𝗗𝗢 𝗡𝗢𝗧 𝗦𝗛𝗢𝗨𝗧
𝘀𝗲𝗮𝘀𝗼𝗻 2
Sehemu ya............ 6
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
ILIPOISHIA ...
Jambo ambalo mark Moon hakujua ni kuwa tayari alikua katika vita kali dhidi na mkewe wa zamani (X-wife) madam Jane. Mbaya zaidi mtoto wake wa kiume John ambae hajui Kama Mark moon ni baba yake wala baba hamjui mwanae ndiye aliyekua anagombea nafasi kubwa ya Urais wa chuo chake.
Je, nini kitafuata?
SONGA NAYO....
****
Kikao kilichukua mda mfupi, Mark moon pamoja na wafanyakazi wake wakapanga mikakati namna ya kuimarisha ulinzi chuoni hapo kuhakikisha hakuna jambo lolote baya linatokea katika kipindi hicho muhimu cha uchaguzi wa viongozi.
Kwa sasa hali ilikua shwari , hakukua kumetokea tukio lingine la kutishia usalama wa wanafunzi, ingawa hawakufanikiwa kumpata mhusika wa matukio hayo baada ya mtu waliekuwa wakimhisi (Caren) kuwapoteza maboya,
Lakini mark moon aliwataka Simigo na wenzake kuhakikisha wanaongeza jitihada kumpata mhusika na wasiruhusu tukio lingine tena.
Mwisho alihairisha kikao chake na kila mmoja akatakiwa kurudi kwenye nafasi yake. Brandina alikua wa kwanza kufika mlango lakini akasimama macho yake akiwa anamtazama Yusto kijana aliyekua ameuteka moyo wake vilivyo.
Ulikua umepita muda sasa tangu Brandina na Yusto walipokutana kwa mara ya mwisho hakika moyo wake ulikua umemmiss sana kijana huyo.
Mwisho aliwano Yusto na Frank wanakuja, Brandina aliachia tabasamu mwanana kiasi cha kuufanya mwanya wake mzuri uonekane.
"Mambo vipi brandina" Yusto alikua wa kwanza kumsalimia
Lakini kabla Brandina hajaitikia salamu hiyo Mara alisikia sauti ikimwita kutokea ndani ya kile chumba walichokua wakifanyia kikao.
"Abeeh" Brandina aliitika Kisha wote wakageuka kuangalia sauti ilikotokea, kwa mbali wakamuona bosi Mark Moon akimpungia mkono akimtaka asogee.
Brandina alishtuka kiasi, hakujua bosi mark moon amemuita kwa sababu gani, haikua kawaida kabisa.
Akasogea taratibu hadi pale alipokua bosi Mark moon na watu wake, Yusto na Frank wakabaki wanataza kwa mbali.
"Ndio bosi"
"Brandina, si ndio"
"Yah ndio mimi bosi"
"Tunaweza kuongozana tafadhali nina mazungumzo na wewe"
Alisema mark moon .
Mwisho Brandina na mark moon waliondoka wakiwa wameongozana, Yusto na Frank wakawa wanasindikiza kwa macho.
"Oya.. Yusto"
"Nambie"
"Ulikua wapi unajua sikuelewi ratiba zako siku hizi, unatoka tu huniagi unarudi husemi chochote, umekuwaje mshkaji wangu?" Frank aliuliza
"Aah..sio hivyo Frank unajua kuna baadhi ya vitu natakiwa kudili navyo mwenyewe sitaki nikusumbue sana kwa matatizo yangu binafsi"
"Sio kweli Yusto, umekua msiri sana siku hizi mtu wangu alafu mwanzo haukuwa hivyo, Sophia ameumia chumbani kwako kalazwa hujasema lolote, umeondoka ghafula tu ukabeba hadi na siraha yako umerudi hujasema lolote" Frank alilalamika
"Sio hivyo mtu wangu, basi nisamehe nitakwambia kila kitu, unajua John alimteka mama"
"Nini wewe? mama gani! mama kule jalalani?"
"Yah mama yangu"
"La haulaa, alimjuwaje sasa? enhe! ikawaje" Frank aliuliza kwa bashasha
"Alimteka mama Kisha akanitisha akitaka niachane na Caren"
"Atiii, kwani wewe na Caren mna nini,ni wapenzi au?"Kila kitu kilionekana kuwa kigeni kwa Frank.
