๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐
(Stay with me)
๐ฌ๐๐๐ฌ๐จ๐ง 2
Sehemu ya...........17
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
๐LIPOISHIA....
"Sikia Janeth hauna haja ya kuogopa hakuna anaejua zaidi yangu, ukifanya kile nachokitaka basi mambo yatakuwa shwari, nitamkabidhi mwanao mikononi mwako, halafu wala sihitaji pesa zako mimi. Ila nakupa onyo, ukijaribu kuleta ujanja wa aina yoyote, yani hata ukiniuwa hakuna utakachokipata na siri zako zote zitakuwa hadharani, kwa mara nyingine tena utapata aibu ya Dunia aibu ambayo sidhani kama safari hii utakuwa na ujasiri wa kuibeba"
Osman Azizi aliongea kwa kumaanisha.
Je, nini kitafuata?
SASA ENDELEA....
Madam jane alihisi kuchanganyikiwa alitamani ardhi ipasuke immeze, hakujua ni vipi Osman Azizi amejua taarifa zake nyingi tena za siri kwa urahisi kiasi kile, ilionyesha wazi alikuwa akimfuatilia tangu muda mrefu, haikuwa bure lazima pia kuna mtu wake wa karibu alikua anavujisha siri zake.
"Unataka nini Osmaniiiiiiii" madam Jane alipaza sauti na kusimama kwa hasira.
Osman Azizi nae akasimama huku akimtazama madam Jane kwa macho ya dharau Kisha akatabasamu, sigara ikiwa mdomoni mwake.
"Kwa sasa ondoka madam Jane, nenda kayatafakari vizuri mambo niliyokwambia leo, subiri simu yangu nitakwambia lini na wapi tukutane kwa ajili ya mazungumzo zaidi, hiyo siku ndio nitakayokwambia nini nataka, kumbuka usilete ujanja wa aina yoyote, nimejipanga"
Alisema Osman Azizi huku akimuonyesha ishara madam Jane kuwa aondoke.
Madam Jane alimtazama Osman Azizi kwa macho makali kisha akachukua mkoba wake pale mezani akatoka nje kwa hasira, akaondoka zake.
Osman alimpa ishara fulani msaidizi wake wa kazi aliyekuwa amesimama mlangoni, akageuka na kumfuata Madam Jane kwa nyuma.
Sekunde chache baadae Revocatus alitoka nyuma ya lile kabati alilokuwa amejificha, akawa anaongea na simu.
"Unasema hujamuona Yusto hadi muda huu" aliuliza Revocatus
"Ee hayupo hapa chuoni, nimeanza kupatwa na wasiwasi tena jamani" Caren alisikika upande wa pili akiongea na Revo.
"Sikiliza Caren, nisikilize mimi, nina uhakika Yusto yuko salama yani yuko salama kabisa trust me"
"Sasa yuko wapi, simu yake imezimwa, chuoni hayupo, ni nani kwani aliondoka nae"
"Ni mdada tu hivi, yaani alikuja akamuokowa na kuondoka nae hawezi kumfanya kitu kibaya niamini mimi, nisinge kuruhusu tutoke kule msituni kama Yusto hayupo salama"
"Mmh sawa basi ngoja niendelee kusuburi, vipi kuhusu mama nae anaendeleaje"
"Nani Zubeda?"
"Ee ndiyo"
"Yupo amelala"
"Umemchoma sindano tena"
"Aah hapana kalala mwenyewe tu" Revo alidanganya.
"Sawa basi ngoja niendelee kumsubiri Yusto"
"Sawa"
Caren akakata simu.
[emoji294][emoji294]
"Vipi ni nani unaongea nae" aliuliza Osman Azizi
"Ni caren, anadai Yusto bado hajarudi chuoni, sio muhimu sana anko hebu tuongee vizuri unampango gani na Madam Jane, yaani tangu nimjue sijawahi ona katetemeshwa kiasi hiki" Alisema Revocatus
"Kijana wangu mambo ndo kwanza yanaanza, subiri utashuhudia mwenyewe"
"Lakini nimesikia unasema hutaki pesa zake, sasa ni nini unataka kutoka kwake mbona nashindwa kukuelewa anko wangu"
"Sikiliza Revo, hebu kaa kwanza tuongee" Alisema Azizi kisha wote wakakaa huku wakitazamana uso kwa uso.
