Simulizi ya ujasusi: Do not shout (Usipige kelele)

Simulizi ya ujasusi: Do not shout (Usipige kelele)

πƒπŽ ππŽπ“ π’π‡πŽπ”π“

Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047


ILIPOISHIA....
Wakati sherehe hiyo ikiendelea ndani ya chuo cha Mark Moon, nje ya geti lilipaki gari moja la kifahari, vijana watatu wakashuka na kuingia ndani ya chuo hicho bila wasiwasi wowote kama vile wanafunzi wanaosoma chuo hicho. la hasha, hawa walikuwa ni vijana kutoka kwa Madam Jane waliotuma kuja kuchukua sampuli yoyote kutoka kwa Yusto ambayo itatumika kufanya kipimo cha vinasaba yaani DNA.
Madam Jane alitaka kuthibitisha kwanza kama Yusto ni mtoto wake au laa...



SASA ENDELEA...
[emoji294][emoji294][emoji294]
Yusto na Caren walikumbatiana kwa zaidi ya dakika 3, hakika kila mmoja alionekana amemkumbuka mwenzake kwa kiwango kikubwa.

Tukio hilo liliteka hisia za wanafunzi wengi waliokuwa wamehudhulia sherehe hiyo. Kwa macho ya kawaida tu kila mtu aliona wazi kuwa Yusto na Caren walikuwa wakipendana sana, haikuwa na sababu ya kujiuliza mara mbili mbili.

"Yusto baba"
"Naam Caren wangu"
"Kwa nini umenifanyia hivi kwa nini lakini"
"Nisamehe mpenzi wangu, nitakueleza kila kitu baadae"
"Kwa hiyo wewe ndio umeandaa hii sherehe"

"Hapana hata sijui ni nani, nahisi ni Frank na marafiki zangu wengine, hata sikuwa nakumbuka siku yangu ya kuzaliwa"

"Hahaha nilijua tu, nafurahi kukuona uko salama mpenzi"

"Asante mimi pia Caren, nilikumiss mno, haya basi twende tukakae tumalizane na hili kwanza"

Yusto na Caren waliokuwa wakiongea kwa sauti ya chini, walishikana mikono na kuongozana kuelekea kwenye viti ambavyo vilikuwa vimeandaliwa kwa ajili yao.

"Ona watu walivyofurahi Yusto, yaani naona kama nafunga ndoa na wewe vile"

"Ahahaha usijali one day yes, bado tunasafiri ndefu sana mimi na wewe, si unajua"
"Najua Yusto ila nimesha kwambia no matter what I'LL STAY WITH YOU, NITABAKI NA WEWE Yusto wangu"

"Asante Caren naomba umaanishe kweli, BAKI NA MIMI kuna mengi makubwa yanakujaa huko mbele"

"Yapi tena babangu, kwanza hawa watu wamejuaje kama sisi ni wapenzi"

"hata sijui ila hii ni akili ya Frank kijana wa hovyo sana yule"
Alisema Yusto huku wote wakikaa kwenye viti vyao.

"Umemuona huyo Frank sasa" aliuliza Caren

"Hapana , yuko wapi"

"Yule pale mbele na Sophia"

"Ooh wow Sophia amepona kumbe"
"Ee yuko vizuri japo si sana, tumeshinda wote tangu jana tunakutafuta"

"Hahaha poleni"

Sophia na Frank walionekana wamekaa viti vya mbele kabisa huku nyuso zao zikionekana kujawa na furaha tere, wakawa wananong'ona maneno fulani huku wakiwatazama Yusto na Caren.
"Ulibuni kitu kizuri sana Sophia" alisema Frank huku akigeuka na kumtazama Sophia.

"Hahah nilikwambia ukabisha ona sasa wanavyopendezana kuwa pamoja" alisema Sophia kisha akatabasamu.

[emoji294][emoji294][emoji294]

Wakati huo wale vijana kutoka kwa madam Jane tayari walishajipenyeza na kuingia ukumbini, wakajichanganya na watu waliokuwa wamehudhulia sherehe hiyo, wakawa wanawinda winda ni vipi watapata sampuli ya kupima vinasaba kutoka kwa Yusto.

"Sasa sikia hapa tunahitaji kitu kidogo sana, damu, nywele, mate au kitu chochote kutoka kwenye mwili wa Yusto, ni hivo tu, ikitokea nafasi tuitumie haraka tusepe" alisema mmoja wa wale vijana ambae alionekana kuwa kiongozi wa wenzake.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Upande wa pili Revocatus alionekana akiongea na mtu kwenye simu mara tu baada ya kurejea kambini akitokea kwa Osman Azizi.

"Anko Azizi"

"Ndiyo Revo niambie"

"Aisee, nimefika kambini sijamkuta Zubeda"

"Mmh kweli, au Caren kaondoka nae"

"Hapana angeniambia, hata hivyo nimekuta milango iko wazi"

"Dah hiyo ni mbaya sana Revo, hebu anza kumtafuta hakikisha unamrudisha si unajua huyo mama ni kama akili yake siku hizi imeanza kusoma vizuri ataleta shida kama akiingia mtaani tena"

"Sawa anko nimekuelewa"
"Lakini usimwambie Caren, akiuliza wewe sema Zubeda yupo"

"Sawa anko"

Revocatus alikata simu huku kijasho kikimtoka, akajifuta na kuvaa koti lake kisha akaanza kazi ya kumtafuta Zubeda ambae alikuwa ameondoka kitambo sana akaingia msituni.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Asubuhi ya siku inayofuta wakati sherehe ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa Yusto ikiendelea kule chuoni Zubeda yeye alikuwa msituni akiendelea kutembea asijue anako elekea.

Alikuwa ametembea usiku kucha lakini mama huyo kichaa hakuonekana kuchoka hata kidogo.

