Simulizi ya ujasusi: Do not shout (Usipige kelele)

Simulizi ya ujasusi: Do not shout (Usipige kelele)

๐ƒ๐Ž ๐๐Ž๐“ ๐’๐‡๐Ž๐”๐“
๐ฌ๐ž๐š๐ฌ๐จ๐ง 2

Sehemu ya.............14
[emoji725][emoji725][emoji725]

Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
Brandina na Yusto wako msituni wamejificha baada ya kufanikiwa kutoka kwenye ngome ya Madam Jane. Brandina anamtaka Yusto walale hapo hadi asubuhi ya siku nyingine kwa ajili ya usalama zaidi.

SASA ENDELEA....
[emoji725][emoji725][emoji725]
Brandina aliingia kwenye maji akiwa na nguo za ndani pekee, hali ya hewa ya eneo hilo ilikuwa na ka ubaridi kiasi lakini hakujali, akawa anajirushia maji taratibu kuuosha mwili wake laini.

Yusto alikua akimtazama kwa kuibia ibia akawa anamshangaa mwanamke huyo ambae hakuonyesha hata chembe ya aibu.

"Labda kwakua ni jasusi, kashazoea" aliwaza Yusto.

Mara Brandina aligeuka akagonganisha macho yake na Yusto, Yusto akazuga kama vile alikua hamtazami yeye, akaangalia pembeni.

Lakini Brandina aliweza kumgundua, akatabasamu, kisha akatoka kwenye maji taratibu na kuanza kumfuata Yusto pale chini ya mti.

Yusto alimtazama Brandina wakati anakuja. Akamkagua kuanzia juu hadi chini, alikua ni mwanamke aliyeumbika haswa.
Mwili wake uliojaa na kujikata vizuri kiunoni, ki sura chake kizuri ukichanganya na vijinguo alivyovaa wakati huo vilimfanya kuonekana kama wale wadada wa kibrazili wakiwa beach.

Yusto alijikuta anamiss Caren wake, hawakupishana sana uzuri na Brandina.

"Vipi mbona unaniangalia sana"
"Nani mimi"
"Ee ndio wewe" alisema Brandina huku akichuchumaa mbele ya Yusto.

"Aah..ha..hapana mimi nawaza yangu tu hapa" alisema Yusto huku akimkagua Brandina aliyekua amechuchuma na kupitisha mikono katikati ya mapaja yake mazuri.
Licha ya kufanya hivyo lakini Yusto aliweza kumchungulia kwa ndani kabisa akaona chupi iliyokua imetuna kiasi kwa mbele.

"Ooh mungu wangu huku sasa kutesana" aliwaza Yusto huku akikwepesha macho yake haraka na kutazama kwingine.
Lakini macho yake yalitua kifuani kwa Brandina, napo hali ilikua ni ile ile ya kumtesa. Chuchu zake za duara zilizotuna zilikua zimebanwa vizuri na sidiria yake.

"Vipi twende basi tukaoge pale mtoni"
Alisema Brandina.

"Ah hapana nahisi baridi harafu si unaona nina kidonda na bado sijakihudumia vizuri hakitakiwi kiingie maji kabisa"

"Aah sema unaogopa baridi Yusto"
"Wala hata, niko fresh mbona"
"Sasa na purukushani yote hii iliyotokea leo utalala hivo hivo bila kujimwagia maji angalau"

"Mmmh"
"Usigune bana wewe njoo uoge utakuwa makini usikitie maji hicho kidonda"

Yusto alijikuta hana ujanja wa kuendelea kubishana.
"Haya poa basi naja"
Alisema Yusto huku Brandina akimtazama kwa macho fulani hivi maregevu.
Wakawa wanatazamana na Yusto, kisha wakatabasamu kwa pamoja.

"Haya tangulia basi nakuja" alisema Yusto, Brandina hakuwa na kizuizi akatembea kwa madaha kama kawaida yake akarudi tena ndani ya maji yaliyokua yanamfika juu kidogo ya kiuno.

Yusto alitoa nguo zake akabaki na bukta na singrendi pekee taratibu akasogea tayari kuingia kwenye ule mto.

Brandina aligeuka na kumtazama huku akijihisi mapigo yake ya moyo kwenda kasi, ilikua ni siri yake na moyo wake namna alivyokua akimuelewa na kumpenda mwanaume huyo.
Japo tayari alikua anajua kuwa moyo wa Yusto umejaa mazima kwenye penzi dhidi ya Caren lakini haikua sababu ya yeye kuacha kumpenda.

Yusto aliingia ndani ya maji taratibu huku wakiwa bado wanatazamana na Brandina.

"Vipi mbona kama unaogopa, au maji ni ya baridi sana?"
"Aah yani we acha tu kama barafu hivi"
"Acha kujiregeza we mwanaume banaa"

"Hata kama ila sio kwa baridi hii hahaha"
Alisema Yusto na kucheka.
Mara Brandina akachota maji kiasi kwenye kiganja cha mkono wake na kumrushia Yusto.

"Aaaa wewee" Yusto akilalamika
Brandina akafanya hivyo kwa mara nyingine tena ya pili na yatatu na baadae akaanza kuyarusha maji kwa mikono yote miwili huku akicheka.

"Brandina acha basi.. aaaah" alisema Yusto huku akijivuta kwenye maji akasogea karibu na Brandina akamshika mikono yote miwili kumzuia lakini Brandina akawa anapambana ajinasue hapo Yusto alimgeuza na kumkumbatia kwa nyuma akambana kwa nguvu huku akiwa bado amemshika mikono akicheka pia.

Hakujua kufanya hivyo alikua anazalisha tatizo kubwa kwa Brandina, ile hali ya kukumbatiwa na Yusto ilimfanya mapigo yake ya moyo kuongezeka kasi zaidi na zaidi, akatamani Yusto aendelee kumkumbatia asimuache.

Kulikuwa na baridi kali wakati huo lakini mwili wa Brandina ulianza kuwa na joto taratibu.

