Simulizi ya ujasusi: Do not shout (Usipige kelele)

Kaka hakuna njia tofauti na whatsapp naeza ipata hii hadithi nku2mie hela un2mie...humu Pm haiwezekani au messenger Fb...
Kuna group fb ukilipia nakupa link unajiunga humo unaikuta yote mwanzo had mwisho
 
Shida nn mkuu, tumeanza wote mwanzo mpaka sasa tuko tunaelekea Mwishoni na sijaacha kupost bado unanilaumu kweli, vipi kama nikiweka intereste ya pesa mbele na kumaliza kwa wale waliolipia tu.
Hujui tuna risk sana kazi zetu kupost public kama hivi mtu anaiba na anauza vipi kama nikipost yote kwa pupa kama unavyotaka.
Tsh elf 1 ndio ikufanye kutoa lawama kama hizo.
Relax boss wangu. Fuatilia SIMULIZI hii na nyingine zote zinazoendelea nitamaliza zote mapka mwisho ila usinipangie ratiba ya kupost
Unataka kubembelezwa ama wee leta riwaya kama hutaki acha hulazimishwi
 
𝐃𝐎 𝐍𝐎𝐓 𝐒𝐇𝐎𝐔𝐓
Season 2
Sehemu ya.........18
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047.

*ILIPOISHIA...

Osman Azizi akiwa na Madam Jane, anatoa siri nyingi sana anazozifahamu, siri ambazo Madam Jane aliamini hakuna mtu anazifahamu zaidi yake.
Madam Jane anaondoka akiwa kwenye hali ngumu akihisi kuchanganyikiwa, hajui ni kwa nini Osman anafanya yote hayo na kwa sababu gani.

Upande wa pili Brandina na Yusto bado wako msituni.
Wakiwa huko Brandina anashindwa kuzuia hisia zake za mapenzi dhidi ya Yusto ambae anajikuta anaingia kwenye mtego wa mwanamke huyo.

Je, nini kitafuata?

SASA ENDELEA....
[emoji294][emoji294][emoji294]

Yusto alishtuka usingizini, akaangaza macho huku na huku ulikua ni usiku lakini ndio kunaelekea kupambazuka majira kama ya saa 11 na nusu adhuhuri, alikua amelala chini ya mti huku Brandina akiwa amejilaza juu ya kifua chake.
Wakati huo Yusto alikua amevaa boska pekee na Brandina nae alikua amevaa nguo za ndani tu yaani chupi na sidiria.

Yusto alitulia akijaribu kuvuta kumbukumbu ya kilichotokea kabla ya wao kupitiwa na usingizi mzito.

"Ooh my God, nimefanya nini mimi" Alisema Yusto huku akifumba macho na kukunja sura kwa uchungu mara tu baada ya kukumbuka kilichotokea usiku ule.

"Nisamehe bure Caren wangu" alisema Yusto, akajaribu kumtoa Brandina kifuani kwake lakini Brandina ndio kwanza akajilaza vizuri kiasi cha kumsababishia Yusto maumivu kwenye bega lake mahali alipokuwa amepigwa risasi.

Ilimbidi Yusto atulie, akawa anamuangalia Brandina ambae alionekana kuwa mwenye uchovu mwingi.
Brandina alikuwa
amefanya kila aliloliweza kumsaidia Yusto, na sasa Yusto alikuwa salama salimini kutoka kwenye mikono ya mama yake madam Jane.
Alichokifanya Brandina alistahiri kitu kikubwa hata zaidi ya kile alichohitaji kutoka kwa Yusto, ingawa alifanya kwa upendo tu.

Yusto aliutumia mda huo pia kutafakari matukio yaliyokuwa yametokea kabla ya usiku wa siku hiyo.

Hapo alijikuta anamkumbuka madam jane pamoja na ile picha aliyoipoteza.
Aliumiza kichwa sana kujaribu kuunganisha matukio lakini hakuwa na majibu kamili.
Alijikuta anamkumbuka pia mama yake mlezi Zubeda, lakini kila alipowaza kuwa yupo kwenye mikono ya Caren wasiwasi ulimuisha.

Alikumbuka maisha aliyoishi na Zubeda tangu akiwa mtoto, mahangaiko yote ambayo amekuwa akielezwa na mengine kuyashuhudia kwa macho yake, hapo ndipo Yusto alipomkumbuka mtu wa muhimu sana ambae pengine angekuwa na majibu ya maswali yake yaani Osman Azizi.
Ndio, ni Osman Azizi mume wa marehemu Asma dada yake Zubeda ambae Zubeda alikimbilia kwake kujificha na mkono wa madam Jane aliyetaka kuwauwa kipindi hicho Yusto akiwa ni mdogo sana.
Baada ya dhoruba yote kutokea Asma akafariki Zubeda akawa kichaa, Yusto yeye akalelewa na Osman Azizi hadi pale alipofikisha miaka 7 ndipo alipoondoka na kuingia mtaani.

"Ba mkubwa Azizi anaweza akanisaidia kujibu maswali kazaa huenda akawa anajua kitu, nakumbuka yeye ndo alikuwa wa kwanza kunambia Zubeda sio mamangu mzazi, anaweza akajua pia kulikua na mahusiano gani kati ya mama na madam Jane"
Yusto aliwaza akaona afanye hivyo mara tu atakapolejea chuoni.
Akiwa bado anaendelea kuwaza mara kwa mbali alisikia sauti za watu wakizungumza na mwisho akawaona wanakuja upande wao huku wakipekua pekua kwenye vichaka mikononi wakiwa na siraha zao za moto.