Mwisho aliifikia barabara ya lami iliyokuwa ikikatisha katika ya msitu huo.

Zubeda alionekana kufurahia sana mara tu baada ya kuiona barabara hiyo, akakimbia na kuanza kugaragara katikati ya barabara hiyo huku akichekelea sana.

Mara alisikia muungurumo wa gari linakuja. Zubeba alisimama akaangaza macho huku na huku kisha akakimbia msituni na kujificha nyuma ya mti mmoja mkubwa hali akiwa bado anacheka.

Kwa mbali aliona msafara wa magari matatu madogo yaliyoongozana unakuja. Alitulia akasubiri hadi pale yalipofika karibu kabisa na usawa aliokuwepo.

Ghafula Zubeda alikimbia na kwenda kusimama katikati ya barabara kisha akatanua mikono yake yote miwili kama vile anataka kuizuia gari isipite.

La haura, dereva aliyekuwa kwenye gari ya mbele alishtuka kumuona mtu anatokea msituni ghafula na kusimama mbele ya gari katikati ya barabara. Lilikuwa ni kutukio ambalo hakulitegemea.

Dereva alijitahidi kufunga breki na kujaribu kumkwepa Zubeda lakini jitihada zake hazikuzaa matunda kwa asilimia mia moja.

Zubeba aligongwa na gari kisha akarushwa pembezoni mwa barabara huku yale magari yaliyofuta nyuma nayo yakagongana baada ya lile gari la mbele kufungua breki ghafula.

Ilikuwa ni ajali ambayo ilileta maafa kwa kiasi. Hakuna gari iliyoanguka lakini hali ilikuwa ngumu kwa Zubeda ambae alikuwa amelala pembeni ya barabara hoi taabani.
Zubeda alikuwa akipumua kwa shida sana, damu ikawa inamtoka puani na masikioni.

Kimya kilitawala kwa sekunde kadhaa.
Mwisho milango ya magari yote ilifunguliwa watu kadhaa wakatoka kwenda kumuangalia yule mtu aliyewasababishia ajali kisha na yeye akajeruhiwa vibaya.

Walimzunguuka Zubeda wakawa wanamshangaa kisha mmoja wao akainama na kumgusa mshipa wa shingoni.

"Vipi?"
"Ni mzima, anapumua pia"alisema yule mtu aliyemgusa Zubeda.

Baada ya kusema hivyo, mmoja kati ya wale watu waliosimama alikimbia hadi lilipokuwa gari la katikati akagonga kioo cha mbele siti ya pembeni kwa dereva.
Kioo kikashushwa taratibu.

"Bosi, yule mama ni mzima" Alisema yule mtu.

"Basi mchukue mpelekeni kwenye hospitali yangu, msiache arama yoyote kuonyesha kulikuwa na ajali, mimi natangulia"
Sauti ya mtu aliyekuwa ndani ya lile gari ilisikika kisha akaonekana anafunga kioo taratibu.
Amani usiamini ndugu msomaji, mtu huyo hakuwa mwingine bali ni bosi Mark Moon tajiri na mmliki wa chuo cha kimataifa cha mark Moon, mume wa zamani wa madam jane yaani baba yake John (master joo).
Mark moon alifunga kioo na dereva akawasha gari, wakaondoka taratibu.

Je, nini kitafuata?

Zubeda kwenye mikono ya mark moon...!!
Wakati huo madam Jane anatafuta sampuli ya Yusto kwa ajili ya kupima vinasaba....!!

Osman Azizi anapanga nini....!!
Nini hatima ya Brandina, Yusto na Caren....!!

WhatsApp
0756862047
 
Mwana hii kitu nzuri ikishushwa ep 2 tatu siku mbili tatu tena
 
DO NOT SHOUT
season 2
Sehemu ya..........24

ILIPOISHIA....
Amini usiamini ndugu msomaji, mtu huyo hakuwa mwingine bali ni bosi Mark Moon tajiri na mmliki wa chuo cha kimataifa cha mark Moon, mume wa zamani wa madam jane yaani baba yake John (master joo).
Mark moon alifunga kioo na dereva akawasha gari, wakaondoka taratibu.

SASA ENDELEA...
[emoji294][emoji294][emoji294]

Upande wa pili sherehe ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa Yusto ilikuwa ikiendelea ndani ya ukumbi mkubwa uliokuwa ndani ya chuo maarufu cha Mark Moon.

Taratibu mbalimbali za sherehe hiyo iliyoteka hisia za wanafunzi wengi chuoni hapo zilikamilika sasa walikuwa wanaelekea kufunga sherehe hiyo.

" Wakati tunaeleka kumalizia malizia, hebu kwanza Dj utuchangamshe kidogo, tuwekee muziki mzuri wa blues tunataka kumuona birthday boy na birthday girl wakicheza kwa pamoja yaani Yusto na Careeeeeen" Alisema mshereheshaji na hapo ukumbi mzima ukaripuka kwa furaha.

Caren na Yusto walitazama kwa aibu, na hapo mziki mzuri laini ukaanza kusikika.

Licha ya kwamba hakuwa mtu anaejua sana kucheza lakini hakutaka kuwaangusha watu waliokuwa wamehudhulia sherehe hiyo, Yusto alisimama kisha akanyoosha mkono wake na kumshika Caren, akamvuta karibu yake wakaanza kucheza taratibu.
Lilikuwa ni tukio lililo wafurahisha wengi si Sophia si Frank, bali kila mtu aliekuwa ndani ya ukumbi huo. Haukupita muda watu wakashikana wawili wawili wakiungana na Yusto na Caren kucheza mziki ule.

"Caren" Yusto aliita akiwa amemsogeza Caren karibu yake zaidi, huku akiwa ameizunguusha mikono yake nyuma nyuma ya kiuno cha Caren.