"Revo, mara ya mwisho kuangalia picha la kihindi ilikua lini?"
Aliuliza Azizi
"Mmh sikumbuki unamaana gani?"
"Hili ni kama picha la kihindi tena picha babu kubwa, ni jambo kubwa nililolisubiri zaidi ya miaka 20 hahah ahahaha" Aliongea Osman Azizi kisha akamalizia na kicheko, kicheko kikubwa sana, kilichojaa dharau na majigambo.
Revo akawa anamuangalia tu huku akitamani kumuelewa.
"Revo, kila kitu kinaenda kama nilivyopanga, muda sahihi ukifika nitakwambia nini nataka kufanya, wewe sasa hivi nisikilize kwanza"
"Sawa anko nakusikiliza, nambie hatua inayofuata"
"Iko hivi, kwa sasa Madam Jane amechanganyikiwa kupita kawaida, namjua vizuri baadae atatuliza akili yake awaze nini cha kufanya, unajua atafanya nini?"
"Sijui anko, ila labda atataka kukuua"
"Hapana hawezi kuniua kwa sababu mimi ndiyo najua Yusto ni nani na yuko wapi"
"Mmh! Sawa lakini si nimeshakwambia madam Jane leo alimteka Yusto na pengine ameshajua kama ni mwanae"
"Hapana hajajua ila kahisi tu ndio maana amekuja kwangu leo, na hata kama akijua bado mimi nitakuwa na umuhimu mkubwa, anajua naweza kumwambia Yusto kile alichokifanya na Yusto akamchukia mama yake milele, si unajua Yusto haelewi chochote mpaka leo anajua tu Zubeda sio mama yake mzazi basi"
"sawa anko, lakini huyu huyu madam Jane si ndio alitaka kumuua Yusto unafikiri kwa sasa Yusto atakuwa na umuhimu kwake hadi atoe hicho kitu unakitaka kutoka kwake"
"Hahah Revo kuwa uyaone, kipindi kile alitaka kumuua kwa sababu alikuwa na shida na pesa sawa, lakini sasa hivi pesa anazo hana cha kupoteza tena, unajua KUNA UMRI UKIFIKA UNAONA FAMILIA NI BORA KULIKO PESA, kwa sasa Madam Jane anamuhitaji Yusto tena sana"
"Mmmh"
"Ndo hivyo anko, sasa atakachokifanya Madam Jane ni kukusanya nguvu kwa ajili ya kupambana na mimi ila sio kuniua, kwanza atataka kujua nini nataka kutoka kwake"
"Kwa hiyo unafanyaje hapo"
"Nataka tumchanganye Madam Jane, kwanza nataka nimvuruge na wale watu anawategemea kumpa nguvu, wewe utanisaidia kwa upande wa Caren"
"Kivipi anko nimuue Caren?"
"Aah hapana, nataka uende uongee na Caren umueleze ukweli wote kuwa madam Jane sio mtu mzuri wala hapokei Oda za serikali kama alivyowambia , mweleze ukweli wote kuwa madam Jane ni jambazi tu na anawatumia ninyi kufanya mambo yake ya uharifu na kulipa kisasi kwa Mark Moon, baada ya hapo unaijua roho ya Caren hawezi kuvumilia hili"
"Enhe baada ya hapo nini kitafuata"
"Ukitoka hapo nenda kwa Madam Jane bosi wako kamweleze kwa unyenyekevu kuwa umegundua vitu vya siri anavyovifanya Caren, mwambie kuwa Caren emevunja agizo lake hataki kumuua Zubeda na badala yake amemficha kambini kwenu, inaonekana kuna mtu mwingine anashirikiana na Caren kwa siri"
"Duuh anko wewe ni nouma, sijui hata unawaza nini, kwa hiyo hapo utakuwa umewagonganisha Caren na Madam Jane si ndiyo"
"Yes, Caren anauwezo mkubwa na nimtu anaependa haki ni lazima atampa shida Madam Jane, Wewe fanya hivyo utanielewa taratibu"
"Sawa haina shida, basi ngoja nirudi kambini au kuna kingine"
"Hapana kukiwa na shida nitakupigia muwahi kwanza huyo Zubeda wenu"
"Sawa anko"
Revocatus alianza kuondoka lakini baada ya kupiga hatua kadhaa akasimama na kugeuka.