"Vipi mbona umetulia hivo" Yusto aliuliza kwa sauti ya chini jirani kabisa na sikio la Brandina.

"Yustoo" Brandina aliita huku akigeuza shingo na kumtazama Yusto.

Yusto alishangaa namna ambavyo macho ya Brandina yalikua yameregea, ilionyesha wazi hakua kwenye hali nzuri hata kidogo
hakuwa Brandina yule aliyemtembezea kichapo kikali Revocatus masaa machache yaliyopita.

"Yes nambie" Yusto aliuliza hali akiwa bado amemkumbatia Brandina.

Brandina akawa kimya akashindwa kabisa kuzungumza.

"Mbona kimyaa.."
"Mmmh"
"Umeniitaa"
"Yes, najiuliza vipi kama wangekuuwa ningefanyaje mimi"
"Mmh unamaana gani"
"Unajua najisikiaje ukiwa karibu na mimi kama hivi"
"Hapana, ila bila shaka unajisikia vizuri si ndiyo"
"Yustoo.."
"Yes tell me"
"I know you're takken, najua moyo wako upo kwa Caren lakini unaweza angalau kua na mimi kwa leo tu, najua unajua nini namaanisha" Brandina aliongea bila kupepesa macho.

Yusto alijikuta anapata kigugumizi cha ghafula, alishagundua kitambo sana kuwa Brandina anampenda lakini hakujua kama ipo siku atakuja kutamka maneno kama hayo waziwazi,
Yusto alijikuta kwenye wakati mgumu na istoshe alikua amezama penzini na msichana wa ndoto zake Caren, tena penzi lao lilikuwa bado ni jipya kabisa.

"You know what nakutania bana, usichukulie serious, its just joking" alisema Brandina baada ya kuona Yusto amekaa kimya kwa muda akajua wazi ilikua ni ngumu kwake kufanya hivyo, akawa hatamani kusikia jibu la kuumiza moyo wake kutoka kwa Yusto.
Brandina alijikuta akijilaumu kwa alichokifanya ilikua ni kama kujidharirisha mbele ya mwanaume yeye kama mwanamke anaejielewa.

"Yah hata mimi nilijua tu unatania," alisema Yusto huku akimuachia Brandina ambae alianza kuondoka,
Yusto akawa anamuangalia akiona kabisa alichokua anakisema Brandina ni tofauti na uharisia
"Lakini ameyasaidia maisha yangu, anastahili hata zaidi ya hili" aliwaza Yusto huku akijihisi kumkosoea Brandina.

"Oga upesi basi niku....."

Alisema Brandina lakini kabla hajamalizia sentensi yake mara alishikwa mkono na kuvutiwa tena ndani ya maji.
Kufumba na kufumbua alijikuta yupo kifuani kwa Yusto. Wakawa wanatazamana uso kwa uso.

Bila kuchelewa Yusto alianza kumpiga mabusu ya hapa na pale jambo lililomfanya Brandina kuwa kwenye wakati mgumu.
Akaanza kutoa miguno, huku na yeye akiuchomeka mguu wake katikati ya miguu ya Yusto.
Akaingiza mkono kwenye maji akamshika Yusto tumboni na kisha akaanza kuushusha chini taratibu.
[emoji294] [emoji294][emoji294]

ITAENDELEA....
๐Œ๐š๐ฅ๐ข๐ณ๐ข๐š ๐ฏ๐ข๐ฉ๐š๐ง๐๐ž 20 ๐ฏ๐ข๐ฅ๐ข๐ฏ๐ฒ๐จ๐ฌ๐š๐ฅ๐ข๐š ๐ค๐ฐ๐š ๐“๐ฌ๐ก ๐ž๐ฅ๐Ÿ 1๐ญ๐ฎ๐ฎ

WhatsApp 0756862047
[emoji16][emoji16] mkuu story ni tamu sana
 
๐๐€๐Š๐ˆ ๐๐€ ๐Œ๐ˆ๐Œ๐ˆ
(Stay with me)
๐ฌ๐ž๐š๐ฌ๐จ๐ง 2

Sehemu ya...........15
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

๐ˆ๐‹๐ˆ๐๐Ž๐ˆ๐’๐‡๐ˆ๐€...
Jasusi Brandina akiwa msituni na Yusto, anashindwa kujizuia, anaweka wazi hisia zake za mapenzi kwa Yusto hali inayomuweka Yusto kwenye mtihani mzito ukizingatia Brandina alikua ameyaokoa maisha yake, hakutaka kuuvunja moyo wa mwanamke huyo.

Upande wa pili Revocatus na Caren wanarejea kambini mara tu baada ya kutoka kule mlimani ilipokuwepo ngome ya Madam Jane.
Wakati huo pia madam Jane yuko njiani kwenda kuzungumza na Osman Azizi kuhusu suala la mtoto wake Yusto.

Je nini kitafuata?

SONGA NAYO...

[emoji294][emoji294][emoji294]
Tayari Revocatus na Caren walishafika kwenye ile kambi yao ndogo baada ya kutoka kule msituni.

Kitu cha kwanza Caren alipofika ni kuangalia hali ya Zubeda mama yake Yusto.
Bahati nzuri alimkuta ndani ya kile chumba alichomuacha ingawa tayari alikua ameamka lakini hakuwa amefanya vurugu ya aina yoyote.

"Yusto, yusto mwanangu yuko wapi" hili ndilo lilikua swali la kwanza kutoka kwa Zubeda mara tu baada ya kumuona Caren.

"Aah yupo anakuja sio mda amepitia kukuletea zawadi" Caren alidanganya
"Kwa nini umemuacha tena madam Jane atamuuwa nenda ukamlete nendaaa" Zubeda alifoka huku akimfukuza Caren kwa kumsukuma

"Basi mama basi naenda kumeleta"
"Nenda sasa hivi au nikuazime baiskeli yangu"
"Baiskeli? baiskeli gani tena, unayo"
"Ee iko hapo nje nimepaki,"
"Aah sawa basi ngoja nikaichukue" alisema Caren huku akitabasamu akatoka na kuingia chumba kingine cha mbele yake. Huko akamkuta Revocatus akijihudumia majeraha yake madogo aliyopata pindi alipokua akipambana na Brandina.

