Simulizi ya ujasusi: Do not shout (Usipige kelele)

Simulizi ya ujasusi: Do not shout (Usipige kelele)

DO NOT SHOUT
(Usipige kelele)

Sehemu ya..…….......32

Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA.....
punde akachomoza mtu akiwa na pikipiki hiyo akija kwa kasi eneo hilo la bandari.

Sura yake haikuwa ikionekana Kutokana na helment aliyokuwa amevaa kichwani,
kasi aliyokuwa anakuja nayo ililifanya koti lake kubwa kupepea Kutokana upepo mkali ulokuwa ukimpuliza.
Naam huyu hakuwa mwingine bali Yusto.

SONGA NAYO....
Abdullah mpambe wa John alisikia muungurumo huo wa pikipiki, yeye na vijana wake wanne walitoka nje ya lile kontena walilomfunga mama mlezi wa Yusto.

Walisimama nje huku macho na masikio yao yakiwa yameelekezwa kule sauti ya muungurumo huo wa pikipiki inakotokea.

Sekunde chache baadae kwa mbali wakamuona mtu anaibuka na pikipiki hiyo akija kwa kasi upande wao.

"Atakuwa ni nani bosi"
"Hata sijui, hebu nipe simu yangu"
"Unataka umpigie John au"
"Ee huenda akawa ametumwa huyu mtu"
"Aah hapana bosi huyu ni Yusto bila shakaa"
"Yusto,hapana haiwezekeani, kapajuaje hapa"

Abdullah na wenzake walikuwa wakiulizana maswali ambayo hakuna aliyekuwa na majibu yake.

Yusto alizidi kukalibia eneo la bandari na hapo uvumilivu ulimshinda bwana Abdullah, akachomoa bastola yake na kuielekeza mbele anakotokea Yusto Kisha akapaza sauti.

"Weweee, simama hapo hapo la sivyo nitakumwaga ubongo, simamaaa"

Maneno hayo ya bwana Abdullah hayakusaidia chochote, Yusto aliendelea kuja na pikipiki yake
kwa kasi
****

Caren alifika eneo lile la soko la matunda Kama alivyo elekezwa na Revocatus mtu aliyekuwa anamsaidia kuangalia location ya simu ndogo ya Yusto.
akashuka haraka na kumlipa dereva bajaji.

"Asante afande kazi njema" alisema yule dereva bajaji Kisha akaondoka zake.

Caren alianza kutembea katikati ya lile soko huku akiangaza macho yake huku na huku katikati ya umati wa watu akimtafuta Yusto lakini hakumuona.

Aliingiza mkono Wake mfukoni akachukua simu yake hapo akakutana na simu zilizopigwa bila kupokelewa kama 11 hivi ' missed call' kutoka kwa Revocatus, akampigia.

"Ee hallo Caren mbona nakupigia sana hujapokea"
"Simu ilikuwa silence Revo, vipi niambie"
"Aah Sasa huyo mtu unamfuatilia katoka hapo sio mda, location inaonyesha anaelekea bandari ya zamani bandari ya uhuru kule"
"Ooh my God, kweli"
"Ndiyo Caren, alafu sijui yuko na usafiri gani maana anaenda kwa kasi sana, kasi mno nahisi kuna shida Caren hebu sema tuje tukusaidie basi"
"Hapana Revo hii ni kazi yangu binafsi siwezi kutumia nguvu ya bosi inaweza kuleta shida acha nipambane mwenyewe"
Aliongea caren kisha akakata simu.

"Bandari ya uhuru"
Caren alijisemea mwenyewe akili yake ikifanya kazi haraka haraka akajua cha kufanya.
*****

"Simama hapo wewe mjinga" Abdullah alizidi kupaza sauti akimtaka Yusto asimame lakini wapi Yusto hakufanaya hivo,
Hapo uvumilivu ukamshinda bwana Abdullah akaikoki bastola yake tayari kufyatua risasi.

Lakini kabla hajafanya hivyo mara Yusto alisimama juu ya pikipiki ikiwa bado inaenda kwa kasi, akaruka na kutua chini kwa ufundi mkubwa.
Pikipiki yake ikawa bado inaendelea kwenda mbele kuelekea kule walipokuwepo Abdullah na wenzake ambao walibaki wametoa macho kwa mshangao wasielewe kinachoendelea.

