SIMULIZI RIWAYA
JF-Expert Member
- Feb 19, 2022
- 417
- 1,285
- Thread starter
- #161
DO NOT SHOUT
(Usipige kelele)
Sehemu ya..…….......32
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
ILIPOISHIA.....
punde akachomoza mtu akiwa na pikipiki hiyo akija kwa kasi eneo hilo la bandari.
Sura yake haikuwa ikionekana Kutokana na helment aliyokuwa amevaa kichwani,
kasi aliyokuwa anakuja nayo ililifanya koti lake kubwa kupepea Kutokana upepo mkali ulokuwa ukimpuliza.
Naam huyu hakuwa mwingine bali Yusto.
SONGA NAYO....
Abdullah mpambe wa John alisikia muungurumo huo wa pikipiki, yeye na vijana wake wanne walitoka nje ya lile kontena walilomfunga mama mlezi wa Yusto.
Walisimama nje huku macho na masikio yao yakiwa yameelekezwa kule sauti ya muungurumo huo wa pikipiki inakotokea.
Sekunde chache baadae kwa mbali wakamuona mtu anaibuka na pikipiki hiyo akija kwa kasi upande wao.
"Atakuwa ni nani bosi"
"Hata sijui, hebu nipe simu yangu"
"Unataka umpigie John au"
"Ee huenda akawa ametumwa huyu mtu"
"Aah hapana bosi huyu ni Yusto bila shakaa"
"Yusto,hapana haiwezekeani, kapajuaje hapa"
Abdullah na wenzake walikuwa wakiulizana maswali ambayo hakuna aliyekuwa na majibu yake.
Yusto alizidi kukalibia eneo la bandari na hapo uvumilivu ulimshinda bwana Abdullah, akachomoa bastola yake na kuielekeza mbele anakotokea Yusto Kisha akapaza sauti.
"Weweee, simama hapo hapo la sivyo nitakumwaga ubongo, simamaaa"
Maneno hayo ya bwana Abdullah hayakusaidia chochote, Yusto aliendelea kuja na pikipiki yake
kwa kasi
****
Caren alifika eneo lile la soko la matunda Kama alivyo elekezwa na Revocatus mtu aliyekuwa anamsaidia kuangalia location ya simu ndogo ya Yusto.
akashuka haraka na kumlipa dereva bajaji.
"Asante afande kazi njema" alisema yule dereva bajaji Kisha akaondoka zake.
Caren alianza kutembea katikati ya lile soko huku akiangaza macho yake huku na huku katikati ya umati wa watu akimtafuta Yusto lakini hakumuona.
Aliingiza mkono Wake mfukoni akachukua simu yake hapo akakutana na simu zilizopigwa bila kupokelewa kama 11 hivi ' missed call' kutoka kwa Revocatus, akampigia.
"Ee hallo Caren mbona nakupigia sana hujapokea"
"Simu ilikuwa silence Revo, vipi niambie"
"Aah Sasa huyo mtu unamfuatilia katoka hapo sio mda, location inaonyesha anaelekea bandari ya zamani bandari ya uhuru kule"
"Ooh my God, kweli"
"Ndiyo Caren, alafu sijui yuko na usafiri gani maana anaenda kwa kasi sana, kasi mno nahisi kuna shida Caren hebu sema tuje tukusaidie basi"
"Hapana Revo hii ni kazi yangu binafsi siwezi kutumia nguvu ya bosi inaweza kuleta shida acha nipambane mwenyewe"
Aliongea caren kisha akakata simu.
"Bandari ya uhuru"
Caren alijisemea mwenyewe akili yake ikifanya kazi haraka haraka akajua cha kufanya.
*****
"Simama hapo wewe mjinga" Abdullah alizidi kupaza sauti akimtaka Yusto asimame lakini wapi Yusto hakufanaya hivo,
Hapo uvumilivu ukamshinda bwana Abdullah akaikoki bastola yake tayari kufyatua risasi.
