𝐃𝐎 𝐍𝐎𝐓 𝐒𝐇𝐎𝐔𝐓
𝐬𝐞𝐚𝐬𝐨𝐧 2
Mtunzi: Saul david
WhatsApp: 0756862047
Email:
saulstewarty@gmail.com
ILIPOSHIA...
uso kwa uso Frabk akakutanisha macho tena na Caren aliyekuwa amesimama nyuma yake, hata hakujua kafika saa ngapi.
"Ca..car...caren" Frank aliita akionyesha kutokujiamini kabisa, ilikuwa ni rahisi kwa Caren kugundua kuna kitu hakipo sawa.
Je, nini kitafuata?
SASA ENDELEA...
" Vipi kuna shida" aliuliza Caren
"Aah hamna kunu jamaa yangu mmoja kanipigia nilimpa taarifa ya kupotea Yusto" alijibu Frank
"Ee kasemaje, amenuona?"
"Aa..ee hapana amedai alikuwa nae kama masaa matatu hivi yamepita" Frank alidanganya kiasi cha kumfanya Caren azidi kumtilia mashaka, masaa matatu yaliyopita anakumbuka alikua na Revocatus kule msitu ambae alimthibitishia kuwa Yusto alikuwa ametekwa.
"Aah sawa" Caren alijibu akajifanya kama vile hajahisi chochote.
Mwisho Frank aliondoka kuelekea bwenini katika chumba anachoishi, akachukua zile nguo alizoagizwa na Simigo kisha akatoka na kufunga mlango.
Akiwa bado mlangoni alihisi ni kama kuna mtu alikuwa kwenye kona moja ya jengo hilo akimfuatilia.
Frank akawa makini zaidi kwani hakutakiwa mtu yeyote ajue uhusiano uliopo kati yake yeye na Yusto dhidi ya upande wa pili wa Simigo na wenzake ambao walikuwa wakitambulika kama wapishi wapya wa chuo tu.
Frank alitembea kwa tahadhali huku akigeuka nyuma mara kadhaa hadi pale alipotoka nje kabisa ya chuo.
Aliliona lile gari aliloelekezwa akaingia upesi na kufunga mlango. Ndani aliwakuta Yusto, jasusi Brandina na jasusi Simigo pekee.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Caren ambae ndie aliekuwa akimfuatilia Frank kwa siri alishindwa kuendelea na zoezi hilo mara tu baada ya kubaini kuwa tayari Frank alishahisi kuwa anafuatiliwa.
Akasubiri mpaka atoke nje kabisa ya chuo kisha na yeye akasogea hadi getini. Kwa bahati mbaya hakuweza kumuona tena Frank.
"Anaficha nini huyu?" Caren alijiuliza wakati akiangaza macho huku na huku bila mafanikio, hakujua Frank ameelekea wapi, wala hakuwaza kuhusu gari aliyoingia Frank ambayo ilikuwa imesimama pembeni ya barabara hatua kadhaa kutoka pale alipokuwa.
[emoji294][emoji294][emoji294]
"Vipi ulimwambia Caren kuhusu Yusto?" Simigo aliyekuwa mbele kama dereva aliuliza baada ya kumuona Caren akihangaika pale mbele yao.
Ilikuwa ni kauli iliyomshtua Yusto ambae wakati huo yeye na Brandina walikuwa wanavaa zile nguo walizoletewa na Frank.
"Unaniuliza mimi?" Aliuliza Frank
"Ndiyo wewe"
"Aah hapana lakini tulikua wote wakati unapiga simu, kwani vipi?"
"Yule pale naona ni kama kuna mtu anamtafuta"
"Yuko wapi" Yusto na Frank walihoji kwa pamoja kisha wote waangalia mbele kule alipokuwa akiangalia Simigo.
Walimuona Caren akipiga hatua kwenda na kurudi, moyo wake ulikuwa haujatulia kabisa bado alikuwa na wasiwasi mkubwa dhidi ya mpenzi wake Yusto hadi dakika hiyo alikuwa hajui mahali alipo.
Alichukua simu yake na kuiweka sikioni mara kadhaa akijaribu kumpigia Yusto lakini majibu yakawa ni yale yale Yusto hapatikani.