"Revo natoka mara moja narudi chuoni, naenda kuona kama Yusto atakuwa amerudi, baki na mama usimuache mwenyewe tafadhali"
"Sawa usijali, mimi nipo"
",Haya, usimchome sindano ya usingizi basi si unakumbuka daktari alivyosema"
"Sawa, lakini vipi sasa Kama kichaa chake kikipanda akaanza kusumbua si unajua mwenzio nimechoka nahitaji kupumzika, nimesikia anaongelea habari za baiskeli gani sijui, huo kama nidalili anaweza kubadilika muda wowote"

"akianza usumbufu wewe nipigie simu nitarudi haraka lakini sio kumchoma sindano"
"Haya poa nimekuelewa, ila hicho chuo chenyewe wanachowapa uhuru wa manyani mda wote mko nje na Yusto wako"

"Ndio maana kikaitwa chuo, muhimu tufanye mtihani tufaulu"
"Hahaha kwa hali hiyo utafaulu kweli, sikumbuki mara ya mwisho umeingia lini darasani"
"Hahahah, achana na mimi, basi baadae"
"Haya poa"
Caren akatoka kurudi chuoni. Akiwa njiani akili yake haikutulia kabisa muda wote alikua akimuwaza mpenzi wake Yusto hakujua kama atamkuta chuo au laa,
Jambo lingine lililomfanya Caren kuwa kwenye wakati mgumu ni kile kitendawili kilichotakiwa kukitegua.
Madam Jane bosi wake kamtuma amuuwe Zubeda wakati huo Zubeda ni mama mlezi wa mpenzi wake yaani Yusto, lakini kingine tayari ameshajua kuwa Yusto ni mtoto halali wa madam Jane. Afanye nini aache nini?
Alitamani kumueleza madam Jane lakini hakujua wapi pa kuanzia. Aliona ni vema azungumze na Yusto kwanza.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Muda mfupi tu baada ya Caren kuondoka Revocatus alichukua simu yake na kupiga mahali.

"Yes anko, Revo hapa naongea....ndio mambo yanaenda kama tulivyopanga anko...sawa...ndiyo nina taarifa muhimu sana nataka kukupa...sawa dakika si nyingi nitakua hapo....sawa ...sawa anko,"
Revo alimaliza mazungumzo kisha akakata simu. Bila kupoteza muda alibadilisha mavazi yake akaingia kwenye gari lake na kuondoka kwa kasi.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Osman Azizi, mwanaume mwenye umri yapata kama miaka 50 hivi, alionekana akiwa amekaa ofisini kwake huku akionekana mwenye mawazo kiasi.
Muda wote alikua na sigira mdomoni. Akawa anavuta taratibu huku akijaribu kutafakari baadhi ya mambo yake muhimu.

Huyu ndiye aliyekuwa akihusika na kutekelezaji wa mauaji ya Zubeda na Yusto miaka mingi iliyopita akifanya kazi hiyo chini ya madam Jane.
Lakini sasa hakuwa na uhusiano wowote na Madam Jane, walibaki tu kama watu wanafahamiana kila mtu aliendelea na biashara zake, japo Azizi alionekana kuna kitu alishakipanga tangu zamani.
Alionekana ni mtu aliyebeba siri nzito baina yake yeye na mwanamke tajiri yaani Madam Jane.

Akiwa ametulia ofisi kwake mara alisikia mtu anagonga mlango.

"Ingiaa" alisema Azizi, mlango ukafunguliwa mtu aliyeingia wakati huo alikua ni Revocatus.
Yes, Revocatus yule aliyekua na Caren muda mfupi uliopita kule kambini.

"Ooh Revo"
"Ndio anko"
"Umewahi au ulipiga simu ukiwa njiani"
"Aah hapana nilikua kambini kule"

"Hahah safi bila shaka unazo habari za moto moto ndio maana umewahi kufika karibu kwenye kiti"

"Asante anko Azizi, kweli leo nina taarifa kama tatu hivi za muhimu sana"

"Ooh basi nambie maana sasa hivi nimetoka napokea simu ya bosi wako madam Jane ameanza kuuliza habari za mtoto wake"

"Hahah kweli anko"
"Yah"
"Basi tumeanza kusogea kwenye lengo, leo hii madam Jane kakutana na Yusto kwenye ngome yake moja ya siri iko msituni huko chini ya mlima, inavyoonekana bado hajajua chochote kuhusu Yusto, lakini ameanza kuhisi.
Caren pia kajua kama Yusto ni mtoto wa Madam Jane, alimleta daktari wa vichaa pale kambini aongee na Zubeda, sikujua kama atagundua chochote lakini yule daktari aligundua kila kitu kuhusu madam Jane na Zubeda, ila kwa bahati nzuri nimemuuwa kabla hajatoa hii siri kwa hiyo anejua mpaka sasa ni Caren peke yake"
Alieleza Revocatus.

"Wee unasema kweli Revo"
"Ndio hivo anko, leo ilikua siku yenye mabalaa sana"

"Safi, sio mbaya lakini najua Caren hawezi kukupa shida unamjua vizuri, umekua nae kambini tangu utotoni mpaka sasa, tena nakumbuka nilikupeleka kule kambini kwa madam jane kabla hata Caren hajaletwa kwa hiyo unamjua vizuri si ndio Revo" alisema Azizi
"Yes anko hawezi kunipa shida muda wake ukifika tu nambie"
"Sawa kwa hiyo kumbe madam Jane anangome nyingine ya siri, hahaha safiii, na sasa ameshaanza kuhoji kuhusu Yusto huu ndo mda nliokuwa nakwambia anko, muda wa kupiga pesa, Yusto ni bomu ambalo nilishalitega tangu muda sasa imefika wakati wa kulilipua" Alisema Osman Azizi huku akitabasamu.