"Mama yangu anaendeleaje, i wish kama tungekuwa wote hapa angefurahi sana"

"Mama anaendelea vizuri Yusto usijali, tukitoka hapa tutaenda wote kambini ukamuona nina hakika amekukumbuka sana." Alijibu Caren.

Hadi dakika hiyo hakuna ambea alikuwa na taarifa ya Zubeda kutoroka kule kambini, hakuna ambae alifahamu juu ya ile ajali mbaya ya gari iliyotokea kule msituni.

"Caren"
"Abeeh"
"Nimeongea habari za mama naona kama umebadilika ghafula, vipi kuna tatizo"

"Aah hamna Yusto..ni..nimejisikia tu vibaya mama kutokuwepo hapa leo"

"Ooh! Usijali, hata hivyo hawezi kuwepo si unajua hali yake, angeleta fujo pengine pasingetosha hapa hahaha" Yusto aliongea Kisha akacheka akiamini na Caren nae atacheka lakini haikua hivyo.

Ukweli Caren alikuwa mbali kimawazo, mbali tena mbali sana. Alikuwa akiwaza juu ya taarifa ambazo alikuwa akizifahamu juu ya Yusto na mama yake mzazi yaani madam Jane. Caren alikuwa akijiuliza mara mbili mbili ataanzia wapi kumweleza Yusto ukweli, bado aliona sio wakati sahihi lakini kuna wakati pia alihisi ni muda sahihi wa kumwambia.

Wakati akiwaza hayo mara mziki ulizimwa ghafula.

"Aaaaaaa..." Ukumbi mzima walilalamika baada ya mziki uliokuwa umewakorea kuzimwa ghafula.

"Jamani samahani kwa kuwakatishia burudani, kuna mtu mkubwa sana yuko hapa, kwa bahati mbaya alichelewa kufika na kachelewa pia kutoa zawadi zake kwa Yusto, kwa heshima kubwa na ruhusa kutoka kwako birthday boy naomba nimruhusu huyo mtu aje hapa mbele" alisema yule dada Mc.

Yusto hakuwa na hiyana alitikisa kichwa kukubali Kisha yeye na Caren wakarudi kwenye viti vyao wakakaa.

Kufumba na kufumbua walimuona John akiingia akiwa ameongozana na vijana wake watatu wakasogea hadi mbele kabisa ya ukumbi.
Ilikuwa ni tukio ambalo si Frank si Sophia si Caren wala si Yusto hakuna alietegema.
Frank alitamani kuwahi kwenda kumzuia lakini alikuwa amechelewa John na watu wake tayari walikuwa wamesimama mbele ya ule ukumbi kisha John akachukua maiki kutoka ka MC.

"Mungu wangu anataka kufanya nini huyu kichaa"Alisema Sophia huku akimuangalia Frank.

"Hata sijui, nitamuuwa huyu mwana haramu" alijibu Frank huku akiuma meno yake kwa hasira.

John alikuwa ni mtu anaeogopeka na kuheshimika pia kutokana na aina ya maisha aliyokuwa akiyaishi chuoni hapo. Kijana mwenye pesa ndefu na jeuri ya kiwango cha juu hii ndiyo ilikuwa sifa yake kubwa.
Alichukua maiki na kisha akaanza kuzungumza kwa kujiamini.

"Niko hapa si kwa ajili ya kuomba kura. najua kura zenu ninyi wote ninazo, mtanipa tu, sidhani kama kuna mtu ataacha kunipigia mimi kura akampigia yule mnyakyusa mshamba kutoka mbeya vijijini. Mimi ndio Rais mtarajiwa wa hiki chuo cha Mark Moon na mimi ndio nimebeba hatima zenu ninyi kama wanafunzi"
Watu wakapiga makofi.
John akatulia kwa muda kisha akaendelea kuzungumza...

" Asante kwa wote mlioandaa sherehe hii naamini haiwezi kuwa nguvu ya Yusto peke yake asinge weza, hana uwezo huo. Lakini nataka pia nikushauri kitu kimoja kijana hata kama sio wewe umehusika na haya maandalizi ya sherehe basi jitahidi kwa wakati mwingine kuhakikisha angalau hata mzazi wako mmoja anahudhuria tukio kama hili, uwongo jamani. Kama baba hayupo basi aje mama, hata kama mama anamapungufu kiasi gani pengine ni kichaa mvuta bangi anaokota makopo aje hivyo hivyo huyo ni mama yako" John alikuwa akiongea kwa kejeri.
Mc alipoona ni kama John anataka kuwaharibia sherehe akasogea kwa ajili ya kwenda kuchukua maiki lakini wale vijana wa John wakasimama mbele yake kumzuia.
Ukumbi wote ukawa kimya wakimsikiliza John, huku minong'ono ya hapa na pale ikisikika.

Maneno ya John yalipita kama msumali wa moto kwenye moyo wa Yusto alitaka kusimama na kwenda kumvaa John lakini Caren akamzuia.

"Jitulize Yusto jaribu kujicontrol mwenyewe unajua kabisa ni nini anakitaka please Usifanye chochote usiingie kwenye mtego wake" alisema Caren
" Kwa hiyo unatakaje nikae kimya nimuache aendelee kunidharirisha mbele ya kadamnasi ya watu"

"Yusto sikiliza, tayari unamjua John ni mtu wa aina gani hebu..."
"Hapana Caren this is too much"

Caren na Yusto waliendelea kubishana, John aliliona hilo akatabasamu kidogo kisha akaendelea kuzungumza.

"Nimekuja hapa kutoa pongezi zangu kwa kijana huyu ambae amefikisha miaka kadhaa tangu azaliwe, nina zawadi kidogo hapa naomba nimpatie" alisema John na hapo kijana wake mmoja akasogea na kuchukua boksi la mipira (kondomu) kutoka kwa John Kisha akasogea na kuliweka juu ya meza mbele ya Yusto na Caren.