Yusto alimtazama Caren kwa macho yaliyojaa huruma, alijua vema kuwa Caren alikuwa anapitia ile hali yote kwa sababu yake.
Brandina alimtazama Yusto usoni akaona kabisa ni kwa namna gani moyo wa mwanaume huyo ulikuwa umezama mazima kwa Caren.
"Kabla hatujashuka kuna mambo nataka tuzungumze sisi wanne, lakini kabla ya yote nataka kujua nini kimetokea, nimeona hilo jeraha la Yusto ni la risasi, kulikuwa na nini, eti Brandina?" aliuliza Simigo, wakati huo walimuona Caren akiondoka kurudi ndani ya chuo.
Brandina alieleza mwanzo mpaka mwisho namna Yusto alivyotekwa pale nje ya chuo akamfuatilia hadi msituni katika ngome ya madam Jane na baadae kufanikiwa kumuokowa.
"Sasa kwa nini hukutupa taarifa mapema Brandina huoni kama mmehatarisha maisha yenu" aliuliza Simigo.
"Hata sikuwaza kama mambo yangekuwa mazito hivi, mwanzo nilijua ni vibaka tu"
"Sawa, kwa hiyo chanzo cha Yusto kutekwa ni kwa sababu ya ugomvi wake na John, mbona haiingi akilini huyu mama ziko timamu kweli kichwani" aliuliza simigo huku akitabasamu, kisha akaendelea kuzungumza...
"Atakuwa anampenda sana mwanae ndio maana, halafu nimeambiwa na bosi Mark Moon kuwa wewe na Yusto mtakuwa na kazi mpya kuanzia sasa ya kumfuatilia huyo madam Jane nafikiri huu utakuwa ni mwanzo wenu mzuri"
Alisema simigo hali akiwatazama Yusto na Brandina kwa zamu.
Wakati wakizungumza hayo, Frank alionekana akiwa bize na simu yake, akawa anaandika ujumbe huu kwenda namba ambayo haikuwa na jina.
"OYA MAZEE, YUSTO KARUDI ULE MPANGO WETU UENDELEE BASI"
Frank aliutuma ujumbe huo kisha akaendelea kusikiliza maelezo ya Simigo, hakuna mtu aliyemshtukia.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Upande wa pili
Baada ya madam Jane kutoka kuonana na Osman Azizi, hakwenda nyumbani alipitiliza moja kwa moja hadi ofisini kwake huku akijaribu kuituliza akili yake.
Aliwasiliana na watu wake wote wa karibu anaowaamini akawataka wafike ofisini kwake mara moja. Azizi alikuwa amemchanganya sio kidogo, ilikuwa ni lazima achukue hatua madhubuti kukabiliana nae, japo ki uharisia hakujua ni wapi pa kuanzia kwani Azizi alikuwa amemshika pabaya.
Aliingia ofisini kwake akatulia na kujaribu kuyatafakari matukio yaliyotokea siku hiyo. Suala ambalo lilizidi kumchanganya ilikuwa ni ile taarifa ya kwamba mtoto wake Yusto yupo hai, huu ndio ulikuwa mtihani mkubwa kwake pengine kuliko hata vile vitisho vya Osman Azizi, alijali sana kuhusu Yusto.
Wakati akiwaza hayo, madam Jane alijikuta anamkumbuka pia yule kijana Yusto aliyeleta kashikashi nzito katika ngome yake ya siri kule msituni na hadi dakika hiyo vijana wake hawakuwa wamempata.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Hatimae wale watu watatu muhimu aliowaita madam Jane walifika ofisini kwake.
Dr Givan, Msigwa na Magdarena Masebo, hawa walikuwa ni watu walioaminiwa sana na madam Jane, walizijua siri nyingi sana za mama huyu, wao ndio waliokuwa wakisuka na kupanga mipango mbalimbali wakishirikiana na bosi wao madam Jane.
Baada ya kufungua kikao madam jane aliwaeleza kwa kifupi yale yaliyotokea siku hiyo, kuanzia sakata la Yusto hadi lile la Azizi.
"Madam hisia zangu zinaniambia lazima Azizi atakuwa alishapandikiza watu wake miongoni mwetu, haiwezekani hata kidogo akayafahamu mambo yote haya kwa urahisi namna hii, mimi naona jambo la kwanza ni kuwatafuta kwanza wasaliti, tukiwapata tutawabana na wao ndio watatupa mwanga namna ya kupambana na Azizi na kisha kumpata Yusto" alisema Magdarena.