Kabla pikipiki haijawafikia Abdullah na wenzake, Yusto alichomoa bastola yake akalenga shabaha kwenye tenki la mafuta Kisha akafyatua risasi mbili mfurulizo.

Pikipiki ilipuka karibu kabisa na eneo walipokuwepo Abdullah na vijana wake wakaruka pembeni huku wangine wakijeruhiwa vibaya mno.

"Shambuliaa" Abdullah alitoa amri kwa vijana wake na hapo wakachomoa bastola zao na kuanza kumimina risasi pale alipokuwepo Yusto.

Yusto aliviringita chini kwa kasi akaenda kujibana kwenye moja kati ya makontena mengi chakavu yaliyokuwepo eneo hilo.

Majibizana ya risasi yalianza. Bandari yote ilizizima kwa milio ya risasi.
****

Jonh alionekana gari yake nje ya jego kubwa la ghorofa lililokuwa likimilikiwa na mama yake.
Hakujua wala kuelewa kisanga alichokiacha nyuma bandarini alikokuwa amemfungia mama yake na Yusto.
Akashuka na kuanza kuelekea kwenye mlango wa kuingilia ndani ya ghorofa hilo la kisasa.

Akiwa mlangoni anakutana na msafara wa mama yake akiwa ndio anatoka nje ameongozana na wasaidizi wake pamoja na walinzi 'bodyguard'. Huyu ndiye madam Jane mwenyewe.

"Jonh" aliita yule Madam Jane hali akionyesha mshangao kidogo.
John hakujibu badala take akamsogerea karibu mama yake.

"Tunaweza kuongea mama"
"Now?"
"Yes, ni muhimu please"
"Lakini si ulitakiwa uwe chuoni, alafu unakujaje bila kuniambia si unajua ratiba zangu"
"Ndiyo mama, ni dharula kama linivyo kwambia hata hivyo hatutatumia mda mrefu"
Alisema John.

"Misheli" Madam Jane alimwita secretary wake.
"Yes madam"
"Piga simu kwa waziri, mwambie tukutane saa kumi na moja sio saa kumi tena"
"Sawa Madam"

Baadae jonh na mama yake madam Jane yake waliongozana, wakapanda lifti hadi ghorofa ya 4 ilipokuwepo ofisi ya madam Jane.

John alionekana kuwa na mawazo kiasi bado alikuwa anajiuliza na kutamani kujua ni uhusiano gani uliokuwepo kati ya mama yake na mama yake Yusto ambae ni kichaa kwa Sasa.

"John uko sawa "
Aliuliza madam Jane baada ya kuona kabisa kuna jambo lilikuwa likiisumbua akili ya Yusto.
****

Bandarini hali iliendelea kuwa ngumu hasa kwa Yusto aliyekuwa na bastola ndogo yenye risasi kumi na mbili pekee.

Alifungua na kutazama Sasa zilikuwa zimesalia risasi tano basi.
Abdullah na wenzake bado waliendela kumuwinda na kila walipopata upenyo walifyatua risasi.

Waliendela kuzungushana kwenye makontena hayo huku kila mmoja akiwa makini kulinda usalama wa maisha yake.
Muda ulizidi kwenda na Sasa Yusto alibakiza risasi mbili pekee.
Ilikuwa ni lazima afanye jambo la sivyo atashindwa kumtoa mama yake kwenye mikono ya watu hao.

Je nini kitafuata?

ITAENDELEA.....

Usiache kufuatilia simulizi yangu mpya ya MOTO kuliko hii inaitwa THE MODERN WAR (vita ya kisasa)

Napatikana WhatsApp +255756862047.
 
Safi uwe unatuma mingi mzee
 
Jioni ya leo mbengo zinafongokaaa....
Episode ya 33.

Jipatie simulizi hii yote kwa tsh 1400 tu
Nichek kwa namba.
0756862047
 
DO NOT SHOUT
(Usipige kelele)

Sehemu ya...............33
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA....
Abdullah na wenzake bado waliendela kumuwinda Yusto na kila walipopata upenyo walifyatua risasi.

