DO NOT SHOUT
Sehemu ya.........30
Mtunzi: Saul David
Email:
saulstewarty@gmail.com
ILIPOISHIA....
"Hapo ndipo Mahali tutakapo kutana kesho kwa ajili ya mazungumzo yetu, kesho ndio siku nitakwambia nini nataka kutoka kwako Madam Jane, karibu tujekushuhudia kwa pamoja jinsi Fiston Mayele anavyotetema" Alisema Osman Azizi kisha akakata simu.
Je, nini kitafuata?
SASA ENDELEA....
"Mpuuzi huyu" madam Jane alitukana mara tu baada ya Osman Azizi kukata simu yake.
"Anapanga nini huyu mwana haramu, kwa nini anataka tukutane uwanjani, ni lazima nitakuuwa Azizi" Madam Jane aliongea huku akionekana kukosa amani kabisa.
Haraka alipiga simu mahali na kuiweka sikioni.
"Hallo, naomba kusanya watu wote, waliopo kambini na walio nje ya kambi pia, wote akina Caren, Revo na wengine nawahitaji sasa hivi tukutane kule kwa siku zote" madam Jane alionge kisha akakata simu akapiga tena namba nyingine
"Ee Roy.. naomba nisaidie kitu kimoja, kata tiketi za watu kama ishirini hadi thelathini hivi za kuingia kesho uwanjani kwenye mechi ya yanga na Kagera Sugar pale Benjamin mkapa...we fanya hivyo maelezo mengine baadae...sawa" madam Jane alitoa agizo kisha akakata simu.
akavuta pumzi ndefu akijaribu kuituliza akili yake ambayo mpaka sasa ilikuwa imeelemewa na mambo ambayo yaliyokuwa yanamkabili.
Akatazama juu ghorofani, kwa mbali alimuona mwanae John akiwa dirishani, wakati huo John nae alikua bize na simu yake, hakujua anafanya nini.
Madam Jane aliwaza deni alilonalo kwa mwanae John, kumuweka wazi kwa kila kitu kuhusu baba yake mzazi pamoja na ule undugu uliopo kati yake na Yusto. Ilikuwa sio kazi rahisi hata kidogo, Madam Jane hakua tayari kuweka wazi kuwa Mark Moon ndiye baba mzazi wa John kwa hili hakua tayari kabisa.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Upande wa pili ndani ya hospitali ya Mountenia.
Mark moon alionekana kuchanganyikiwa mara tu baada ya Zubeda kutaja kitu kinachoitwa code G ambayo ndio hasa ilikuwa shabaha kubwa ya Osman Azizi.
"Mark una nini lakini mbona hutulii" Zubeda alimuuliza Mark Moon baada ya kuona hali yake imebadilika ghafula.
"Zubeda, sijui hata nisemaje, hata nikikueleza huwezi kuelewa, ila jua tu nipo hatarini, Osman Azizi ni mtu hatari sana, sijui hata amefikia wapi mpaka sasa, sijui nitamdhibiti vipi, code G ndio maisha yangu Zubeda vipi kama ameshaipata bila mimi kujua" mark moon aliongea hali akipiga hatua kwenda huku na huku mbele ya kitanda alicholala Zubeda.
"Mark hebu jaribu kutulia basi, kwani nani mwingine ameingia chumbani kwako, Azizi hawezi kuipata hiyo code G unayosema, sielewi ki undani lakini jaribu kutuliza akili yako ili ufanya maamuzi sahihi" Zubeda alijaribu kumtuliza Mark Moon.
Ni kama maneno ya Zubeda yalimuamsha mark moon kutoka usingizini, hasa baada ya kusema neno chumbani, mark moon alisimama ghafula.
"Umesema chumbani ee, yes, uko sahihi, madam Jane, Azizi atakua amemtumia madam Jane kupata Code G, ooh shit, watakua wameshakutana au bado, itakua bado ningejua, lakini vipi kama.....?" Mark moon alikuwa alijiuliza na kujijibu mwenyewe, haraka alitoa simu yake akampigia Brandina.
