Simulizi ya ujasusi: Do not shout (Usipige kelele)

Simulizi ya ujasusi: Do not shout (Usipige kelele)

DO NOT SHOUT 28

NA SAUL DAVID

ILIPOISHIA.....

Mara mlango ulifunguliwa, Zubeda aligeuka na kumtazama mtu anaeingia wakati ule, aliweza kumtambua.

"Mark moon" Zubeda aliita.
Mark moon aliingia taratibu akafunga mlango, akavuta kiti na kukisogeza pembeni ya kitanda alicholala Zubeda, akakaa huku akimtazama Zubeda usoni.

SASA ENDELEA....

"Aah Zubeda..." Mark moon alianzisha mazungumzo lakini Zubeda akainua mkono wake akimtaka Mark Moon asiongee lolote.

"Usijali daktari ameshaniambia kila kitu, nilikuwa na tatizo la akili si ndiyo hivyo, nilichanganyikiwa yani," Zubeda aliongea kinyonge.

Mark moon alizuga kama anakohoa vile kisha akamjibu.
"Ee ni kweli, nilikufuatilia nikaambiwa na madaktari kuwa nikuache tu huwezi kupona kwa matibabu ya kawaida ila ipo siku akili yako itakuja kukaa sawa japo itakuchukua miaka na miaka sikuwa na la kufanya zaidi ya hapo Zubeda" alieleza mark moon.

Zubeda alitulia kwa muda uso wake ukionekana kujaa simanzi nzito, akageuka taratibu na kumtazama mark moon.

"Mwanangu, mwanangu je, vipi nae ulimtelekeza kama mimi"

"Hapana usiseme hivyo Zubeda, Yusto yeye yupo, nilikuwa nikimfuatilia tangu dada ako Asma alipofariki Yusto akawa anaishi na shemeji yako Osman Azizi hadi alipoamua kuondoka, niliendelea kumfuatilia na kumlinda lakini nilipoona maisha yake yanazidi kuwa magumu nikamchukua mpaka sasa ni mmoja kati vijana wangu waaminifu"

"Nini, usiniambie umemuingiza mwanangu kwenye kazi zenu chafu Mark..."

"Aah hapana unanijua vizuri sina kazi yoyote haramu, Yusto yupo ni mlinzi wa kawaida tu kwenye chuo changu"
"Vipi ulishamwambia ukweli wowote, anajua kuhusu mama yake Madam Jane"

"Hapana, hajui kitu wala hajui kama Mimi namfahamu tangu akiwa mtoto, sijawahi mwambia chochote"

"Afadhali, sitamani hata ajue chochote kuhusu ujinga wa mama yake" Alisema Zubeda.

Kwa mazungumzo haya ilionyesha wazi Mark Moon na Zubeda walikuwa wakifahamiana vizuri sana tangu zamani wakati Zubeda hajapata ugonjwa wa akili, lakini bado haikujulikana wanajuana kwa kiwango gani, kulitokea nini kati ya Zubeda, madam Jane na mark moon mwenyewe.

"Kwa hiyo yule muuwaji Azizi aliamua kumfukuza kabisa Yusto wangu?" Zubeda aliuliza

"Kumbe ulikuwa unajua ni muuwaji, kwa nini sasa ulikataa kuja kuishi na mimi Zubeba, ukaendelea kung'ang'ania kubaki kuishi kwa huyo Azizi hali unajua si mtu mzuri"

"Azizi alinitishia, alitaka nije kwako ki masrahi zaidi, yaani niwe kama mpelelezi wake, alisema kama nisinge fanya hivyo basi angemuuwa dada Asma" alieleza Zubeda.

"Mmh kumbe"
"Ndio hivyo Mark, nilielewa ombi lako lakini sikutaka kuja kuwa changamoto kwenye maisha yako tayari madam Jane alikuwa amekuvunja moyo, mimi tena niingie kwenye maisha yako alafu niwe chawa wa Azizi roho yangu ilikataa kabisa, alafu niambie kwani wewe na Azizi mlikuwa na tatizo gani mbona kama kuna kitu sikukielewa?" Zubeda alieleza na mwisho akamalizia kwa kuuliza swali, swali lililomfanya Mark moon abaki kimya kwa muda.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Upande wa pili Revocatus na Osman Azizi walionekana wakiwa na mazungumzo nyeti ndani ya nyumba moja iliyojengwa pembeni kidogo ya mji.