Waliendela kuzungushana kwenye makontena hayo huku kila mmoja akiwa makini kulinda usalama wa maisha yake.
Muda ulizidi kwenda na Sasa Yusto alibakiza risasi mbili pekee.
Ilikuwa ni lazima afanye jambo la sivyo atashindwa kumtoa mama yake kwenye mikono ya watu hao.

Je nini kitafuata?

SASA ENDELEA...
Paaa!! Paaaa!!

Paa!! Paaa!!

Milio ya risasi iliendelea kulindima eneo hilo la bandarini.
Yusto akiwa amebakiwa na risasi mbili tu kwenye bastola yake aliendelea kuwazunguusha Abdullah na vijana wake kwenye yale makontena.
Ilikuwa ni ngumu kwake kukabiriana nao kwani mpaka sasa alibakia na risasi mbili pekee, ilimbidi atumie akili ya ziada.

Yusto alivua kiatu chake kimoja akakisogeza hadi kwenye Kona moja ya kontena alilokuwepo, kikawa kinaonekana upande wa pili.

Abdullah na wenzake walipokiona kiatu kimotokeza moja kwa moja wakajua ni Yusto, wakawa wanarusha risasi nyingi kuelekea eneo lile kwa kasi.
Yusto alitoka na kuzunguuka upande wa pili wa kontena akakimbia kwa tahadhali na kuwazunguuka kwa nyuma Abdullah na wenzake waliokuwa bize wakilenga shabaha zao pale kwenye kiatu.

Akanyata taratibu Kisha akamvaa na kumkaba mmoja wa vijana wa Abdullah kimya kimya akamlaza chini taratibu akiwa amepoteza fahamu akachukua siraha yake, hakuna aliyeshtuka.

Abdullah baada ya kuona wamepiga risasi nyingi bila manufaa yoyote aliinua mkono juu ikiwa ni ishara ya kuwataka vijana wake waache kwanza kushambulia.
Ni kama vile Abdullah alishtukia mchezo wa Yusto akaanza kusogea taratibu huku akiwa amenyoosha mbele bastola yake, vijana wake wakawa wanamfuata nyuma.

Walifika na kuzunguuka upande wa pili wa kontena, hakukuwa mtu.

"Shitttt, mjinga" Abdullah alifoka kwa hasira baada ya kugundua yusto kawachezea.

Wakiwa hawajajipanga vizuri mara walisikia mlio wa risasi na mara kijana mmoja wa Abdullah akalia kwa sauti na kuanguka chini akiwa amepigwa risasi kwenye paja la kushoto.
Haraka walikimbia na kujificha nyuma ya lile kontena.

"Yustoooo" Abdullah aliita kwa sauti akionekana kuanza kupaniki.

"Huwezi kushinda utakufa wewe na mama yako kichaa,, woote mtakufa leooooo"

" Jisalimishe mwenyewe kabla sijaripua hili eneo lote, nakuuwa wewe na mama yako, nahesabu moja hadi kumi"

"Moja, mbili, tatu, nne, tano, sita......."

Abdullah aliendelea kuhesabu huku Yusto akiwa amesimama nyuma ya kontena moja akimsikiliza.
Alijiuliza mara mbili mbili ni nini anataka kufanya lakini mwisho akajipa moyo kuwa huenda ni mikwara tu.

"Saba...nane....tisa.........kumi"
Abdullah alimaliza kuhesabu huku akiwa amekunja sura yake kwa hasira.
Akalenga shabaha ndani ya kontena moja lililokuwa karibu kabisa na kontena walilomfunga mama yake Yusto.

Abdullah aliwapa ishara fulani vijana wake waliosalia taratibu wakaanza kujivuta kusogea mbali na eneo lile.
Yusto alisogea tena kuwachungulia ndipo alipomuona Abdullah akiwa amelenga shabaha kwenye moja ya kontena,
hakuelewa Abdullah anataka kufanya nini, lakini baada ya kuangalia kwa makini kwenye lile kontena aliona kuna mitungi mingi na mikubwa ya gesi ndani yake.