Minong'ono ya hapa na pale ilisikika huku baadhi ya wanafunzi wakishindwa kujizuia kucheka.

"Aah kudadeki huyu mwamba anadharau sana"
"Sio dharau tu kwanza anajikubali kupita kiasi anajikuta mungu mtu, silipendi"
"Navyomjua Yusto hawezi kumuacha we subiri utaona, kuna moto utawaka hapa sio mda"

Watu kadhaa walisikika wakizungumza kutoka kwenye kona moja ya ukumbi.

Wakati huo wale vijana wa madam Jane waliotumwa kuchukua sampuli kutoka kwa Yusto kwa ajili ya vipimo vya DNA (vinasaba) walikuwa bado wakitafuta namna ya kumfikia Yusto, na hadi dakika hiyo tayari walikuwa wamevaa mavazi ya wahudumu wa ukumbi huo ambao walikuwa wakisambaza vinjwaji.

John akaendelea kuzungumza...
"Aah msicheke ndugu zangu hizi ni kinga tu, kwani ni nani kati yenu hajawahi tumia kondomu maishani mwake. nataka kumlinda mwanamke mrembo hapa chuoni Caren ambae ameingia kwenye mikono ya Yusto maskini bila kujua historia yake, sasa sisi kama washikaji tunaemjua Yusto nje ndani hatuna budi kumkinga Miss wa chuo chetu cha mark moon, halafu kingine...." John alikuwa akiendelea kuzungumza lakini mara akakatisha mazungumzo baada ya mtu mwingine aliyekuwa na maiki kuingilia.

"Asante asante ndugu John, tunashukuru sana kwa muitikio wako" ilikuwa ni sauti ya Yusto ambae aliongea akiwa ndo kwanza anainuka kutoka kwenye kiti chake akiwa na maiki mkononi.
John aligeuka na kumungalia, hakutegemea kama Yusto angekuwa hata na nguvu ya kusimama.

"Usijali Caren" Yusto alimnong'oneza Caren
"NΓ ombΓ  usilete fujo Yusto nakuomba sana" caren alisisitiza
" Niamini siwezi kufanya hivyo" alijibu Yusto huku akianza kupiga hatua taratibu akisogea pale alipokuwa John na vijana wake.

"Nashukuru sana ndugu yangu kwa kuja, hakika ujio wako umekuwa ni wapekee sana kwenye sherehe yangu, sikutegema" alisema Yusto huku akiinama kwa heshima kubwa mbele ya John.

Watu walipigwa na butwaa wasielewe ni nini kilikuwa kinaendelea kati ya wawili hao yaani Yusto na John.

"Nashukuru sana kwa zawadi ya kondomu hizi ulizonipa, umetumia akili kubwa sana akili ambayo laiti kama angekuwepo mtu kama wewe kipindi hicho akampa zawadi kama hii baba yako au mama yako naamini asinge zaliwa kiumbe kama wewe. Lakini kwa bahati mbaya hakuwepo na ukazaliwa wewe ambae mpaka leo hii humjui baba yako ni nani, hata mama yako ambae aliachika siku 91 baada ya ndoa yake hajawahi kukwambia ukweli na badala yake amekupa hela nyingi ambazo zimekufanya uwe kipofu hujui uliko toka wala unakoenda ewe mheshimiwa John"

Yusto aliongea maneno ambayo yalikuwa ni mwiba mchungu kwa John, maneno ambayo hakuwahi kuambiwa tangu azaliwe. Alishangaa ni vipi Yusto anataarifa ambazo yeye hana.

John aligeuka na kuutazama ukumbi akaona ni jinsi gani watu walikuwa wanajaribu kujizuia kucheka. Akageuka na kumtazama Yusto. Yusto akainama kwa heshima kama alivyofanya mwanzo kisha akainuka.

Ndugu hawa wawili wa damu ambao hawajuani wakawa wanatazamana kwa macho makali huku kila mmoja akiwa na maiki yake mkononi.

ITAENDELEA...

Malizia vipande vyote vilivyobaki kwa tsh Elf 1 tu.
0756862047
 
BAKI NA MIMI
(Stay with me)

*Sehemu ya ............25
Mtunzi: Saul David
Whatsapp: 0756862047

ILIPOISHIA...

John aligeuka na kuutazama ukumbi akaona ni jinsi gani watu walikuwa wanajaribu kujizuia kucheka. Akageuka na kumtazama Yusto. Yusto akainama kwa heshima kama alivyofanya mwanzo kisha akainuka.

Ndugu hawa wawili wa damu ambao hawajuani wakawa wanatazamana kwa macho makali huku kila mmoja akiwa na maiki yake mkononi.

SASA ENDELEA....
Ukumbi wote ulikiwa kimya kabisa, wanafunzi wakawa wanawatazama Yusto na John wakitamani kuona nini kitatokea kati ya mafahari hao wawili wa chuo cha Mark Moon.

Caren ambae mwanzo alikuwa amesima, alikaa kwenye kiti chake hali akionekana kuchanganywa na tukio lililokuwa likiendelea wakati huo.

"Yusto kajua vipi habari za madam Jane, hii inamaana atakua anamfahamu Mark Moon pia, inaonekana anajua kila kitu, pengine anajua pia kuwa madam Jane ni mama yake mzazi, mmh hapana hajui, lakini sasa hizi taarifa kazitoa wapi anazijua tangu lini?" Caren alikuwa akijiuliza na kujijibu mwenyewe.

Jonh ni kama alikuwa amepigwa na ganzi, alikuwa akiyafananisha maneno ya Yusto na uhalisia wa maisha yake, ni kweli hakuwahi kuyafuatilia maisha yake na ya mama yake kiundani, alichojua tu ni kwamba baba yake mzazi alishafariki, hivyo ndivyo alivyoaminishwa na mama yake, lakini ilikuwaje, kivipi, kwanini haya yote hakuyajua. Taarifa za mama yake kuolewa na kuachika baada ya siku 91 ndio kwanza alikuwa anazisikia kwa mara ya kwanza kutoka kwa Yusto tena akiwa mbele ya umati wa watu.