Yusto hakuwa na sababu ya kujiuliza mara mbili mbili moja kwa moja alijua ni watu kutoka kwenye ngome ya madam jane wanaendelea kuwatafuta.

Yusto alikurupuka akamuweka Brandina pembeni na kuanza kumtikisa taratibu.

"Brandina...brandinaa...amkaa"

"Yuustoo banaaa" Brandina aliongea kwa sauti ya manung'uniko akitamani kuendelea kulala.

"Shiii shiiii, usipige kelele amka wanakuja..."
Kabla hajakamilisha sentensi yake mara Brandina alikurupuka kwa kasi na kukaa, Sasa alikua amerudi kwenye uharisia wake kama Jasusi Brandina.

"Wako wapi" alihoji
"Wale palee.., ooh hii ni hatari wako wengi sana wanakuja, bado kidogo watatuonaa"alisema Yusto.
[emoji294][emoji294]

"Oyaaa mazee hawa wapuuzi walikua hapa hapa, unaona hii nguo itakuwa ya yule jamaa" Alisema mmoja wa wale watu huku akiinyanyua bukta ya Yusto iliyokuwa pembeni ya ule mto, akawaonyesha wenzake.

"Ni kweli pikipiki yao hii hapa" mara mwingine akadakia, wote wakakusanyika na kuizunguuka ile pikipiki, huku siraha zao zikiwa mbele, walikuwa kama watu 20 hivi.

"Hii ndio ile pikipiki iliyopaa juu ya ukuta kweli, mbona ya kawaida" alihuoji mmoja wao

"Kwa hiyo unataka kusemaje, hebu tugawanyike chapu kila mtu upande wake, tuwe makini, mliwaona wale watu ni hatari sawa"
"Sawa jomba"
[emoji294][emoji294]

"Hatuna muda Brandina tuondoke"
Alisema Yusto huku akivaa shati lake haraka haraka bila kujali lilikuwa na damu iliyokauka.

"Koti langu lile kuna simu, itabidi nilifuate"
"Aah Brandina, kumbe ulikua na simu na hukusema, kwa nini sasa usingeomba msaada kwa Simigo tangu jana"

"Nilitaka kuwa na wewe usiku huu," alisema Brandina kisha akamkonyeza Yusto.

"Acha utoto basi huoni kama tuko kwenye hatari"
"Acha woga wewe hawana lolote hawa, kwa hiyo tunaondoka tukiwa hivi" Brandina alihoji huku akijiangalia.
Alikuwa amevaa chupi na sidiria pekee yake, yusto yeye alivaa shati na boksa basi.

"Sasa nguo ziko pale mbele tunazichukuaje"
"Ngoja mi nataka koti tu koti basi, muhimu niipate simu subiri hapa nakujaa" alisema Brandina kishaa akaanza kunyata akiwa amechuchumaa.
Yusto akawa anamtazama huku na yeye akijaribu kuangaza macho yake huku na huku akaona kipande cha mti mkavu, akakiokota na kukishikiria vizuri tayari kwa lolote.

Brandina alisogea hadi nyuma ya mti mmoja mkubwa, akalivuta koti lake taratibu kwa mguu wake wa kulia na baadae akalikamata mkononi.

"Hey, wewe nani, jamani huyu hapa mmoja, wewe simama nakupiga ri...."
Mtu mmoja alifanikiwa kumuona Brandina akapaza sauti kuwataarifu wenzake lakini kabla hajamaliza sentesi yake mara kipande cha mti mkavu kilitua kwenye paji lake la uso, akaanguka chini huku akigugumia kwa maumivu makali.

Hapo Brandina na Yusto aliyerusha ule mti wakapata mwanya, wakaanza kukimbia huku nyuma yao wakikimbizwa na wale watu kutoka ngome ya madam jane.
Wakawa wanafyatua risasi mara kadhaa zilizo wakosa kosa Yusto na Brandina ambao walikua wanaelewa namna ya kukimbia na kumkwepa mtu anaekukimbiza akiwa na siraha, wote walikua vizuri hakuna hata risasi moja iliyowapata.

Waliendelea kukimbia kwa kasi huku mmoja akiwa amevaa boksa na shati pekee, mwingine amevaa chupi,sidiria na koti mkononi.

Je nini kitafuata?

Yusto na jasusi Brandina watatoka salama safari hii"
Vipi kuhusu sakata la Osman Azizi na Madam Jane?

ITAENDELEA....
 
𝐃𝐎 𝐍𝐎𝐓 𝐒𝐇𝐎𝐔𝐓
Season 2

Sehemu ya.................19

Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA....

Risasi zikawa zinawakosakosa Yusto na Brandina ambao walikua wanaelewa namna ya kukimbia na kumkwepa mtu anaekukimbiza akiwa na siraha, hakuna hata risasi moja iliyowapata.

Waliendelea kukimbia kwa kasi huku mmoja akiwa amevaa boksa na shati pekee, mwingine amevaa chupi,sidiria na koti mkononi.

Je nini kitafuata?

SASA ENDELEA....

Yusto na Brandina bado walikuwa wakiendelea kukimbia.