Yusto alibaini kuwa ni kweli alikua amemficha rafiki yake vitu vingi mno.
"Ee sisi ni wapenzi tuliachana na tumerudiana, sa sikia unajua ilikua kidogo mimi na mama tufe alimpeleka sijui wapi huko kwenye makontena ya bandarini, kwa bahati nzuri Caren na wenzake wakatokea na kutusaidia"
"Wenzake, akina nani? Caren anawenzake gani? Alafu yule si ameolewa na anamtoto kwani hukusikia jamaangu" aliuliza Frank
Yusto akapatwa na kigugumizi kutoa maelezo mengine zaidi ilikua ni kuvunja makubaliano yake na Caren.
Hakutakiwa kumweleza mtu ile siri aliyoelezwa na Caren kuhusu uhalisia wake.
"Mbona kimya?"
"Mmh hebu subiri unajua Caren kanipigia sana wakati tupo kwenye kikao, sikupokea simu yake" alisema Yusto huku akizuga kwa kuitazama simu yake.
Ni kweli Caren alikua amempigia simu mara kadhaa baada ya kuona simu haipokelewi akamtumia sms.
"MPENZI MAMA AMEAMKA ANATAKA KUKUONA ANATUSUMBUA SANA"
Ilikuwa ni sms iliyomfanya Yusto kupatwa na ubaridi wa furaha, akajaribu kumpigia simu Caren ili ampe maelekezo zaidi kwani hakuwa akijua ile kambi ndogo ya akina Caren mahali ilipo. Kwa bahati mbaya simu ya Caren ikawa haipatikani.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Upande wa pili Caren alionekana akiwa amesimama nje ya chumba alicholazwa zubeda mama mlezi wa Yusto.
Caren alikua akitembea anapiga hatua huku kisha anarudi tena, alionekana ni mtu mwenye mawazo sana mda huo.
Ndani ya chumba kilichokuwa mbele ya Caren alionekana Daktari wa magonjwa ya saikolojia na akili akiongea na Zubeda huku mkononi akiwa na picha kubwa na madam Jane, ya zamani na ya sasa.
Caren aliendelea kubaki pale nje huku akisubiria kwa hamu majibu kutoka kwa daktari.
Alitamani sana kujua ni uhusiano gani uliokuwepo kati ya zubeda mama mlezi wa Yusto na bosi wake madam Jane.
Aliamini lazima Daktari angekuja na majibu yatakayompa mwanga.
Hatimae dakika chache baadae daktari alitoka.
" Niambie Daktari, vipi umepata chochote?" Caren aliuliza kwa bashasha
"Aah ndio, kuna vitu vingi sana nimebaini kutoka kwa huyu mama kichaa, vipi tunaweza kuketi tukazungumza"
"Sawa twende kile chumba pale"
Alisema Caren Kisha wakaongozana na Daktari.
Wakiwa bado njiani walikutana na Revocatus.
"Revo naongea na daktari mara moja, naomba muone mama mle ndani asije kuleta vurugu tena" alisema Caren.
Revo akatikisa kichwa kukubaliana na maelezo hayo, Kisha akawa anawatazama Caren na daktari wakati wanaingia kwenye kile chumba kwa ajili ya mazungumzo.
Lakini macho ya Revocatus yalionyesha wazi kuwa naye alikua na jambo lake tena jambo la siri sana.
[emoji294][emoji294][emoji294]
"Kwanza kabla sijaendelea Yusto ni nani?" Daktari aliuliza swali kabla ya kuanza kutoa majibu ya kile alichokipata baada ya kufanya mazungumzo na mama kichaa Zubeda.
"Ni kijana flani hivi sijui hata nikuelezaje ila amelelewa na huyo mama kabla hajaugua kichaa"
"Ooh kumbe, sio mtoto wake wa kumzaa si ndio"
"Hapana ni mama mlezi tu"
"Yes, ni Kama nilivyotegemea"
" Una maana gani Daktari"
"Aah nilichobaini ni kwamba madam Jana aliwahi kuwa mtu wa karibu na huyu mama kichaa lakini kuna Jambo lilitokea likawafanya wao kuwa maadui kiasi cha kumfanya madam Jane ajaribu kumuuwa huyu mama na mtoto wake anaemwita Yusto zaidi ya Mara moja, huyu mama anadai Yusto ni mtoto wa madam Jane yaani madam Jane ndio aliyemzaa Yusto lakini kuna Jambo lilitokea likamfanya madam Jane kutaka kuwauwa wote huyu mama na mtoto wake lakini walinusurika"
Daktari alitoa maelezo yaliyomfanya Caren abaki mdomo wazi, haikua rahisi kuamini kile alichokisikia
"Eti nini, Yusto ni mtoto wa madam Jane?"