Lakini kabla hajafanya hivyo mara Yusto alisimama juu ya pikipiki ikiwa bado inaenda kwa kasi, akaruka na kutua chini kwa ufundi mkubwa.
Pikipiki yake ikawa bado inaendelea kwenda mbele kuelekea kule walipokuwepo Abdullah na wenzake ambao walibaki wametoa macho kwa mshangao wasielewe kinachoendelea.
Kabla pikipiki haijawafikia Abdullah na wenzake, Yusto alichomoa bastola yake akalenga shabaha kwenye tenki la mafuta Kisha akafyatua risasi mbili mfurulizo.
Pikipiki ilipuka karibu kabisa na eneo walipokuwepo Abdullah na vijana wake wakaruka pembeni huku wangine wakijeruhiwa vibaya mno.
"Shambuliaa" Abdullah alitoa amri kwa vijana wake na hapo wakachomoa bastola zao na kuanza kumimina risasi pale alipokuwepo Yusto.
Yusto aliviringita chini kwa kasi akaenda kujibana kwenye moja kati ya makontena mengi chakavu yaliyokuwepo eneo hilo.
Majibizana ya risasi yalianza. Bandari yote ilizizima kwa milio ya risasi.
****
Jonh alionekana gari yake nje ya jego kubwa la ghorofa lililokuwa likimilikiwa na mama yake.
Hakujua wala kuelewa kisanga alichokiacha nyuma bandarini alikokuwa amemfungia mama yake na Yusto.
Akashuka na kuanza kuelekea kwenye mlango wa kuingilia ndani ya ghorofa hilo la kisasa.
Akiwa mlangoni anakutana na msafara wa mama yake akiwa ndio anatoka nje ameongozana na wasaidizi wake pamoja na walinzi 'bodyguard'. Huyu ndiye madam Jane mwenyewe.
"Jonh" aliita yule Madam Jane hali akionyesha mshangao kidogo.
John hakujibu badala take akamsogerea karibu mama yake.
"Tunaweza kuongea mama"
"Now?"
"Yes, ni muhimu please"
"Lakini si ulitakiwa uwe chuoni, alafu unakujaje bila kuniambia si unajua ratiba zangu"
"Ndiyo mama, ni dharula kama linivyo kwambia hata hivyo hatutatumia mda mrefu"
Alisema John.
"Misheli" Madam Jane alimwita secretary wake.
"Yes madam"
"Piga simu kwa waziri, mwambie tukutane saa kumi na moja sio saa kumi tena"
"Sawa Madam"
Baadae jonh na mama yake madam Jane yake waliongozana, wakapanda lifti hadi ghorofa ya 4 ilipokuwepo ofisi ya madam Jane.
John alionekana kuwa na mawazo kiasi bado alikuwa anajiuliza na kutamani kujua ni uhusiano gani uliokuwepo kati ya mama yake na mama yake Yusto ambae ni kichaa kwa Sasa.
"John uko sawa "
Aliuliza madam Jane baada ya kuona kabisa kuna jambo lilikuwa likiisumbua akili ya Yusto.
****
Bandarini hali iliendelea kuwa ngumu hasa kwa Yusto aliyekuwa na bastola ndogo yenye risasi kumi na mbili pekee.
Alifungua na kutazama Sasa zilikuwa zimesalia risasi tano basi.
Abdullah na wenzake bado waliendela kumuwinda na kila walipopata upenyo walifyatua risasi.
Waliendela kuzungushana kwenye makontena hayo huku kila mmoja akiwa makini kulinda usalama wa maisha yake.
Muda ulizidi kwenda na Sasa Yusto alibakiza risasi mbili pekee.
Ilikuwa ni lazima afanye jambo la sivyo atashindwa kumtoa mama yake kwenye mikono ya watu hao.
Je nini kitafuata?
ITAENDELEA.....
Usiache kufuatilia simulizi yangu mpya ya MOTO kuliko hii inaitwa THE MODERN WAR (vita ya kisasa)
Napatikana WhatsApp +255756862047.