"Anko sijampata Zubeda, nina wasiwasi labda kashambuliwa na wanyama wakali kule msituni" alieleza Revocatus.

"Usihofu ni hatari kama angekuwa mikononi mwa adui zetu lakini kama kafia huko msituni sio mbaya, siku ya Kiama ni kesho, kesho ndio siku napata kile nachokitaka kutoka kwa madam Jane". Azizi aliongea kwa kujiamini.

"Mmh! sasa anko kwa nini umechagua kukutana na madam Jane ndani ya uwanja wa mpira kwa mkapa tena mda wa mechi ya yanga na Kagera Sugar. Nini unataka bosi?" Revocatus aliuliza.

"Usijali leo nitakwambia nini nataka, unajua mlengwa mkubwa hapa sio madam Jane bali ni Mark Moon mumewe wa zamani"

"Eti nini, yaani mzunguuko wote huu kumbe unamtaka mark Moon, wa nini yani, kivipi? madam Jane atakusaidia nini wakati alishaachana na Mark Moon kitambo sana" Revocatus aliuliza maswali mfurulizo akionekana kutomuelewa kabisa Osman Azizi.

"Nitakwambia kila kitu Revo kijana wangu, ngoja nikusimulie ilivyokuwa, kwanini namtaka Mark Moon kwa miaka yote hii"

Azizi alitulia kwa muda huku akionekana kuvuta kumbukumbu za mbali sana
[emoji294][emoji294][emoji294]

Zubeda alimtazama Mark Moon ambae alikuwa kimya baada ya kuulizwa swali lile,

"Mark moon nimekuliza kwani wewe na Osman Azizi kulikuwa na nini kati yenu?" Zubeda aliuliza tena swali kwa mara nyingine.

"Ni historia ndefu ila kwa kuwa umetaka kujua nitakusimulia" Alisema Mark moon kisha akajaribu kuvuta kumbukumbu za mbali sana miaka mingi iliyopita.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Wakati huo Osman Azizi nae alianza kumsimulia Revocatus kisa kilichopo kati yake na Mark Moon
Ni wakati huo huo pia Mark moon alikuwa akimsimulia Zubeda

Ilikuwa hivi.....
(Anasimulia mark moon)
[emoji294][emoji294][emoji294]

"Tangu nianze kupambana na maisha sijawahi kutana na mfanyakazi mjinga na mpumbafu kama Osmaz Azizi, kipindi hicho alikuwa ni masikini wa kutupwa alikuwa akifanya kazi kwenye migodi yangu huko Katavi. Kuna siku yeye na wenzake watatu wakiwa kazini walipata dhahabu kubwa ilikuwa ni dhahabu kubwa sana, Azizi aliingia tamaa ya kuitaka ile dhahabu kinyume na makubaliano ya mikataba yetu ya kazi inavyosema kwamba kila wanachopata ni mali yangu halafu mimi nawalipa mshahara.
Azizi aliwashawishi wenzake wakimbie na kuiiba ile dhahabu lakini wenzake walikataa kuungana nae.
Baada ya kuona hivyo Azizi aliwauwa wenzake wawili, masikini nakumbuka wale watu aliowauwa walikuwa ni ndugu yaani baba na mtoto wake.
Baada ya kufanya hivyo Azizi alianza kutafuta upenyo wa kutoroka migodini lakini hakufika mbali alikamatwa na walinzi wangu akiwa na ile dhahabu, japo alifanikiwa kuwauwa walinzi wangu watatu, lakini walimdhibiti.
Nilipata taarifa hii nikiwa Madagascar, nililazimika kurudi hadi Tanzania haraka nikasafiri tena hadi Katavi kwenda kusuruhisha kesi hii.

