Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwandishi Nimejiuliza sana kuhusu Jina lako, ni lenyewe, limepangwaau ni coincidenceFO NOT SHOUT
.…..27
NA SAUL DAVID
Baada ya kumaliza kuisoma tayari machozi yalikuwa yakimtiririka, John akainua uso wake na kumtazama mama yake.
"Ma..mama" John aliita kwa sauti ya uchungu.
Madam Jane alikaa kimya kwa sekunde kadhaa Kisha akajibu huku nae machozi yakimlenga.
"Yes, he is your brother, Yusto"( ndiyo ni kaka yako, Yusto)
SASA ENDELEA...
" Mama" John aliita tena
"Nitakweleza kila kitu mwanangu,"
"Kila kitu kitu gani mama,ulikuwa wapi siku zote, kwanini hukuwahi kuniambia ukweli, ulikuwa unasubiri nini mama, ni mangapi umenidanganya hadi leo" John aliongea kwa jazba.
"Nina sababu ya kufanya hivyo John, jaribu kunipa nafasi nikueleze"
"Utaniambia nini nikuelewe mama, wakati wote huu umeniweka gizani sielewi chochote, eti leo ndio uniambie ukweli, ukweli upi?, kipindi tupo Dubai ni mara ngapi nilikuuliza kuhusu hili, ni mara ngapi nilikuomba unikutanishe na ndugu zangu ulinijibu nini mama ulisemajeeee!!!,ona sasa leo hii mimi nagombana hadi na kaka yangu, kaka ambae tumezaliwa tumbo moja mama kweli, kweli mama?" John aliongea kwa uchungu.
"Nisamehe John sikujua kama haya yatatokea nili..."
"Hukujua eti, hukujua kabisa si ndiyo, haya umeshaona yaliyotokea sasa ni wakati wa kusema kila kitu unachokificha, sema yote sasa hivi, baba yetu mimi na yusto ni nani, ni nani ulifunga nae ndoa mkaachana, kwa nini mkaachana?, Yule mama kichaa kule mtaani ambae umetuaminisha kwa miaka yote kuwa ni mama yake yusto nae ni nani"
" John utajua kila kitu, usijali, hapa sio mahala pake"
"Sitaki sema sasa hivi nambie, nataka kumjua baba yanguuuuu....." John alipaza sauti kwa nguvu, mara alihisi kuna mtu amemshika bega nyuma yake.
"Kijana hii ni hospitali, kwanini unapiga kelele, nendeni mkakae mahali mzungumze, kuna wagonjwa wanahitaji utulivu" ilikuwa ni sauti ya mzee mmoja aliyemshika John begani. John akageuka na kumtazama.
Alikuwa ni Mark Moon akiwa ameongozana na walinzi pamoja na jopo la madaktari, walikuwa wakielekea kwenye chumba alicholazwa Zubeda, kwa bahati nzuri au mbaya wakakutana na purukushani ile iliyokuwa ikiendelea kati ya John na Madam Jane.
Mwanzo Mark Moon hakuwa amemuona madam Jane wala madam Jane hakuwa amemuona mark moon, baada ya Mark Moon kumshika bega John ndipo alipokutanisha macho na Madam Jane mkewe wa zamani.
Ilikuwa ni kipindi kirefu kimepita tangu Madam Jane kuonana na mark moon kwa mara ya mwisho, leo hii wanakutana Mountenia hospital tena pamoja na mtoto wao John.
Ilikuwa ni kwa mara ya kwanza pia John kumuona baba yake uso kwa uso na asijue kama ni baba yake, wakati wote aliishia kuona picha zake kwenye mitandao, akimuona kama mzee mmoja tajiri na mmiliki halali wa chuo anachosoma.
Kimya kilitawala kwa dakika kadhaa, wote wakawa wanatazamana kwa zamu, lilikuwa ni tukio ambalo hakuna aliekuwa ametegemea kama wangekutana pale.
