SIMULIZI RIWAYA
JF-Expert Member
- Feb 19, 2022
- 417
- 1,285
- Thread starter
- #381
DO NOT SHOUT
Sehemu ya 76
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
Email: saulstewarty@gmail.com
ILIPOISHIA....
"Nakuja mamangu" Alisema Caren hali akiwa amevaa sura ya kazi.
Wakati huo ilikuwa ni saa moja kamili.
Refa alipuliza kipyenga na mechi kati ya Yanga na Kagera Sugar ikaanza.
SASA ENDELEA...
"Azizi"
"Nambie Madam Jane"
"Unajua sikuelewi"
"Kivipi yani"
"Kwani tumekuja hapa kuongea au kuangalia mpira?"
"Aah kwa hiyo unataka tuanze kuongea, huangalii mpira kwani?"
"Jaribu kuwa serious basi Osman, sina muda wa kupoteza na unajua, mimi na mpira wapi na wapi?"
"Kama huna huo mda basi ondoka" Osman Azizi alijibu kwa jeuri huku akiendelea kula karanga taratibu.
Madam Jane akamtazama kwa macho makali akionyesha kuwa na hasira za wazi wazi.
"Sikiliza huna haja ya kukasirika Madam Jane, hapa tunafanya kila kitu tunaongea na kuangalia mpira pia" alisema Azizi.
"Unaongea kama utani lakini tambua huu mda unaoniweka hapa utaulipia"
"Okay basi sikia ninamambo kama manne hivi nahitaji kuongea na wewe, ukitimiza yote basi utakuwa umemalizana na mimi kabisa, sitakusumbua tena, nitakwambia moja baada ya lingine, likifungwa goli moja nakwambia kitu cha kwanza likifungwa la pili nakwambia kitu cha pili hivyo hivyo hadi yatimie yote manne"
Madam Jane alibaki kimya akiwa ameduwaa asimuelewe Azizi anawaza nini.
"Hivi huyu mpuuzi ananichukuliaje kwani" aliwaza Madam Jane
"Kwa hiyo wasipofungana inakuwaje?"
"Aah haiwezekani Mayele yupo uwanjani, subiri uone, ila kama itatokea hivyo basi tutaongea ba.....oooh goaaaaaal hahahahah, nilikwambia nilikwambia madam Jane goal"
Aliongea Osman Azizi lakini kabla hajamalizia sentensi yake mara yeye pamoja na mashabiki wa yanga walilipuka kwa furaha mara tu baada ya mchezaji Fiston Mayele kupachika goli la kwanza dakika ya 30' ya mchezo .
Madam Jane alibaki anamtazama Azizi aliyekuwa amesimama kushangilia gori hilo, hakujua ni kwa nini Osman Azizi anarahisisha mambo kiasi kile. Lakini kwa kuwa alikuwa ameshikwa pabaya Madam Jane hakuwa na budi zaidi ya kuendelea kumsikiliza na kumnyenyekea Osman Azizi ili asije kuharibu mambo.
Kwa namna alivyokuwa akishangilia ilionyesha wazi Azizi alikuwa ni shabiki kindakindaki wa timu ya Yanga, lakini ukweli haukuwa hivyo, wala Osman Azizi hakuwa mtu wa kushabikia mambo ya mpira kama alivyokuwa akionekana hivi sasa, kila alichokuwa akikifanya Azizi kilikuwa katika mpango wake.
Alikuwa akijua fika kuwa madam Jane sio mtu wa mchezo hata kidogo licha ya kwamba alikuwa amemshika pabaya lakini ilikuwa nilazima achukue tahadhali ya kutosha.
"Haya niambie hilo jambo la kwanza" alisema madam jane mara baada ya Azizi kukaa.
"Usijali mimi ni mtu wa kutimiza ahadi"
"Haya ongea nakusikiliza"
"Jambo la kwanza nalolitaka kutoka kwako ni hili, najua tayari ushamjua mtoto wako Yusto ni nani, jana umefanya vipimo vya DNA na ukathibitisha hilo sasa nataka unitambulishe mimi kama baba mzazi wa Yusto na John pia" Alisema Osman Azizi.
"Nini wewe unawazimu eti hu...." Madam Jane aliongea kwa kupayuka huku akisimama, Azizi akanyoosha mkono kumuzia asiendelee kuongea.
"Mmm mmm madam Jane hebu tulia kaa chini kwanza, kuna kamera hapa, tuko live Azam Tv, usitake kesho tuwe gumzo magazetini kuliko ushindi wa yanga"
"Ee iwe hivyo hata sijali unaongea nini sasa" Madam Jane alijibu huku akikaa na kuwa mpole.
"Hiki ndio kitu cha kwanza nakuomba bado mengine matatu, kama hutaki basi tuishie hapa mimi niondoke"
"Aah hapana lakini inawezekanaje, kwanza umeishi na huyo Yusto nyumbani kwako, anakufahamu kama Baba mkubwa wake inakuwaje leo uwe baba yake mzazi?"
