Simulizi ya ujasusi: Do not shout (Usipige kelele)

Simulizi ya ujasusi: Do not shout (Usipige kelele)

DO NOT SHOUT

Sehemu ya 76
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
Email: saulstewarty@gmail.com

ILIPOISHIA....
"Nakuja mamangu" Alisema Caren hali akiwa amevaa sura ya kazi.
Wakati huo ilikuwa ni saa moja kamili.
Refa alipuliza kipyenga na mechi kati ya Yanga na Kagera Sugar ikaanza.

SASA ENDELEA...
"Azizi"
"Nambie Madam Jane"
"Unajua sikuelewi"
"Kivipi yani"
"Kwani tumekuja hapa kuongea au kuangalia mpira?"
"Aah kwa hiyo unataka tuanze kuongea, huangalii mpira kwani?"
"Jaribu kuwa serious basi Osman, sina muda wa kupoteza na unajua, mimi na mpira wapi na wapi?"

"Kama huna huo mda basi ondoka" Osman Azizi alijibu kwa jeuri huku akiendelea kula karanga taratibu.
Madam Jane akamtazama kwa macho makali akionyesha kuwa na hasira za wazi wazi.

"Sikiliza huna haja ya kukasirika Madam Jane, hapa tunafanya kila kitu tunaongea na kuangalia mpira pia" alisema Azizi.

"Unaongea kama utani lakini tambua huu mda unaoniweka hapa utaulipia"

"Okay basi sikia ninamambo kama manne hivi nahitaji kuongea na wewe, ukitimiza yote basi utakuwa umemalizana na mimi kabisa, sitakusumbua tena, nitakwambia moja baada ya lingine, likifungwa goli moja nakwambia kitu cha kwanza likifungwa la pili nakwambia kitu cha pili hivyo hivyo hadi yatimie yote manne"

Madam Jane alibaki kimya akiwa ameduwaa asimuelewe Azizi anawaza nini.
"Hivi huyu mpuuzi ananichukuliaje kwani" aliwaza Madam Jane

"Kwa hiyo wasipofungana inakuwaje?"

"Aah haiwezekani Mayele yupo uwanjani, subiri uone, ila kama itatokea hivyo basi tutaongea ba.....oooh goaaaaaal hahahahah, nilikwambia nilikwambia madam Jane goal"
Aliongea Osman Azizi lakini kabla hajamalizia sentensi yake mara yeye pamoja na mashabiki wa yanga walilipuka kwa furaha mara tu baada ya mchezaji Fiston Mayele kupachika goli la kwanza dakika ya 30' ya mchezo .
Madam Jane alibaki anamtazama Azizi aliyekuwa amesimama kushangilia gori hilo, hakujua ni kwa nini Osman Azizi anarahisisha mambo kiasi kile. Lakini kwa kuwa alikuwa ameshikwa pabaya Madam Jane hakuwa na budi zaidi ya kuendelea kumsikiliza na kumnyenyekea Osman Azizi ili asije kuharibu mambo.

Kwa namna alivyokuwa akishangilia ilionyesha wazi Azizi alikuwa ni shabiki kindakindaki wa timu ya Yanga, lakini ukweli haukuwa hivyo, wala Osman Azizi hakuwa mtu wa kushabikia mambo ya mpira kama alivyokuwa akionekana hivi sasa, kila alichokuwa akikifanya Azizi kilikuwa katika mpango wake.
Alikuwa akijua fika kuwa madam Jane sio mtu wa mchezo hata kidogo licha ya kwamba alikuwa amemshika pabaya lakini ilikuwa nilazima achukue tahadhali ya kutosha.

"Haya niambie hilo jambo la kwanza" alisema madam jane mara baada ya Azizi kukaa.

"Usijali mimi ni mtu wa kutimiza ahadi"

"Haya ongea nakusikiliza"

"Jambo la kwanza nalolitaka kutoka kwako ni hili, najua tayari ushamjua mtoto wako Yusto ni nani, jana umefanya vipimo vya DNA na ukathibitisha hilo sasa nataka unitambulishe mimi kama baba mzazi wa Yusto na John pia" Alisema Osman Azizi.

"Nini wewe unawazimu eti hu...." Madam Jane aliongea kwa kupayuka huku akisimama, Azizi akanyoosha mkono kumuzia asiendelee kuongea.

"Mmm mmm madam Jane hebu tulia kaa chini kwanza, kuna kamera hapa, tuko live Azam Tv, usitake kesho tuwe gumzo magazetini kuliko ushindi wa yanga"

"Ee iwe hivyo hata sijali unaongea nini sasa" Madam Jane alijibu huku akikaa na kuwa mpole.

"Hiki ndio kitu cha kwanza nakuomba bado mengine matatu, kama hutaki basi tuishie hapa mimi niondoke"

"Aah hapana lakini inawezekanaje, kwanza umeishi na huyo Yusto nyumbani kwako, anakufahamu kama Baba mkubwa wake inakuwaje leo uwe baba yake mzazi?"

"Kila kitu niachie mimi, wewe kubali kwanza, kama hutaki basi ila Yusto yupo mikononi mwangu, nitamueleza kila kitu kuhusu unyama uliomfanyia wakati ule unalazimisha kuolewa na mark moon, sijui kama utakuwa tayari mwanao wa kumzaa akuchukie milele"
Osman Azizi aliongea huku akimuangalia madam Jane usoni.
Maneno yake yakaonekana kumgusa, akawa mpole.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Kindoki kiongozi wa ulizi wa ngome ya madam Jane kule msituni alikuwa ndani ya ofisi yake akiwa pamoja na mama na mdogo wake Caren (Dokii).
Ilikuwa imepita saa moja na nusu tangu Dokii na mama yake waletwe kwenye ngome hiyo kama mateka, lilikuwa ni agizo la Madam Jane.

"Kwa hiyo ninyi mmekaa India kwa miaka yote hiyo hata kuzungumza kiswahili hamuwezi, mtanisaidia nini hapa kambini kwangu, madam nae bana. lakini wewe katoto unaweza ukanifaa ee, kwanza unasura nzuri" alisema Kindoki huku akizishika shika nywele za Dokii binti mdogo anaemfuata Caren ambae alikuwa na umri wa miaka kama 15 hivi.

Mara mlango ulifunguliwa ghafula akaingia mwanaume mmoja mwenye asili ya kiarabu.

"Ooh Shafii, umekuja" Kindoki aliongea mara tu baada ya kumuona.

"Ee nimekuja tangu mda nmeleta mzigo sema nikaambiwa uko bize hivi ndio naondoka nikaona nije hata nikuage,"
Alieleza Shafii.

"Sawa nashukuru, anti zuu ameshakagua mzigo si ndio?" Aliuliza Kindoki, Wakati huo Dokii na mama yake walikuwa kimya kabisa, walikuwa wameshalia vya kutosha tangu mambo yalipobadilika kule uwanja wa ndege baada ya kupokelewa na watu wasiowaelewa.

"Ndiyo ameukaguwa tayari uko sawa, basi mimi natoka"
"Powa safari njema Shafii, ila ifike mahali urefuke basi hahahah"

"Hahaha achana na mimi, kwa heri"

Shafii aliaga na kuondoka, akaingia kwenye gari yake aina ya Jeep[emoji2400].