"Uko sahihi Magdarena, lakini kipaombele changu kwanza nimpate mwanangu Yusto, nimfahamu kwanza, Azizi atanisumbua sana kupitia Yusto inabidi nicheze na akili yake, tena mambo haya inatakiwa tuyafanye kwa siri kubwa kwa sababu tayari tumejua kuna wasaliti kati yetu"
"Sawa bosi lakini mi nafikiri tungefanya kama Magdarena alivyoeleza, tuwatafute wasaliti kwanza wao ndio wataturahisishia yote pamoja na hilo la kumpata Yusto" Msigwa aliunga mkono hoja ya Magdarena.
"Nesema hivyo kwa sababu wakati naongea na Azizi leo alisema huenda nikawa tayari nimekutana na Yusto bila kujua ni mwanangu, hii inaonyesha wazi huenda kweli nimeshakutana na yusto,
Yule kijana aliyeleta shida kambini kwangu nahisi anaweza kuwa ndiye Yusto mwenyewe, yaani mwanangu, hata jina lake ni Yusto nahitaji kupata vipimo vya DNA haraka iwezekanavyo, Dr. Givan"
"Yes madam, nimekuelewa tatizo hamna, nitashiriki na Caren alete sample ya Justo today, then nitatowa majibu immediately" alisema Dr Givan, mzungu ambae kiswahili kilionekana kumsumbua.
"Hapana Caren nimempa kazi nyingine ngumu, hebu tafuta vijana waingie mle chuoni walete hiyo sampuli unayo ihitaji kwa ajili ya kupima vinasaba"
"No problem"
" Kwa hiyo mapaka Sasa Caren hajafanikiwa kumuuwa Zubeda" alihoji Msigwa.
"Hata mimi nashangaa mlinihakikishia kwamba ni binti mzuri anaeweza kazi sasa anachukua vipi mda mrefu kiasi hiki, lakini tushughulike na hili la Yusto kwanza, baada ya hapo tutapanga nini kifuate, kuanzia sasa na kuendelea nahitaji muwe makini kupita kawaida, sitaki Azizi ajue nini nafanya sawa sawa"
Madam Jane alisistiza tena.
"Swali lingine la muhimu, tuna uhakika gani kama Yusto atarudi chuoni, vipi kama lile tukio la kutekwa likawa limemtisha akaamuwa kuondoka" aliuliza Magdarena.
"Aah uko sahihi, ila nina asilimia kama 70 Yusto atarudi chuoni, ni kijana mwenye nguvu anajiamini sizani kama anaweza kutishika kiasi hiki, tayari anajua nilimteka kwa sababu gani, tuliongea tukayamaliza atarudi tu" madam Jane alieleza, akionekana kuisoma vizuri saikolojia ya Yusto kwa ule mda mfupi waliokuwa wote.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Nusu saa baadae Yusto akiwa ameongozana na Frank rafiki yake aliingia chumbani kwake, chumba ambacho alikitelekeza kwa siku mbili mfurulizo kutona na mikiki mikiki ya hapa na pale, hatimae alikuwa amerejea.
"Vipi unaenda wapi mbona hukai" Yusto aliuliza baada ya kuona Frank ni kama anataka kuondoka.
"Ah naona utakuwa umechoka, oga kwanza upumzike mimi nitakuja baadae" Frank aliongea kwa unyonge
"Aah unajua nini Frank mshikaji wangu, najua hujapenda jinsi navyofanya mambo yangu kimya kimya bila kuk...."
Aliongea Yusto lakini kabla hajamalizia Frank akadakia.
"Najua, si nimemsikia Brandina wakati anaeleza kasema ulitekwa ama kunakingine umefanya sikijui? usijali mi niko poa" alisema Frank, akawasha taa kisha akafungua mlango na kuondoka zake.
Yusto alibaki ameduwaa kwa sekunde kadhaa, akajua wazi kabisa kuwa Frank alikuwa amekasirika.
"Huwezi jua Frank, nayopitia mimi ni makubwa mno sitaki nikuingize kwenye matatizo"
Yusto alijisemea mwenyewe kisha akili na mawazo yake yote yakahamia kwa Caren, alikuwa amemkumbuka sana mwanamke huyo, alijikuta anapata shauku kubwa ya kumuona.