Lilikuwa ni tukio ambalo lingenichafua kwa kiwango kikubwa na pengine serikali ingeninyang'anya migodi yangu sehemu ambayo ilikuwa ni moja ya vitega uchumi vyangu tegemezi kipindi kile.

Niliichukua ile dhahabu kisha nikamfukuza Osman Azizi apotee kwenye uso wangu milele, nilitamani kimuuwa lakini hiyo haikuwa sifa yangu. Azizi aliondolewa mgodini akiwa mikono mitupu licha ya kufanya zaki kwa miezi minne. Azizi alikuwa akilia na kudai ile ni dhahabu yake siku moja atarudi kuifuata.

Miaka ilienda hadi pale nilipokutana na wewe Zubeda nikakupenda lakini ukanikatalia ukisema tayari ulikuwa umeshaharibiwa kutokana na kazi yako ya ukahaba niliyaelewa mawazo yako ila kwa bahati nzuri na mbaya Janeth (Madam Jane) akajisogeza kwangu kupitia mgongo wako mwisho nikamuowa yeye, niseme ukweli nilikurupuka baadae nakuja kujua kumbe madam Jane ana mtoto, nilikutafuta nikakuhoji ukakataa kata kata kuwa madam Jane hana mtoto kumbe huyo mtoto wake (Yusto) ulikuwa nae wewe umemficha, ila mwisho nilijua ukweli nikampa taraka madam Jane.

Nilikutafuta baada ya kusikia madam Jane anakutafuta akuuwe kama kisasi, ndio siku ile nilikuleta hapa nyumbani ukiwa na Yusto nikakuomba tuishi wote nimlee Yusto pamoja na wewe lakini kwa bahati mbaya ulikataa na mbaya zaidi shemeji yako Osman Azizi akakufuata hadi nyumbani.

Hiyo ndio ilikuwa siku naonana na Osman Azizi kwa mara nyingine tena tangu kipindi kile kule mgodini wala sikujua kama unaishi kwake na sikujua kuwa kamuowa dada yako, siku hiyo alikuchukua mikononi mwangu na sikutaka kugombana nae, nikakuacha uende.
Bado Osman Azizi alionekana kuwa na kisasi na mimi kwani kuna ishara alinionyesha ambayo sikuielewa.

Ilikuwa hivyo hadi pale niliposikia kuwa umepata ajali wewe na marehemu dada yako(Asma) na wewe ukaugua kichaa, niliumia sana lakini basi ndiyo hivyo mungu alipanga iwe. Lakini baada ya kipindi chote hicho katukutanisha tena leo tukielekea uzeeni.

Mark moon alimaliza kusimulia.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Ilikuwa ni stori iliyomsikitisha sana Zubeda.

"Ndio maana kumbe, unajua siku ile alipokuja kunichukua kutoka kwako akanirudisha nyumbani kwake nilimweleza kuwa hukuwa na nia mbaya unataka kuniowa na kumlea Yusto pia, Azizi alibadilisha mawazo ghafula na kunitaka nikubali kuolewa na wewe"

"Mmh unasema kweli?"

"Ndiyo mark moon"
"Sasa kwa nini ulikataa Zubeda,"
"Osman alinipa masharti kuwa nitakuwa nikivujisha taarifa kutoka kwako kuja kwake yaani niwe panya wake, nikakataa katakata, akanitishia kuwa nisipofanya hivyo atamuuwa dada na mwanangu Yusto, nikubali kulala na wewe kwako hata kwa wiki moja tu, lakini nilikataa na kubaki na msimamo wangu hadi pale tulipopata ajali, nahisi ni yeye alihusika kusababisha ajali ile, hata hakuwa akimpenda dadangu Asma, ni tamaa zake za pesa basi" Alieleza Zubeda.

"Kwa hiyo ungemsaidiaje ndani ya wiki moja mbona sijaelewa"

"Yeye alisema tu kama nitafanikiwa kuingia chumbani kwako basi kazi yangu ingeisha anasema chumbani kwako kuna Code sijui Code G mimi hata nilikuwa simuelewi kwa kweli"
Alieleza Zubeda lakini baada ya kusema hivyo mark moon alitoa macho kwa mshangao ni kama vile aliambiwa kitu ambacho hakuwa ametegemea kuambiwa.

