𝐁𝐀𝐊𝐈 𝐍𝐀 𝐌𝐈𝐌𝐈
(Stay with me)
𝐬𝐞𝐚𝐬𝐨𝐧 2
Sehemu ya..............13
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
ILIPOISHIA....
Revocatus anapata msaada kutoka kwa Caren anaemchukua na kuondoka nae, wakati huo upande wa pili bado Brandina na Yusto wanaendelea kuandamwa na vikosi vya ulinzi kutoka kwenye ngome ya madam Jane.
Wakati huo pia madam jane anajikuta kwenye wakati mgumu na mawazo mengi mara tu baada ya kukutana na Yusto.
Je, nini kitafuata?
SASA ENDELEA...
[emoji294][emoji294][emoji294]
Akiwa bado ni mtu mwenye mawazo mengi madam Jane alikaa kitandani huku akijaribu kuwaza ni nini afanye.
Tayari alishamtuma Caren ahakikishe anammaliza Zubeda lakini bado hisia zake zilimbeba mbali mno na kujikuta anamkumbuka mwanae Yusto ambae alimtelekeza angali akiwa na miezi sita tu, akaendelea na biashara yake ya ukahaba ya kujiuza, ndipo alipojikuta anaokota dodo kwa kupendwa na tajiri mark moon, lakini uwepo wa mtoto wake Yusto ukawa kikwanzo cha ndoa yake na tajiri huyo mwisho akajikuta anaachana na mark moon kwa sababu hiyo licha ya kujitahidi sana kumficha Yusto.
Madam Jane akajikuta anamchukia Zubeda na Yusto akawachukia kiasi cha kutoa agizo wauwawe, akiamini wao ndo sababu ya kuharibu bahati yake.
Madam jane alikumbuka yote haya akiwa amekaa pale kitandani, akamkumbuka hadi mtu aliyempa kazi hiyo ya kumuuwa Zubeda na Yusto kipindi hicho yeye akiwa Dubai, mtu huyo aliitwa Azizi.
Baadae Azizi akamtaarifu kuwa amefanya kazi yake ipasavyo, Zubeda amepata ajali mbaya ya gari, ajali ya kutengenezwa, amekua kichaa na hawezi kukumbuka chochote Yusto nae alikufa pale pale kwenye ajali hio.
Hivyo ndivyo alivyoelezwa na Azizi.
"Yes sikua na kosa mlistahili kufa ninyi wote mlistahili kufa, kwa nini mliharibu ndoto zangu, niwaza kuwa malkia wa Dunia nzima lakini badala yake mkanifanya niaibike na kugeuka kituko Dunia nzima, hasa wewe Zubeda wewe ambae hadi leo unaishi, pengine mwanangu hakuwa na kosa alikua ni malaika yule, lakini kwa sababu yako Zubeda kwa sababu yako nikamuua hadi mwanangu Yusto aaaah!"
Madam Jane alikua akiongea mwenyewe ndani ya kile chumba kama mwenda wazimu, akili yake haikua imetulia kabisa.
Wakati akiwaza hayo mara taswira ya yule kijana Yusto alieleta kashikashi nzito mda mfupi uliopita katika ngome yake alimjia tena akili mwake.
"Aah, nini hiki nawaza hawezi kuwa mwanangu yule, kivipi ani, mwanangu alikufa, sina mtoto mwingine zaidi ya John mimi, sinaa"
Madam Jane alijisemea huku akijaribu kuifuta taswira ya kijana huyo akilini mwake lakini ikawa ngumu, sura na sauti ya Yusto vilimganda, akajikuta anakumbuka jinsi Yusto alivyopigwa risasi mbele yake, moyo wake ukamuuma tena.
"Kwa nini naumia sasa aaaah aaaah" madam Jane alijilaumu huku akipiga piga kichwa chake kwa hasira hapo akachukua simu yake na kupiga namba aliyoi-save Osman Azizi.
Mtu aliyempa kazi miaka mingi iliyopita, kuwauwa Zubeda na Yusto.