John alihisi kichwa chake kuwa kizito, hakujua afanye nini kwa muda huo kuikabili aibu kubwa iliyokuwa mbele yake.
Aligeuka akawatazama wale vijana wake ambao anapenda kuongozana nao, nao wakainamisha vichwa vyao chini kwa aibu, hawakuweza kumtazama John usoni.

John akageuka tena na kumtazama Yusto, wakati akifanya hivyo mara aliona tukio lingine ambalo lilimshangaza pia, alimuona kijana mmoja ambae huwa anamuona mara kadhaa akiagizwa vitu mbalimbali na mama yake madam Jane.
Wakati huo kijana huyo alikuwa amevalia mavazi ya wahudumu ambao wanasambaza vinywaji katika sherehe hiyo.

John aliendela kufuatilia nyendo za kijana huyo, akamuona anaenda hadi pale kwenye meza waliyokaa Caren na Yusto, lakini kwa wakati huo alikuwepo Caren peke yake. Yule kijana alifika na kuweka kinywaji juu ya meza kisha akachukua glasi ambayo Yusto alikuwa akiitumia, akaishika ile glasi kwa tishu kisha akaondoka taratibu. Badala ya kuelekea sehemu maalum ya vinywaji yule kijana alikatisha na kuelekea upande wa pili vilipokuwa vyoo vya ukumbi huo tena cha kushangaza zaidi alielekea vyoo vya wanawake.

Taa nyekundu iliwaka kwenye kichwa cha John akahisi kuna kitu ambacho si cha kawaida kilikuwa kikiendelea, akatamani kujua zaidi kwani hata hivyo kunabaadhi ya mambo yalikuwa yakiendelea ambayo John alikuwa hayaelewi elewi kabisa, kwanza ni ile picha aliyoiona mama yake akiwa pamoja na zubeda mama yake Yusto, pili ni haya maneno aliyoyasema Yusto na mwisho ni huyu kijana wa mama yake kuwepo kwenye sherehe ya Yusto. Matukio yote hayo yalihitaji majibu. John akawaza kuanzia na huyu kijana wa mama yake.

Alipiga hatua akamsogelea Yusto, wakawa wanawatazama uso kwa uso.

"Leo umeshinda, lakini subiri zamu yako" John aliongea huku akiuma meno kwa hasira

"Kila wakati mimi ni mshindi kwako John usisahau hilo" Yusto alijibu kwa kujiamini

"Sawa tutaona, umesahau nilichomfanya mama yako subiri".

"Nitahakikisha haupati tena nafasi ya kufanya hivyo John, sahau"
"Sawa"
"Sawa"
"Tutaona"
John aliongea akatupa maiki chini kisha akaanza kuelekea kule alikoelekea yule kijana wa mama yake.
[emoji294][emoji294][emoji294]

"Kuna mwingine ana zawadi alete?" Yusto aliuliza kwa sauti kubwa.
Ukumbi mzima ukaangua kicheko huku waandishi wa habari wa gazeti la chuo wakiwa makini kuchapisha na kupiga picha ya kila kilichoendelea.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Madam Jane akiwa nyumbani kwake, bado akili yake ilikuwa haijatulia kabisa wakati wote alikuwa akiwaza ni jinsi gani atakabiliana na bwana Osman Azizi mtu ambae alikuwa ni kikwazo kizito kwake kwa wakati huo. Madam alikuwa akiitazama simu yake aliyoiweka mezani kila wakati ilionyesha wazi kuna taarifa anaisubiri kwa hamu kubwa.
Ndio, ilikuwa ni taarifa ya kupatikana kwa sampuli ya Yusto kwa ajili ya kupima vinasaba (DNA), alisubiri taarifa hiyo kwa hamu kubwa.

Mara simu yake ikaita, haraka madam Jane aliruka kwenda kuipokea, lakini mara akionekana kunyong'onyea mara tu baada ya kuona jina la mpigaji, hakuwa Dokta Givan bali ni Enock mlinzi wa siri wa mtoto wake John ambae humfuatilia John kwa siri. Huyu ndiye aliyekuwa mtu wa Kwanza kabisa kutoa taarifa baada ya John kuchomwa na mkasi siku ile.

"Eee unasemaje?"aliuliza madam Jane mara tu baada ya kupokea ile simu.
"Madam kuna tatizo hapa"
"Lipi, mwanangu John kafanyaje tena"
"Ni Yusto na John pia"
"Yusto? amesharudi chuoni, si alipigwa risasi huyo lakini"
"Aah sijui, ila yuko hapa alikuwa na sherehe ya kuzaliwa"
"Kuzaliwa?, Enhe vipi wamegombana tena ama?"

"Angalia kuna video nakutumia sasa hivi madam" alisema enock kisha akakata simu.

Madam jane alifungua data kisha akawa anaisubiri video hiyo kwa hamu kubwa.

"Yusto, inamaana leo ni siku yake ya kuzaliwa?, Mmh hivi mwanangu Yusto alizaliwa tarehe ngapi vile, yaani hata sikumbuki jamani, lakini ulikuwa mwezi kama huu" aliwaza madam Jane, mara ile video aliyoingoja ikaingia, haraka akafungua kuangalia.

Ilikuwa ni video inayoonyesha wakati ule Yusto na John wanaongea mbele ya ukumbi, kuanzia John alipochukua maiki akijaribu kumdharirisha Yusto mbele ya wanafunzi wenzie, lakini Yusto nae akachukua maiki na kujibu mapigo.