"Enhe anko nilikusikia unasema eti madam Jane ndio aliyesababisha kivuko cha MV NYERERE kuzama kivipi yani?"
"Ni stori ndefu Revo hebu kwanza niache nipumzike, nina mambo mengi ya kufanya" alijibu Azizi huku akijilaza kwenye kiti.
"Noo anko hebu nambie hata kwa kifupi tu, unajua niwatu wengi sana walikufa kwenye ile ajali sababu ilikuwa ni nini Madam Jane kufanya hivo"
"Alitaka kupoteza ushahidi"
"Ushahidi? ushahidi gani yani"
"Kuna kesi ilikuwa mahakamani mwaka 2018, John mtoto wa Madam Jane aliuwa mtu kwa makusudi kisa ikiwa ni wivu wa mapenzi huko visiwani ukerewe, kwa bahati nzuri kulikuwa na mashahidi kama watano hivi, tarehe 30/11/2018 walitakiwa kusimama mahakamani kutoa ushahidi huo, wakiwa wanajiandaa kuja dar es salaam ndio wakapata hiyo ajali wakiwa ndani ya kivuko cha Mv nyerere wote walikufa pamoja na mawakiri wao wawili upande wa mashtaka, hakukuwa na ushahidi mwingine tena, John aliachiwa huru baada ya kuonekana hana hatia lakini ukweli mchezo wote alicheza Madam Jane na watu wake" Osman Azizi alieleza kwa kifupi.
" Dah huyu mama kumbe sio poa, lazima tumshikishe adabu, anko nakushauri uwe makini sana, inavyoonekana madam Jane hakuna kitu anashindwa"
"Naelewa hata usijali"
"Powa basi badae"
Revocatus akaondoka.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Upande wa pili kule msituni walipo Yusto na Brandina mambo yalizidi kuwa makubwa, tayari kila mmoja alikua hana uwezo wa kujizuia tena dhidi ya mwenzake.
Yusto alianza kumpiga mabusu ya hapa na pale jambo lililomfanya Brandina kuwa kwenye wakati mgumu. Wakati huo walikuwa bado ndani ya maji katikati ya ule mto.
Brandina akaanza kutoa miguno, huku na yeye akiuchomeka mguu wake katikati ya miguu ya Yusto.
Akaingiza mkono kwenye maji akamshika Yusto tumboni na kisha akaanza kuushusha chini taratibu.
Mwisho alimshika mwanajeshi wa Yusto ambae tayari alikua amesimama imara, akaanza kumminya minya taratibu akianzia juu kushuka chini.
Walizidi kumwagiana mvua ya mabusu na mwisho Brandina alimshika Yusto kwenye mabega kisha akamrukia, akaibana miguu yake miwili nyuma mgongoni kwa Yusto.
Yusto nae akapitisha mikono yake na kumshika Brandina kwa nyuma asianguke.
Hapo Brandina alianza kuzungusha kiona chake laini kiasi cha kumfanya Yusto asiwe na uwezo wa kuvumilia tena, akiwa amembeba Brandina juu juu alisogea nae hadi sehemu yenye kina kifupi cha maji.
Hapo wakaanza kufurahia penzi kwa hamu kubwa, hakuna aliyekumbuka tena kama wanatafutwa na walinzi kutoka ngome ya madam Jane. Yusto hakuwaza tena kuhusu Caren, licha ya kutaka kusimama kwenye msimamo wake lakini alijikuta anashindwa kuikwepa mitego ya Brandina mwanamke aliyekua amepambana kwa hali na mali kuyaokoa maisha yake.
Je, nini kitafuata?
Ni nini mpango wa Osman Azizi?
Anataka nini?
Vipi kuhusu penzi la Caren na Yusto ambalo tayari limeingia doa kubwa?
ITAENDELEA.....
TUNAENDELEA KUUWASHA MOTO NA BAKI NA MIMI...
Kupata simulizi hii yote kwa pamoja lipia tsh elf 1 tu kisha nipigie... Namba 0756862047-saul