Haraka aliingia bafuni akaoga kisha, akavaa nguo upesi upesi.
Alichukua kitabu chake cha kumbukumbu kisha akaandika kwa kifupi.
....
Madam Jane ...
picha na Zubeda ....
ndoa na bosi mark moon ...
Osman Azizi ...
John mtoto wa madam Jane ...
zubeda na mtoto mchanga ...
kufuatiliawa....
Baada ya kuandika hayo Yusto alifunika kitabu chake kisha akakitupia kitandani, alifanya hivyo ili kutunza kumbukumbu juu ya suala la vitu ambavyo alitakiwa kuvifuatilia kiundani sana lakini hakuwa na muda ilikuwa ni lazima kwanza aonane na Caren ndipo mambo mengine yaendelee.
Akiwa anaelekea mlangoni mara alisikia sauti ya mwanamke akipiga kelele nje ya chumba chake.
"Yusto ... Yusto... Yusto...anakufa, wahi kimbia Yusto...."
Kelele hizo zilimfanya Yusto kufungua mlango kwa kasi akatoka nje.
"Kuna nini, Anna vipi?" Aliuliza Yusto huku akimtazama mwanamke huyo (Anna) ambae alikuwa anasoma nae darasa moja.
"Frank, frank kapigwa na shoti ya umeme" alieleza yule mwanamke.
"Nini" Yusto alitahamaki
"Wahi kamsaidie, atakufaa"
"Yuko wapiiiiiii..."
"Kuleee"
"Ukumbini, ukumbini kule"
Kabla Anna hajamalizia maelezo hayo tayari Yusto alikuwa amekimbia kuelekea ulipokuwa ukumbi mkubwa wa chuo cha mark moon.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Caren alikuwa amejilaza kitandani ndani ya chumba chake, akili yake ikiwa imehama kabisa huku hofu ya kupotea kwa Yusto ikizidi kumtawala.
"Nitakaa kusuburi hadi saa ngapi"
Alisema Caren, akakurupuka na kukaa kitandani lakini kabla hajafanya lolote mara alisikia mtu akigonga mlango wa chumba chake kwa nguvu.
"Naniii" Caren alifoka
"We umejifungia humo, hujasikia kinachoendelea huko nje"
"Aah! kumbe ni wewe Taby, kuna nini kwani"
"Kuna watu wamepigwa na shoti ya umeme huko ukumbini, yule kaka handsome Yusto yuko hoi huko" alieleza yule dada, akiwa amesimama nje usawa wa mlango wa chumba cha Caren.
kufumba na kufumbua alimuona Caren akitoka kama mshare nje ya chumba chake, akakimbia na kuteremka ngazi kwa kasi bila hata kuzungumza chochote na taby.
"Eeh jamani taratibu basi we dada, unawahi hivyo kwani wewe umekuwa tanesco hahahha mapenzi bana, mbona mimi sijawahi penda au kupendwa hivi jamani, ajitokeze kijana mmoja basi hahaha" alisema Taby huku akiufunga mlango wa chumba cha Caren na funguo kisha akaondoka.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Yusto alifika na kuingia ukumbini moja kwa moja.
"Frank, Frank, uko wapi" Yusto aliita huku akitembea na kuangaza macho yake kila upande, ukumbi ulikuwa ni mtupu, hakukuwa na dalili ya kuwepo mtu mle ndani.
Yusto alikuwa amefika katikati ya ukumbi huo ambao ulikuwa mkubwa sana, ulikuwa na sehemu za kukaa juu na chini kama ghorofa vile, ulikuwa ni ukumbu uliojengwa kisasa.
Taratibu alianza kuingiwa na wasiwasi kwani ndani ya ukumbi huo kulikuwa giza kiasi, taa zilikuwa zimezimwa zote.
"Frank..." Yusto aliita, lakini kimya.
Mara ghafula taa zilikuwa kwa pamojaa...
"Sapraiiiiiiiiiiiizi"
kelele za wanafunzi wa kike na wa kiume zilisikika na hapo wakajitokeza kutoka kona tofauti tofauti za ukumbi huo.