Baada ya kutoka nje kabisa ya ngome hiyo Shafii alienda kwa mwendo wa kasi kama dakika 20 hivi na baadae aliicha barabara ya vumbi akaingia barabara ya rami kuelekea mjini.

Mara ghafula kunamtu aliruka kutoka chini ya uvungu wa gari akagaragara hadi pembeni ya barabara kisha akatulia na kusimama. Shafii hakumuona akaendea na safari yake. Mtu huyo hakuwa mwingine bali Caren.

Tayari Caren alikuwa amefanikiwa kuingia na kutoka katika ngome ya Madam Jane, lakini alishindwa kufanya chochote kutokana na ulinzi mkali ulikuwepo eneo hilo. Ulinzi ulikuwa umeimarishwa mara dufu hasa baada ya Brandina na Yusto kuleta sekeseke la aina yake siku za hivi karibuni.

Kwa mbinu ile ile ya kudandia gari la shafii na kuning'inia kwenye uvungu, Caren aliingia kwenye ngome hiyo wakati Shafii anaingia kuleta siraha.
Caren alitafuta upenyo akatoka na kuyasoma mazingira yote ya ngome hiyo akajua hadi mahali walipo mama na mdogo wake, kisha akarudi kwenye uvungu wa gari hilo bila kuonekana na mtu yoyote hadi pale Shafii aliporudi akawasha gari na kuondoka.

Ilikuwa imepita miaka mingi sana tangu Caren alipomuona mama na mdogo wake kwa mara ya mwisho leo hii anawaona tena wakiwa kwenye kipindi cha matatizo. Ilikuwa ni lazima afanye jambo kuhakikisha mama na mdogo wake wanakuwa salama.

Akapiga hesabu za haraka haraka ni jinsi gani atawaokoa kutoka kwenye ngome ya Madam Jane yenye ulinzi mkali.

Haukupita muda aliliona roli moja kubwa linakuja, Lilikuwa ni roli kubwa lenye tera nyuma likiwa limebeba tenki la mafuta ya petroli.

Caren akasimama katikati ya barabara akawa anapunga mkono akimtaka dereva asimamishe lile gari.
Dereva nae pasipo kujua akajikuta anasimama akiamini msichan huyo mrembo alikuwa akihitaji lifti.

"Wapi mrembo ingia twende" Alisema yule dereva huku akijilambalamba midomo.
[emoji294][emoji294][emoji294]

ITAENDELEA....

Malizia vipande vilivyobaki kwa tsh 400 tu
0756862047

Usiache kufuatilia SIMULIZI zangu mpya.

1.SASHA MLINZI WA NAFSI
2. THE MODERN WAR- vita ya kisasa
Njoo Whatsap 0756862047
 
DO NOT SHOUT

Sehemu ya...............,77
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
Caren akasimama katikati ya barabara akawa anapunga mkono akimtaka dereva asimamishe lile gari.
Dereva nae pasipo kujua akajikuta anasimama akiamini msichan huyo mrembo alikuwa akihitaji lifti.
"Wapi mrembo ingia twende" Alisema yule dereva huku akijilambalamba midomo.
[emoji294][emoji294][emoji294]

SASA ENDELEA...
Sasa ilikuwa ni kipindi cha pili cha mchezo uwanja wa Benjamini mkapa, dakika ya 50 ya mchezo yanga wanafunga goli la pili kupitia mchezaji yuleyule Fiston Mayele.

"Haya niambie hilo jambo la pili, unataka nini?" Madam Jane aliuliza.
"Aah! Jambo la pili nataka mimi na wewe tufunge ndoa yaani tuwe mke na mume halali kabisaa" alisema Azizi.

"Hahaha, unawazimu wewe, huoni kama utanipa nafasi ya kukuua ndani ya siku moja tu au hujui kama nakuchukia"

" Wala sijali, namaanisha nachokisema, hakuna kinachoshindikana kama wewe umeweza kufanya mambo ya ajabu ndani ya miaka michache, mambo ambayo tusipoelewana hapa nitaenda kusimama mbele ya waandishi wa habari na kueleza utumbo wako wote nikianzia na mauaji uliyoyafanya kuzamisha meli ya Mv Nyerere" alisema Osman Azizi.

"Haya nimekuewa kitu cha tatu unataka nini nambie"

"Kwanza hayo mawili tumeshakubaliana utafanya si ndio hivyo"

"Si nimesema nimekuelewa wewe endelea sema hicho kitu cha tatu"
"Subiri basi bado goli la tatu halijafungwa" Azizi aliendelea kuongea kwa kujiamini.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Dakika chache baadae ikiwa ni dakika ya 60 ya mchezo, Saido ntibanzokinza anafunga goli la tatu.

" Mnh nakusikiliza" madam Jane aliongea na kumgeukia Osman Azizi.

"Baada ya kuwa umenitambulisha kama baba kwa Yusto na John kisha nikakuoa, nataka nusu ya mali zako zote uzikabidhi kwangu yaani mimi ndio niwe mmiliki halali"

"Azizi sema tu unahitaji pesa kiasi gani, masuala ya kuniambia nikupe nusu ya mali yangu kwani unajua nina utajiri kiasi gani?"

"Hivi kwa nini kila jambo ninalosema mpaka upinge kwanza, najua karibu vitu na biashara zote unazomiliki Madam Jane kuwa na amani hahaha, sijaanza kukufuatilia leo"
Alijibu Osman Azizi.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Wakati Mark moon akiwa nyumbani kwake aliendelea kuwafuatilia Osman Azizi na madam Jane kwa ukaribu kupitia ile screen yake kubwa.

"Simigo Simigo" mark moon aliita kupitia vifaa maalum vya mawasiliano walivyovaa sikioni.

"Ndio bosi nakupata" alijibu Simigo akiwa uwanja wa Benjamini mkapa.

"Mazungumzo yao yanakuwa ni marefu sana hakikisha hakuna kitu madam Jane atampatia Azizi sawa"
"Sawa bosi nimeelewa, tuko tayari kwa kazi" alijibu jasusi Simigo aliyevalia jezi ya Simba akiwa amekaa viti vya VIP, mstari wa tatu kutoka alipokuwa madam Jane na Azizi.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Muda ulikwenda na hatima zikatimia dakika 90 pamoja na zile za nyongeza yanga akiibuka na ushindi wa 3-0.
Tayari watu walikuwa wametoka uwanjani na wengine walikuwa wanamalizika kutoka, waliobaki uwanjani walikuwa wachache sana. Wengi wakiwa ni vijana wa Osman Azizi madam Jane na mark Moon.

Mara Osman Azizi nae akasimama, madam Jane akafuata, wakageukiana huku wakiwa wanatazamana mafahari hawa wawili.

"Kitu cha nne na cha mwisho ni kipi Azizi?" Aliuliza Madam Jane safari hii akionyesha kuvaa sura ya kazi, hakuwa hata na chembe ya masihara.

Badala ya kijibu Azizi aliingiza mkono mfukoni akatoa karatasi moja iliyokunjwa vizuri na kumpatia Madam Jane ambae aliipokea na kuifungua.