"Nashukuru sana kwa zawadi ya kondomu hizi ulizonipa, umetumia akili kubwa sana akili ambayo laiti kama angekuwepo mtu kama wewe kipindi hicho akampa zawadi kama hii baba yako au mama yako naamini asinge zaliwa kiumbe kama wewe. Lakini kwa bahati mbaya hakuwepo na ukazaliwa wewe ambae mpaka leo hii humjui baba yako ni nani, hata mama yako ambae aliachika siku 91 baada ya ndoa yake hajawahi kukwambia ukweli na badala yake amekupa hela nyingi ambazo zimekufanya uwe kipofu hujui uliko toka wala unakoenda ewe mheshimiwa John "

Madam alikirudia kipande hiki mara mbili mbili huku akijihisi kuishiwa nguvu, akakaa chini huku akihema kwa nguvu, simu ikiwa bado mkononi mwake. Hakuwahi kumwambia John habari hizi za ndoa na Mark Moon na siku zote alikuwa akihonga na kuzuia vyombo vya habari kuandika taarifa zake hasa za maisha yake ya nyuma, alifanya hivyo vyote ili kumlinda John asiujue ukweli, hasa juu ya baba yake mzazi Mark Moon, lakini leo taarifa hizi zinaanikwa hadharani mbele ya umati wa watu. Madam jane alichoka.

Mara kuna ujumbe mfupi wa maandishi ukaingia kutoka kwa Dokta Givan.

TAYARI TUMEPATA SAMPULI YA MATE KUTOKA KWENYE GLASI ALIYOTUMIA YUSTO, TUNAPIMA DNA SASA, UNAWEZA KUSOGEA HAPA MOUNTENIA HOSPITAL ....

Madam jane alivuta pumzi ndefu na kuitoa taratibu, akajikongoja na kusimama, uso wake ukionekana kupauka sana.
[emoji294][emoji294][emoji294]

John na vijana wake walikuwa ndani ya choo kimoja cha wasichana wakiwa wamembananisha kijana mmoja kati ya wale watatu waliotumwa kuchukua sampuli kutoka kwa Yusto. Wawili walifanikiwa kukimbi na hadi dakika hii tayari walikuwa wameifikisha ile glasi kwa Dr givan. Huyu mmoja alijikuta anaingia kwenye mikono ya John, alipigwa sana akilazimishwa aseme ukweli ametumwa na madam Jane kufanya nini, mwisho uvumilivu ukamshinda akaamuwa kuweka wazi kila kitu.

"Usiniuwe John nitasema ukweli, nitasema, tumetumwa kuja kuchukua sampuli kutoka kwa Yusto kwa ajili ya vipimo vya DNA, nilivyosikia ni kuwa madam Jane anahisi Yusto ni mwanae pia, ni hivyo tu kaka hakuna kingine ninachokijua, naomba usinitese"
Alieleza yule kijana, John ambae alikuwa amekunja ngumi kwa hasira alijikuta anakosa nguvu ya kuendelea kukunja ngumi ile, aliduwaa huku mdomo wake ukiwa wazi.

"Umesemaje" John aliuliza kwa sauti ya upole safari hii, akihisi labda amesikia vibaya.
" Ni hivyo kaka, ni kwa ajili ya DNA tu sio kingine" Yule kijana alisisitiza.

ITAENDELEA......
Sasa tunaelekea kufika mwisho wa SIMULIZI hii
Njoo WhatsApp umalizie vipande vyote 16 vilivyobaki kwa tsh 800 tu
0756862047
 
Mambo ni moto, kama naiona picha ya mbele itakavyokuwa. John atakuwa wa kwanza kujua Yusto ni kaka ake na Yusto baada ya kujua kuwa Madame Jane ni mama yake mzazi ataukataa ukweli huo na kumkumbatia/kumtambua mama kichaa kama ndiye mama ake. Jane na John wataumia na kudhalirika sana. Mark Moon atashukuru kumtambua Yusto kama ni mwanae na hatamsamehe Madame Jane kwa ujinga wote aliokuwa akiufanya miaka yote juu ya miradi yake. Zubeda atapona ukichaa baada yakupata matibabu makubwa chini ya usimamizi wa Mark Moon
 
fyddell umeanza kupiga ramli chonganishi?[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hahaha simulizi nyingi za kibongo mwisho wake unajulikana. Nawasifu sana watengeneza scripts na waandishi wa vitabu wa kimagaribi coz unaweza fuatilia simulizi zao na usijue mwisho itakuwaje
 
Hahaha simulizi nyingi za kibongo mwisho wake unajulikana. Nawasifu sana watengeneza scripts na waandishi wa vitabu wa kimagaribi coz unaweza fuatilia simulizi zao na usijue mwisho itakuwaje
We jamaa una maono sana hiz niaje. Aniwei ngoja tuone mwisho wake[emoji16][emoji16]
 
Hahaha simulizi nyingi za kibongo mwisho wake unajulikana. Nawasifu sana watengeneza scripts na waandishi wa vitabu wa kimagaribi coz unaweza fuatilia simulizi zao na usijue mwisho itakuwaje
Wewe ulishawahi kuandika simulizi yoyote au unaleta ujuaji wa shule ya msingi.

Tunga yako inayofanana na hizo za magharibi tuone.
 
Mambo ni moto, kama naiona picha ya mbele itakavyokuwa. John atakuwa wa kwanza kujua Yusto ni kaka ake na Yusto baada ya kujua kuwa Madame Jane ni mama yake mzazi ataukataa ukweli huo na kumkumbatia/kumtambua mama kichaa kama ndiye mama ake. Jane na John wataumia na kudhalirika sana. Mark Moon atashukuru kumtambua Yusto kama ni mwanae na hatamsamehe Madame Jane kwa ujinga wote aliokuwa akiufanya miaka yote juu ya miradi yake. Zubeda atapona ukichaa baada yakupata matibabu makubwa chini ya usimamizi wa Mark Moon
Hahha sikuzote mwandishii mzuri ni yule ambaye stori yake huwezi jua inaenda vipi itaishaje,,,, Ngoja tuone [emoji16]
 
BAKI NA MIMI
(stay with me)
season 2

Sehemu ya.............26
Mtunzi: Saul David
Whatsapp: *0756862047

ILIPOISHIA....
Alieleza yule kijana, John ambae alikuwa amekunja ngumi kwa hasira alijikuta anakosa nguvu ya kuendelea kukunja ngumi ile, aliduwaa huku mdomo wake ukiwa wazi.