Simu iliita mara ya kwanza bila kupokelewa, akapiga tena mara ya pili na ya tatu hapo ikapokelewa.
"Janeth, ni muda umepita tangu nione simu yako" sauti nzito ya kiume iliyojaa kitetemeshi ilisikika upande wa pili.
"Pengine unaweza ukawa umeshajua sababu ya mimi kukupigia simu" Madam Jane aliuliza.
"Nitajuaje sasa, okay let me guess, unataka gari kutoka Japan au China"
Azizi aliongea kwa kiburi, hakuwa Azizi yule aliekua akifanya kazi chini ya madam Jane miaka kama 20 iliyopita, sasa alikua ni mtu anaejitegemea mwenye pesa zake, anamiliki kampuni kubwa ya kuuza na kununua magari.
"Ni kuhusu mwanangu" madam Jane alijibu
"Mwanao, yupi, kafanyaje" Azizi aliuliza akijaribu kumuelewa madam Jane.
"Nakuja tuongee"
"Aah niko bize kwa sasa usijali nitakutafuta mwenyewe nikipata muda" alisema Azizi kisha akakata simu.
"Hallo...halloo...mjinga mmoja wewe, unanikatia mimi simu, hunijui Azizi, ole wako kama ulicheza na akili yangu"
[emoji294][emoji294][emoji294]
Upande wa pili Azizi mzee wa makamo mwenye asili ya kiarabu hivi alionekana anatabasamu mara tu baada ya kumalizia kuzungumza na Madam Jane.
"Sasa muda umewadia, muda niliousubiri zaidi ya miaka 20, sasa ni wakati wa kupiga pesa, pesa ndefuuu" alisema Azizi kisha akacheka kwa sauti tena sauti kubwa.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Madam Jane alichukua koti na mkoba wake akavibebe kisha akatoka nje ya kile chumba akateremsha ngazi na kutoka hadi nje kabisa ya lile jengo.
Akakutana na Kindoki, kiongozi wa ulinzi ndani ya ngome yake.
"Vipi" aliuliza madam Jane huku akimuangalia Kindoki usoni.
"Hatujawapata bosi, wamepotelea msituni lakini bado vijana wanaendelea kuwafuatilia" Kindoki alitoa taarifa ya namna opareshini ya kuwafuatilia Brandina na Yusto ilivyokuwa ikiendelea.
"Helkopta iko wapi"
"Ilienda huko pia kuongeza nguvu kama ulivyosema Madam"
"Mpigie rubani arudi hapa mara moja kuna sehemu nataka kwenda"
"Sawa bosi"
"Sasa hivi"
"Sawa"
Kindoki alifanya kama alivyo agizwa muda mfupi baada helkopta ilifika na kutua, madam Jane akapanda, na kuondoka.
[emoji294][emoji294][emoji294]
"Aaaiiiggghh" kelele za manung'uniko zilisikika kutoka msituni pembezoni mwa mto.
Watu wawili walionekana wamekaa chini ya mti mmoja akiwa ameuma kipande cha mti mdomoni huku akilalamika kwa maumivu na mwingine alikua akihangaika kuichomoa risasi iliyokuwa imezama kwenye bega la mwenzake kushoto, hatimae akafanikiwa kuitoa.
Walikua ni Brandina na Yusto.
Baada ya Brandina kufanikiwa kuitoa risasi iliyokua imezama kwenye bega la kushoto la Yusto, alichana kipande cha nguo yake nyepesi aliyokua amevaa ndani ya koti, akamfunga Yusto eneo alilo jeruhiwa.
"Vipi umeshaangalia kama hawatufuati tena" aliuliza Yusto
"ee hawapo tumeshawaacha mbali hawawezi tena kutuona, helkopta yao pia imerudi"
"Dah afadhali, ila Brandina ulijuaje niko huku yani umefikaje"
"Hilo sio la muhimu kwa sasa, labda nikulize wewe inakuwaje madam Jane akakuteka, mnajuana"
"Ataa, eti kwa sababu nlichoma mwanae John na mkasi"
"John yupi, yule wa chuoni, ni mtoto wa madam Jane?"