"Lakini anko hivi unaweza kujua kwa nini madam Jane alimteke Yusto, najiuliza sipati majibu pengine ameshajua kama ni mwanae ama"
"Hapana hawezi kujua, hata kama amejua hawezi kumteka, ni kweli zamani alikua akimchukia Yusto hadi akataka kumuuwa lakini kwa sasa hawezi, Yusto atakuwa udhaifu mkubwa wa madam Jane punde tu atakapogundua yupo hai" alisema osman Azizi .
mara mlango ukagongwa tena akaingia msaidizi wa kazi wa Azizi.

"Bosi madam Jane yuko nje hapa anataka kukuona" alisema yule msaidizi.

"Sawa mruhusu aingie" alisema Azizi kisha akampa ishara fulani Revo.
Revo akasimama na kwenda kujificha nyuma ya kabati moja kubwa lililokua ndani ya ofisi hiyo.

Punde Madam Jane akaingia, wakatazamana na Azizi ambae alionyesha hana shida yoyote.

"Karibu kwenye kiti madam Jane ingawa sikutegemea ujio wako"
Alisema Azizi huku akimuangalia madam Jane usoni, akanyoosha mkono kumsalimia.
Wakati akifanya hivyo Azizi akavuta kumbukumbu ya miaka kadhaa iliyopita nyuma.
[emoji294][emoji294][emoji294]

MIAKA 20 ILIYOPITA

Kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwa Zubeda kipindi ambacho hakuwahi kuwaza kama angekipitia kwenye maisha yake.
Zubeda alikua akiandamwa kila alipokwenda na watu wa Madam Jane wakitaka kumuuwa yeye pamoja na mtoto mdogo aliekuwa habanduki mikononi mwake yaani Yusto.

"Janeth wewe ni shetani, ibilisi muuwaji mkubwa, unathubutuje kutaka kumuuwa mwanao wa kumzaa, mungu akulaani janeth sijui hata kwa nini nilichagua kuwa rafiki yako"

Hii ni kauli ambayo Zubeda alikua akiitoa mara kwa mara wakati akihangaika kuukimbia mkono wa madam Jane.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Baada ya kuhangaika sana mwisho Zubeda alienda kuanguka tena miguuni kwa dada yake aliyeitwa Asma akimuomba amchukue yeye na mwanae licha ya kujaribu hivyo mara kadhaa lakini Asma hakuwa akimtaka Zubeda.

Baada ya kujieleza sana mwisho Asma aliregeza msimamo wake na kukubali kumchukua Zubeda na Yusto akawakaribisha nyumbani kwake.

Asma alikua ni dada mwenye pesa zake alikua ni mpambanaji aliejua nini afanye na nini asifanye.
Asma alikua amezama penzini na mwanaume mmoja maskini aliyeitwa Osman Azizi. walifunga ndoa ya kiserikali wakayaanza maisha yao kama mke na mume.

Kwa habati mbaya Osman Azizi hakuwa akimpenda Asma kilichomfnya akubali kufunga ndoa na kuishi na mwanamke huyo haukua upendo bali pesa.
Wakati wote Osman alikua akizikodolea macho pesa za mkewe licha ya kwamba alipata kila alichohitaji lakini haikuishia hapo alitamani sikumoja kila kitu cha mkewe kiwe chake.

Ndipo hapo alipotafutwa na kuunganishwa na watu wa madam Jane, Madam Jane aliwasiliana na Osman Azizi akiwa Dubai akamuahidi kama angewauwa Zubeda na Yusto waliokuwa wakiishi ndani ya nyumba yake basi angepata pesa nyingi sana.

Osman Azizi hakutaka habati hiyo upitie bure zilikua ni pesa nyingi mno kiasi cha kumfanya ahisi kumuuwa Zubeda na kitoto Yusto lilikua jambo rahisi sana.
Lakini pia Osman Azizi aliitumia fursa hiyo kuuwa ndege wawili kwa jiwe moja.
Kwa kuwa Azizi alizitamani pia mali za mkewe aliwaza kumuuwa na yeye.
Akategeshea siku moja Asma Zubeda na Yusto walipokuwa wakipanga kutoka kwa pamoja, Azizi alikua ni fundi wa magari kabla hata ya kumuoa Asma.
Usiku alilichokonoa gari la mkewe na kuharibu vifaa kadhaa ikiwa ni pamoja na kukuta breki.
Asubuhi yake baada ya Asma kuondoka akiwa pamoja na mdogo wake Zubeda aliyembeba Yusto, Azizi yeye alibaki nyumbani.

Haukupita muda akapata habari kuwa Asma na wenzie wamepata ajari mbaya sana ya gari.
Asma alifariki pale pale, Zubeda na Yusto walijeruhiwa vibaya.
Baada ya matibabu Zubeda alitoka hospitali akiwa ni kichaa(mwendawazimu). Yusto yeye alipona lakini Osman akahonga pesa nyingi ikatangazwa kuwa yusto nae amekufa. alifanya hivyo kwa makusudi kabisa mara tu baada ya nakubaliano yake na madam Jane kwenda kinyume.

"Nilitaka umuuwe Zubeda lakini kwa kuwa amekuwa kichaa basi muache hivyo hivyo nitakupa pesa nusu"
Alisema Madam Jane kauli iliyomkasirisha sana Osman Azizi, akaahidi kulipa kisasi.
Akaamua kumuacha Yusto bila kumuuwa huku akimdanganya madam Jane kuwa yusto alikufa pia.

Azizi alikuwa anajua nini anafanya, hasa baada ya kugundua kuwa Yusto alikua ni mtoto halali kabisa wa Madam Jane na si Zubeda.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Huo ndio ukawa mwanzo wa maisha mapya ya Azizi akiwa kama mrithi na mmliki halali wa mali zote za marehemu mkewe Asma.
Zubeda akapotelea mtaani kama kichaa.
Yusto nae baada ya kufikisha miaka saba maisha yalimshinda nyumbani kwa Azizi kutokana na mateso makali aliyokuwa akiyapata kutoka kwa mke mpya wa Azizi, akatoroka na kuwa mtoto wa mitaani. Azizi hakuchukua hatua yoyote lakini akawa anamfuatilia na kumuita kama bomu lake la baadae kwa ajili ya madam Jane.