Wakati huo Brandina alikua ndani ya chuo chake eneo la stoo jikoni, alikua akiangalia video aliyoletewa na Simigo ikonyesha matukio yaliyotokea ukumbini kwenye sherehe ya kuazimisha siku ya kuzaliwa kwa Yusto.
"Hallo bosi"
"Vipi Brandina, mmeshaanza kazi ya kumfuatilia Madam Jane"
"Aa..bosi...ee tuli..."
"Brandina please nipo kwenye matatizo makubwa, nahitaji kujua ratiba zote za hivi karibu za Madam Jane, alienda wapi alikutana na nani saa ngapi kwa ajili gani, yuko wapi sasa na anapanga nini, kama ukihitaji msaada niambie, naomba lisimamie hili kwa nguvu kubwa kuanzia sasa hivi nipe ripoti" mark moon aliongea kwa msisitizo, Brandina alielewa, akakata simu.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Brandina hakua na muda wa kupoteza haraka alijiandaa kisha akaenda kumfuata Yusto chumbani kwake kwani ndie mtu alietakiwa kuambatana nae kwenye kazi hiyo.
Brandina alifika hadi mlango wa kuingilia chumba cha Yusto, akataka kugonga lakini akasita mara baada ya kusikia sauti za watu wakiongea na kucheka ndani ya chumba hicho.
Brandina hakua na sababu ya kujiuliza mara mbili, alijua wazi kuwa Yusto yupo mle ndani na Caren.
Wivu ulimuingia kiasi, akajikuta anayakumbuka yale matukio ya msituni akiwa na Yusto lakini Sasa hakuwa na cha kufanya tayari mwenye chakula alikuwa anajipakulia na kula mwenyewe.
Brandina aliamua kuondoka na kumuacha Yusto afurahie wasaa alioupata na mpenzi wake Caren, akapanga kumtafuta baadae.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Brandina alianza kuifanya kazi aliyoagizwa na mark moon, alienda moja kwa moja hadi nyumbani kwa madam Jane, kwa bahati nzuri alifika wakati ule madam Jane anaingia kutoka Mountenia hospital akiwa pamoja na mwanae John ndani ya gari.
Waliposhuka Brandina aliweza kushuhudia lile tukio la bodaboda kuleta tiketi kutoka kwa Osmaz Azizi kwenda kwa madam Jane.
Akiwa amejificha mahali Brandina alilishuhudia tukio hilo kwa makini lakini hakujua ni nini hasa kinaendelea. Akatamani kujua zaidi ikiwa kama hatua ya kwanza ya kazi yake.
Alianza kumfuatilia yule dereva boda boda mara tu baada ya kutoka nyumbani kwa madam Jane.
Brandani akiwa na pikipiki, nyuma ya yule bodaboda alimuona akisimama mahali kisha akashuka na kwenda kwenye kibanda cha M-pesa.
Brandina alisimama mahali akiwa anachunguza nyendo za kijana huyo, alimuona akitoa pesa kama laki 4 hivi akaziweka mfukoni, hizi zilikua ni pesa alizolipwa na Osman Azizi mara baada ya kuifanya kazi ile ya kukata na kupeleka tiketi kwa Madam Jane.
Akiwa anarudi mahali alipoiacha pikipiki yake mara ghafula wakatokea vijana wanne wakamvaa yule dereva bodaboda kisha wakambeba juu juu na kuingia nae vichochoroni, lilikua ni tukio la ghafula na haraka sana ambalo halikuzua taharuki yoyote kwa watu wachache waliokuwepo eneo hilo, hakuna aliyeona.
Brandina alishuhudia yote akiwa nyuma ya mti mmoja mkubwa, hakutaka kuwaacha waende, bado kuna vitu alitamani kuvijua zaidi ili awe na taarifa kamili ya kuripoti kwa bosi wake mark moon.
Alianza kuwafuatilia vijana wale taratibu kwa nyuma hadi walipofika kwenye eneo moja la kichochoro palipojificha, wakamshusha chini yule kijana kisha wakaanza kumuhoji huku wakimpiga.