"Umesama Code G?" aliuliza mark moon.
"Ndio kwani vipi mark" Zubeda aliuliza huku akishangazwa na namna Mark Moon alivyobadilika ghafula.

" Nina msaliti, kuna mtu kati ya watu wangu naowaamini ni msaliti, ee mungu wangu Azizi kajuaje kuhusu Code G, hii ni hatari,yaani kumbe tangu kipindi kile anajua, atakuwa kafanya nini hadi sasa, hapana, hapana, hapanaaaaaa"
Marke moon alihisi kuchanganyikiwa.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Upande wa pili Osman Azizi alimaliza kumsimulia kila kitu Revocatus, kama ilivyokuwa kwa Mark Moon na Zubeda.

"Sasa hapo anko unamtaka madam Jane wa nini" aliuliza Revocatus.

"Madam Jane pekee ndio mwanamke aliyewahi kuingia chumbani kwa Osman Azizi, atanipatia Code G" alisema Osman Azizi.
"Code G ndio nini sasa"
"Subiri utajua kila kitu kesho uwanjani kwa mkapa" alisema Osman Azizi.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Wakati haya yakiendelea Caren na Yusto walikuwa bado chumbani wakiendelea kufurahia penzi lao, zilikuwa zimepita dakika 40 mpaka sasa lakini bado kila mmoja alionyesha kumtaka mwenzake kwa hamu kubwa, walikuwa wamekumbukana sio kidogo.

Walihama kitandani na sasa walikuwa juu ya meza, hakuna hata mmoja alionyesha dalili za kuchoka.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Je, nini kitafuata...?

Code G ni kitu gani?
Mark atafanya nini?
Nini kitatokea uwanja wa mpira kwa mkapa?
Nini hatima ya Caren, Yusto, Brandina na John?

ITAENDELEA..
 
IMG_9645.jpg
 
DO NOT SHOUT

SEHEMU YA 29
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
Hatimae Osman Azizi anaweka wazi ni kitu gani hasa anataka kutoka kwa Madam Jane. Anaeleza kisa chake na Mark Moon ambae ndiye target yake kubwa.
Wakati huo mark moon anagundua kuwa kumbe Osman Azizi alikuwa akimfuatilia na anajua kuhusu kitu anachokiita Code G
Upande wa pili Caren na Yusto wanaendelea kufurahia penzi lao chumbani baada ya kupita kipindi kirefu bila kukutana.

SONGA NAYO....
Revocatus na Osman Azizi walikuwa wakiendelea na mazungumzo, lakini kwa kiasi Revocatus alionekana kutoka kwenye mudi, si kama alivyokuwa awali.

"Anko si ungeniambia tu hiyo Code G ni kitu gani natamani kujua, alafu madam Jane atakusaidia vipi kuipata"

"Nimekwambia mtu pekee ambae anaweza kunisaidia kupata Code G ni yule ambae ameshawahi kuingia chumba anacholala Mark Moon, nani mwingine zaidi ya madam Jane?" aliuliza Osman Azizi.

"Mh sawa, vipi pia kuhusu hao watu uliowauwa kwenye migodi ya Mark Moon kipindi hicho walipelekwa wapi" aliuliza Revocatus huku akimtazama Osman Azizi usoni, akisubiri kusikia jibu lake kwa hamu kubwa.
"Sikumbuki vizuri ila mark alirudisha maiti zao nyumbani wanakotoka kule Morogoro akadanganya kuwa walipata ajali wakiwa ndani ya mgodi wake, akalipa kiasi fulani cha fedha wakafanya mazishi basi ni hivyo tu" Osman Azizi alieleza kwa kifupi, Revocatus akawa kimya kwa muda huku akionekana kuyatafakari maelezo hayo.

"Vipi uko sawa, mbona kama.... au ilikuwa unawafahamu hao watu"
"Hapana hata sijui chochote nahisi nilikua bado sijazaliwa..."