Karatasi hiyo ilikuwa na Ramani ambayo juu yake iliandikwa kwa maandishi makubwa KAIMU FOREST ( MSITU WA KAIMU) huu ulikuwa ni msitu uliopo mkoa wa Iringa jirani na kijiji cha Ifunda pembeni ya barabara kuu kuelekea mkoani mbeya. Ulikuwa ni msitu maarufu sana wenye miti aina ya msonobari pekee. Msitu huu ulikuwa ukimilikiwa na Mark Moon tangu zamani na ulikuwa na ukubwa wa heka 21.

"Nini hiki Azizi" Madam Jane aliuliza kama vile haelewi kitu, lakini taratibu mapigo yake ya moyo yalianza kubadilika akawa na wasiwasi usoni. Azizi aliligundua hilo.

"Sielewi nini hiki Azizi" madam Jane alisisitiza.

"Nionyeshe Code G ilipo kwenye hiyo ramani" alisema Osman Azizi huku nae safari hii akiwa amevaa sura ya kazi.

Madam Jane aliinua uso wake taratibu na kumtazama Azizi usoni huku akiwa na mshangao baada ya kusikia kitu ambacho hakutegemea kukisia.
***
Wakati huo Mark moon nae kiti kilikuwa hakikariki akasimama akiwa na remoti mkononi akishuhudia kila kitu

"My forest"(msitu wangu) alisema mark moon huku akiregeza vifungo vya shati lake.
***

"Wewe ni nani Azizi?, Umejuaje kuhusu Code G ya mark moon?" Madam Jane aliuliza akiwa bado kwenye hali ile ya mshangao.
Badala ya kujibu swali Osman Azizi alitabasamu kwa dharau.

"Siwezi, siwezi kukupa code G, ni yangu mimi ndio nitachukua kila kitu kutoka kwa Mark Moon huu nimpango wangu wa muda mrefu huwezi kuniingilia Azizi" madam Jane aliongea kwa hasira.

"Sikia madam Jane, utamaliza miaka na miaka lakini hutoweza, angalia mimi nina kila kitu nimebakisha hiyo code G peke yake, wewe una nini? una nini nakuliza? nionyeshe hiyo Code G"
Alisema Azizi.

"Hahahah, unataka kujua nina nini? mpaka sasa nina hiyo code G na nina hii ramani" Madam Jane aliongea kwa jeuri.
"Ramani sio yako ni yangu"
"Ila kwa sasa ipo mikononi mwangu"

"Usinijaribu madam Jane, nitakusambaratisha vipande vipande"
"Huna huo uwezo Azizi, sijali tena kuhusu siri zangu unazozijua, matarajio yako ni makubwa kuliko kitu ulichonacho, nakuua"
Alisema madam Jane kisha akatoa ishara fulani kwa kunyoosha mkono juu.

Azizi akatabasamu, alikuwa akijiamini kwa namna alivyokuwa amejipanga kwani aliingia uwanjani humo siku moja kabla.

"Siku zote umekuwa msaliti kwangu madam Jane, huwezi kutoka nje ya huu uwanja ukiwa hai" Osman Azizi aliongea kwa kujiamini, akakunja ngumi na kuiachiaa, hii ikawa ni ishara tosha kwa vijana wake waliowepo ndani ya uwanja huo.

[emoji294][emoji294][emoji294]

"Simigo" Mark Moon aliita
"Ndiyo bosi nakusikia"
"Hakikisha unamleta Osman Azizi kwangu akiwa hai, fanyeni haraka msizuiliwe na askari wa ulinzi"
"Sawa bosii usiwe na shaka"
"Hakikisha Yusto anakuwa salama pia, sio mzoefu sana wa kazi kama hizi, nahisi Azizi kajipanga zaidi ya tunavyowaza anaweza akawa ameingia na siraha humo uwanjani"

"Sawa bosi" Simigo alimaliza mazungumzo na Mark Moon kisha haraka akatoa ishara fulani kwa watu wake haraka wakavaa vitambaa(maski) usoni zenye rangi nyeusi.

"Tunamuhitaji Osman Azizi akiwa hai" jasusi Simigo alitoa amri.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Upande wa pili katika ngome ya madam Jane kule msituni.
Walinzi wakiwa hawana hili wala lile ghafula wanashtushwa na ujio wa roli moja kubwa lenye tela lililobeba mafuta ya petroli linakuja kwa kasi.
Roli hilo likiwa limekaribia getini, Caren ambae ndiye aliyekuwa dereva alifungua mlango na kuruka, akaliacha roli hilo linaenda lenyewe.

Geti liligongwa na kurushwa mbali, walinzi wakawa wanakimbia huku na huku kujiokoa wasigongwe, waliokuwa mbali nao wakasogea kuangalia kinachoendelea.

"Wewe simama, nani wewe simama, mpuuzi mmoja" baadhi ya walinzi walianza kupaza sauti wakimtaka dereva asimamishe gari hilo baada ya kuona limeanza kugonga na kuangusha vibanda vyao ndani ya kambi yao wasijue kuwa gari haikuwa na dereva.

Mwisho uvumilivu uliwashinda, sasa wakaanza kufyatua risasi kuyapiga mataili ya gari hilo.
Naam hili Lilikuwa ni kosa kubwa, baadhi ya risasi zililenga kwenye tenki la mafuta, mripuko mkubwa sana ukatokea, walinzi waliokuwa karibu na hata waliokuwa mbali walirushwa na mripuko huo huku wengine wakilia na kukimbia huku na huku miili yao ikiwa imeshika moto.
Ulikuwa ni mripuko mkubwa sana ulioitikisa ngome nzima ya Madam Jane.

Mwisho Caren alichomoa bastola zake mbili kutoka kwenye lile koti lake refu jeusi alilolivaa, bastola moja akaishika mkono wa kushoto na nyingine mkono wa kulia, akaanza kuingia ndani ya ngome ya Madam Jane taratibu huku akiwa ameikunja sura yake, hakuonyesha hata chembe ya masihara.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Moto ulikuwa umewaka pia katika uwanja wa Benjamini mkapa kati ya vikosi vitatu tofauti kikosi cha mark moon, Madam Jane na Osman Azizi, kwa mkapa palikuwa hapatoshi.

Sasa ni tsh 300 tu kumalizia simulizi hii lipa kwa namba 0756862047 kisha njoo WhatsApp namba hiyo hiyo nikutumie mpaka mwisho.

SIMULIZI YA SASHA MLINZI WA NAFSI IMEANZA...
0756862047
 
0756862047
IMG-20230117-WA0011.jpg
 
DO NOT SHOUT

Sehemu ya.................78
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA....
Wakati Caren akivamia kambi ya Madam Jane kule msituni.
Upande wa pili Moto ulikuwa umewaka pia katika uwanja wa Benjamini mkapa kati ya vikosi vitatu tofauti kikosi cha mark moon, Madam Jane na Osman Azizi, kwa mkapa palikuwa hapatoshi.

SASA ENDELEA....

John mtoto wa madam Jane aliamua kufuatilia nyendo za mama yake kwa ukaribu, hata baada ya kupata zile taarifa kuwa mama yake amepewa tiketi ya kuingia uwanja wa mkapa wakati wa mechi ya yanga na Kagera Sugar aliamini kuna kitu mama yake anafanya kwa siri akaamua kumfuatilia, nae akafanya utaratibu akapata tiketi VIP akaingia uwanjani wakati wa mechi.

Mazungumzo yote yaliyokuwa yakiendelea kati ya mama yake na Osman Azizi, John aliyashuhudia kwa mbali kutoka pale alipokuwa amekaa.