"Ooh! Noo" alisema Yusto huku akigeuka kwa kasi kutaka kumpiga risasi Abdullah lakini alikuwa kachelewa Abdullah alifyatua risasi kuelekea kwenye ile mitungi ya gesi.
****

Caren alionekana anakimbia kuelekea kwenye ile bandari,
akiwa mbali alikuwa anasikia majibizano ya milio ya risasi eneo lile, akazidi kupatwa na wasiwasi akihofia usalama wa Yusto mwanaume aliempenda kuliko chochote kile.

Alizidi kukimbia na sasa alikuwa amebakiza hatua chache kufika eneo lile la bandari,
Ghafula ukatokea mlipuko mkubwa mno.

"Yusto"
Caren aliongea kwa sauti ya chini iliyojaa hofu huku akiwa amesimama mapigo yake ya moyo yakienda mbio.
Akawa anashuhudia jinsi makontena kadhaa yakirushwa hewani na kutua chini.
Wingu kubwa la moshi lilikuwa limetanda hewani.

Akiwa amekata Caren alianza kukimbia tena kuelekea eneo lile lililokuwa limetapakaa moshi mwingi kila mahali.
Kwa mbali ving'ora vya gari za polisi vilisikika. Tayari polisi walipata taarifa na Sasa walikuwa wanakuja eneo hilo kwa kasi.
***

Abdullah alionekana akiwa amesimama katikati ya moshi mwingi, alikuwa akiangaza macho huku na huku akimtafuta Yusto lengo lake ni kuhakikisha anammaliza kabisa hata kama atakuwa amesalimika kwenye mlipuko huo kubwa.
Lakini mara tu aliposikia ving'ora vya gari za polisi alighairi kufanya kile anachokifanya kisha yeye na vijana wake wakakimbia na kuondoka eneo hilo.
***

Jonh na madam Jane mama yake walishuka kwenye lifti na kuingia moja kwa moja ndani ya chumba kimoja kikubwa ambacho ndio ilikuwa ofisi ya mama yake.

Madam Jane alikaa kwenye kiti chake Kisha akamuonyesha ishara mwanae akae kwenye kiti kingine mbele yake.

" Mnh, nambie mwanangu hauko sawa kabisa nakuona"
Madam Jane alianzisha mazungumzo.
"Hapana niko sawa isipokuwa nina swali kidogo hapa, hebu iangalie hii picha mama"
Alisema John kisha akainuka pale kwenye kiti akaosogea na kumpatia mama yake ile picha.

Madam Jane aliipokea na kuitazama. Alipatwa na mshituko kiasi lakini hakutaka kuonyesha mshituko wake mbele ya John.
Ilikuwa ni ile picha ya miaka kadhaa iliyopita inayomuonyesha yeye akiwa pamoja na mama yake Yusto ambae kwa sasa ni kichaa.

"Umepata wapi hii picha John"
"Huyo ni nani mama" badala ya kujibu swali John akauliza swali.

" Alikuwa rafiki yangu kitambo sana, hata kabla sijakuzaa wewe"madam Jane alijibu kwa kujiamini.

"Alikuwa rafiki yako, ila kwa sasa sio, je unajua alipo".
John aliuliza swali jingine huku akijaribu kumuangalia mama yake kwa macho ya kumdadisi.

"Aah.. hapana sifahamu, ni mda mrefu sana umepita, kwani vipi mbona hivyo"

Kabla John hajamjibu mama yake hilo swali mara simu yake iliita.
Aliitazama namba ya mpigaji, hakuwa mwingine bali kijana wake Abdullah.

Ilikuwa ni lazima John apokee simu hiyo kujua ni nini kinaendelea kule bandarini walikomfungia mama yake Yusto.
Aliomba ruhusu kwa mama yake Kisha akatoka nje kuongea na simu hiyo ya Siri.

Baada tu ya John kutoka, Madam Jane alikurupuka kutoka pale kwenye kiti akasimama.
Ukweli alikuwa amejikaza sana, habari za John na ile picha zilimshtua sana.
Kwa haraka haraka ilionyesha kuna Siri kubwa ilivyokuwa imejificha kati ya mama yake Yusto na madam Jane.

Madam Jane alichukua simu yake haraka akapiga simu mahali, wakati huo John hakuwa ameenda mbali alikuwa mlangoni anamsikiliza.