"Ndio, nina uhakika wa asilimia 99%, binti mimi ni daktari wa vichaa naelewa vizuri Code za watu wa aina hii, Yusto ni mtoto wa madam Jane amini ninachokwambia" Daktari alisisitiza.
"Hapana haiwezekani Dr kivipi yani?"
"Binti sina sababu yoyote ya kuongea kitu ambacho sina uhakika nacho, mimi nimefanya kazi uliyoniambia"
Caren alitulia kimya baada ya kuona daktari anaongea kwa kukaanisha.
Caren akajaribu kuunganisha baadhi ya matukio, alikumbuka ni kweli Yusto alimwambia kuwa hakua akimfahamu mama wala baba yake mzazi, Zubeda alikua ni mama mlezi tu kwake.
Caren alivuta pumzi ndeefu, kisha akaitoa taratibu.
"Sawa Dr nimekuelewa, vipi kingine kipi natakiwa kujua."
"Aah hayo ndio muhimu sana labda kingine nikutoe tu hofu kuwa kichaa cha mama sio kikubwa sana, anajielewa kwa kiasi, haitochukua mda mrefu anaweza kupona na Kama mtampeleka hospitali ya vichaa itakuwa ni nzuri zaidi, huyu mama anampenda sana Yusto lakini anamchukia sana Madam Jane ni hivyo tu" alisema Dr
Baada ya maelezo hayo Caren alichukua simu yake akampigia Revocatus.
Simu ya Revocatus ilisikika ikiita mlangoni nje ya chumba walichokuwepo Caren na Daktari.
Caren akakata simu,
Revo akafungua mlango na kuingia ndani.
"kumbe ulikua hapa" aliuliza Caren huku akimtazama Revo usoni
"Aah ee...ndio.. nimekuja sio mda mama ameshalala kule"
Revo aliongea kwa kujiuma uma lakini ukweli alikua mlango tangu kitambo na alikua akifuatilia mazungumzo yote kati ya Caren na Daktari tangu mwanzo.
Ilionekana wazi kuwa Revocatus alikua anajambo lake analolifanya kwa Siri licha ya kwamba yeye na Caren waliaminiana sana.
" Amelala kivipi, umemchoma tena sindano ya usingizi"
"Yaah nimemchoma anasumbua sana kila wakati anapiga kelele Yusto, Yusto"
"Revo lakini dawa za usingizi sio nzuri kwa mama, hii ni sindano ya nne sasa unamchoma na hata siku haijaisha, daktari au wewe unasemaje"
"Ni sahihi sahihi kabisa, dawa za usingizi zinaweza kumfanya mtu akawa teja kwa kitaalam tunaita drug addiction, kichaa anatakiwa kufanyiwa vile vitu anavyovipenda Kama tu havina madhara, Kama anamtaka Yusto basi mleteeni Yusto" alisema Dr, huku Caren alitikisa kichwa kuunga mkono maelezo hayo.
" Sawa tutafanya hivyo Dr, basi Revo msindikize Daktari Kisha utapitia chuoni umlete Yusto hapa ninaimani hata yeye anatamani kumuona mama yake akiwa ameamka, nitampigia simu" alisema Caren.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Dakika chache baadae Revocatus na Daktari walionekana wakiwa ndani ya gari wakitoka nje ya kambi ndogo ya akina Caren.
Kama kawaida Revocatus alikua ndiye dereva, Daktari alikua amekaa siti ya nyuma akiwa amefungwa kitambaa usoni,
Hakutakiwa kuona njia ya kufika kambini hapo.
Kwenye mapaja yake daktari alikua amepakata briefcase (begi) ndogo la pesa ikiwa ni malipo yake baada ya kufanya kazi ile ngumu ya kuzungumza na kichaa.
Kwa mwendo wa zaidi ya dakika 15, kila mmoja alikua kimya, hakuna aliyekua amefungua kinywa kuzungumza na mwenzake tangu safari ilipoanza.