Brandina alisogea karibu yao zaidi kwa tahadhari kubwa akawa anasikiliza na kuona kila kinachoendelea.
Haukupita muda mara akaja mtu mwingine, alikuwa ni John mtoto wa madam Jane. Yeye ndiye aliyewaagiza vijana hao wamteke yule dereva bodaboda na kumuhoji ni kitu gani alileta kwa mama yake.
"Vipi ameongea" John alifika na kuuliza swali moja kwa moja.
"Ndiyo bosi ameongea" alijibu Abdullah, kijana wa John ambae ndie aliekuwa kiongozi wa wengine.
"Kasemaje?"
"Amesema yeye aliagizwa tu akakate tiketi mbili za kuingia kesho kwenye uwanja wa mkapa wakati wa mechi ya Yanga na Kagera Sugar, tiketi moja amepeleka kwa alie muagiza na nyingine ndio kamletea mama yako."
"Kaagizwa na nani?"
"Osman Azizi, yule jamaa muuza magari, unamfahamu hata ile gari yako ya mwisho ulinunua kwake"
"Sawa kuna kingine"
"Hamna bosi"
John alianza kuondoka huku akiwa bado anaonekana kutokuwa na furaha kabisa.
"Sasa bosi huyu jamaa tunamfanyaje?" aliuliza Abdullah.
"Mfungieni mpaka kesho kutwa ndio mmuachie" John alijibu kwa kifupi na kuondoka zake.
Brandina alisikia na kuona kila kilichoendelea nae aliondoka huku akipiga simu kwa mark moon akamueleza kila kitu.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Mark moon alikuwa bado yuko pale hospitali ndipo alipopokea taarifa hizo kutoka kwa Brandina, akamueleza kila kitu kuwa Madam Jane kaletewa tiketi ya kuingia uwanjani kwa mkapa na Osman Azizi siku ya kesho.
Mark moon aliipokea taarifa hizo na kutafakari kwa kina, mwisho akawa na jibu kamili.
"Hii yote ni kwa sababu ya code G, anataka kumtumia madam Jane, sijui hatua uliyofika Osman, ila ninauhakika nitakudhibiti tu" Mark Moon aliongea taratibu huku akiuma meno yake kwa hasira, hakuwa mtu wa ogomvi kabisa lakini ilionekana wazi kuwa Osman Azizi amemgusa pabaya.
"NAOMBA ITA VIJANA WOTE PAMOJA NA WALE MAJASUSI WETU NINAKAZI MUHIMU SIKU YA KESHO, PIA KATA TIKETI ZA KUWATOSHA KUINGIA KWENYE MECHI YA KESHO UWANJA WA BENJAMIN MKAPA"
Mark moon aliandika ujumbe huu kwa mtu wake wa kazi, akimtaka afanye maandalizi hayo haraka iwezekanavyo.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Caren na Yusto walikuwa hoi kitandani baada ya kufurahia penzi lao kwa zaidi ya saa moja na nusu, sasa walikuwa wamechoka mno, wakawa wanatazamana tu huku wakifanya mazungumzo ya hapa na pale wakiwa ndani ya shuka moja.
"Tumeongea sana Caren hebu twende basi kambini kwenu nikamuone mama yangu"
Alisema Yusto, ni kweli alikuwa amemkumbuka mno mama yake mlezi Zubeda.
"Aah sawa tutaenda lakini subiri kwanza bana tupumzike mi nimechoka sana, mama yuko salama yuko na Revo kule hakuna kitakacho haribika" alisema Caren na hapo akajikuta anakumbuka kuhusu maelezo aliyopewa na daktari wa saikolojia na akili yakimuhusu mpenzi wake Yusto, bosi wake madam Jane,na Zubeda mama mlezi wa Yusto.
Bado caren alikuwa na kigugumizi, hakujua wapi aanzie kumpa taarifa hizo Yusto kumweleza kuwa Madam Jane ndie mama yake mzazi.