Baada ya mpira kumalizika John aliona yale mabishano yaliyokuwa yakiendelea kati ya mama yake Madam Jane na Osman Azizi, akawa anasogea taratibu.

Hapo ndipo mambo yalipobadilika, Madam Jane akatoa amri kwa vijana wake kuwa Azizi auwawe, Azizi nae akatoa amri kwa vijana wake Madam Jane auwawe huku jasusi Simigo nae akatoa amri Osman Azizi akamatwe akiwa hai.

Varangati la aina yake likatokea ndani ya uwanja wa benjamini mkapa. Mashabaki wachache waliokuwa wamesalia uwanjani walishindwa kuelewa ni nini kinaendelea baada ya kuona watu wameanza kupigana ghafula ukizingatia hali ilikuwa tulivu kabisa hapo awali.
Askari wachache wa usalama walipata taarifa na taratibu wakaanza kusogea eneo la tukio.

"Shambuliaaaa, piga risasi" hatimae Osman Azizi alipaza sauti, haraka baadhi ya vijana wake wakaanza kung'oa viti vya mashabiki na kuchukua siraha za moto zilizokuwa zimefichwa chini ya viti hivyo.
Maandalizi haya ya kuficha siraha waliyafanya siku ya jana walipoingia kurekodi tangazo la biashara.

Mara milio ya risasi ilianza kusikika mfurulizo huku watu wa madam Jane na Mark Moon wakianza kuanguka chini mmoja baada ya mwingine baada ya kupigwa risasi, hasa wale waliokuwa wamemzunguuka madam Jane kumlinda.

Ilikuwa ni kitendo kilichowatisha sana mashabiki waliokuwa bado uwanjani hapo ambao awali walikuwa wakichukulia poa tukio hilo wakabaini kuwa hali haikuwa shwari kabisa.
Wakaanza kukimbia huku na huku hali wakipiga kelele kwa hofu.

Jasusi Simigo na watu wake walikuwa wamepanga mipango yote vizuri, walitegea kuwa huenda Azizi na watu wake wakawa wameingia na siraha, na ndivyo ilivyokuwa.

Punde tu baada ya milio ya risasi kuanza kusikika kundi lingine la vijana sita wa Mark Moon liliingia kwa kasi uwanja wa benjamini mkapa, watu hawa sita walikuwa wamevalia nguo nyeusi kuanzia juu mpaka chini kama maninja.
Hawa walikuwa ni maninja kweli kweli kwa namna walivyokuwa wakikimbia na kupaa hewani ilionyesha wazi walikuwa ni watu wenye mafunzo ya kutosha.
Hali hii iliwapa ugumu vijana wa Osman Azizi wakashindwa kulenga shabaha na kujikuta wanaanza kushambuliwa mmoja baada ya mwingine na vifaa maalum vya chuma 'nyota' walivyokuwa wakivirusha maninja hao.

Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya kwa upande wake madam jane akaanza kukimbia akitafuta mlango wa kutokea.

John aliyekuwa amejificha nyuma ya lililokuwa benchi la ufundi la timu ya Yanga alimuona mama yake katikati ya uwanja akikimbia. John aliogopa sana, akaanza kukimbia kumfuata.

"Mama, mama, maamaaa...." John aliita mfurulizo.
Madam Jane aliyekuwa akikimbia hakuamini masikio yake mara baada ya kusikia sauti ya mwanae John akimwita.

Akasimama na kugeuka haraka kuhakikisha kama kweli alikuwa ni John.
Uso kwa uso akakutanisha macho na mwanae ambae alisimama kama hatua tano kutoka pale alipokuwa, wakawa wanatazamana kwa mshangao.

Yusto akiwa amevaa maski usoni kama ilivyokuwa kwa watu wote wa Mark moon alimuona John na mama yake wakiwa wamesimama pembeni ya gori la upande wa mashariki ya uwanja.

Hakujua John kafikaje pale lakini alichojali zaidi ilikuwa ni hatari kubwa iliyokuwa mbele yao kwani shabaha kubwa ya Osman Azizi ilikuwa ni kumuua Madam Jane, licha ya kupewa wakati mgumu na wale maninja lakini bado walionyesha kutokukata tamaa.

Wakati Yusto akiendelea kutazama mara kwa mbali alimuona Osman Azizi akiinuka kutoka chini mara tu baada ya kupigwa teke kali kutoka kwa jasusi Brandina. Akiwa pale chini Osman Azizi aliiona bastola ikiwa imeangushwa na moja ya mtu wake ambae alikuwa amelala pembeni amekufa.
Wakati huo pia Azizi akawaona Madam Jane na mwanae kwa mbali wakiwa wamesimama pembeni ya gori.

Azizi alitabasamu huku akifuta damu kidogo inayomtoka mdomoni akaiokota ile bastola. Brandina aliruka na kujibana nyuma ya kiti kujiokoa asipigwe risasi na Osman Azizi lakini kumbe shabaha haikuwa yeye. Azizi alitaka kumshambulia Madame jane na John.

Kwa bahati nzuri tayari Yusto alikuwa ameshamuona Azizi haraka akakimbia kuelekea uwanjani walipokuwa John na mama yake.

"Joooohn" Yusto aliita huku akikimbia kwa kasi.

John akiwa hana hili wala lile alishtuka baada ya kumuona mtu aliyevaa maski usoni anakuja upande wao kwa kasi.
Kabla hajajua nini afanye mtu huyo(Yusto) alifika na kumrukia wakaanguka chini kwa pamoja.

Wakiwa pale chini walishuhidia Madam Jane anapigwa risasi zaidi ya sita zilizompata kifuani na tumboni, akaanguka chini kama gunia.

"Mamaaaa...." John aliita huku akitaka kuinuka lakini Yusto akamshika kumuzia, baada ya kuona kuna usalama akamuachia.

John alikimbia hadi pale alipolala mama yake.

"Mama, mama , mamaaa" John aliita huku machozi yakianza kumtoka. Hali ya mama yake ilikuwa ni mbaya sana.

"Jo..john mwa..mwa..mwanangu" Madam Jane aliita kwa taabu sana.
"Mama, niko hapa mama yangu"
"Ni..nisa..nisame..samehe"

Wakati huo Yusto nae akasogea na kupiga magoti pembeni ya madam Jane bila kujua kuwa wakati ule alipoanguka chini na John maski yake ilivulika na kukaa upande, sura yake ikawa inaonekana.

Mara tu baada ya kusogea madam Jane aliweza kumuona usoni.
Akawa ananyoosha mkono wake kwa shida akitaka mtoto wake wa kwanza Yusto asogee zaidi. Haraka Yusto akavaa vizuri maski yake na kusogea.
Angalau Madam Jane alipata faraja baada ya kuwaona watoto wake wote wawili wakiwa pembeni yake. Licha ya kwamba alikuwa kwenye hatua za Mwisho za uhai wake lakini jambo hili lilimpa faraja angalau.

Akanyoosha mkono wa kulia akamshika Yusto na mkono wa kushoto akamshika John.

" Nakupe..pe..penda nisa..me.me...me..mehe mwa..mwana...mwanagu..Yu..yus..." Alisema Madam Jane huku hali yake ikionekana kuwa mbaya zaidi, mara akahowa damu mara tatu mfurulizo kisha akatulia tuli, akiwa tayari amekata roho.