Osma Azizi hakuishia hapo, alimtafuta mtoto mwingine wa kiume yaani Revocatus akampandikiza na kuwa mmoja kati ya wale watoto waliokuwa wakikusanywa na kuwekwa kambini kwa Madam Jane kwa ajili ya kupewa mafunzo mbalimbali.

Revocatus akaingia kambini pamoja na akina Caren lakini akijua kabisa yupo pale kwa ajili ya Osman Azizi, hivyo kwa kipindi chote hicho Revo alikua akivujisha siri mbalimbali na kuzileta kwa Azizi.
Naam hivyo ndivyo ilivyokuwaaa...
[emoji294][emoji294][emoji294]

Osman Azizi alimaliza kumbukumbu zake huku akimpa mkono Madam Jane.

"Karibu kwenye kiti madam Jane ingawa sikutegemea ujio wako" alisema Azizi

"Asante" madam Jane aliitika kwa kifupi na kukaa.

Wakati huo Revocatus kijana wa Azizi alikua nyuma ya kabati akisikiliza kila kilichozungumzwa.

JE, NINI KITAFUATA?

ITAENDELEA.....

Ni tsh elf 1 tu vipande vyote hadi mwisho
0756862047
 
USIACHE KUFUATILIA SIMULIZI ZANGU ZINAZOENDELEA HUKU JAMII FORAM

1. DO NOT SHOUT - usipige kelele
2. THE MODERN WAR- Vita ya kisasa
3. STAY WITH ME- baki na mimi
4. KARANI
 
DO NOT SHOUT
season 2
Sehemu ya..........16

Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
Osman Azizi alimaliza kumbukumbu ya miaka karibu 20 iliyopita kisha akamkaribisha madam Jane.

"Karibu kwenye kiti madam Jane ingawa sikutegemea ujio wako" alisema Azizi

"Asante" madam Jane aliitika kwa kifupi na kukaa.

Wakati huo Revocatus kijana wa Azizi alikua nyuma ya kabati akisikiliza kila kilichozungumzwa.

Je, nini kitafuata?

SASA ENDELEA....

Madam Jane na Azizi walitazama kwa muda huku kila mmoja akiwa kimya kabisa.
Wakati huo Revocatus alikua amejificha nyuma ya lile kabati kubwa lililokuwa ndani ya ofisi hiyo ya Osman Azizi.

"Ndio madam Jane, karibu nakusikiliza" hatimae Azizi alivunja ukimya

"Nimeshakaribia Osman"

"Ee nambie, sikutegemea kabisa ujio wako leo"

"Ila ulitegemea siku moja nitakuja si ndiyo bwana Azizi" madam Jane aliuliza swali la mtego

"Mmh sina hakika sana, nambie unataka nikuagizie gari la aina gani"

"Hapana sijaja kununua gari hapa"

"Mmh nini kimekuleta sasa?" Alisema Osman huku akitanua mikono yake kuuliza.

"Ni habari za kitambo kidogo lakini nimekuja kuhakikisha taarifa ulizonipa juu ya kazi niliyokupatia kipindi kile, ni kuhusu mwanangu yaani Yusto nataka kujua ulimuuwa au hukumuuwa?"
Madam Jane aliuliza huku akiwa amemtolea macho Osman Azizi ambae nae alitoa macho kwa mshangao.

"Unamaana gani mbona unaleta habari za zamani sana madam are you serious?" Azizi aliuliza akijifanya kutokuelewa.

" Azizi you know very well what i mean, please stop your drama right now" (Azizi unajua vizuri sana nini namaanisha, tafadhali acha maigizo yako sasa hivi) madam Jane aliongea kwa msisitizo.

"Aa..aaa Janeth!, What are you taking about, He died many years ago and you knew that, so why you're now asking, why, what is the reason?"
(Aa..aaa Janeth! unaongea kuhusu nini, alikufa miaka mingi iliyopita na unalijua hilo, sasa kwa nini unauliza, kwanini, nini sababu?) Azizi aliendelea kusimamia msimamo wake.

"Sina sababu ya kukwambia nini kimetokea Azizi, unanijua vizuri sifanyagi mambo kwa kubahatisha"

"Ooh wow, basi vizuri" Osman alijibu, akachukua sigara yake akavuta pafu moja kisha akatoa moshi mwingi na kukohoa kidogo akamtazama Madam Jane usoni kwa muda.

"Sawa acha twende kwenye pointi sasa, sina sababu ya kuzunguuka saaana hayo ni matumizi mabaya ya muda kwa watu kama sisi, hasa wewe madam"

Madam Jane alijiweka sawa kusikia atakachokisema Azizi, wakati huo mapigo yake ya moyo yalikua yakimuenda mbio, akajikaza, moyo wake ukawa tayari kupokea habari ambazo aliamini zitakuwa sio nzuri.

"NI KWELI YUSTO YUPO HAI" alisema Azizi

Madam Jane alihisi mshare wa moto umepenya katikati ya moyo wake kisha akalisikia tumbo lake likipatwa na ubaridi uliomsababishia maumivu makali.

Mwanae aliyemzaa kisha akaagiza auwawe, akapata taarifa kuwa amekufa eti leo hii anambiwa yuko hai.
Zilikua ni taarifa zilizomchanganya sana Madam Jane.
Sio kwamba kwa sasa alikuwa hampendi Yusto au hataki Yusto aishi hapana, tayari alishayatambua makosa aliyoyafanya kipindi cha nyuma, lakini aliacha ipite kwa sababu aliamini Yusto alishakufa.
Lakini leo hii anaambiwa Yusto yuko hai, atafanyaje?, atamtazama vipi? atamwambia nini? haya ni maswali yaliyopita mfurulizo kwenye kichwa cha madam Jane punde tu baada ya kupokea taarifa hizo nzito.