"Yusto" Caren aliita
"Niambie mama"
"Kunakitu bado hujawahi kuniweka wazi mpenzi, kila nikitaka kukuuliza mambo yanaingiliana"
"Nini hicho Caren, hebu uliza"
"Kama nilivyokwambia mimi ni agent wa siri wa shirika fulani linalofanya kazi kwa oda maalum za kiserikali kwa siri, vipi kuhusu wewe, inakuwaje una siraha na unajua kuitumia"
Aliuliza Caren.
Yusto alibaki kimya kwa sekunde kadhaa, mwisho akageuka na kumtazama Caren usoni.
"Hunie, nitakuambia ukweli, mimi sio mwanafunzi hapa chuoni kama mnavyofikiri, mimi mlinzi tu, mlinzi wa siri pamoja na rafiki yangu Frank tunalinda usalama wa hiki chuo, tumeajiliwa moja kwa moja na mmiliki mark moon, tuna miaka miwili mpaka sasa" alieleza Yusto.
Ilikuwa ni taarifa iliyomshtua sana Caren, alijikuta akipigwa nakaubaridi ka hofu, kumbe wakati wote huo alikuwa na ukaribu na Yusto asijue kama ni mlinzi wa siri wa Mark Moon, yaani kwa tafsiri fupi alikuwa kwenye mahusiano na mpinzani wake kwani lengo kubwa la Caren kuwepo chuoni hapo ilikuwa ni kwa ajili ya kukiangusha chuo cha mark moon akiamini ni oda iliyotolewa na serikali kwa siri kupitia madam Jane, lakini haikuwa hivyo.
"Vipi mbona hivyo unaogopa?" Aliuliza Yusto baada ya kuona ni kama Caren amebadilika ghafula.
"Aah hapa niko sawa" alisema Caren,
Mara ujumbe mfupi wa maandishi ukaingia kwenye simu ndogo ya Yusto na simu ya Caren kwa pamoja.
Yusto na Caren wakatazama na kucheka, tukio hilo likionekana kuwafurahisha wote.
"Haya basi kila mtu asome meseji zake baby huenda ni taarifa muhimu" alisema Caren, akachukua simu ya Yusto na kumkabidhi kisha na yeye akachukua ya kwake, wote wakafungua zile meseji.
Yusto akawa wa kwanza kusoma.
"AISEE BOSS MARK MOON ANATUHITAJI WOTE SASA HIVI KULE UKUMBI WA MIKUTANO KUNA KAZI YA DHARULA MWAMBIE NA FRANK"
Ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa jasusi Simigo.
"CAREN, MADAM JANE ANAWAHITAJI WOTE KULE KAMBINI KUNA KAZI YA DHARULA IMEJITOKEZA" na hii ilikuwa ni meseji kutoka kwa Revocatus.
Caren na Yusto wakatazama usoni huku kila mmoja akionyesha kuwa na siri yake moyoni.
"Vipi kwema?" aliuliza Yusto
"Mmmh kwema, vipi wewe?"
"Ah fresh tu"
[emoji294][emoji294][emoji294]
Dakika 45 baadae tayari vikao vitatu katika sehemu tatu tofauti vilikuwa vikiendelea, na vyote vilikuwa vikilenga maandalizi ya siku ya kesho katika uwanja wa Benjamini mkapa.
Madam Jane na watu wake akiwemo Caren na Revo walikuwa wakijadili na kujipanga namna watakavyo mkabili Osman Azizi siku ya kesho kama tu mambo yatabadirika.
Osman Azizi nae na vijana wake walikuwa wakipanga mikakati jinsi ya kujilinda na kumkabili madam Jane na watu wake kama mambo yatabadilika kule uwanjani.
Na kikao cha mwisho kilikuwa cha mark moon na vijana wake wakiwemo Yusto, Frank na wale majasusi watatu yaani Brandina,Simigo na Mpili, wakawa wanapanga namna ya kumkabili Osman Azizi ambea anafuatilia kitu cha muhimu sana kutoka kwa bosi wao yaani Code G kupitia mke wa zamani wa mark moon, madam Jane.
Je, nini kitafuata?
ITAENDELEA...
USIACHE KUFUATILIA SIMULIZI YANGU MPYA
THE MODERN WAR-VITA YA KISASA.
MUHUMUHU JF
0756862047