"Tumesha waacha mbali Yusto hebu punguza kasi basi mimi nachoka"

"Mbona vingine hukuchoka"

"Vingine vinini hahahaha"
"Utajua"

"Yusto kweli mimi nimechoka jamani"

"Twende bana, umesahauu kuwa wana helkopta hawa jamaa"

"Sawa sasa inabidi tuvuke upande wa pili wa huu mto" alisema Brandina

"Kwa nini tuvuke"

"Huko mbele, upande wa kulia ndio kuna barabara, nimeshamuomba msaada simigo anakuja kutuchukua"

"Kivipi, mbona mda wote tunakimbia, alafu atapajuaje hapa"

"Kuna programu maalum ipo kwenye simu zetu sisi majasusi, ukibonyeza tu mara moja hii batani inapiga alarm kwa wenzangu kuwapa taarifa kuwa nipo kwenye matatizo nahitaji msaada, inaonyesha hadi sehemu nilipo"

"Duh"

"Ndo hivyo"

"Sasa kwa nini hukufanya hivyo tangu jana"

"Kwani si nimekwambia sababu kuwa nilitaka kuwa na wewe usiku wote"

"Hauko serious hata kidogo Brandina, haya tunavukia wapi"

"Tusogee kwa pale mbele naona nipafupi" Alisema Brandina.

"Umeonaje au ni hiyo simu yako tena"

"Aah hapana we twende"

Taratibu waliingia ndani ya maji wakatembea kwa haraka hadi walipovuka upande wa pili, kwa bahati nzuri hakukuwa na kina kirefu sana, maji yaliwafika kwenye mabega hadi walipovuka upande wa pili salama.

"Mmh Brandina embu angalia kule" alisema Yusto huku akinyoosha kidole kwenye ule mto mara tu baada ya wao kuvuka upande wa pili.

"Nini wanakuja au?" Brandina aliuliza huku akifuata uelekeo wa kidole cha Yusto hapo akawaona mamba wakubwa wawili wakirandaranda ndani ya maji katika ule mto.

"Mungu wangu! ukisikia bahati ndio hii, hivi kwa nini tulivuka bila hata kuwaza"
Alisema Brandina huku akishika mdomo wake kwa mshangao.

" Haikuwa bahati yao, tuondoke basi, tunaelekea upande upi hapa"

"Twende huku kuna barabara mita kadhaa mbele, Simigo tutakutana nae hapa"
Alisema Brandina akimuonyesha Yusto ramani iliyokuwa kwenye simu yake.
"Poa"

Wakaendelea kukimbiaa.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Gari mbili nyeusi aina ya Noah , zilifunga breki kali katikati ya msitu maarufu kama msitu wa Zengo,,,
Wakashuka kikosi cha watu kama 8 waliokuwa wamevalia mavazi yenye rangi nyeusi juu mpaka chini, sura zao zikiwa zimefunikwa na vitambaa vyeusi pia.
Kila mmoja alikua na bunduki mkono, wakaweka Target kila mahali kuzunguuka gari zao.

Haukupita muda mara Brandina na Yusto walichomoza kutokea msituni huku wakikimbia, bila kuuliza waliingia ndani ya gari moja iliyokuwa mbele wakaa kwenye siti za nyuma na kutulia huku wakihema kwa nguvu, wale watu nao wakarudi kwenye gari na kufunga mlango.

Jasusi Simigo ambae ndiye aliyekuwa amekaa kwenye usukani ndani ya lile gari waliloingia Brandina na Yusto akawa akawatazama kwa zamu mmoja baada ya mwingine kupitia kioo cha mbele.

"Kuna nini Brandina, mbona hatuoni chochote halafu mbona mko uchi"
Simigo aliuliza.

"Nani yuko uchi" Brandina alidakia huku akiweka koti lake vizuri ambalo alilivaa punde tu baada ya kuvuka ule mto.

"Ndo nini sasa hivyo, unajua umetushtua sana, umepiga alarm mara mbili mfurulizo nikajua mpo kwenye shida kubwa, unajua tumetumia nguvu kiasi gani hadi kufika hapa" simigo aliongea kwa ukali kidogo.

"Simigo tunaendelea kupoteza muda hapa, hebu tuondoke kwanza nitakueleza kila kitu mbele acha kuniuliza maswali yasiyo na lazima , wanakuja na wakitukuta hapa itakuwa ni habari nyingine, halafu huoni kama shati la Yusto lina damu"
Alieleza Brandina hapo Simigo aligeuka kuhakikisha, ilikua ni kweli. Haraka akatoa ishara kwa mmoja wa watu wake aliokuja nao, yule mtu akafungua sehemu akatoa kijibegi cha huduma ya kwanza akaanza kumuhudumia Yusto.
Bila kupoteza muda Simigo akawasha gari na kuondoka kwa kasi, lakini bado alikua akiwaangaalia Brandina na Yusto kwa zamu kupitia kioo cha mbele, akawa anajiuliza maswali yasiyo na majibu.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Majira ya saa 12 jioni, katika kambi ndogo ya akina Caren palikua na ukimya sana. Zubeda mwanamke kichaa ambae ni mama mlezi wa Yusto yeye pekee ndiye aliyekuwepo ndani ya jengo hilo. Caren hakuwepo wala Revocatus aliyeachiwa jukumu la kumuangalia nae pia hakuwepo.

"Sio rahisi, sio rahisi hata kidogo, lazima arushe moja kwa moja hadi kwangu"

Zubeda aliongea maneno ambayo ni yeye pekee ndiye aliyekua akiyaelewa, aliinuka pale kitandani taratibu akaanza kutembea kuelekea mlangoni.