"Mamaaaaaaa......." John alipiga kelele na kukumbatia mwili wa mama yake kwa nguvu.

Yusto nae alibaki ametulia huku roho yake ikimuuma asijue kwa nini, hakujua kama madam jane ndiye mama yake mzazi.

"Yusto" mara Yusto alishtushwa na sauti ya mtu ikimuita nyuma yake, akageuka haraka, alikuwa ni Brandina.

"Vaa vizuri maski, twende nje upesi Osman Azizi anakimbia" alisema Brandina, haraka Yusto akainuka na kuanza kumfuata wakaanza kukimbia kutoka nje.

"Tutokee geti hili, huko polisi wameshafika" alisema Brandina.

Wakati huo jasusi Simigo alikuwa akiwasiliana na mark moon ambae kwa sasa alikuwa haoni chochote kinachoendelea uwanjani mara baada ya mtu aliyekuwa akirekodi kuingia kwenye mapambano.

"Hakikisha mnaondoka hapo haraka, polisi wamejaa nje, usiache ushahidi wowote"
"Sawa bosi, vijana waliokufa je?"
"Waacheni hatuna jinsi, muhimu Osman Azizi apatikane" alieleza mark moon.

Wakati huo simu yake ikaingia ujumbe mfupi wa maandishi kutoka namba aliyosave Dr.tony.

"BOSI ILE SAMPULI YA NYWELE ZA JOHN ULIYONIPA NIMEIFANYIA VIPIMO VYA DNA(VINASABA) AISEE HONGERA SANA, JOHN NI MTOTO WAKO KABISA"

Mark moon alirudia rudia kuusoma ujumbe huu mara mbili mbili asiamini anachokisoma.

"Asante mungu, wewe ndio uliyenipa ugonjwa huu nisiwe na uwezo wa kuzalisha tena lakini kumbe ulijua ninae mtoto, tena mkubwa tu, asante sana mungu, ninae mtu wa kuniita baba na mimi nikamwita mwanangu" aliwaza mark moon huku akiwa ameyafumba macho yake na kutabasamu.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Kama walivyokuwa wamepanga na kukubaliana, baada ya Osman Azizi kutoka nje ya uwanja wa benjamini mkapa akiwa salama alimpigia simu Revocatus ambae alikuwa ndani ya gari akisubiri atoke. Akamuelekeza alipo na punde akamuona Azizi anakuja anakimbia huku akigeuka geuka nyuma mara kadhaa kuangalia usalama.

"Hatimae umejileta mwanaharamu wewe, leo ndio siku yako ya mwisho kuliona jua" alisema Revocatus huku akimuangalia Osman Azizi kupitia kioo cha gari 'site mirror'.

Osman Azizi alifika na kuingia kwenye gari moja kwa moja.

"Twende, twende uwanja wa ndege inabidi nikimbie niende nchi za nje kwanza, mambo yameshaharibika, nikiendelea kubaki Tanzania nitakamatwa" alisema Osman Azizi huku akihema kwa nguvu wakati huo tayari Revocatus alishawasha gari na kuondoka kwa kasi.

ITAENDELEA....
0756862047
 
WAKATI TUNAMALIZIA SIMULIZI HII YA DO NOT SHOUT TAYARI SIMULIZI YA SASHA MLINZI WA NAFSI IMEANZA BINYA LINK HAPA CHINI KUINGIA KWENYE UZI WA SASHA

BAKI NA MIMI
(Stay with me)

Sehemu ya..........….79
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA....
"Twende, twende uwanja wa ndege inabidi nikimbie niende nchi za nje kwanza, mambo yameshaharibika, nikiendelea kubaki Tanzania nitakamatwa" alisema Osman Azizi huku akihema kwa nguvu wakati huo tayari Revocatus alishawasha gari na kuondoka kwa kasi.

SASA ENDELEA....
Revocatus alikuwa akiendesha gari kwa kasi sana.

"Vipi unaenda wapi tena si nimekwambia twende airport?" Azizi alihoji baada ya kuona Revocatus amebadili njia na kuanza kwenda tofauti na alivyo muelekeza.

Revocatus hakujibu chochote badala yake akaongeza mwendo kiasi cha kumfanya Azizi asimuelewe, lakini alishindwa kufanya chochote kutokana na Kasi ya gari. Sasa walikuwa wameenda umbali mrefu sana kiasi cha kutoka kabisa nje ya mji.

"Una nini wewe mbona sikuelewi, Revocatus, unanisikia lakini, wapi tunaenda?" Azizi aliendelea kuuliza maswali mfurulizo.
Revocatus alichukua picha moja aliyokuwa ameiweka pembeni ya siti ya dereva akampatia Osman Azizi ambae aliipokea haraka huku akimtazama Revo usoni.

Azizi alishtuka sana mara tu baada ya kuiona ile picha.
Katika picha ile Walionekana Watu watatu. Licha ya kuwa ni picha ya zamani sana lakini Azizi aliwatambua wote.

Wawili walikuwa ni mtu na baba yake aliowaua kule mgodini miaka mingi iliyopita, na huyu wa tatu alikuwa ni Revocatus mwenyewe kipindi hicho akiwa mdogo kabisa.

Akili ya Osman Azizi iliweza kufanya kazi upesi akagundua tatizo lililopo kuwa kumbe aliowaua kipindi kile walikuwa ni ndugu zake Revo.

"Kwa hiyo unataka kusema hawa walikuwa ni ndugu zako?" Azizi aliuliza swali kujihakikishia

"Ndiyo, huyo ni baba yangu huyo mwingine ni kaka yangu" alijibu Revocatus huku akitazama kwenye kioo cha gari 'site mirror' ndipo alipoona pikipiki mbili nyuma yake zikimfuata kwa kasi ile ile kama aliyokuwanayo.

Revocatus alitabasamu kisha akaendelea kukanyaga mafuta. Ni kama vile alijua kila kitu kinachoendelea.
Gari ikazidi kwenda kwa kasi kiasi cha kumfanya Osman Azizi kuogopa.
Watu waliokuwa wakimfuata nyuma na pikipiki walikuwa ni Brandina na Yusto ambao tayari walikuwa wamevua maski zao.
Hawakutaka kumpa nafasi Osman Azizi atoroke hilo lilikuwa ni kosa kubwa kwani mark moon alisisitiza Azizi akamatwe.

"Revocatus sikia hii ilikuwa ni bahati mbaya tu sikuwaua kwa makusudi, wala sikua najua kama ni ndugu zako, ningejuaje sasa eee, anko hebu nielewe tafadhali kumbuka mimi na wewe ni kitu kimoja, tumetoka mbali anko wangu, punguza mwendo basi tuongee" Osman Azizi alijaribu kujieleza kwa Revo ambae wala hakuwa akimjali.

"Anko punguza mwendo basi tutapata ajali" alisema Osman Azizi, Ghafula Revo akafunga breki kali na kusimama, kisha bila kuchelewa akakunja kona kushoto akaacha barabara ya rami na kufuata barabara ya vumbi.
"Tunaenda wapi anko?" Azizi aliuliza kwa upole.

Wakati huo Brandina na Yusto nao walifika na kukunja kona kuelekea upande uleule lilipoelekea gari lililombeba Osman Azizi.
Wakati wakikata kona Brandina alimgeukia Yusto na kumuliza.

