilika, nenda kamalize kazi kisha tutakwenda wote kuwapokea airport"

Alisema madam Jane huku akimpa Caren ile picha ya Zubeda kisha akampa ishara Caren aondoke.

Ilikuwa ni taarifa nyingine iliyouchanganya ubongo wa Caren kwa kiwango kikubwa.
Kwa heshima kubwa Caren aliinuka Kisha akatoka nje ya ofisi ya Madam Jane akaondoka kurudi kambini, kule alikomuacha zubeda(mama Yusto) akiwa anaendelea na matibabu.
****

Sekunde chache tu baada ya Caren kuondoka madam Jane alichukua simu yake akapiga mahali huku uso wake ukionekana kukunjamana kwa hasira Kali aliyokuwanayo wakati huo.

Simu illita upande wa pili na mwisho ikapokelewa.

"Hello, wewe Zius ni kazi gani huwa unafanya huko kambini"
"Kazi? Aaa.. kwa nini bosi kuna shida"
"Ipo ndio, inakuwaje mtu anakaa kambini zaidi ya miaka saba hajawahi uwa wala hajui kuuwa, hivyo ndivyo tulivyokubaliana Zius"
Madam Jane alifoka.

"Aah..ha..ha..hapana bosi lakini tulishawafundisha kila kitu hata uki......"

"Acheni ujinga, sipendi mtu anaefanya kazi kinyume na maagizo yangu"
Madam Jane alikata simu kwa hasira, Kisha akapokea simu yake nyingine ikiyokuwa ikiita.

"Ee sema"
"Kuna taarifa mbaya madam"alisikika mtu akizungumza upande wa pili
"Taarifa mbaya za nani?"
"Kutoka kwa mtu tuliemuagiza kumfuatilia mwanao John kwa ukaribu"
"Eenhe"
"John amechomwa kisu"
"Unasema nini wewe?"
"Aah ni kidogo tu bosi lakini hajaumia sana"
"Nani, nani kamfanyia hivyo mwanangu?"
"Bado anafuatilia tutajua hivi punde"
"Fanya haraka fuatilieni nataka aliefanya hilo tukio akamatwe mara moja"
"Sawa bosi akamatwe na polisi au"
"Polisi wa kazi gani mleteni mbele yangu"
Madam Jane alifoka huku akionekana kuzidi kuchanganyikiwa.
Akakata simu Kisha akakimbia hadi kwenye kabati kubwa lililokuwa ofisini humo akatoa vidonge fulani kwenye kopo akameza viwili kisha akafuatisha na maji kwa wingi.

Baada ya hapo akajitupa kwenye kiti chake, akatulia huku uso wake akiwa ameuinua akimtazama juu.

Akawa anawaza Mambo mengi sana ikiwa ni pamoja na rafiki yake wa zamani Zubeda ambae alikua na kisasi kizito juu yake akamfanyia fitina na kumgonga na gari kwa makusudi hali iliyomfanya mama huyo kuwa kichaa, lakini leo tena ametoa agizo mama huyo auwawe baada tu ya mwanae John kugusia habari zake akahisi huenda mambo yataharibika Kama John atajua siri za maisha yake ya nyuma.

Madam Jane akawaza pia namna atakavyo endelea kulipa kisasi kwa mumewe wa zamani tajiri mark moon, tayari alishafanikiwa kwa hatua kadhaa na sasa aliwaza kuelekeza nguvu zake kwenye chuo kikubwa cha mark moon bila kujua kuwa mwanae wa kwanza Yusto yupo hai na ni mmoja kati ya watu wanaokilinda chuo hicho, na ndio huyo huyo aliemchoma kisu John.

Je, nini kitafuata....
ITAENDELA!!

Bado safari yetu na simulizi hii i ndefu....
Kuipata yote kwa pamoja WhatsApp 0756862047
 
Back
Top Bottom