"Hello,unachelewa kupokea simu kwa nini....okay sasa sikia unamkumbuka yule mwanamke Zubeda rafiki yangu wa zamani... Eee huyo huyo tuliemgonga na gari kipindi kile.....yes......naomba fuatilia habari zake nataka kujua sasa hivi yuko wapi......ndio ni kichaa lakini mfuatilie nahisi kuna shida John kaja hapa anauliza habari zake......sawa ukimpata tu nitaarifu haraka kabla hajaharibu mambo...ok"

Madam Jane alimaliza mazungumzo Kisha akakata simu, akachukua kitambaa akajifuta jasho jembamba lililokuwa limeanza kumtoka.

Je, kuna Siri gani hapo?
Madam Jane na mama Yusto kuna nini kati yao?
Yusto na mama yake watasalimika na mripuko ule?
Vipi kuhusu penzi la Caren Yusto John na Sophia?

ITAENDELEA....

Njoo WhatsApp na Tsh elf 1 tu umalizie simulizi hii (30-80)

Usiache kufuatilia simulizi yangu mpya THE MODERN WAR(Vita ya kisasa)

WhatsApp 0756862047
20220625_140319-BlendCollage.jpg
 
DO NOT SHOUT
USIPIGE KELELE

Sehemu ya............34

ILIPOISHIA....
"Hello,unachelewa kupokea simu kwa nini....okay sasa sikia unamkumbuka yule mwanamke Zubeda rafiki yangu wa zamani... Eee huyo huyo tuliemgonga na gari kipindi kile.....yes......naomba fuatilia habari zake nataka kujua sasa hivi yuko wapi......ndio ni kichaa lakini mfuatilie nahisi kuna shida John kaja hapa anauliza habari zake......sawa ukimpata tu nitaarifu haraka kabla hajaharibu mambo...ok"

Madam Jane alimaliza mazungumzo Kisha akakata simu, akachukua kitambaa akajifuta jasho jembamba lililokuwa limeanza kumtoka.
****

(TAFADHALI SOMA SEHEMU HII KWA MAKINI HAPA NDIPO KILIPO KIINI CHA SIMULIZI YETU--- stay with me)

Madam Jane alionekana kutokuwa sawa kabisa, habari alizoletewa na mwanae kumuhusu mama mlezi wa Yusto zilionekana kumshtua sana. Alivuta kiti na kukaa tena akatulia kwa muda huku akivuta kumbukumbu ya mambo yaliyotokea miaka 25 iliyopita.

MIAKA 25 ILIYOPITA....
Janeth(madam Jane) na Zubeda(mama mlezi wa Yusto) wakiwa bado ni wasichana wadogo walikuwa ni marafiki wakitokea kwenye familia duni za kimasikini.
Kwa pamoja walikubaliana kutoka kijijini na kuja mjini Dar es salaam kutafuta maisha
Hali ilikuwa ngumu tofauti na walivyotegemea mara tu walipowasili Dar es salaam hawakuwa na kitu cha kufanya na mwisho wakajikuta wanaingia katika biashara ya ukahaba na kuuza miili yao ili tu wapate pesa.
Katika hali ambayo hakutegema Janeth alijikuta anabeba ujauzito. Alitamani na kujaribu kuitoa mimba hiyo mara kadhaa lakini ilishindikana.

"Janeth rafiki yangu, fanya uzae tu huwezi jua kwa nini hii mimba imegoma kutoka usilazimishe sana" alisema Zubeda rafiki wa karibu wa Janeth

"Zubeda unanitakia nini wewe, nikizaa halafu iwaje, huyo mtoto nitamleaje kazi zangu nitafanya vipi, nitaishije mjini hapa"

"Kwa Sasa hauna namna janeth zaa tu"

Ilikuwa hivyo na mwisho Janeth(Madam Jane) alijifunga mtoto wa kiume akampa jina YUSTO.

Janeth alimnyonyesha Yusto kwa miezi sita tu na hapo akaacha na kuanza kumpa maziwa ya ng'ombe na vyakula mbalimbali. Alifanya hivyo ili kuhurusu mwili wake ujirudi haraka ili aendelee na biashara yake ya kujiuza kutokana na hali ngumu ya kimaisha.