"Kila kitu niachie mimi, wewe kubali kwanza, kama hutaki basi ila Yusto yupo mikononi mwangu, nitamueleza kila kitu kuhusu unyama uliomfanyia wakati ule unalazimisha kuolewa na mark moon, sijui kama utakuwa tayari mwanao wa kumzaa akuchukie milele"
Osman Azizi aliongea huku akimuangalia madam Jane usoni.
Maneno yake yakaonekana kumgusa, akawa mpole.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Kindoki kiongozi wa ulizi wa ngome ya madam Jane kule msituni alikuwa ndani ya ofisi yake akiwa pamoja na mama na mdogo wake Caren (Dokii).
Ilikuwa imepita saa moja na nusu tangu Dokii na mama yake waletwe kwenye ngome hiyo kama mateka, lilikuwa ni agizo la Madam Jane.
"Kwa hiyo ninyi mmekaa India kwa miaka yote hiyo hata kuzungumza kiswahili hamuwezi, mtanisaidia nini hapa kambini kwangu, madam nae bana. lakini wewe katoto unaweza ukanifaa ee, kwanza unasura nzuri" alisema Kindoki huku akizishika shika nywele za Dokii binti mdogo anaemfuata Caren ambae alikuwa na umri wa miaka kama 15 hivi.
Mara mlango ulifunguliwa ghafula akaingia mwanaume mmoja mwenye asili ya kiarabu.
"Ooh Shafii, umekuja" Kindoki aliongea mara tu baada ya kumuona.
"Ee nimekuja tangu mda nmeleta mzigo sema nikaambiwa uko bize hivi ndio naondoka nikaona nije hata nikuage,"
Alieleza Shafii.
"Sawa nashukuru, anti zuu ameshakagua mzigo si ndio?" Aliuliza Kindoki, Wakati huo Dokii na mama yake walikuwa kimya kabisa, walikuwa wameshalia vya kutosha tangu mambo yalipobadilika kule uwanja wa ndege baada ya kupokelewa na watu wasiowaelewa.
"Ndiyo ameukaguwa tayari uko sawa, basi mimi natoka"
"Powa safari njema Shafii, ila ifike mahali urefuke basi hahahah"
"Hahaha achana na mimi, kwa heri"
Shafii aliaga na kuondoka, akaingia kwenye gari yake aina ya Jeep[emoji2400].
Baada ya kutoka nje kabisa ya ngome hiyo Shafii alienda kwa mwendo wa kasi kama dakika 20 hivi na baadae aliicha barabara ya vumbi akaingia barabara ya rami kuelekea mjini.
Mara ghafula kunamtu aliruka kutoka chini ya uvungu wa gari akagaragara hadi pembeni ya barabara kisha akatulia na kusimama. Shafii hakumuona akaendea na safari yake. Mtu huyo hakuwa mwingine bali Caren.
Tayari Caren alikuwa amefanikiwa kuingia na kutoka katika ngome ya Madam Jane, lakini alishindwa kufanya chochote kutokana na ulinzi mkali ulikuwepo eneo hilo. Ulinzi ulikuwa umeimarishwa mara dufu hasa baada ya Brandina na Yusto kuleta sekeseke la aina yake siku za hivi karibuni.
Kwa mbinu ile ile ya kudandia gari la shafii na kuning'inia kwenye uvungu, Caren aliingia kwenye ngome hiyo wakati Shafii anaingia kuleta siraha.
Caren alitafuta upenyo akatoka na kuyasoma mazingira yote ya ngome hiyo akajua hadi mahali walipo mama na mdogo wake, kisha akarudi kwenye uvungu wa gari hilo bila kuonekana na mtu yoyote hadi pale Shafii aliporudi akawasha gari na kuondoka.
Ilikuwa imepita miaka mingi sana tangu Caren alipomuona mama na mdogo wake kwa mara ya mwisho leo hii anawaona tena wakiwa kwenye kipindi cha matatizo. Ilikuwa ni lazima afanye jambo kuhakikisha mama na mdogo wake wanakuwa salama.
Akapiga hesabu za haraka haraka ni jinsi gani atawaokoa kutoka kwenye ngome ya Madam Jane yenye ulinzi mkali.
Haukupita muda aliliona roli moja kubwa linakuja, Lilikuwa ni roli kubwa lenye tera nyuma likiwa limebeba tenki la mafuta ya petroli.
Caren akasimama katikati ya barabara akawa anapunga mkono akimtaka dereva asimamishe lile gari.
Dereva nae pasipo kujua akajikuta anasimama akiamini msichan huyo mrembo alikuwa akihitaji lifti.
"Wapi mrembo ingia twende" Alisema yule dereva huku akijilambalamba midomo.
[emoji294][emoji294][emoji294]
ITAENDELEA....
Malizia vipande vilivyobaki kwa tsh 400 tu
0756862047
Usiache kufuatilia SIMULIZI zangu mpya.
1.SASHA MLINZI WA NAFSI
2. THE MODERN WAR- vita ya kisasa
Njoo Whatsap 0756862047