"Haipo najua watakuwa wamechukua baiskeli yangu, alaah! nitawauwa wote" aliongea Zubeda.
Mlango ulikuwa wazi akatoka, akatembea tena hadi ulipokuwa mlango wa kutoka nje kabisa ya jengo hilo nao pia ulikuwa wazi, Zubeda akatoka nje akaendelea kutembea na mwisho akatokomea msituni, hakuna mtu aliyemuona.
[emoji294][emoji294][emoji294]

CHUONI...

Sophia alikuwa amekaa kwenye viti ambavyo hukaa mashabiki wanaoangalia mpira wa kikapu katika kiwanja kilichokuwa kimejengwa kwa ustadi mkubwa ndani ya chuo hicho cha Mark Moon.
Alikua peke yake anasikiliza mziki kupitia simu yake ndogo. Hali yake ya kiafya wakati huu ilikuwa imeimalika kabisa licha ya kuwa na bandaji kubwa kichwani.

Kwa mbali alionekana Caren anakuja, akasogea hadi pale alipokuwa Sophia, akakaa pembeni yake.

"Enhe vipi umepata chochote" aliuliza Sophia.

"Aah wapi shoga angu, huyu mwanaume atanipa wazimu sasa, sijui hata yuko wapi Mungu wangu" alisema Caren

"Lakini una uhakika uliwasiliana nae?"
"Sophy niamini nachokwambia Yusto alikuwa sawa kabisa aliniaga akasema anarudi sio mda"
"Alikuaga wapi wakati ninyi wote hamkuwepo tangu asubuhi, wewe ndio kwanza umerudi sio mda"
"Aah bana kuna mahali tulikuwa wote, nikamuacha akasema atanikuta chuoni" Caren alidanganya.
"Aah shoga angu unanidanganya, hata macho yako yanaonyesha wewe ni muongo, yaani umeninyang'anya mwanaume wangu halafu hata humchungi hahaha unahatari wewe"
Alisema Sophia kisha wote wakacheka kwa pamoja.
"Hapana bana atakuwa hataki kusikia makelele ya kampeni kipindi hiki cha uchaguzi" Caren aliongea
"Eeee! halafu kweli na hivi hapatani kabisa na John mgombea wa Urais, hahahaha"

Hakukuwa na ugomvi tena kati ya Caren na Sophia. Ilifika mahali alimbidi Sophia akubali matokeo tu, hasa baada ya kugundua kuwa Caren nae alikuwa akimpenda Yusto kupita kawaida, istoshe Caren alitoa damu kuyaokoa maisha yake hakuona sababu tena ya kuendelea kuweka chuki baina yao.

"Yusto hana hisia zozote na Mimi, ananiheshimu tu kama mdogo wake, Caren anampenda Yusto, Yusto nae anampenda Caren, licha ya kugundua kuwa Caren ana mchumba na mtoto lakini bado hajataka kumuacha" aliwaza Sophia kipindi kile akiwa hospitalini baada ya kuumizwa na Caren aliyemkuta chumbani kwa Yusto.
Sophia bado alikuwa akiamini kile alichokiona na kukisikia kule ARENA HOTEL, baada ya kuona Yusto bado anaendelea kuwa karibu na Caren, alikata tamaa kabisa akiamini hakuna kitakacho badilika Japo roho ilimuuma lakini hayo ndiyo yalikuwa maamuzi yake ya mwisho.

"Nacheka lakini ukweli nina wasiwasi sana sophy, vipi Frank rafiki ake Yusto umemuliza" aliuliza Caren

"Ee halafu huyo hapo amekuja"

Caren aligeuka, uso kwa uso akagonganisha macho na Frank.

"Habari zenu jamini, warembo wa chuo" Frank alisalimia
"Nzuri, za kwako" Caren na Sophia wakaitikia kwa pamoja.

"Fresh aisee huyu jamaa yenu sijampata kwa kweli sielewi hata kaenda wapi" alisema Frank huku akijiandaa kukaa pembeni ya Sophia lakini mara simu yake ikaita, akatazama jina la mpigaji.

'SIMIGO'

Frank alipata kigugumizi cha kupokea ile simu, alipogeuka akakuta Caren amemkazia macho, ikambidi asogee pembeni kisha akapokea ile simu.

"Hallo"
"Eee we dogo uko wapi, hebu njoo na suruali na shati na ile track suti ya njano niko hapa na akina Yusto utaona ile gari yetu nyeusi, haraka" Simigo alisikika upande wa pili kisha akakata simu.

Frank alishikwa na butwaa kwa sekunde kadhaa.

"Vipi kwema"
Mara alisikia sauti ya mtu nyuma yake akiuliza. Frank aligeuka haraka kutazama, uso kwa uso akakutanisha macho tena na Caren aliyekuwa amesimama nyuma yake, hata hakujua kafika saa ngapi.

"Ca..car...caren" Frank aliita akionyesha kutokujiamini kabisa, ilikuwa ni rahisi kwa Caren kugundua kuna kitu hakipo sawa.

Je, nini kitafuata?

Osman Azizi anataka nini kutoka kwa Madam Jane?
Madam Jane atafanya nini?
Vipi kuhusu Zubeda?

USIACHE KUFUATILIA SEHEMU ZILIZOBAKIA KUMALIZIA SIMULIZI HII...
 