"Samahani mzee, ilikuwa ni lazima nipige kelele hata ungekuwa wewe usinge kubali kudanganywa kwa miaka zaidi ya ishirini tena na mama yako mzazi, inauma sana mzee wangu" John alieleza kwa uchungu.
Madam Jane na Mark Moon wakatazamana kwa macho yanayozungumza, ni kama vile Mark Moon ameanza kuielewa kesi iliyokuwa ikiendelea kati ya John na mama yake.
"Nimesikia unalalamika humjui baba yako si ndio hivyo?" aliuliza mark moon huku akiwa bado amemshika John begani.
"Ndiyo mzee wangu embu fikiria tangu nizaliwa naambia baba yangu amekufa alafu leo ni......" John alieleza lakini mark moon akamkatisha.
"Basi basi inatosha, sasa hili ni suala nyeti sana kijana wangu halimalizwi kwa kupiga kelele kama hivi, mchukue mama yako, nendeni sehemu tulivu kaeni mzungumze atakuambia kila kitu kwa sababu huyu ni mama yako na huna mama mwingine ziadi yake, sawa kijana" alisema mark moon safari hii akimshika John kichwani huku akimvuta vuta nywele taratibu kumfariji. Yalikuwa ni maneno ya hekima yaliyomuingia vizuri John.
Baada ya kusema hivyo, mark moon, walinzi na lile jopo la madaktari waliondoka, wala hakuonyesha kujuana na madam Jane.
Baada ya sekunde chache John nae akaondoka akiwa bado na hasira.
"John, we john embu simama hapo" madam Jane ambae ni kama alikuwa ameshikwa na ganzi ya ghafula alishituka kutoka usingizini, haraka akaanza kumfuata mwanae John huku akimwita.
Mark moon ambae kwa sasa alikuwa ndani ya lift ya kioo aligeuka na kuwatazama kwa chini madam Jane na mwanae John wakikimbizana.
Baadae Mark Moon alijitazama mkononi kwenye vidole vyake kulikuwa na nywele kidogo sana alizozipata kutoka kwenye kichwa cha John wakati ule akimshika shika na kumvuta nywele. Mark moon alijua nini anafanya, akageuka na kumnong'oneza kitu fulani daktari aliyekuwa pembeni yake, yule daktari akatoa mipira (gloves) mfukoni haraka Kisha akachukua zile nywele kwa uangalifu mkubwa kutoka kwenye vidole vya mark moon kisha akaziweka kwenye lailoni moja maalum na kupachika kwenye mfuko wa koti lake jeupe.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Upande wa pili....
Yusto alifungua mlango wa chumba chake kwa nguvu na kuingia ndani, mara Caren nae akafuata nyuma.
Ilikuwa ni dakika chache tu mara baada ya kutoka ukumbini baada ya kumalizika kwa sherehe ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa Yusto.
"Ndio umefanya nini pale Yusto" Caren aliuliza kwa ukali kiasi.
"Ulitaka nifanye nini Caren, nimuache aendelee kutuaibisha mbele za watu, aharibu sherehe ambayo watu wametumia pesa zao kuiandaa kwa ajili yetu?"
"Sawa Yusto lakini hukutakiwa kufanya vile, umemdharirisha sana mwenzio"
"Mwenzangu kivipi yani? Mbona yeye kanidharirisha pia"
"Sawa yule ni John, na wewe ni Yusto hamuwezi kuwa sawa tabia zenu ni tofauti sana, sijakuzoea hivyo mimi"
"Caren unanilaumu bure,John ni katiri, ile ndio adhabu anayostahili, kuaibika mbele za watu anaotaka wamuheshimu kwa nguvu"
"Basi basi baba usiwe na hasira hivyo, lakini tambua umefanya makosa Yusto, vipi kama maneno yale ungeambiwa wewe, ungekubali mama yako aongelewe vibaya kiasi kile mbele za watu, hata kama ni kweli lakini noo...."