Ikawa hivyo, muda ulipita na mwisho katika hali ambayo hakutegemea Janeth alijikuta anapendwa na mwanaume mmoja tajiri sana Mwanaume huyo aliitwa kwa jina maarufu bosi Mark Moon.
Mwanaume huyo alikuwa tayari kumuoa Janeth haraka iwezekanavyo. hii ilikuwa ni bahati ambayo janeth hakutaka kuichezea.

"Zubeda rafiki angu naomba uende mbali na Yusto, Mark Moon hajui Kama nina mtoto na wala hatakiwi kujua, ondoka Zubeda nitakulipa kiasi chochote utakachotaka"

Haya yalikuwa ni maelezo ya Janeth kwa Zubeba.
Mambo yalikuwa hivyo, tajiri Mark Moon akamuoa Janeth, ndoa yao ikawa kubwa na ya kifahari sana, Janeth akatafuta ndugu wa bandia na kuwawe kwenye sherehe hiyo.
Magazeti na vyombo vya habari vyote vikaripoti tukio hilo la kihistoria la ndoa ya tajiri Mark Moon, jambo lililompa umaarufu mkubwa Janeth ambae alipewa jina la umaarufu Kama Madam Jane.

Umaarufu huo ndio ukawa mwanzo wa matatizo mwanzo wa kufukua historia ya nyuma ya maisha ya Janeth (madam Jane) kila kukicha gazeti hili likiandika hivi lingine linaandika hivi.
Mara
"Mark moon aowa kahaba"
"Madam Jane ni mama wa mtoto mmoja"
"Bishara ya ngono yambeba madam Jane"
"Mke feki, harusi feki, ndugu feki"
"Janeth alipata zali la mentali"
"Janeth afunga ndoa mara ya tatu"

Taarifa hizo zilimshtua mark moon ambaye alijiona ni Kama alifanya Mambo kwa kukurupuka sana, ni kweli alimpenda Janeth lakini alihisi kuna mahali amedanganywa na mwanamke huyo.

Akatuma watu wake kuanza kuchimba maisha ya nyuma ya Madam Jane (Janeth).

" Ni vema ukaniambia ukweli leo wewe mwenyewe kwa mdomo wako kabla sijautafuta mwenyewe"

"Mume wangu kwa nini unakuwa mwepesi hivyo kuamini taarifa za magazetini, huoni kama hunitendei haki na unanikosea heshima mimi kama mkeo"
" Kwa nini kila siku ni wewe tu kwenye magazeti, kwanini sio wengine? kwani matajiri hapa Tanzania ni sisi tu Janeth?"

"Hapana mume wangu, kumbuka mimi ni maarufu tayari alafu bado ni mdogo kuolewa na tajiri Kama wewe wengi hawajapenda"
"Janeth unafikiri leo ndio mara ya kwanza nazungumziwa vibaya kwenye magazeti na vyombo vya habari, haya ni maisha ambayo mimi nishazoea, lakini kwenye hili siwezi kukaa kimya, kunakitu naona kabisa hakiko sawa, nitamtafuta huyo mtoto wanaedai ni wako na ikibidi hata DNA utapima" alisema mark moon mwanaume ambaye alikuwa na misimamo thabiti katika mambo yake.

Madam Jane naye hakuwa mzembe, tayari alikuwa ni mwanamke maarufu sana hakuwa tayari aibu hiyo impate, angeiweka wapi sura yake Kama angeachika.

Tayari alishamficha mbali Zubeba na mwanae Yusto ili asifikiwe na waandishi wa habari, lakini aliona hiyo haitoshi akiwa na akili zake timamu Janeth aliagiza Zubeba na mwanae Yusto wauwawe kisha miili yao ichomwe moto akaamini kwa kufanya hivyo atakuwa amemaliza kila kitu, hata mumewe akifuatilia hakuna atakacho ambulia.
Pesa kwake ilikuwa ni kila kitu, hakujali chochote.