"Unaikumbuka hii njia Yusto?"
"Hapana kwa nini?"
"Inaelekea kwenye ile ngome ya madam Jane, hukumbuki walipokuteka walikuleta huku"
"Aah kumbe, sasa unataka kusema Azizi kachukuliwa na watu wa madam jane au?"
"Hapo ndio sielewi sasa, pengine inaweza ikawa hivyo" alijibu Brandina, wakiwa kwenye maongezi hayo mara wakasikia kishindo kikubwa mbele yao na sekunde chache baadae mripuko mkubwa ukasikika.
Yusto na Brandina wakatazamana
"Wameanguka" alisema Yusto, kisha wakaongeza kasi kusonga mbele.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Baada ya Osman Azizi kuona kijana wake Revocatus ni kama hamsikilizi licha ya kuonyesha kujishusha aliona hakuna namna yoyote ya kufanya zaidi ya kutetea maisha yake yeye mwenye la sivyo Revo atamuua tena kifo kibaya sana kwa namna alovyoonekana kuwa na hasira.

Osman azizi aliinuka kutoka kwenye ile siti ya nyuma taratibu na kumvaa Revocatus aliyekuwa ameshikira usukani, akamkaba shingoni kwa nguvu.

Hili Lilikuwa ni kosa kubwa kwani Revocatus aliachia usukani na kuanza kujaribu kujinasua kutoka kwenye mikono ya Azizi.

Hapo gari likakosa muelekeo na kuingia msituni. Azizi anakuja kushituka tayari alishachelewa kwani gari ilikuwa kwenye kasi kubwa sana.

"Ooh my God"(ooh mungu wangu) alisema Azizi huku akimuachia Revocatus, wote wakawa wametoa macho kwa hofu wakati gari ikienda moja kwa moja kugonda mti mkubwa uliokuwa mbele yao.
Likapaa hewani kisha likatua chini kwa kishindo kikubwa likiwa nyang'anyang'a.

Sekunde chache baadae Revocatus alionekana anajaribu kujichomoa kutoka kwenye vipande vipande vya gari hilo huku mwili wake ukivuja damu karibu kila mahali.

Alifanikiwa kutoka akaanza kutembea huku akipepesuka, lakini hakufika mbali gari ikaripuka.
Revocatus alirushwa umbali wa mita kadhaa kutoka pale alipokuwa. Osman Azizi yeye alitawanywa vipande vipande na mripuko ule, huo ndio ukawa mwisho wake.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Sekunde chache baadae Yusto na Brandina walifika eneo la tukio baada ya kusikia kishindo na mripuko ule. Wakapaki pikipiki zao na kusogea haraka hadi pale alipokuwa amelala Revocatus akiwa hoi taabani.

"Yu...yusto" Revocatus aliita kwa taabu.
"Oya jamaa yangu vipi? imekuwaje uko hapa?" Yusto aliuliza maswali mfurulizo kuhusu akijaribu kumuinua Revocatus.

"Acha..usi.usihangaike na..na mimi, nendeni...huko..mbe...mbele mkamsaidie...care...caren yupo kwe...kwenye....ha..ha..hatari kubw...kubwa"

"Unasemaje, Caren? Caren yuko wapi Revo?" Yusto aliuliza hali akiwa ametoa macho kumtazama Revo ambae hali yake ilizidi kuwa mbaya kadri muda unavyokwenda hakuwa na matumaini ya kuendelea kuishi.

"Nime...nimewaleta...hu..huku..ma..ma..maku..sudi, nende..ne..nendeni ..hu..huko mbele...ku...ku..na ngome...kaenda..kumuo...kumuokoa...mama..na...na...na ..m..mdogo..wa...wake, nendeni hara...haraka...ata...ata..ku..ku..fa" Aliongea Revocatus na baada ya kusema hivyo akatulia kimya akiwa tayari amekata roho.

"Oya wewe, Revo, Revo amka basi, Revo, Revoooo aah shiiit" Yusto aliita na mwisho akauachia mwili wa Revocatus kisha akasimama huku akionekana kuchanganyikiwa.

"Relax Yusto, najua hiyo ngome ilipo wewe twende tu naamini tutamsaidia Caren" Alisema jasusi Brandina.

"Sidhani Brandina, kwa nini lakini asiniambie kwa nini asinishirikishe, anafanyaje mambo ya hatari namna hii kimya kimya" Yusto alilalamika huku akiwa ameweka mikono kichwani akawa anapiga hatua kwenda huku na kurudi.

"Huu ni wakati wa kuchua hatua na sio kulalamika Yusto, kwani wewe kuna mambo mangapi hujamuweka wazi mpaka sasa, hebu rudi kwenye ufahamu wako basi caren atakufa ukileta uzembe" Brandina alifoka.

Baada ya kusema hivyo mara walisikia sauti ya mtu akigugumia.

"Mmm mmmm mmmm
Mmmm"

Brandina na Yusto walitazamana kisha wakaanza kufuata uelekeo inakotoka ile sauti hali wakiwa na tahadhali kubwa.

Mwisho walifika mahali wakamkuta mtu mmoja akiwa kifua wazi amefungwa kwenye mti na kujaziwa nguo (singrendi) mdomo asiweze kutoa sauti.

Brandina alikuwa wa kwanza kufika, akamtoa ile nguo mdomoni haraka. Mtu huyu alikuwa ni yule dereva wa roli la mafuta ya petroli aliyekutana na Caren.

"Asante sana ndugu zangu asante sana, hii dunia inawatu wabaya sana yani wabaya mno ina....." Dereva aliongea mfurulizo mara tu baada ya kutolewa ile nguo mdomoni, Brandina akadakia.

"Eleza nini kimekukuta, kwa nini umefungwa hapa"
"Eee bwana wee, mimi nilikuwa zangu safari na roli la mafuta, kufika maeneo haya nikakutana na dada mmoja mzuri tu, akaniomba lifti, alipoingia tu kwenye gari akanibadirikia, alikuwa na siraha akaniteka na kunileta huku akanifunga, kachukua roli langu kaelekea nalo huku msituni, sijui nitamwambia nini bosi mimi jamani" Derava alitoa maelezo haraka haraka.
Baada ya maelezo hayo Yusto na Brandina wakatazamana, kila mmoja aliwaza kama alivyowaza mwenzake wakaamini moja kwa moja kuwa Caren ndiye kafanya hivyo, haraka wakaanza kuondoka.

"Jamani sasa mbona mnaniacha mwenyewe tena" alisema yule Dereva, haraka Brandina akarudi, tofauti na alivyotegemea, Brandina alichukua ile nguo na kuisindilia tena mdomoni kwa yule dereva.

"Mmmm... mmmm....mmmm...... mmmm" dereva alilalamika lakini hakuna aliyejali.
Yusto na Brandina wakapanda kwenye pikipiki zao na kuondoka kwa kasi.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Upande wa pili hali ilikuwa si hali ndani ya ngome ya madam Jane, wingu kubwa la moshi lilikuwa limetanda hewani huku milio ya risasi ikizidi kushika kasi eneo hilo.

Caren alikuwa akifanya majibizano ya risasi na walinzi wa ngome hiyo ambao walikuwa wamesalia wachache baada ya mripuko ule mkubwa uliosababishwa na roli la mafuta.