"Umesemaje" John aliuliza kwa sauti ya upole safari hii, akihisi labda amesikia vibaya.
" Ni hivyo kaka, ni kwa ajili ya DNA tu sio kingine" Yule kijana alisisitiza.

SASA ENDELEA....
Hii ilikuwa ni ngumu kumeza kwa kijana John, hakuwa na sababu ya kuendelea kukaa pale aliinuka taratibu akaondoka bila hata kuzungumza na mtu yeyote.

"Kwa hiyo inakuwaje kuhusu mimi kaka mbona unaniacha bila kusema chochote kwa hawa jamaa zako" aliuliza yule kijana aliyekuwa amebananishwa na John hadi akafunguka ukweli wote, ukweli ambao ilikuwa ni ngumu kueleweka kwenye akili ya John. Hakujibu kitu badala yake aliondoka hali akiwa amekunja sura kutokana na hasira kali aliyokuwa nayo wakati huo.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Mark Moon alionekana akiwa eneo moja tulivu lenye bustani nzuri nje ya nyumba moja kubwa ya kifahari akiwa pamoja na wazee wenzake watatu matajiri wakicheza na kufurahia mpira wa gofu.
Mara simu yake ikaita, akachukua kutoka mfuko wa koti lake kisha akaipokea na kuiweka sikioni.
"Hallo bosi" alisikia mwanaume mmoja upande wa pili wa simu ile
"Eeh dokta vipi hali ya huyo mama"
"Hali yake sio mbaya sana lakini kuna lingine kubwa zaidi bosi wangu"
"Lipi hilo?"
"Uko mazingira salama hapo"
"Hapana hebu subiri sekunde chache"

Mark moon alimkabidhi mzee mmoja fimbo yake ya kuchezea gofu, akasogea mbali kidogo kisha akaonekana anazungumza na daktari kwa zaidi ya dakika 5 baada ya hapo akarudi upesi pale alipokuwa.

"Samahani jamani nimepata dharula ndogo hapa naomba niwaache wazee wenzangu" alisema mark.
"Kawaida yako, haujawahi kutulia hata siku moja, ndio sababu ulimuacha mkeo ndani ya miezi mitatu tu ha ha hah"
Alisema mzee mmoja kisha wote wakacheka kwa sauti.

Mark moon alitabasamu kidogo, akaondoka eneo lile huku walinzi wake wakimfuata nyuma taratibu, wakaingia kwenye gari.

"Wapi bosi" aliuliza dereva
"Hospitali, MOUNTENIA hospital naenda kumuona yule mama tuliemgonga"
"Lakini si tulimuacha kule hospitali yetu bosi"
"Ee wamemuhamisha twende upesi".
Alisema Mark moon na safari ikaanza kuelekea hospitali ya MOUNTENIA.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Njiani Mark Moon alionekana kuwa mwenye mawazo kiasi, maelezo aliyopewa kwenye simu na daktari ndiyo haswa yalimfanya kuwa katika hali ile, maelezo hayo yakawa yanajirudia rudia kwenye kichwa chake wakati safari ikiendelea.
Daktari alisema hivi...

"Bosi huyu mama aliyegongwa ni yule mama ambae alikuwa rafiki wa madam Jane kipindi kile, yule ambae tuliwahi kumhoji kipindi fulani kuhusu mtoto wa madam Jane akakataa akasema hana mtoto wa madam Jane wala taarifa zake"

"Unasema nini dokta, unamaanisha Zubeda, yule alituficha ukweli kuhusu Madam Jane kuwa na mtoto"

"Ndiyo bosi"
"lakini nakumbuka mara ya mwisho mwaka juzi kama sikosei nililetewa taarifa kuwa ameonekana mahali lakini ni kichaa, mwendawazimu si ndiyo?"

"Ndiyo bosi, ila sasa ni kama hii ajari imemsababishia akili yake kukaa sawa tena na kumbukumbu zake kurejea upya, anaongea vitu vya ajabu sana anamtaja madam Jane anakutaja wewe na watu wengine wengine, hizi kumbukumbu zinamuumiza sana ubongo wake
tumeshindwa kumtuliza kabisa kuna huduma anatakiwa aipate ya mapema 'memory reboot' hapa hatuna nafikiria tumpeleke pale hospitali ya MOUNTENIA wako vizuri watamuhudima haraka atakaa sawa"

"Sawa basi fanyeni hivyo mimi nakuja sio mda, hakikisheni hakuna mtu anaonana nae kabla yangu"

Mark moon alimaliza kumbukumbu yake wakati huo safari ikiendelea kwa kasi kuelekea hospitali aliko Zubeda.
[emoji294][emoji294][emoji294]

John alitelemka kutoka kwenye taxi nje ya ghorofa kubwa sehemu ilipokuwepo ofisi ya mama yake.
Bado sura yake ilionekana ana hasira isiyopimika, alitaka kuonana na mama yake amjibu kinaga ubaga ni kwa nini alipiga picha na mama yake Yusto, kwa nini Yusto atamke maneno yale ukumbini,kwa nini anataka kupima vinasaba (DNA) na Yusto, ni siri gani nyingine anamficha, haya yote ni maswali ambayo John alihitaji majibu.