Mtu aliyepewa jukumu la kutekeleza mauaji hayo ya kikatili akawa na huruma kwa Yusto na Zubeda. Akamueleza Zubeda kila kitu kuwa Janeth anataka kumuuwa yeye na Yusto, akawataka waende mbali. Zubeda akakimbia na kuanza kuishi maisha ya kujificha akiwa pamoja na Yusto.

Lakini pamoja na yote mwisho Mark moon aliupata ukweli, japo hakufanikiwa kumpata Yusto lakini alithibitisha kila kitu.
Madam Jane alikuwa amemdanganya sana, sio kidogo. Kwa kuwa mark moon alikuwa mtu wa haki mtu makini na asiye na makandokando mengi aliamua kuachana na mkewe akampa taraka na wala hakuona shida kumpa sehemu ya Mali alizokuwa nazo Kama sheria ilivyotaka, wakaachana rasmi.

Hii ilikuwa ni aibu ya mwaka kwa madam Jane alichafuliwa kwenye mitandao vibaya mno. pamoja na kumbembeleza mumewe asifanye hivyo lakini Mark Moon hakumuangalia usoni.
Madam Jane akawa gumzo kila Kona kila mahali

Mgao wa pesa na mali alizopewa zilikuwa ni nyingi mno akayaanza maisha yake mapya huku akiwa ameweka kisasi kizito kwa mark moon na rafiki yake Zubeda aliyebaini kuwa bado yuko hai akiamini hawa ndio chanzo cha maisha yake kuharibika.

Wakati madam Jane anaachana na mumewe mark moon alikuwa tayari na ujauzito wa miezi mitatu. Akaamua kuficha hilo na kuhamia Dubai.

"Nitakuzaa mwanangu na siku unaonana na baba yako itakuwa ndio siku tutakayo mnyang'anya kila kitu na kumuacha mikono mitupu. Ametutelekeza na kutuaibisha leo lakini tutarudi tukiwa na nguvu na kulipa kisasi"
Alisema madam Jane wakati akiwa ndani ya ndege kuelekea Dubai.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Akiwa huko aliendeleza biashara zake Dubai na nyingine Tanzania. Madam Jane alikuwa ni mtu mwenyewe nyota yake, kwa muda mfupi tu tayari utajiri wake ulikuwa umekuwa kwa kasi sana Sasa alikuwa mama mwenye pesa zake.
Tayari alishajifungua na akampa jina mwanae akamwita JOHN.
hakuwahi kumwambia baba yake halisi, akadai kuwa alishakufa.
Haya ndiyo mazingira waliyozaliwa vijana hawa wawili YUSTO na JOHN ambao kwa sasa ni maadui wakubwa.

Madam Jane hakuacha kuwaza kuhusu kisasi kila alipomuona John aliwaza kisasi dhidi ya mark moon na Zubeda rafiki yake.
Akiwa bado Dubai alipata habari kuwa Zubeba ameonekana mahali, haraka bila kupepesa alitoa agizo kuwa auwawe.
Zubeba alisababishiwa ajali ya gari kwa makusudi na watu waliotumwa na madam Jane,
alipigiza kichwa chini na baada ya kupelekwa hospitali alitoka akiwa na matatizo ya akili yaani mwenda wazimu(kichaa) hayo ndiyo yakawa maisha yake mapya.
Madan Jane aliiona hiyo Kama adhabu tosha kwa Zubeba. Sasa kisasi chake kikabaki dhidi ya Mark Moon
****
MIAKA KADHAA BAADAE...
Tayari madam Jane alikuwa amerejea Tanzania na jina lake likawa kubwa akitajwa Kama miongoni mwa matajiri wakubwa nchini Tanzania.
Lengo lake kubwa likawa ni kuangusha biashara zote kubwa za Mark Moon.

Alichokifanya madam Jane ni kuanza kuwalea watoto wadogo waliokuwa wakiishi kwenye mazingira magumu akachukuwa na kuwaunganisha pamoja huku wakipewa mafunzo maalumu ya upambanaji.
Miongoni mwa watoto hawa aliowalea alikuwepo binti CAREN kutoka burundi.
Lengo la madam Jane ilikuwa ni kuwatumia baadae katika harakati za kuangusha biashara za Mark moon.