𝐃𝐎 𝐍𝐎𝐓 𝐒𝐇𝐎𝐔𝐓
𝐬𝐞𝐚𝐬𝐨𝐧 2

Mtunzi: Saul david
WhatsApp: 0756862047
Email: saulstewarty@gmail.com

ILIPOSHIA...
uso kwa uso Frabk akakutanisha macho tena na Caren aliyekuwa amesimama nyuma yake, hata hakujua kafika saa ngapi.

"Ca..car...caren" Frank aliita akionyesha kutokujiamini kabisa, ilikuwa ni rahisi kwa Caren kugundua kuna kitu hakipo sawa.

Je, nini kitafuata?

SASA ENDELEA...
" Vipi kuna shida" aliuliza Caren
"Aah hamna kunu jamaa yangu mmoja kanipigia nilimpa taarifa ya kupotea Yusto" alijibu Frank
"Ee kasemaje, amenuona?"
"Aa..ee hapana amedai alikuwa nae kama masaa matatu hivi yamepita" Frank alidanganya kiasi cha kumfanya Caren azidi kumtilia mashaka, masaa matatu yaliyopita anakumbuka alikua na Revocatus kule msitu ambae alimthibitishia kuwa Yusto alikuwa ametekwa.

"Aah sawa" Caren alijibu akajifanya kama vile hajahisi chochote.

Mwisho Frank aliondoka kuelekea bwenini katika chumba anachoishi, akachukua zile nguo alizoagizwa na Simigo kisha akatoka na kufunga mlango.

Akiwa bado mlangoni alihisi ni kama kuna mtu alikuwa kwenye kona moja ya jengo hilo akimfuatilia.
Frank akawa makini zaidi kwani hakutakiwa mtu yeyote ajue uhusiano uliopo kati yake yeye na Yusto dhidi ya upande wa pili wa Simigo na wenzake ambao walikuwa wakitambulika kama wapishi wapya wa chuo tu.

Frank alitembea kwa tahadhali huku akigeuka nyuma mara kadhaa hadi pale alipotoka nje kabisa ya chuo.
Aliliona lile gari aliloelekezwa akaingia upesi na kufunga mlango. Ndani aliwakuta Yusto, jasusi Brandina na jasusi Simigo pekee.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Caren ambae ndie aliekuwa akimfuatilia Frank kwa siri alishindwa kuendelea na zoezi hilo mara tu baada ya kubaini kuwa tayari Frank alishahisi kuwa anafuatiliwa.
Akasubiri mpaka atoke nje kabisa ya chuo kisha na yeye akasogea hadi getini. Kwa bahati mbaya hakuweza kumuona tena Frank.

"Anaficha nini huyu?" Caren alijiuliza wakati akiangaza macho huku na huku bila mafanikio, hakujua Frank ameelekea wapi, wala hakuwaza kuhusu gari aliyoingia Frank ambayo ilikuwa imesimama pembeni ya barabara hatua kadhaa kutoka pale alipokuwa.
[emoji294][emoji294][emoji294]

"Vipi ulimwambia Caren kuhusu Yusto?" Simigo aliyekuwa mbele kama dereva aliuliza baada ya kumuona Caren akihangaika pale mbele yao.

Ilikuwa ni kauli iliyomshtua Yusto ambae wakati huo yeye na Brandina walikuwa wanavaa zile nguo walizoletewa na Frank.

"Unaniuliza mimi?" Aliuliza Frank
"Ndiyo wewe"
"Aah hapana lakini tulikua wote wakati unapiga simu, kwani vipi?"
"Yule pale naona ni kama kuna mtu anamtafuta"
"Yuko wapi" Yusto na Frank walihoji kwa pamoja kisha wote waangalia mbele kule alipokuwa akiangalia Simigo.
Walimuona Caren akipiga hatua kwenda na kurudi, moyo wake ulikuwa haujatulia kabisa bado alikuwa na wasiwasi mkubwa dhidi ya mpenzi wake Yusto hadi dakika hiyo alikuwa hajui mahali alipo.
Alichukua simu yake na kuiweka sikioni mara kadhaa akijaribu kumpigia Yusto lakini majibu yakawa ni yale yale Yusto hapatikani.

Yusto alimtazama Caren kwa macho yaliyojaa huruma, alijua vema kuwa Caren alikuwa anapitia ile hali yote kwa sababu yake.
Brandina alimtazama Yusto usoni akaona kabisa ni kwa namna gani moyo wa mwanaume huyo ulikuwa umezama mazima kwa Caren.

"Kabla hatujashuka kuna mambo nataka tuzungumze sisi wanne, lakini kabla ya yote nataka kujua nini kimetokea, nimeona hilo jeraha la Yusto ni la risasi, kulikuwa na nini, eti Brandina?" aliuliza Simigo, wakati huo walimuona Caren akiondoka kurudi ndani ya chuo.

Brandina alieleza mwanzo mpaka mwisho namna Yusto alivyotekwa pale nje ya chuo akamfuatilia hadi msituni katika ngome ya madam Jane na baadae kufanikiwa kumuokowa.

"Sasa kwa nini hukutupa taarifa mapema Brandina huoni kama mmehatarisha maisha yenu" aliuliza Simigo.