"Hahaha ulikuwepo bana usijione mdogo sana, basi achana na hizo habari, akili na mawazo yako yote elekeza kwenye misheni yetu ya kesho pale uwanja wa taifa kwa mkapa, sisi tutakuwa ndani wewe utabaki nje na gari kama mambo yakienda hovyo utanichukua na kunitoa haraka eneo lile sawa Revo"

"Sawa anko haina shida"
"Nakuamini sana Revocatus nitakuelekeza mpango wote ulivyo, nimechagua uwanjani kwa sababu ndio eneo ambalo nitakuwa salama, namjua vizuri madam Jane pengine anaweza kutaka kuniuwa, lakini itakuwa ngumu kwa sababu hawezi kuingia na siraha yoyote mle ndani ya uwanja halafu mechi itakuwa live Azam Tv, hawezi fanya ujinga, nimeshawapanga vijana wangu vizuri hata kama atakuwa na mpango mbaya dhidi yangu hawezi fanikiwa...." Alieleza Osman Azizi, Akatulia na kupokea simu yake iliyokuwa ikiita.

Revocatus ambae alionekana kunyong'onyea sana aliinuka taratibu bila kuzungumza chochote akaelekea mlango wa kuingia msarani ndani ya nyumba hiyo kubwa.
Wakati huo Osman Azizi alikuwa akiendelea kuzungumza na mtu aliyekuwa upande wa pili wa simu ile.

"Ee bodaboda...sawa.... vizuri....kazi nzuri....safi....sawa...napiga sasa hivi" Aliongea Azizi Kisha akakata simu akapiga tena kwingine, safari hii alimpigia Madam Jane.

Wakati Osman Azizi akifanya hayo Revocatus alikuwa bafuni anajitazama kwenye kioo huku akionekana mwenye hasira sana.

"Haiwezekeani, yaani nimekutumikia kwa kipindi chote hiki Anko kumbe wewe ndiye uliyewauwa kaka na baba yangu kule mgodini, Kwa nini sikulijua hili mapema, Azizi ningekuuwa mwenyewe kwa mikono yangu, siku zote niliamini baba na kaka yangu walikufa kwa bahati mbaya mgodini Katavi kumbe ni wewe Anko uliwauwa kwa sababu hawakutaka kushiriki tamaa zako, leo umejisema mwenyewe anko, wewe ndie uliepoteza dira ya maisha yangu nikajikuta mtoto wa mtaani, Azizi utalipa kwa hili nakuambia nitakuuwa Azizi" Revocatus aliongea huku aking'ata meno yake kwa hasira akijitazama kwenye kioo.

Ni kweli, wale watu aliowauwa Osman Azizi kipindi kile yaani mtu na baba yake walikuwa ni ndugu wa Revocatus ambae alijikuta anapoteza dira ya maisha yake akiwa mtoto mdogo kabisa mara baada ya baba na kaka yake kufa kwenye migodi ya Mark Moon. Baada ya miaka kadhaa kupita ndipo alipojikuta anaangukia mikononi mwa Osman Azizi mwenyewe ambae alimpandikiza katikati ya watoto waliokuwa wakilelewa na Madam Jane yaani akina Caren na wengine.

Revocatus aliumia mno, alitamani kumtafuna Osman Azizi mzima mzima.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Madam Jane akiwa na mwanae John ndani ya gari, ndio kwanza walikuwa wanafika nyumbani mara tu baada ya kutoka kule MOUNTENIA hospital, madam Jane na mwanae John walikuwa wamekaa siti za nyuma ya gari hilo la kifahari wakiwa kimya kabisa, Hakuna aliefungua mdomo kujaribu kuzungumza. John alikuwa amefura kwa hasira, Madam Jane nae alikuwa mbali mno kimawazo. Alikuwa akiyatafakari matatizo yake ambayo yalikuwa yanazidi kuelemea siku hadi siku.
Hata lile tukio la kukutana na Mark Moon pale hospitali aliamini haikuwa bure, tayari alimuagiza mtu afutatilia kujua Mark Moon amefuata nini pale hospitali, akili yake ikawa tayari kupokea taarifa ambayo aliamini itamchanganya.