Caren na wenzake hawakuwa wakijua Siri ya kisasi hicho kwa bosi wako.
CAREN alijitoa kwa kila hali kuhakikisha anafanya kila atakacho agizwa kwani watu hao walikuwa wamemsaidia yeye na familia yake kwa kiasi kikubwa.
***

Yusto nae baada ya kukulia kwenye mazingira magumu baadae alifika mjini akamtafuta mama yake mlezi ambaye hakuwahi kumweleza juu ya wazazi wake harisi lakini pamoja na kulijua hilo Yusto alizidi kumpenda Zubeda akimuona Kama mama na ndugu pekee aliyenae.

Alihangaika akiwa na rafiki yake Frank na mwisho walipata bahati ya kuajiliwa chini ya tajiri Mark moon Kama vijana walinzi wa biashara zake.
Walipelekwa katika chuo cha Mark Moon wakawa Kama walinzi wa Siri wa chuo hicho wanao jifanya wanafunzi.

Target ya kwanza ya Madam Jane katika harakati ya kumuangusha kiuchumi mumewe wa zamani Mark moon( baba Jonh) ilikuwa ni kuharibu sifa ya chuo cha Mark Moon ambacho alikijenga kwa mabilioni ya fedha.
Kwa makusudi Madam Jane alimpeleka mwanae John akawa mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho. Madam Jane alijua nini anafanya.
Baadae akatoa amri vijana wake waende kwenye chuo hicho kuhakikisha wanakiharibia sifa.
Caren akiwa ndiye aliyepewa jukumu hilo akaingia ndani ya chuo hicho Kama mwanafunzi lakini ni agent wa Siri wa madam Jane.
NAAM MADAM JANE ALIFIKA MWISHO WA KUKUMBUKA MAISHA YAKE YA NYUMA NA HUO NDIO ULIKUWA UHALISIA WA MAISHA YA NYUMA KATI YA MADAM JANE(MAMA JOHN) ZUBEDA(MAMA KICHAA NA MLEZI WA YUSTO)
[emoji294][emoji294][emoji294]

Yusto akiwa ndani ya chuo cha Mark Moon pamoja na ndugu yake John pasipo kujuana,
wote wanajikuta wanampenda binti Caren na hapa linaibuka balaa jingine chanzo kikiwa ni mapenzi na kupelekea uhasama mzito kati ya ndugu hao waliozaliwa na mama mmoja.

John haelewi chochote kuhusu Siri ya kisasi cha mama yake yaani madam Jane, wala hajui Kama Caren ni mfanya kazi wa mama yake, wala hajui kama Yusto ni kaka yake na mbaya zaidi amepanga kumuua kwa sababu ya wivu wa mapenzi kwa Caren.
Caren naye anazama kwenye penzi zito na Yusto pasipo kujua kuwa Yusto ni mtoto wa bosi wake yaani Madam Jane.
[emoji294][emoji294][emoji294]

SASA TUENDELEA...

John alikuwa bado anaongea na simu
"Abdullah kwa hiyo unataka kusema Yusto na yule mama yake kichaa wamekufa"

"Ndio nahisi hivyo bosi lakini sina hakika sijahakikisha polisi walikuwa wanakuja tukakimbia"
" Sawa nitakupigia baadae"
John alikata simu kisha akarudi ofisi kwa mama yake, akakaa kwenye kiti huku akizidi kumtazama mama yake kwa macho ya udadisi.
*****

Upande wa pili Caren alionekana akiwa eneo la bandarini pale kulipotokea mripuko mkubwa akiwa anahangaika kumtafuta Yusto. Moshi mwingi ulikuwa umetanda kila mahali, Caren alizidi kuwa na hofu hakuwa na uhakika Kama Yusto yuko hai au laa!

ITAENDELEA BAKI NA MIMI season 2...

Full story 1200 /= (1-80)
0756862047

Like comment and share twende chapu...
Usisahau kusoma simulizi MPYA ya THE MODERN WAR-Vita ya kisasa
 
KWA MAONI YAKO MPAKA SASA QUEEN WA SIMULIZI YETU NI NANI....

1. SOPHIA
2. CAREN
3. BRANDINA

weka maoni yako!!
 
Back
Top Bottom