Yusto akawa kimya huku hasira yake ikionekana kushuka taratibu, Caren akasogea na kumkumbatia kwa nyuma mgongoni.
"Sorry kama nimekuudhi Yusto wangu" Caren aliongea kwa sauti ya kudeka.
Yusto akaweka mikono yake kiunoni ilipo mikono ya Caren kisha akawa anaipapasa taratibu.
"Nimekuelewa mpenzi wangu, samahani pia, sikujua kama nitakuudhi'
Alisema Yusto.
Caren akavuta pumzi ndefu na kuitoa taratibu.
"Usijali naelewa, enhe niambie za huko ulikokuwa? " Aliuliza Caren.
"Nzuri kiasi nimepitia...." Yusto alijibu lakini kabla ya kumalizia sentesi yake, Caren alimgeuza ghafula na kumuwekea kidole chake mdomoni.
"Shiiiii, utanieleza baadae hizo habari mwenzio nimekumiss sana" alisema Caren huku akimtazama Yusto kwa macho yaliyoregea.
"Mmmh jamani baby" Yusto aliongea huku akitabasamu.
"Mmh nini? ..." Caren aliuliza huku akimsukumia Yusto kitandani, Kisha akamrukia na kumkalia kwa juu.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Osman Azizi alionekana akiwa ndani ya uwanja wa taifa maarufu kama uwanja wa mkapa. Alikuwa ameongozana na vijana wengi sana karibu 20 hivi wakirekodi mkanda wa video kwa ajili ya tangazo la bishara yake ya kununua na kuuza magari.
Osman Azizi alikuwa amekamilisha taratibu zote za kuingia na kuutumia uwanja wa mkapa licha ya kwamba kesho yake iligetemewa kucheza mechi kubwa kati ya timu ya Young Africa (yanga) dhidi ya Kagera sugar lakini Osman na watuwake ambao walivaa kama dancer(wachezaji) waliruhusiwa kurekodi tangazo hilo kutokana na ushawishi na nguvu ya kifedha aliyoitumia Osman Azizi.
Haikuwa kama walivyofikiri, Osman Azizi alikuwa na jambo lake tofauti.
Alikuwa akijiandaa na tukio kubwa alilotegemea kulifanya kesho yake, wale watu hawakuwa wachezaji bali vijana wake wa kazi waliofika hapo kufanya maandalizi kwa kivuli cha kurekodi tangazo.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Zubeda alifumbua macho yake taratibu akajikuta yupo kitandani ndani ya chumba ambacho hakuwa na sababu ya kujiuliza mara mbili, ilionyesha wazi yupo hospitali tena hospitali kubwa ya gharama.
Kumbukumbu zake zilikuwa zimerejea vizuri kabisa, akawa anakumbuka kila tukio lililotokea kwenye maisha yake.
Zubeda mama mlezi wa Yusto akajikuta machozi yanamtoka kama maji, alikuwa amepitia kipindi kigumu mno kwenye maisha yake.
Mara mlango ulifunguliwa, Zubeda aligeuka na kumtazama mtu anaeingia wakati ule, aliweza kumtambua.
"Mark moon" Zubeda aliita.
Mark moon aliingia taratibu akafunga mlango, akavuta kiti na kukisogeza pembeni ya kitanda alicholala Zubeda, akakaa huku akimtazama Zubeda usoni.
Je, Nini kitafuata?
Zubeda anakumbuka nini kuhusu Mark moon?
Mark anampango gani dhidi ya Zubeda lakini pia vipi kuhusu zile nywele za John alizochukua?
Caren na Yusto bado wahawajajuana kwa asilimia zote, watatoboaa?
Osman Azizi nae anaandaa kitu gani kwa mkapa(uwanja wa taifa)?
USIKOSE VIPANDE VICHACHE VYA MWISHO KUMALIZIA SIMULIZI YETU, ASANTE.
0756862047
HakikaTumfungulie kesi polis huyu