Caren alikuwa amefanikiwa kuwachukua mama na mdogo wake Dokii lakini namna ya kutoka ilikuwa ni kazi pevu.

Wakiwa wamejificha nyuma ya gari moja bovu Caren aliendelea kufanya majibizano ya risasi na walinzi wa ngome hiyo wakiongozwa na Kindoki. Majibizano hayo ya risasi yalidumu kwa zaidi ya dakika saba mwisho Caren aliishiwa risasi.
Akawaza afanye nini kujiokoa yeye na familia yake lakini hakuwa na majibu.
Wazo la mwisho ambalo alilipata ni kujitokeza yeye mbele ya maadui kisha mama na mdogo wake wakimbie. Ilikuwa ni hatari sana na ilikuwa ni sawa na kujitoa mhanga lakini Caren hakujali hakuwa na namna nyingine yoyote.

"Mama muhungire muri irya misozi, kugira ngo ntimutikire.’'(mama kimbieni msije mkauliwa) Alisema Caren kwa lugha ya kirundi akimtaka mama na mdogo wake waondoke eneo hilo.

"Ntidushobora kubigira Diana" ( Hatuwezi kufanya hivyo Diana) Mama Caren alibisha.

Wakati huo wale walinzi walianza kusogea taratibu huku siraha zao zikiwa mbele tayari kwa mashambulizi. Caren alikata tamaa hakuwa na ujanja tena. Akafumba macho huku akiwa amewashikiria ndugu zake, mama yake akiwa mkono wa kulia mdogo wake mkono wa kushoto.

Walinzi wakiwa wamebakiza hatua kama nne hivi kuwafikia mara ghafula walishtushwa na milio ya pikipiki mbili zikija kwa kasi.

Yusto na Brandina walikuwa wamefika. Licha ya geti kuwa wazi lakini Brandina hakutaka kuonyesha unyonge aliirusha pikipiki yake na kupaa juu ya geti kama kawaida yake.

Walinzi walipogeuka kutazama wanashangaa kuona pikipiki mbili zikiingia ndani ya ngome yao kwa kasi ya ajabu moja ikiwa juu nyingine chini.

ITAENDELEA....

Mkuje WhatsApp sasa tumalizie bureee 0756862047
(USIKOSE SEHEMU YA MWISHO 80 KUMALIZIA SIMULIZI YETU).
 
BAKI NA MIMI
(stay with me)
Mtunzi: Saul David
Email: saulstewarty@gmail.com
WhatsApp: 0756862047

Sehemu ya...............80(MWISHO)

ILIPOISHIA 79....
Yusto na Brandina walikuwa wamefika. Licha ya geti kuwa wazi lakini Brandina hakutaka kuonyesha unyonge aliirusha pikipiki yake na kupaa juu ya geti kama kawaida yake.

Walinzi walipogeuka kutazama wanashangaa kuona pikipiki mbili zikiingia ndani ya ngome yao kwa kasi ya ajabu moja ikiwa juu nyingine chini.

SASA ENDELEA...
Yusto na Brandina hawakuwa na muda wa kujiuliza, moja kwa moja walianza kufyatua risasi huku wakiwazunguuka maadui kwa kupishana. Ndani ya dakika tano kila kitu kilikwisha walinzi wote walikuwa chini wakivuta pumzi zao za mwisho.
Caren aliinuka pale alipokuwa asiamini anachokiona. Ulikuwa ni msaada uliokuja kwa wakati sahihi sana.

"Yusto" Caren aliita, akakimbia na kwenda kumkumbatia Yusto kwa nguvu.

"Umekuja babangu" alisema Caren huku akizidi kumkumbatia Yusto kwa nguvu.

"Nimekuja caren, imekwisha sasa, kila kitu kimekwisha mpenzi wangu" alisema Yusto huku nae akizidi kumkumbatia caren kwa nguvu ambae alishindwa kuyazuia machozi yasimtoke.

Brandina alikuwa amesimama pembeni yao akiwatazama huku akiwa ameachia tabasamu.
Alielewa ni kwa namna gani penzi la wawili hao limepitia misukosuko mingi na mikubwa.

"Nureke ikibiiiiiiiiiii"( geukeniiiiii)
Mara ghafula Dokii mdogo wake Caren alipiga kelele akiwataka wageuke baada ya kumuona mmoja wa walinzi aliyekuwa amelala chini akiinuka na kushika siraha yake akaielekeza upande walipokuwa wamesimama Caren na Yusto, mlinzi huyu alikuwa ni Kindoki ambaye alijeruhiwa kwa kupigwa risasi mbili tumboni.

Caren ndiye aliyekuwa mbele ya Yusto, akiwa amempa Kindoki mgongo. Licha ya Dokii kupiga kelele lakini haikusaidia kitu, walikuwa wamechelewa.

Paaaa!!
Paaaa!!
Paaaaa!!
Kindoki alifyatua risasi tatu mfurulizo.

Yusto alijitahidi akamgeuza Caren kwa kasi yeye ndiye akawa mbele lakini mara Brandina ambaye ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kumuona Kindoki aliwahi na kusimama mbele ya Yusto na Caren.

Risasi tatu zilitua mfurulizo kwenye mgongo wa Brandina, akawa anaanguka taratibu.

Kabla Brandina hajafika chini Yusto alimuwahi akamdaka, wakati huo Caren nae aliwahi na kumpiga kindoki risasi moja kichwani.

"Brandina" Yusto aliita
"Yustoo..naumia, inaumaa" alisema Brandina akiwa kwenye mikono ya Yusto.
Wakati huo Caren, mama caren na Dokii walisogea na kusimama pembeni yao huku kila mmoja akionyesha sura iliyojaa huzuni.

"Jikaze Brandina, tutapata msaada usijali utapona"
"Siwezi Yusto, najisikia fu...furaha kufia kwenye mikono yako" alisema Brandina huku akitabasamu.

"Hapana usife Brandina huwezi kufa, usiniache tafadhali" Yusto aliongea huku machozi yakimlenga.

"Yusto..." Brandina aliita.
"Naam niko hapa"
"U..unaweza ku..ni..nibusu" alisema Brandina, Yusto akatulia kidogo, akainua macho kumtazama Caren, Caren akatikisa kichwa kumtaka Yusto aendelee.

Yusto alishindwa kujizuia, chozi likamdondoka, taratibu akainama na kumbusu Brandina mdomoni, busu lenye hisia na mahaba makubwa.
Brandina alitabasamu na mwisho tabasamu lake likafifia taratibu kwenye uso wake akatulia kimya.
[emoji294][emoji294][emoji294]

[emoji294] BAADA YA MIAKA MITATU(3).
[emoji294][emoji294][emoji294]

(miaka 3 baadae)

"Babu babu babuuuuu"
Mtoto mdogo wa kike mwenye miaka 2 na nusu alionekana anakimbia kwenye bustani moja nzuri ya maua nje ya nyumba moja kubwa ya kifahari. Akawa anamfuata babu yake ambae alijitokeza na kumkumbatia kwa furaha.
Alikuwa ni Mzee Mark Moon.

"Ooh mjukuu wangu mzuri Yusta umekujaa" mark moon aliongea kwa furaha huku akiwa amechuchumaa mbele ya Yusta.