"Mbona unaendesha kwa kasi sana kijana vipi?" hatimaye daktari alifungua kinywa kuzungumza
"Kijanaaa" Daktari aliita tena kwa sauti baada ya kuona Revocatus yuko kimya hamjibu chochote.
Licha ya kufanya hivyo lakini Revocatus aliendelea kuwa kimya huku akizidi kuongeza kasi ya gari yake.
Hapo Daktari akaanza kuwa na wasiwasi haraka akavua kile kitambaa alichokuwa amefungwa usoni.
Revo alifunga breki ghafula mara tu baada ya Daktari kuvua kile kitambaa.
Vumbi jingi likatimka na kupaa hewani, gari ya Revo ikiwa imesimama katikati ya daraja moja refu.
"Unajaribu ku...kufanya nini?" Daktari aliuliza huku akimtazama Revo kwa macho ya kuuliza.
Revo hakuzungumza chochote, alifungua mlango akashuka na kuzunguuka nyuma ya gari akamfungulia mlango Daktari.
"Teremka" Revo aliongea kwa sauti ya kuamrisha
"Nini?"
"Shuka kwenye gariiiii" Revo alifoka huku safari hii akichomoa bastola yake na kumnyoshea Daktari, uso wake ukiwa serious hakuonyesha hata chembe ya masihara.
"Sa.sa..wa nashuka"
Alisema Daktari kwa sauti iliyojaa kitetemeshi, huku akiteremka kwenye gari.
"Sogea nyuma"
Alisema Revo, Daktari akatii na kusogea hadi pembeni kabisa ya lile daraja
"Kwani nimekosa nini kijana, lakini si mliniita wenyewe"
"Hujui ulichokosea sio, wewe ni Daktari au mpelelezi, inakuwaje unatoa siri za mtu kwa mtu mwingine"
"Aah hapana lakini si....."
"Lakini nini, umejisahau sana dokta, Siri za madam Jane ni zake mwenyewe huwa hazitoki kirahisi hivyo, haya ruka kwenye maji ujiokoe mwenyewe"
Daktari akigeuka na kutazama nyuma yake, daraja lilikua ni refu sana lakini mbaya zaidi aliwaona mamba wakirandaranda juu ya maji, hali ilitisha mno
Daktari akageuka na kumtazama Revo huku mikono yake akiwa amenyoosha juu.
Revo akamuonyesha ishara kwa kichwa kuwa aruke huku akiwa amemnyoshea bastola.
Jasho jembamba likawa linazidi kumtoka daktari, akawa anatetemeka mwili mzima.
Mara ghafula akakimbia kwa lengo la kwenda kumvaa Revo ajiokoe mwenyewe, lakini kabla hajamfikia Revo akafyatua risasi.
Paaa!!
Daktari alihisi kitu cha moto kimepenya kifuani kwake akainama taratibu kuangalia huku damu ikimtoka mdomo.
Paaa!!
Revo akamuongeza risasi nyingine ya pili ya tatu ya nne ya tano ya sitaa, Daktari akaanguka chini.
Revo akasogea hadi pale ulipolala mwili wa daktari wakati huo simu yake ilikua ikiita.
Revo akausukuma ule mwili kwa mguu wake wa kulia, ukaanguka majini chini ya daraja huku mamba wakiupokea kwa shangwe.
Revo akapokea simu yake.
"Ndio Caren"
"Vipi umemfikisha Daktari"
"Yah hivi ndio anaingia kazini kwake"
"Asante Revo basi naomba kamchukue Yusto nimeongea naye tayari"
"Sawa dakika 7 tu nitakuwa nimefika mwambie nimkute pale nje getini"
"Powa, nisamehe bure Revo nakutumikisha kama vile nimekua bosi wako"
"Hahahah hata usijali Caren tuko pamoja"
Alisema Revo kisha akakata simu, akachungulia chini darajani akawaona wale mamba namna wanavyo ugombania vipande vya nyama ya mwili wa daktari.
Akarudi kwenye gari akaliwasha na kuondoka zake kwa kasi.
𝗜𝗧𝗔𝗘𝗡𝗗𝗘𝗟𝗘𝗔𝗔𝗔...
Simulizi hii sasa itapatikana kwa wiki mara 2 tu.
Jipatie vipande 30 vilivyosalia kwa Tsh elf 1 tu
0756862047