"Unasema nini Azizi?"
"Kama ulivyo sikia, He is alive, mwanao anaishi"

Madam Jane alitulia kwa muda huku akimtazama Osman Azizi, alionyesha wazi anamaanisha kile anachokisema.

"Kumbe hisia zangu zilikua ni sahihi" aliwaza Madam Jane huku akijitahidi kutoonyesha tofauti yoyote. Hakutaka kumfanya Azizi ajue kuwa Yusto ni udhaifu wake mkubwa. Hakujua kuwa tayari Azizi alishapiga hesabu za mbali sana, kila kilichokuwa kinaendelea kilikuwa ndani ya mpango wake.

"Madam huna sababu ya kushangaa kumbuka wewe ndio chanzo cha haya yote ulivunja makubaliano yetu siku ile, ulini......."
"Sawa sasa unataka nini sema, Yusto yuko wapi" madam Jane alidakia huku akiwa amemkazia macho Azizi.
"Yusto yupo na pengine unaweza ukawa umeshahawi kuonana nae"

"Unataka nini Osman Azizi, acha kupiga porojo najua kuna kitu unataka haya sema"

"Ooh! come on, hauna haja ya kukasirika Janeth twende taratibu tu halafu nitakwambia nini nataka"

"Sina muda wa kupoteza Osman unajua hilo"

"Basi kama huna muda ondoka unasubiri nini, hebu acha mambo ya ajabu bwana wewe" Azizi alifoka, ilimbidi Madam Jane awe mpole.
"Haya sema basi nakusikiliza"

"Okay sasa sikia, leo sitakwambia nini nataka ila nitakwambia nini najua."
Osman Azizi alitulia kwa muda Kisha akaendelea kuzungumza.

"Janeth mimi ni mmoja wa watu wachache ambao nakujua nje ndani, yaani najua hadi vitu ambavyo wewe hujui kama najua, kwanza najua Yusto ni mwanao wa kumzaa hilo liko wazi, pili najua John ni mtoto wako wa pili na baba yake ni Mark Moon, tatu najua kama unakisasi kizito dhidi ya mark moon mumeo wa zamani na ulishawahi kumfanyia tukio la hatari kabla hujaenda Dubai, ulimuwekea mark moon madawa kwenye mishumaa ambayo huwa anapenda kuiwasha ofisini kwake ukamfanya Mark Moon asiweze kupata mtoto mwingine yaani jogoo hapandi mtungi, nne najua wewe ndio uliyesababisha kivuko cha Mv nyerere kuzama mwaka 2018 ukauwa watu wengi sana na ushahidi ninao, tano najua mpango wako wa kukisambalatisha chuo cha mark moon alichowekeza pesa zake nyingi, na mpango huo umeshaanza kuutekeleza kupitia kijana wako mmoja anaitwa Caren yuko pale chuoni, na najua utafanya tukio lingine kubwa kumtumia mtoto wako John mara tu atakapochaguliwa kuwa Rais wa kile chuo, niendelee?"
Osman Azizi alitoa maelezo ambayo yalimfanya madam Jane ashikwe na kizunguzungu cha ghafula alimanusura aanguke

"Sikia Janeth hauna haja ya kuogopa hakuna anaejua zaidi yangu, ukifanya kile nachokitaka basi mambo yatakuwa shwari, nitamkabidhi mwanao mikononi mwako, halafu wala sihitaji pesa zako mimi. Ila nakupa onyo, ukijaribu kuleta ujanja wa aina yoyote, yani hata ukiniuwa hakuna utakachokipata na siri zako zote zitakuwa hadharani, kwa mara nyingine tena utapata aibu ya Dunia ambayo sidhani kama safari hii utakuwa na ujasiri wa kuibeba tena"
Osman Azizi aliongea kwa kumaanisha.

Je, nini kitafuata?
Osman Azizi ni nani anataka nini?
Vipi kuhusu Caren?
Vipi kuhusu Brandina na Yusto kule msituni?

Awam hii umeifanya fupiiiiii
 
๐๐€๐Š๐ˆ ๐๐€ ๐Œ๐ˆ๐Œ๐ˆ
(Stay with me)
๐ฌ๐ž๐š๐ฌ๐จ๐ง 2

Sehemu ya...........17

Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

๐ˆLIPOISHIA....

"Sikia Janeth hauna haja ya kuogopa hakuna anaejua zaidi yangu, ukifanya kile nachokitaka basi mambo yatakuwa shwari, nitamkabidhi mwanao mikononi mwako, halafu wala sihitaji pesa zako mimi. Ila nakupa onyo, ukijaribu kuleta ujanja wa aina yoyote, yani hata ukiniuwa hakuna utakachokipata na siri zako zote zitakuwa hadharani, kwa mara nyingine tena utapata aibu ya Dunia aibu ambayo sidhani kama safari hii utakuwa na ujasiri wa kuibeba"
Osman Azizi aliongea kwa kumaanisha.

Je, nini kitafuata?

SASA ENDELEA....

Madam jane alihisi kuchanganyikiwa alitamani ardhi ipasuke immeze, hakujua ni vipi Osman Azizi amejua taarifa zake nyingi tena za siri kwa urahisi kiasi kile, ilionyesha wazi alikuwa akimfuatilia tangu muda mrefu, haikuwa bure lazima pia kuna mtu wake wa karibu alikua anavujisha siri zake.

"Unataka nini Osmaniiiiiiii" madam Jane alipaza sauti na kusimama kwa hasira.
Osman Azizi nae akasimama huku akimtazama madam Jane kwa macho ya dharau Kisha akatabasamu, sigara ikiwa mdomoni mwake.