"Hata sikuwaza kama mambo yangekuwa mazito hivi, mwanzo nilijua ni vibaka tu"

"Sawa, kwa hiyo chanzo cha Yusto kutekwa ni kwa sababu ya ugomvi wake na John, mbona haiingi akilini huyu mama ziko timamu kweli kichwani" aliuliza simigo huku akitabasamu, kisha akaendelea kuzungumza...
"Atakuwa anampenda sana mwanae ndio maana, halafu nimeambiwa na bosi Mark Moon kuwa wewe na Yusto mtakuwa na kazi mpya kuanzia sasa ya kumfuatilia huyo madam Jane nafikiri huu utakuwa ni mwanzo wenu mzuri"
Alisema simigo hali akiwatazama Yusto na Brandina kwa zamu.
Wakati wakizungumza hayo, Frank alionekana akiwa bize na simu yake, akawa anaandika ujumbe huu kwenda namba ambayo haikuwa na jina.

"OYA MAZEE, YUSTO KARUDI ULE MPANGO WETU UENDELEE BASI"

Frank aliutuma ujumbe huo kisha akaendelea kusikiliza maelezo ya Simigo, hakuna mtu aliyemshtukia.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Upande wa pili
Baada ya madam Jane kutoka kuonana na Osman Azizi, hakwenda nyumbani alipitiliza moja kwa moja hadi ofisini kwake huku akijaribu kuituliza akili yake.
Aliwasiliana na watu wake wote wa karibu anaowaamini akawataka wafike ofisini kwake mara moja. Azizi alikuwa amemchanganya sio kidogo, ilikuwa ni lazima achukue hatua madhubuti kukabiliana nae, japo ki uharisia hakujua ni wapi pa kuanzia kwani Azizi alikuwa amemshika pabaya.

Aliingia ofisini kwake akatulia na kujaribu kuyatafakari matukio yaliyotokea siku hiyo. Suala ambalo lilizidi kumchanganya ilikuwa ni ile taarifa ya kwamba mtoto wake Yusto yupo hai, huu ndio ulikuwa mtihani mkubwa kwake pengine kuliko hata vile vitisho vya Osman Azizi, alijali sana kuhusu Yusto.

Wakati akiwaza hayo, madam Jane alijikuta anamkumbuka pia yule kijana Yusto aliyeleta kashikashi nzito katika ngome yake ya siri kule msituni na hadi dakika hiyo vijana wake hawakuwa wamempata.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Hatimae wale watu watatu muhimu aliowaita madam Jane walifika ofisini kwake.
Dr Givan, Msigwa na Magdarena Masebo, hawa walikuwa ni watu walioaminiwa sana na madam Jane, walizijua siri nyingi sana za mama huyu, wao ndio waliokuwa wakisuka na kupanga mipango mbalimbali wakishirikiana na bosi wao madam Jane.

Baada ya kufungua kikao madam jane aliwaeleza kwa kifupi yale yaliyotokea siku hiyo, kuanzia sakata la Yusto hadi lile la Azizi.

"Madam hisia zangu zinaniambia lazima Azizi atakuwa alishapandikiza watu wake miongoni mwetu, haiwezekani hata kidogo akayafahamu mambo yote haya kwa urahisi namna hii, mimi naona jambo la kwanza ni kuwatafuta kwanza wasaliti, tukiwapata tutawabana na wao ndio watatupa mwanga namna ya kupambana na Azizi na kisha kumpata Yusto" alisema Magdarena.

"Uko sahihi Magdarena, lakini kipaombele changu kwanza nimpate mwanangu Yusto, nimfahamu kwanza, Azizi atanisumbua sana kupitia Yusto inabidi nicheze na akili yake, tena mambo haya inatakiwa tuyafanye kwa siri kubwa kwa sababu tayari tumejua kuna wasaliti kati yetu"

"Sawa bosi lakini mi nafikiri tungefanya kama Magdarena alivyoeleza, tuwatafute wasaliti kwanza wao ndio wataturahisishia yote pamoja na hilo la kumpata Yusto" Msigwa aliunga mkono hoja ya Magdarena.

"Nesema hivyo kwa sababu wakati naongea na Azizi leo alisema huenda nikawa tayari nimekutana na Yusto bila kujua ni mwanangu, hii inaonyesha wazi huenda kweli nimeshakutana na yusto,
Yule kijana aliyeleta shida kambini kwangu nahisi anaweza kuwa ndiye Yusto mwenyewe, yaani mwanangu, hata jina lake ni Yusto nahitaji kupata vipimo vya DNA haraka iwezekanavyo, Dr. Givan"

"Yes madam, nimekuelewa tatizo hamna, nitashiriki na Caren alete sample ya Justo today, then nitatowa majibu immediately" alisema Dr Givan, mzungu ambae kiswahili kilionekana kumsumbua.

"Hapana Caren nimempa kazi nyingine ngumu, hebu tafuta vijana waingie mle chuoni walete hiyo sampuli unayo ihitaji kwa ajili ya kupima vinasaba"

"No problem"
" Kwa hiyo mapaka Sasa Caren hajafanikiwa kumuuwa Zubeda" alihoji Msigwa.

"Hata mimi nashangaa mlinihakikishia kwamba ni binti mzuri anaeweza kazi sasa anachukua vipi mda mrefu kiasi hiki, lakini tushughulike na hili la Yusto kwanza, baada ya hapo tutapanga nini kifuate, kuanzia sasa na kuendelea nahitaji muwe makini kupita kawaida, sitaki Azizi ajue nini nafanya sawa sawa"
Madam Jane alisistiza tena.