"Ee mekuja babu, mekuja kwenye badai yako" Yusta aliongea kwa kuchangamka.

"Ee baba na mama wako wapi sasa"
"Mewaacha kenye gari, kule nje oo shi wale shi wale pale" alisema Yusta huku akinyoosha kidole, kumuonyesha babu yake mark moon walipo baba na mama yake.

Kwa mbali Yusto na Caren wakaonekana wanakuja huku wakiwa wameshikana mikono, nyuso zao zikionyesha kujawa na furaha sana.

"Karibu wanangu, sikuzani kama mngefika mapema hivi, nilipoambiwa mko burundi nikakata tamaa kabisa" alisema Mzee Mark Moon akionekana mwenye furaha.

"Aah baba tungewezaje kukosa siku yako ya muhimu kama hii" alisema Caren.

"Haya njooni huku wanangu, wengine wapo huku" alisema mark moon, wakasogea hadi eneo maalum lililokuwa nimeandaliwa kwa ajili ya sherehe ya kuazimisha siku ya kuzaliwa mzee mark moon.

Huko walikuta wageni wengine wameshafika, wakaanza kusalimiana kwa furaha.

Alikuwepo Zubeda mama mlezi wa Yusto ambae hivi sasa alikuwa ni mke halali wa mzee mark moon. Alikuwepo Frank, alikuwepo jasusi Simigo, jasusi mpili pamoja na Jasusi Brandina.

Yusto na Brandina walikumbatiana kwa furaha sana. Hawakuwa wameonana kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.

"Haya jamani tuendelee na sherehe yetu, kwa faida ya Yusto na mrs yusto waliochelewa kufika, tulikuwa kwenye ratiba ya kila mtu kutoa maneno ya baraka katika siku hii ya kuzaliwa baba yetu mark moon, sasa ilikuwa ni zamu ya Brandina, tuambie una wish nini jasusi wetu uliyenusurika kifo hahahaha"
Frank ambae ndiye aliyekuwa mshereheshaji aliongea na kuleta utani wote wakacheka kwa furaha kisha kukawa kimya wote wakageuka kumsikiliza Brandina.

"Mmmh jamani mimi nawish, mmmm ukweli nawish litokee sekeseke lingine tena watu tuingie kazini, sijazoea kabisa kukaa miaka mitatu bila hata kusikia sauti ya risasi" alisema Brandina hapo watu wote wakaangua kicheko.

"Jamani zamu yetu ya kusema lolote imepita au bado?" mara sauti ya kiume ilisikika, wote wakageuka kuangalia, alikuwa ni John akiwa pamoja na Sophia, ndio kwanza walikuwa wanafika.

"Ooh jamani wanangu mmekuja, mmefikaje mapema hivi, mmetoka lini india" Zubeda aliuliza huku akionekana mtu mwenye furaha sana baada ya kumuona Sophia na John ambao kwa sasa walikuwa ni mke na mume kama ilivyo kwa Yusto na Caren.

"Mama tumefika tangu jana mbona" alijibu John huku akivuta kiti na kukaa.

"Haya wenzenu wamenileta mjukuu hapa, huyu hapa Yusta vipi nyie imekuwaje huko kwenye matibabu?"aliuliza Mark Moon huku akitabasamu.

"Aah mzee huwezi kuamini, shemeji Caren amesababisha mke wangu Sophia sasa hawezi kushika mimba" alisema John.

"Aah acha kumsingizia mke wangu bana, hao madokta wanakudanganya tu, siku ile nakumbuka Caren wangu alimuuliza Sophia kichwani sasa kichwa na tumbo la uzazi vinahusiana nini eti jamani? " Yusto aliongea akimalizia na kicheko.

"Ooh muone huyu sijui kasoma shule gani hujui kichwa ndio injini wa mwili wote homoni zote za uzazi zinatoka kichwani kaka yangu Yusto hajui lolote, hahahah"

"Joo hebu acheni utani wenu tumechelewa halafu bado mnaleta stori za uongo, baba usiwasikilize hawa, ki ufupi nimetibiwa na niko salama kabisaa, tegemea mjukuu mwingine kwanzia sasa" alieleza Sophia.

"Ooh mashallah nafurahi kusikia hivyo binti yangu, haya kaeni sasa"

"Haya jamani tuendelee na sherehe yetu, nitoe nafasi ya upendeleo kwa bi Zubeda, atoe baraka zake kwa niaba yetu sote, karibu sana"
Alisema Frank,
Zubeda alisimama na wote wakakaa kimya kumsikiliza.

"Asante sana mwanangu, Binafsi napenda kuchukua nafasi kumshukuru mungu kwa kutukutanisha hapa pamoja kwenye sherehe ya mume wangu tukiwa wazima wa afya.
Mungu ni mwema ni mwema sana, kila mmoja hapa anaelewa ni kwa namna gani tumepita kwenye kipindi kigumu, kipindi ambacho bila mungu kuwa upande wetu basi tungekuwa tunazungumza mengine hii leo.
Kila mtu hapa ana stori yake ambayo inaeleza ni magumu yapi ameyapitia mpaka hivi leo, si Yusto si John si Caren si mimi si Brandina, wote tumepitia magumu mengi lakini ashukuriwe mungu wa mbinguni kwa kutuvusha tukiwa salama. Niombe furaha yetu tuliyonayo leo basi idumu daima kwenye kizazi chetu na hata kizazi cha mjukuu wangu Yusta na wengineo.
Maisha tuliyoyapitia yamebeba tafsiri halisi ya changamoto za dunia, ukiangalia kuna vitu vingi sana vya watu kujifunza kutoka kwetu, kuna suala la uvumilivu, uaminifu, visasi, usaliti mapenzi ya dhati, na mambo mengine mengi mno, nimemtafuta mtu aandike simulizi ya maisha yetu ili hata wale ambao hawatufahamu basi wajifunze kupitia hiyo SIMULIZI, na tayari mtu huyo ameshaanza kazi ya kuandaa simulizi hiyo ambayo ameipa jina la STAY WITH ME yaani BAKI NA MIMI na kapendekeza kuwa wahusika wakuu wawe Caren na Yusto, naamini watu watakaoisoma simulizi hii pamoja na kuburudika lakini pia watajifunza mambo mengi sana, asanteni"
Zubeda aliyekuwa akizungumza kwa hisia, alimaliza na kukaa kwenye kiti. Maneno yake yakamgusa kila mmoja aliyekuwa mahali pale.

"Asante sana bi Zubeda, jamani naomba kwa heshima wote tusimame tugonge chiazi kumpongeza bi Zubeda kwa wazo zuri" alisema Frank, wote wakasimama huku kila mmoja akiwa na glasi ya kinywaji mkononi.

"Haya cheers kwa ajili ya simulizi ya BAKI NA MIMI"

"Cheiaaaaaaaaazi"

[emoji294]MWISHO[emoji294]
SAUL DAVID MWANAWIMA
+255756862047
saulstewarty@gmail.com
2022.

SIMULIZI ZA SAUL DAVID LIZOPO SOKONI NI:-

1. SASHA MLINZI WA NAFSI

2. MODERN WAR- vita ya kisasa

3. STAY WITH ME - Baki na mimi

Ni simulizi gani unahitaji kati ya hizi
 
Umetisha mkuu
 
Back
Top Bottom