[emoji445] _Happy birthday to you
Happy birthday to you
Happy birthday dear Yusto
Happy birthday to you_ [emoji445]
Mamia ya wanafunzi walijitokeza huku wakiimba kwa nguvu kelele zilizopaa na kupasu anga la chuo cha Mark Moon.
Ilikuwa ni siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Yusto, sherehe ambayo ilikuwa ifanyike siku moja jana yake lakini ikashindikana kutokana na Yusto kutokuwepo chuoni hivyo wakaamua kumsubiri hadi atakaporudi.
Taratibu zote hizi zilikuwa zikiongozwa na Frank rafiki wa karibu wa Yusto pamoja na marafiki wengine wa Yusto, walifanya maandalizi yote hadi siku ya jana yake lakini kwa bahati mbaya Yusto hakuwepo chuoni siku hiyo.
Taarifa za sherehe ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Yusto (birthday) zilisambaa kwa kasi sana chuoni hapo. Watu wengi walikuwa wakimpenda Yusto hivyo wakaungana na akina Frank kuhakikisha wanamfanyia 'suprise' ya viwango.
"Jamani naombeni utulivu tafadhali, kabla hatujaendelea kwenye hatua nyingine ya kukata keki kuna sapraizi nyingine tunataka kuifanya kwa ajili ya kaka yetu hapa Yusto kisha tutaendelea" alisema dada mmoja aliekuwa ameandaliwa kama mshereheshaji.
Ukimya ukatawala na taa zikazimwa tena.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Caren alionekana anakimbia kwa kwa kasi kuelekea ukumbini, taarifa alizopewa kuhusu Yusto kupigwa na shoti ya umeme zilimshtua sana. Njiani alikuwa akimuomba Mungu amnusuru mwanaume huyo ambae alikuwa akimpenda kuliko kitu kingine chochote.
Kelele alizokuwa akizisikia kutoka ukumbini zilitoweka ghafula, kukawa kimya, Caren alishindwa kuelewa ni nini kinaendelea, hofu na wasiwasi vikamzidia. Alitembea taratibu kuingia ukumbini akawa anaangaza macho huku na huku.
Ingawa kulikuwa na giza kiasi lakini kwa uzoefu wa Caren alipata hisia kuwa kuna watu mle ndani.
"Nini kinaendelea, Yusto yuko wapi, au ni mtego...."
Haya ndiyo mawazo yaliyopita kwenye kichwa cha Caren, akajipapasa kiunoni,kwa bahati mbaya au nzuri kwa upande mwingine, hakuwa amebeba bastola yake.
Mara taa ziliwashwa tena hapo ndipo Caren aliweza kuwaona mamia ya wanafunzi waliokua wamekusanyika ndani ya ukumbi huo.
"Hatimaeee birthday giiiiirl amekujaaaaaa" yule dada mshereheshaji aliongea kwa mbwembwe, hapo ukumbi mzima ukaripuka kwa shangwe na wimbo wa birthday ukaanza kuimbwa upya.
Caren alipotupa macho yake mbele hakuamini alichokiona, Yusto alikuwa amesimama mbele yake anamtazama huku akiwa ameachia tabasamu mwanana.
"Yustoo.." Caren aliita kwa sauti ya chini huku akishika mdomo wake kwa mshangao, hapo akashindwa kujizuia akakimbia na kwenda kumkumbatia Yusto kwa nguvu sana.
Shangwe, makofi nderemo na vifijo vikasikika tena wakati huo Yusto na Caren wakiwa wamekumbatiana kwa hisia kali sana.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Wakati sherehe hiyo ikiendelea ndani ya chuo cha Mark Moon, nje ya geti lilipaki gari moja la kifahari, vijana watatu wakashuka na kuingia ndani ya chuo hicho bila wasiwasi wowote kama vile wanafunzi wanaosoma chuo hicho. la hasha hawa walikuwa ni vijana kutoka kwa Madam Jane waliotumwa kuja kuchukua sampuli yoyote kutoka kwa Yusto ambayo itatumika kufanya kipimo cha vinasaba yaani DNA.
Madam Jane alitaka kuthibitisha kwanza kama Yusto ni mtoto wake au laa...
ITAENDELEA.....
Njoo WhatsApp malizia vipande 19 vilivyobaki kwa tsh Elf 1 tu...0756862047