"Swali lingine la muhimu, tuna uhakika gani kama Yusto atarudi chuoni, vipi kama lile tukio la kutekwa likawa limemtisha akaamuwa kuondoka" aliuliza Magdarena.

"Aah uko sahihi, ila nina asilimia kama 70 Yusto atarudi chuoni, ni kijana mwenye nguvu anajiamini sizani kama anaweza kutishika kiasi hiki, tayari anajua nilimteka kwa sababu gani, tuliongea tukayamaliza atarudi tu" madam Jane alieleza, akionekana kuisoma vizuri saikolojia ya Yusto kwa ule mda mfupi waliokuwa wote.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Nusu saa baadae Yusto akiwa ameongozana na Frank rafiki yake aliingia chumbani kwake, chumba ambacho alikitelekeza kwa siku mbili mfurulizo kutona na mikiki mikiki ya hapa na pale, hatimae alikuwa amerejea.

"Vipi unaenda wapi mbona hukai" Yusto aliuliza baada ya kuona Frank ni kama anataka kuondoka.

"Ah naona utakuwa umechoka, oga kwanza upumzike mimi nitakuja baadae" Frank aliongea kwa unyonge

"Aah unajua nini Frank mshikaji wangu, najua hujapenda jinsi navyofanya mambo yangu kimya kimya bila kuk...."

Aliongea Yusto lakini kabla hajamalizia Frank akadakia.

"Najua, si nimemsikia Brandina wakati anaeleza kasema ulitekwa ama kunakingine umefanya sikijui? usijali mi niko poa" alisema Frank, akawasha taa kisha akafungua mlango na kuondoka zake.

Yusto alibaki ameduwaa kwa sekunde kadhaa, akajua wazi kabisa kuwa Frank alikuwa amekasirika.

"Huwezi jua Frank, nayopitia mimi ni makubwa mno sitaki nikuingize kwenye matatizo"
Yusto alijisemea mwenyewe kisha akili na mawazo yake yote yakahamia kwa Caren, alikuwa amemkumbuka sana mwanamke huyo, alijikuta anapata shauku kubwa ya kumuona.

Haraka aliingia bafuni akaoga kisha, akavaa nguo upesi upesi.

Alichukua kitabu chake cha kumbukumbu kisha akaandika kwa kifupi.

.... Madam Jane ... picha na Zubeda .... ndoa na bosi mark moon ... Osman Azizi ... John mtoto wa madam Jane ... zubeda na mtoto mchanga ... kufuatiliawa....

Baada ya kuandika hayo Yusto alifunika kitabu chake kisha akakitupia kitandani, alifanya hivyo ili kutunza kumbukumbu juu ya suala la vitu ambavyo alitakiwa kuvifuatilia kiundani sana lakini hakuwa na muda ilikuwa ni lazima kwanza aonane na Caren ndipo mambo mengine yaendelee.

Akiwa anaelekea mlangoni mara alisikia sauti ya mwanamke akipiga kelele nje ya chumba chake.

"Yusto ... Yusto... Yusto...anakufa, wahi kimbia Yusto...."

Kelele hizo zilimfanya Yusto kufungua mlango kwa kasi akatoka nje.

"Kuna nini, Anna vipi?" Aliuliza Yusto huku akimtazama mwanamke huyo (Anna) ambae alikuwa anasoma nae darasa moja.

"Frank, frank kapigwa na shoti ya umeme" alieleza yule mwanamke.

"Nini" Yusto alitahamaki

"Wahi kamsaidie, atakufaa"
"Yuko wapiiiiiii..."
"Kuleee"
"Ukumbini, ukumbini kule"
Kabla Anna hajamalizia maelezo hayo tayari Yusto alikuwa amekimbia kuelekea ulipokuwa ukumbi mkubwa wa chuo cha mark moon.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Caren alikuwa amejilaza kitandani ndani ya chumba chake, akili yake ikiwa imehama kabisa huku hofu ya kupotea kwa Yusto ikizidi kumtawala.

"Nitakaa kusuburi hadi saa ngapi"
Alisema Caren, akakurupuka na kukaa kitandani lakini kabla hajafanya lolote mara alisikia mtu akigonga mlango wa chumba chake kwa nguvu.

"Naniii" Caren alifoka
"We umejifungia humo, hujasikia kinachoendelea huko nje"

"Aah! kumbe ni wewe Taby, kuna nini kwani"

"Kuna watu wamepigwa na shoti ya umeme huko ukumbini, yule kaka handsome Yusto yuko hoi huko" alieleza yule dada, akiwa amesimama nje usawa wa mlango wa chumba cha Caren.
kufumba na kufumbua alimuona Caren akitoka kama mshare nje ya chumba chake, akakimbia na kuteremka ngazi kwa kasi bila hata kuzungumza chochote na taby.

"Eeh jamani taratibu basi we dada, unawahi hivyo kwani wewe umekuwa tanesco hahahha mapenzi bana, mbona mimi sijawahi penda au kupendwa hivi jamani, ajitokeze kijana mmoja basi hahaha" alisema Taby huku akiufunga mlango wa chumba cha Caren na funguo kisha akaondoka.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Yusto alifika na kuingia ukumbini moja kwa moja.

"Frank, Frank, uko wapi" Yusto aliita huku akitembea na kuangaza macho yake kila upande, ukumbi ulikuwa ni mtupu, hakukuwa na dalili ya kuwepo mtu mle ndani.