"Mama yako hayupo hapa, alikuwa nyumbani lakini kwa sasa kaelekea hospitali" John alipata majibu hayo kutoka kwa msaidizi wa kazi ofisi ya mama yake.

"Hospitali gani"
"MOUNTENIA"
Alisema yule msaidizi, John aligeuka na kuondoka bila hata kuaga.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Majira ya saa 8 mchana tayari madam Jane alikuwa ameshafika hospitali kubwa ya kimataifa MOUNTENIA hospital, alikuwa amesimama nje ya chumba cha Dr Givan akili yake ikionekana kutokuwa sawa kabisa, alikuwa akipiga hatua mbele kisha anarudi nyuma.
Punde mlango wa chumba cha daktari ukafunguliwa, dokta Givan akatoka akiwa na karatasi nyeupe mkononi.

Madam Jane alimkimbilia kwa papara na kusimama mbele yake.
"Dokta" madam Jane aliita
"Ndiyo madam majibu yako tayari" dr Givan aliongea kinyonge akamkabidhi madam Jane ile karatasi kisha akarudi ndani.

Roho ilikuwa ikimdunda madam Jane, taratibu alianza kuikunjua ile karatasi, wakati akifanya hivyo, wauguzi wanne walipita mbele yake wakiwa wanamsukuma mgonjwa kwenye toroli.

Mgonjwa aliyekuwa amelala juu ya machela ile hakuwa mwingine bali Zubeda, alikuwa ameletwa hapo kwa ajili ya huduma ya 'memory reboot' kama alivyoagiza mark moon ambae nae alikuwa njiani anakuja hapo Mountenia hospital.

Kwa bahati nzuri au mbaya kwa madam Jane hakuweza kumtazama mgonjwa aliyekuwa juu ya machela ile, yeye alikuwa bize kuisoma karatasi ile yenye majibu ya vipimo vya DNA kati yake yeye na Yusto.

Laiti kama angemuona Zubeda, ilikuwa ni habari nyingine hasa kwa Caren aliyepewa jukumu la kumuuwa mama huyo.

Hali akitetemeka madam Jane alianza kusoma majibu yale, mwishoni kabisa kwa ile karatasi ilisomeka hivi:-

*****************************

According to the method of Essen-MΓΆller. The probability of Madam Jane being the biological mother of Yusto is > 99.9999 %.
Conclusion: Based on our analysis, it is practically proven that Madam Jane is the biological mother of the child Yusto.
*******************************

Yusto na madam Jane vinasaba vyao vilishabihiana kwa asilimia 99.9, hii ikiwa na maana kwamba madam Jane alikuwa ni mama mzazi wa Yusto.

Karatasi ilidondoka kutoka kwenye mikono ya madam Jane, akaweka mkono wake kichwa asijue alie ama acheke, afurahi ama anune, mambo yalikua ni mazito mno kwa upande wake.

Simu ya madam Jane ilikuwa ikiita mfurulizo kwa zaidi ya mara mbili, mwisho madam Jane alijikaza na kuipokea.

"Madam" ilikuwa ni sauti ya secretary wake(msaidizi wa kazi).
"Yes what's up"
"John ametoka hapa sio mda anakuja huko hospitali, lakini anaonekana mwenye hasira sana sijajua shida nini... Madam... madam umenisikia...bosi ....bosi......." Msaidizi wa Madam Jane alisikika akizungumza upande wa pili lakini madam Jane akawa kimya, ameduwaa si kwa makusudi bali ni baada ya kumuona mtu anaekuja mbele yake, hakuwa mwingine bali John.

Wakati anapokea taarifa tayari John alishafika hospitali ya Mountenia, akawa anakuja huku akipiga hatua ndefu ndefu kumfuata mama yake madam Jane.

Madam Jane akiwa katika hali ile ya kuduwaa hakujua afanye nini, wakati huo simu akiwa bado ameiweka sikio asijue cha kumjibu msaidizi wake wa kazi akawa anamtazama John ambae alikuwa karibu kumfikia.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Nje ya hospitali ya Mountenia mark moon akiwa na walinzi wake walishuka kutoka ndani ya gari kisha taratibu wakaanza kupiga hatua kuingia ndani ya hospitali hiyo ya kimataifa.
[emoji294][emoji294][emoji294]

John alifika na kusimama mbele ya mama yake, uso wake ukiwa umekunjamana kwa hasira, madam Jane akawa anamtazama mwanae kwa wasiwasi mkubwa.
John alitazama chini ndipo alipoiona ile karatasi ya majibu ya DNA, akainua macho kumtazama mama yake ambae alionyesha wasiwasi mwingi, kisha taratibu John akaninama na kuikota ile karatasi akaanza kuisoma.

Baada ya kumaliza kuisoma tayari machozi yalikuwa yakimtiririka, John akainua uso wake na kumtazama mama yake.

"Ma..mama" John aliita kwa sauti ya uchungu.
Madam Jane alikaa kimya kwa sekunde kadhaa Kisha akajibu huku nae machozi yakimlenga.

"Yes, he is your brother, Yusto"( ndiyo ni kaka yako, Yusto)

ITAENDELEA.....

Bei imepungua hadi 800 lipa kwa namba 0756862047 kisha njoo WhatsApp umalizie simulizi hii
 
Hahaha patamu hapo, mzee nae yuko njiani. Baada ya memory reboot kufanyika yaonekana kila jambo litakuwa wazi zaidi.
 
KWA MAONI YAKO MPAKA SASA QUEEN WA SIMULIZI YETU NI NANI....

1. SOPHIA
2. CAREN
3. BRANDINA

weka maoni yako!!
Mimi ni msomaji wa hadithi nyingi...
Na kama msomaji kwa maoni yangu hadithi nyingi za waandishi wa kitanzania unafanana,
Unaweza ukatabiri mwisho wa hadithi utakuaje na ikawa hivo
 
Back
Top Bottom