"Ee ndiyo, mimi pia nimejua leo"
Wakati wakiendelea na mazungumzo hayo Brandina aliitumia nafasi hiyo pia kumuelekeza Yusto kazi waliyokuwa wamepewa na bosi wao mark moon ya kumfuatilia huyo madam Jane.
Hapo ndipo Yusto akakumbuka zile picha alizoziona chumbani kwa madam jane, akatamani kujua zaidi.
Hapo Brandina akamueleza kila kitu anachokijua kua Madam Jane aliwahi kuwa mke wa bosi wao Mark Moon lakini ndoa yao haikudumu kwa muda mrefu wakaachana.
"Waliachana kwa shari hivyo mark moon anahisi kuwa huenda madam Jane akawa ni adui yake anaemtafuna kimya kimya ukizingatia Sasa hivi biashara zake nyingi zinaandamwa" alieleza Brandina.
"Vipi unajua nini kuhusu madam Jane huyu kwenye picha hapa unamfahamu pia"
Alisema Yusto huku akiingiza mkono mfukoni kuchukua ile picha ambayo aliichukua kwenye chumba cha madam jane.
"Mwanamke gani?" Aliuliza Brandina huku akimuangalia Yusto aliekua ameduwaa baada ya kugundua kuwa alishaidondosha ile picha.
"Aaa..eee..unajua... Sema nini madam Jane aliwahi kuwa na rafiki au ndugu yake hivi mwanamke amenaniliii yanii.. " Yusto alieleza kitu ambacho hata yeye hakuelewa.
"Sikiliza Yusto niliyokweleza mimi ndio hayo ninayoyafahamu, kumbuka kipindi wanafunga ndoa ni zamani sana pengine mimi nilikua hata sijazaliwa hayo maswali yako majibu yake tutayapata wakati tunaendelea kufanya hii kazi aliyotupa bosi" alieleza Brandina huku akivua koti lake kubwa akamvisha Yusto baada ya kubaini alikua akitetemeka kwa baridi.
"Asante" alisema Yusto huku mawazo yake yakimbeba mbali sana akaona kuna kila sababu ya kuifanya kazi hiyo kwa nguvu zote ili kujua ni vipi madam Jane alipiga picha akiwa na mama yake mlezi Zubeda.
"Yusto uko sawa?"
"Yaa niko sawa Brandina"
"Tutalala hapa hadi kesho asubuhi, angalau hali inaweza ikawa imetulia"
Alisema Brandina huku akimtazama Yusto kwa macho yaliyoregea.
"Tulale hapa?"
"Yah hawa watu wapo kila mahali bado wanatutafuta, sio salama kuondoka mapema"
"Mmh! tunalalaje sasa hapa Brandina"
"Aah jamani unauliza kama sio kamanda vile, subiri nitakuonyesha"
Alisema Brandina huku akisimama akasogea karibu na ule mto wa maji yaliyokua yakienda kwa kasi ndogo.
Akanza kuvua nguo zake mbele ya Yusto bila aibu yoyote akabaki na nguo za ndani pekee, kisha taratibu akaingia ndani ya maji kwenye ule mto.
Yusto alibaki akimtazama mwanamke huyo aliyejaaliwa kwa kila idara, akawa anawaza ni jinsi gani atakabiriana na jaribu hilo lililokua mbele yake.
"Aah! ndio usiku kucha jamani, sasa itakuwaje" aliwaza Yusto.
Je, nini kitafuata?
[emoji294][emoji294][emoji294]
Vipi kuhusu sakata jipya la madam Jane na Osman Azizi?
Osman Azizi ni nani hasa?
Vipi kuhusu Revocatus na Caren?
Nini kitatokea, ukizingatia Brandina anampenda sana Yusto?
*USIACHE KUFUATILIA,
ITAENDELEA....
0756862047