"Kwa sasa ondoka madam Jane, nenda kayatafakari vizuri mambo niliyokwambia leo, subiri simu yangu nitakwambia lini na wapi tukutane kwa ajili ya mazungumzo zaidi, hiyo siku ndio nitakayokwambia nini nataka, kumbuka usilete ujanja wa aina yoyote, nimejipanga"
Alisema Osman Azizi huku akimuonyesha ishara madam Jane kuwa aondoke.

Madam Jane alimtazama Osman Azizi kwa macho makali kisha akachukua mkoba wake pale mezani akatoka nje kwa hasira, akaondoka zake.
Osman alimpa ishara fulani msaidizi wake wa kazi aliyekuwa amesimama mlangoni, akageuka na kumfuata Madam Jane kwa nyuma.

Sekunde chache baadae Revocatus alitoka nyuma ya lile kabati alilokuwa amejificha, akawa anaongea na simu.

"Unasema hujamuona Yusto hadi muda huu" aliuliza Revocatus
"Ee hayupo hapa chuoni, nimeanza kupatwa na wasiwasi tena jamani" Caren alisikika upande wa pili akiongea na Revo.

"Sikiliza Caren, nisikilize mimi, nina uhakika Yusto yuko salama yani yuko salama kabisa trust me"

"Sasa yuko wapi, simu yake imezimwa, chuoni hayupo, ni nani kwani aliondoka nae"

"Ni mdada tu hivi, yaani alikuja akamuokowa na kuondoka nae hawezi kumfanya kitu kibaya niamini mimi, nisinge kuruhusu tutoke kule msituni kama Yusto hayupo salama"

"Mmh sawa basi ngoja niendelee kusuburi, vipi kuhusu mama nae anaendeleaje"

"Nani Zubeda?"
"Ee ndiyo"
"Yupo amelala"
"Umemchoma sindano tena"
"Aah hapana kalala mwenyewe tu" Revo alidanganya.

"Sawa basi ngoja niendelee kumsubiri Yusto"
"Sawa"
Caren akakata simu.
[emoji294][emoji294]

"Vipi ni nani unaongea nae" aliuliza Osman Azizi
"Ni caren, anadai Yusto bado hajarudi chuoni, sio muhimu sana anko hebu tuongee vizuri unampango gani na Madam Jane, yaani tangu nimjue sijawahi ona katetemeshwa kiasi hiki" Alisema Revocatus

"Kijana wangu mambo ndo kwanza yanaanza, subiri utashuhudia mwenyewe"

"Lakini nimesikia unasema hutaki pesa zake, sasa ni nini unataka kutoka kwake mbona nashindwa kukuelewa anko wangu"

"Sikiliza Revo, hebu kaa kwanza tuongee" Alisema Azizi kisha wote wakakaa huku wakitazamana uso kwa uso.

"Revo, mara ya mwisho kuangalia picha la kihindi ilikua lini?"
Aliuliza Azizi
"Mmh sikumbuki unamaana gani?"
"Hili ni kama picha la kihindi tena picha babu kubwa, ni jambo kubwa nililolisubiri zaidi ya miaka 20 hahah ahahaha" Aliongea Osman Azizi kisha akamalizia na kicheko, kicheko kikubwa sana, kilichojaa dharau na majigambo.

Revo akawa anamuangalia tu huku akitamani kumuelewa.

"Revo, kila kitu kinaenda kama nilivyopanga, muda sahihi ukifika nitakwambia nini nataka kufanya, wewe sasa hivi nisikilize kwanza"

"Sawa anko nakusikiliza, nambie hatua inayofuata"

"Iko hivi, kwa sasa Madam Jane amechanganyikiwa kupita kawaida, namjua vizuri baadae atatuliza akili yake awaze nini cha kufanya, unajua atafanya nini?"

"Sijui anko, ila labda atataka kukuua"

"Hapana hawezi kuniua kwa sababu mimi ndiyo najua Yusto ni nani na yuko wapi"

"Mmh! Sawa lakini si nimeshakwambia madam Jane leo alimteka Yusto na pengine ameshajua kama ni mwanae"

"Hapana hajajua ila kahisi tu ndio maana amekuja kwangu leo, na hata kama akijua bado mimi nitakuwa na umuhimu mkubwa, anajua naweza kumwambia Yusto kile alichokifanya na Yusto akamchukia mama yake milele, si unajua Yusto haelewi chochote mpaka leo anajua tu Zubeda sio mama yake mzazi basi"

"sawa anko, lakini huyu huyu madam Jane si ndio alitaka kumuua Yusto unafikiri kwa sasa Yusto atakuwa na umuhimu kwake hadi atoe hicho kitu unakitaka kutoka kwake"

"Hahah Revo kuwa uyaone, kipindi kile alitaka kumuua kwa sababu alikuwa na shida na pesa sawa, lakini sasa hivi pesa anazo hana cha kupoteza tena, unajua KUNA UMRI UKIFIKA UNAONA FAMILIA NI BORA KULIKO PESA, kwa sasa Madam Jane anamuhitaji Yusto tena sana"

"Mmmh"
"Ndo hivyo anko, sasa atakachokifanya Madam Jane ni kukusanya nguvu kwa ajili ya kupambana na mimi ila sio kuniua, kwanza atataka kujua nini nataka kutoka kwake"

"Kwa hiyo unafanyaje hapo"

"Nataka tumchanganye Madam Jane, kwanza nataka nimvuruge na wale watu anawategemea kumpa nguvu, wewe utanisaidia kwa upande wa Caren"

"Kivipi anko nimuue Caren?"

