Simulizi ya Watoto waliofanyiwa ukatili wa Kingono na baba yao mzazi, mmoja asema "NATAMANI BABA AFE"

Simulizi ya Watoto waliofanyiwa ukatili wa Kingono na baba yao mzazi, mmoja asema "NATAMANI BABA AFE"

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607

Bashiru Abdallah Mkazi wa Buswelu Jijini Mwanza anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuwafanyia ukatili wa kingono watoto wake wanne, ambao inadaiwa amekuwa akiwafanyia kwa miaka kadhaa sasa.

Mtuhumiwa alishikiliwa baada ya wananchi kutoa taarifa kwa Taasisi ya Nitetee (NITETEE FOUNDATION), ndipo Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Florah Lauo akafika katika makazi ya mtuhumiwa na kubaini juu ya ukatili huo.

Florah Lauo anasimulia ilivyokuwa tukio hilo la Mei 2022: “Tulipata taarifa kuwa kuna baba amejifungia na mwanaye kwenye chumba, tukafika tukiwa hatuelewi nini hasa ambacho kimetokea.

“Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa anaitwa Pascal akiwa na wananchi wengine na viongozi wenzake wakagonga mlango wakimtaka mtuhumiwa afungue, haikuwa hivyo, baadaye ikakubaliwa mlango uvunjwe, alivyosikia mazungumzo hayo ya kuvunja mlango mtuhumiwa akafungua.

“Alikutwa akiwa na binti yake ndani amejifungia pia alikuwa amemfungia mkewe na watoto wake wengine katika chumba kingine.

“Wakati nafika hapo nilikuwa na mtu mmoja wa usalama, tukamchukua Bashiru kumpeleka kituoni, nilimbeba katika gari yangu, tukiwa njiani nikamuuliza ‘kwa nini unatembea na wanao’ akanijibu ‘kwani mtu kula mali yake ni dhambi’, nilikasirishwa sana na jibu hilo.

“Tulipofika Polisi walimuweka ndani na mpaka sasa bado yupo ndani, Polisi wamenijulisha kuwa uchunguzi unaendelea.

“Watoto tuliwachukua na kuwapeleka hospitali kwa ajili ya vipimo, aliyeathirika zaidi ni mkubwa ambaye alisema alianza kuingiliwa kingono na baba yake huyo kuanzia akiwa na umri wa miaka nane. Wapo kwenye kituo chetu cha NITETEE FOUNDATION hapahapa Mwanza.

“Huyo mtoto mkubwa yupo kidato cha nne, alichukuliwa na baba yake kutoka kwa mama yake akiwa na umri wa miaka minne, anasema hamjui mama yake na hataki kurudi kwa baba yake.

“Huyo mtoto wa pili anayesoma darasa la sita anasema anatamani baba yake afe, watoto wengine wanasoma darasa la nne na la tatu.”

MTOTO WA KWANZA AZUNGUMZA
“Baba alikuwa ananiingilia nyuma na mbele, damu zilikuwa zikinitoka, akawa ananitishia na panga kuwa ataniua. Sikuwahi kumwambia mtu yeyote kwa kuwa nilikuwa naogopa, hata mama sikumwambia kwa kuwa nilihisi ataona namsingizia baba hivyo nataka kuwagombanisha.

“Pia nilianza kuona mdogo wangu wa pili anapigwa sana na baba, nikamuuliza huyo mdogo wangu akasema baba anataka mumuingilia lakini alikataa ndipo akaanza kumpiga.

“Nilipowauliza wote (wadogo zake) vizuri wakasema tayari baba ameshawaingilia wote kwa kuwalazimisha na alichokuwa akitaka ni kuendelea kufanya kitendo hicho.

“Nilipokuwa naumwa na kutoka damu akawa ananipa dawa ambazo sizijui, nilipokunywa nikawa napata usingizi mzito, nikiamka nakuta ameshaniingilia.

“Siku walipokuja kumkamata tulipokuwa tumejifungia kwenye kile chumba, baba alinishikia panga na kusema kuwa nikipiga kelele atanikata shingo.

“Natamani niendelee kusoma ili niwe Hakimu, lengo langu niwe natetea watoto wanaofanyiwa vitendo kama nilivyofanyiwa hivyo.

MTOTO WA PILI
“Baba alikuwa akiniingilia nyuma na mbele, alikuwa akifanya hivyo huku ananitishia panga. Nilipochoka nikamwambia mama, mama alipouliza alianza kupigwa na baba.

“Natamani ikiwezekana baba afe (analia). Ninachotaka kwa sasa ni kutorudi kwenye ile nyumba tena kwa kuwa majirani wameona alichonifanyia baba.”

KINACHOFUATA
Wakati suala hilo likiwa chini ya Polisi, Flora anaeleza kuwa mipango yake ni kuwahamisha shule watoto wote hao ili kuwa sawa kisaikolojia.

“Mmoja wao aliporejea shuleni wenzake walikuwa wameshajua kilichotokea wakaanza kumtania, hiyo ilimuondolea amani, akatamani kujiua. Sasa hicho ni kitu kibaya, tunafanya mpango kila mmoja ahamie katika shule mpya ili waendelee na masomo yao wakati tukisubiri utaratibu mwingine,” anasema Flora.



Source: NITETEE FOUNDATION
 
Bora Sheria za kiislam huyo angekuwa ameshaliwa kichwa haijalish zimo au zimepungua
 
Ni muda wa serikali kutekeleza ile adhabu ya kuhanithi kwa wanaume kama hawa
 
Alifungia mke wake chumba kingine. Na hawa wanawake wanapata shida sana
 
Dah aisee,kichwa kidogo kikisimama kikubwa hakifanyi kazi,familia ndio hivyo tena imevunjika mzee sio mtu mzuri kwenye jamii
 
Back
Top Bottom