Yusto alikuwa amefika katikati ya ukumbi huo ambao ulikuwa mkubwa sana, ulikuwa na sehemu za kukaa juu na chini kama ghorofa vile, ulikuwa ni ukumbu uliojengwa kisasa.
Taratibu alianza kuingiwa na wasiwasi kwani ndani ya ukumbi huo kulikuwa giza kiasi, taa zilikuwa zimezimwa zote.

"Frank..." Yusto aliita, lakini kimya.

Mara ghafula taa zilikuwa kwa pamojaa...

"Sapraiiiiiiiiiiiizi"

kelele za wanafunzi wa kike na wa kiume zilisikika na hapo wakajitokeza kutoka kona tofauti tofauti za ukumbi huo.

[emoji445] _Happy birthday to you
Happy birthday to you
Happy birthday dear Yusto
Happy birthday to you_ [emoji445]

Mamia ya wanafunzi walijitokeza huku wakiimba kwa nguvu kelele zilizopaa na kupasu anga la chuo cha Mark Moon.
Ilikuwa ni siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Yusto, sherehe ambayo ilikuwa ifanyike siku moja jana yake lakini ikashindikana kutokana na Yusto kutokuwepo chuoni hivyo wakaamua kumsubiri hadi atakaporudi.

Taratibu zote hizi zilikuwa zikiongozwa na Frank rafiki wa karibu wa Yusto pamoja na marafiki wengine wa Yusto, walifanya maandalizi yote hadi siku ya jana yake lakini kwa bahati mbaya Yusto hakuwepo chuoni siku hiyo.
Taarifa za sherehe ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Yusto (birthday) zilisambaa kwa kasi sana chuoni hapo. Watu wengi walikuwa wakimpenda Yusto hivyo wakaungana na akina Frank kuhakikisha wanamfanyia 'suprise' ya viwango.

"Jamani naombeni utulivu tafadhali, kabla hatujaendelea kwenye hatua nyingine ya kukata keki kuna sapraizi nyingine tunataka kuifanya kwa ajili ya kaka yetu hapa Yusto kisha tutaendelea" alisema dada mmoja aliekuwa ameandaliwa kama mshereheshaji.
Ukimya ukatawala na taa zikazimwa tena.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Caren alionekana anakimbia kwa kwa kasi kuelekea ukumbini, taarifa alizopewa kuhusu Yusto kupigwa na shoti ya umeme zilimshtua sana. Njiani alikuwa akimuomba Mungu amnusuru mwanaume huyo ambae alikuwa akimpenda kuliko kitu kingine chochote.

Kelele alizokuwa akizisikia kutoka ukumbini zilitoweka ghafula, kukawa kimya, Caren alishindwa kuelewa ni nini kinaendelea, hofu na wasiwasi vikamzidia. Alitembea taratibu kuingia ukumbini akawa anaangaza macho huku na huku.

Ingawa kulikuwa na giza kiasi lakini kwa uzoefu wa Caren alipata hisia kuwa kuna watu mle ndani.

"Nini kinaendelea, Yusto yuko wapi, au ni mtego...."
Haya ndiyo mawazo yaliyopita kwenye kichwa cha Caren, akajipapasa kiunoni,kwa bahati mbaya au nzuri kwa upande mwingine, hakuwa amebeba bastola yake.

Mara taa ziliwashwa tena hapo ndipo Caren aliweza kuwaona mamia ya wanafunzi waliokua wamekusanyika ndani ya ukumbi huo.

"Hatimaeee birthday giiiiirl amekujaaaaaa" yule dada mshereheshaji aliongea kwa mbwembwe, hapo ukumbi mzima ukaripuka kwa shangwe na wimbo wa birthday ukaanza kuimbwa upya.

Caren alipotupa macho yake mbele hakuamini alichokiona, Yusto alikuwa amesimama mbele yake anamtazama huku akiwa ameachia tabasamu mwanana.

"Yustoo.." Caren aliita kwa sauti ya chini huku akishika mdomo wake kwa mshangao, hapo akashindwa kujizuia akakimbia na kwenda kumkumbatia Yusto kwa nguvu sana.
Shangwe, makofi nderemo na vifijo vikasikika tena wakati huo Yusto na Caren wakiwa wamekumbatiana kwa hisia kali sana.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Wakati sherehe hiyo ikiendelea ndani ya chuo cha Mark Moon, nje ya geti lilipaki gari moja la kifahari, vijana watatu wakashuka na kuingia ndani ya chuo hicho bila wasiwasi wowote kama vile wanafunzi wanaosoma chuo hicho. la hasha hawa walikuwa ni vijana kutoka kwa Madam Jane waliotumwa kuja kuchukua sampuli yoyote kutoka kwa Yusto ambayo itatumika kufanya kipimo cha vinasaba yaani DNA.
Madam Jane alitaka kuthibitisha kwanza kama Yusto ni mtoto wake au laa...

ITAENDELEA.....

Njoo WhatsApp malizia vipande 19 vilivyobaki kwa tsh Elf 1 tu...0756862047
 
Hatar sana mkuu uko vzur. Endelea kushusha vitu
 
USIACHE KUFUATILIA SIMULIZI YANGU MPYA

THE MODERN WAR-(Vita ya kisasa)
Ipo WhatsApp, Facebook na Jamii Forum pia.

0756862847
FB_IMG_1664201403654.jpg
 
Back
Top Bottom