"Aah hapana, nataka uende uongee na Caren umueleze ukweli wote kuwa madam Jane sio mtu mzuri wala hapokei Oda za serikali kama alivyowambia , mweleze ukweli wote kuwa madam Jane ni jambazi tu na anawatumia ninyi kufanya mambo yake ya uharifu na kulipa kisasi kwa Mark Moon, baada ya hapo unaijua roho ya Caren hawezi kuvumilia hili"

"Enhe baada ya hapo nini kitafuata"

"Ukitoka hapo nenda kwa Madam Jane bosi wako kamweleze kwa unyenyekevu kuwa umegundua vitu vya siri anavyovifanya Caren, mwambie kuwa Caren emevunja agizo lake hataki kumuua Zubeda na badala yake amemficha kambini kwenu, inaonekana kuna mtu mwingine anashirikiana na Caren kwa siri"

"Duuh anko wewe ni nouma, sijui hata unawaza nini, kwa hiyo hapo utakuwa umewagonganisha Caren na Madam Jane si ndiyo"

"Yes, Caren anauwezo mkubwa na nimtu anaependa haki ni lazima atampa shida Madam Jane, Wewe fanya hivyo utanielewa taratibu"

"Sawa haina shida, basi ngoja nirudi kambini au kuna kingine"

"Hapana kukiwa na shida nitakupigia muwahi kwanza huyo Zubeda wenu"

"Sawa anko"

Revocatus alianza kuondoka lakini baada ya kupiga hatua kadhaa akasimama na kugeuka.

"Enhe anko nilikusikia unasema eti madam Jane ndio aliyesababisha kivuko cha MV NYERERE kuzama kivipi yani?"

"Ni stori ndefu Revo hebu kwanza niache nipumzike, nina mambo mengi ya kufanya" alijibu Azizi huku akijilaza kwenye kiti.

"Noo anko hebu nambie hata kwa kifupi tu, unajua niwatu wengi sana walikufa kwenye ile ajali sababu ilikuwa ni nini Madam Jane kufanya hivo"

"Alitaka kupoteza ushahidi"

"Ushahidi? ushahidi gani yani"

"Kuna kesi ilikuwa mahakamani mwaka 2018, John mtoto wa Madam Jane aliuwa mtu kwa makusudi kisa ikiwa ni wivu wa mapenzi huko visiwani ukerewe, kwa bahati nzuri kulikuwa na mashahidi kama watano hivi, tarehe 30/11/2018 walitakiwa kusimama mahakamani kutoa ushahidi huo, wakiwa wanajiandaa kuja dar es salaam ndio wakapata hiyo ajali wakiwa ndani ya kivuko cha Mv nyerere wote walikufa pamoja na mawakiri wao wawili upande wa mashtaka, hakukuwa na ushahidi mwingine tena, John aliachiwa huru baada ya kuonekana hana hatia lakini ukweli mchezo wote alicheza Madam Jane na watu wake" Osman Azizi alieleza kwa kifupi.

" Dah huyu mama kumbe sio poa, lazima tumshikishe adabu, anko nakushauri uwe makini sana, inavyoonekana madam Jane hakuna kitu anashindwa"

"Naelewa hata usijali"

"Powa basi badae"
Revocatus akaondoka.

[emoji294][emoji294][emoji294]

Upande wa pili kule msituni walipo Yusto na Brandina mambo yalizidi kuwa makubwa, tayari kila mmoja alikua hana uwezo wa kujizuia tena dhidi ya mwenzake.

Yusto alianza kumpiga mabusu ya hapa na pale jambo lililomfanya Brandina kuwa kwenye wakati mgumu. Wakati huo walikuwa bado ndani ya maji katikati ya ule mto.
Brandina akaanza kutoa miguno, huku na yeye akiuchomeka mguu wake katikati ya miguu ya Yusto.
Akaingiza mkono kwenye maji akamshika Yusto tumboni na kisha akaanza kuushusha chini taratibu.

Mwisho alimshika mwanajeshi wa Yusto ambae tayari alikua amesimama imara, akaanza kumminya minya taratibu akianzia juu kushuka chini.

Walizidi kumwagiana mvua ya mabusu na mwisho Brandina alimshika Yusto kwenye mabega kisha akamrukia, akaibana miguu yake miwili nyuma mgongoni kwa Yusto.

Yusto nae akapitisha mikono yake na kumshika Brandina kwa nyuma asianguke.

Hapo Brandina alianza kuzungusha kiona chake laini kiasi cha kumfanya Yusto asiwe na uwezo wa kuvumilia tena, akiwa amembeba Brandina juu juu alisogea nae hadi sehemu yenye kina kifupi cha maji.

Hapo wakaanza kufurahia penzi kwa hamu kubwa, hakuna aliyekumbuka tena kama wanatafutwa na walinzi kutoka ngome ya madam Jane. Yusto hakuwaza tena kuhusu Caren, licha ya kutaka kusimama kwenye msimamo wake lakini alijikuta anashindwa kuikwepa mitego ya Brandina mwanamke aliyekua amepambana kwa hali na mali kuyaokoa maisha yake.

Je, nini kitafuata?

Ni nini mpango wa Osman Azizi?
Anataka nini?
Vipi kuhusu penzi la Caren na Yusto ambalo tayari limeingia doa kubwa?

ITAENDELEA.....

TUNAENDELEA KUUWASHA MOTO NA BAKI NA MIMI...
Kupata simulizi hii yote kwa pamoja lipia tsh elf 1 tu kisha nipigie... Namba 0756862047-saul
 
Ungetupia hata vipande viwili mwanangu dude linanoga kinoma.
 
Hta kma story n Yako ila Kuna wakat mnazingua serious
Shida nn mkuu, tumeanza wote mwanzo mpaka sasa tuko tunaelekea Mwishoni na sijaacha kupost bado unanilaumu kweli, vipi kama nikiweka intereste ya pesa mbele na kumaliza kwa wale waliolipia tu.
Hujui tuna risk sana kazi zetu kupost public kama hivi mtu anaiba na anauza vipi kama nikipost yote kwa pupa kama unavyotaka.
Tsh elf 1 ndio ikufanye kutoa lawama kama hizo.
Relax boss wangu. Fuatilia SIMULIZI hii na nyingine zote zinazoendelea nitamaliza zote mapka mwisho ila usinipangie ratiba ya kupost
 
Kaka hakuna njia tofauti na whatsapp naeza ipata hii hadithi nku2mie hela un2mie...humu Pm haiwezekani au messenger Fb...
 
Back
Top Bottom