"Huu mwaka ni wangu jamani, kwa nini haya mambo yamefuatana hivi ee mora wangu hebu nipumzishe basi, huku Azizi, huku Yusto huku John huku Zubeda huku Mark Moon aah jamani kichwa changu kitapasuka sasa" Madam Jane aliwaza wakati huo gari ikifunga breki nje ya jumba lake kubwa la kifahari.

Madam Jane alikuwa ni wa kwanza kushuka wala hakusubiri mlinzi amfungulie mlango kama alivyozoea, huo mda wa kusubiri hakuwa nao kabisa.

Ile anakanyaga ardhi tu, mara simu yake ikaita, alipotazama mpigaji hakuwa mwingine bali Osman Azizi.

Madam Jane alitazama huku na huku kisha akavuta pumzi ndefu na kuitoa taratibu. Alimuona John ambae tayari alikuwa ameshashuka akiingia ndani ya nyumba kwa hasira.

Madam Jane aliipokea ile simu huku mapigo yake ya moyo yakimuenda mbio.

"Azizi"

"Habari yako madam Jane"
"Ni nzuri, nambie"

"Kuna kijana yuko mbele yako hapo nje ya geti"

"Wapi mbona simuoni" aliuliza madam Jane huku akiangalia vizuri ndipo alimuona kijana mmoja akiwa na pikipiki nje ya geti la nyumba yake.

"Yupo hapo nje ge..."

"Nimemuona tayari" Madam Jane alidakia

"Ana mzigo wako naomba uchukue"
"Mzigo gani?"
"Hebu chukua kwanza kisha tuzungumze"

Madam Jane alitulia kwa muda akionekana mwenye wasiwasi, baadae akamuonyesha ishara mlinzi wake mmoja akachukue huo mzigo kutoka kwa yule kijana bodaboda.

Haraka yule mlinzi alifanya hivyo akachukua ule mzigo akarudi nao kwa madam Jane kisha akamkabidhi, yule boda boda aliondoka haraka haraka baada ya kukabidhi mzigo.


Wakati haya yakiendelea John alikuwa ndani ya chumba chake juu ghorofani aliweza kuona kila kinachoendelea pale chini nje ya nyumba yao. Kwa kuwa tayari alishaujua uongo wa mama yake, alitaka kufanya mambo yake kimya kimya, aliinakili namba ya pikipiki ya yule kijana mleta mzigo kisha akapiga picha kadhaa kwa kutumia simu yake.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Madam Jane aliutazama kwa makini ule mzigo aliopewa, ilikuwa ni bahasha ndogo tu.

" Nimepokea tayari"
"Basi fungua hiyo bahasha, hata usiogope Madam Jane, sio bomu hilo" alisema Osman Azizi.
Madam Jane aliifungua ile bahasha kwa tahadhari kubwa. Ndani alikutana na tiketi VIP ya kuingia uwanjani, uwanja wa mkapa kesho yake wakati wa mechi dhidi ya Young African (yanga) na Kagera Sugar.

"Nini hiki Azizi"

"Hapo ndipo Mahali tutakapo kutana kesho kwa ajili ya mazungumzo yetu, kesho ndio siku nitakwambia nini nataka kutoka kwako Madam Jane, karibu tujekushuhudia kwa pamoja jinsi Fiston Mayele anavyotetema" Alisema Osman Azizi kisha akakata simu.

Je, nini kitafuata?
Nini kitatokea kwa mkapa?
Revocatus atafanya nini?
Vipi kuhusu John?

ITAENDELEA....

Malizia simulizi hii kwa tsh 500 tu
Usiache kufuatilia SIMULIZI nyingine nzuri za SAUL DAVID
Njoo WhatsApp au piga 0756862047
 
Usiache kufuatilia SIMULIZI yangu mpya kali kuliko DO NOT SHOUT, bonyeza hapa chini [emoji116]

 
Back
Top Bottom