Simulizi za Abunuasi...

Simulizi za Abunuasi...

Hekaya za Abunuasi..
Part 4.
Abunuasi Aliingia Kwa Kinyozi Na Mtoto,
Akasema Anyolewe Nywele Na Ndevu Alipomaliza
Akasema Na Mtoto Naye Anyolewe,
Wakati Mtoto Ananyolewa Yeye Akaaga Anaenda
Kumnunulia Mtoto Juisi,
Masaa 3 Yakapita Bila Abunuasi Kutokea Kinyozi
Akamwambia Dogo "Vipi Baba Ako Amekusahau?"
Mtoto"Yule Sio Baba Angu Alinikuta Njiani Akaniambia
Tuingie Hapa Tunyolewe Bure."

Kama ichi ni moja ya kizazi chake
 
Abunuasi alijenge nyumba
Lakini Kila mtu akipita anamwambia
Huu mlango ungekaa pale hii nyumba ingependeza
Abunuasi baada kuona nyumba yake Imejaa viraka akaamua
Kujenga nyumba nyingine hii pia jamaa wakaanza kutoa ushauri tena Abunuasi akasema nyumba ya marekebisho ile pale
 
Hekaya za Abunuasi..
Part 4.
Abunuasi Aliingia Kwa Kinyozi Na Mtoto,
Akasema Anyolewe Nywele Na Ndevu Alipomaliza
Akasema Na Mtoto Naye Anyolewe,
Wakati Mtoto Ananyolewa Yeye Akaaga Anaenda
Kumnunulia Mtoto Juisi,
Masaa 3 Yakapita Bila Abunuasi Kutokea Kinyozi
Akamwambia Dogo "Vipi Baba Ako Amekusahau?"
Mtoto"Yule Sio Baba Angu Alinikuta Njiani Akaniambia
Tuingie Hapa Tunyolewe Bure."
Hii nitaiapply, mkuu Senator jr upo wapi
 
Kuna wakati, Abunuwasi aliamua kuwa mfuga mbuzi. Alinunua mbuzi wa kufuga huku akiwa na lengo la kujiongezea kipato chake pindi mbuzi huyo atapoanza kuzaa, ili awafuge ndama wawe wengi na kumuwezesha kuwa tajiri kuliko wote waliokuwepo katika mji ule..

Siku moja Abunuwasi akipokuwa anampeleka mbuzi wake malishoni, alikuta kiatu kimoja kizuri sana katikati ya njia. Alisimama na kukiangalia. Kiatu kilipendeza machoni mwake ila akasema "kiatu hiki ni kizuri lakini mbona kipo kimoja tu?" Alitafuta kiatu cha pili pembezoni mwa njia ila hakukiona. Alipoona hawezi kuvaa kiatu kimoja, aliamua kukiacha palepale. .

Abunuasi akachukuwa mbuzi wake na mbele kidogo akaona kile kiatu cha mguu wa pili. Abunuwas alishangaa na akaona bora angelikichukua kile cha mwanzo kwa sababu cha pili kimepatikana.

Aliporudi pale mwanzo kukitafuta alichokiacha awali lakini hakukikuta tena, alijaribu kukitafuta lakini hakukiona. Basi akadhani kuna mtu amekiokota. Akarudi haraka alipomfunga mbuzi wake nako pia hakumkuta mbuzi wala kile kiatu kimoja. Mwisho akawa amemkosa mbuzi na viatu, Ndoto zote za Abunuwasi kupata utajiri zikaruka na akabaki na umasikini wake kwa sababu ya tamaa yake.
 
Hekaya za Abunuasi..
Part 4.
Abunuasi Aliingia Kwa Kinyozi Na Mtoto,
Akasema Anyolewe Nywele Na Ndevu Alipomaliza
Akasema Na Mtoto Naye Anyolewe,
Wakati Mtoto Ananyolewa Yeye Akaaga Anaenda
Kumnunulia Mtoto Juisi,
Masaa 3 Yakapita Bila Abunuasi Kutokea Kinyozi
Akamwambia Dogo "Vipi Baba Ako Amekusahau?"
Mtoto"Yule Sio Baba Angu Alinikuta Njiani Akaniambia
Tuingie Hapa Tunyolewe Bure."

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
ABUNUASI NA KISA CHA
PUNDA..jirani yake abunuasi alikua
anataka punda kwa ajil ya kusafirisha
mizigo yake,akamwendeaabunuasi
akamwabia jiran naomba niazimishe
punda wako,abunuas akamjibu mimi sina punda,jamaa akafadhaika sana
akawa anatoka lkn kabla ajakwenda
mbali akamsikia punda akilia toka kwa
abunuasi akarudi haraka akamwambia
abunuasi umesema huna punda lkn
nimeskia mlio wake,abunuasi akamjibu kwan unataka punda au
mlio?akimaanisha yeye ana mlio tuu
lkn hana punda..
 
siku moja Abunuas kamkodishia
muhindi moja vyumba kwenye ghorofa
yake ila yeye anakaa chin muhind
juu.sasa abunuas akataka kuuza ile
ghorofa muhind akakubal kununua juu
tu na hivyo abunuas kumfanya muhind anunue yote akaanza kumfanyia vituko
mara abomoe ngaz za kupandia
muhind akajenga zake,abunuas
akafanya vituko ving muhimd anunue
ghorofa ya chin ikashindikana
mwishowe akamwita muhind akamwambia nimewaita mafundi
wabomoe ghorofa yangu ya chin shika
yako ya juu usije ukasema
sikukwambia.muhind hoi kwa presha
 
Ile kali zaidi ya Abunuwasi ni pale
alipokuwa na shida na Sultani. Kufika
mlangoni kwa sultani wale mlinzi
akakataa kumruhusu aingie kumwona.
Abunuwasi akaomba sana aruhusiwe
kumwona Sultani maana alikuwa na shida kubwa. Mlinzii alijuwa kuwa
abunuwasi akiingia kwa sulatani
atapata anachotaka maana alipendwa
sana na sultani. Mkwara aliompa ni
kwamba aahidi kuwa atakachopata
kwa sultani wagawane nusu kwa nusu na mlinzi wa sultani, abunuwasi
akakubali na akaingia kwa sultani.
Kufika ndani sulatani anamuuliza sema
shida yako abunuwasi maaana leo
unaonyesha una huzuni. Abunawasi
akasema Seyidina wangu naomba unichape viboko mia, Sultani
akashangaa, kwa kosa gani?
Abunuwasi akasema nichape tu
Seyidina wangu na akasisitiza kuwa
haondoki mpaka achapwe. Sulatani
akaamura askari pale kwenye kiti cha enzi amtandike Abunuwasi taratibu
sana viboko mia. Walipomchapa
mpaka viboko hamsini Abunuwasi
akasema vimetosha maana mlinzi wa
pale getini tumekubaliana kuwa
nitakachopata humu ndani kwa sultani lazima na yeye apate nusu
 
Kulikuwa na sherehe
kubwa kwa mfalme na akaalika watu
kibao matajiri, kwenye eneo hilo
kulikuwa na maskini mmoja alikuwa
na njaa sana ila ndio hivyo hakualikwa
kwenye sherehe. Ndani alikuwa na kiporo chake cha wali akakichukua na
kukaa nje akisikilizia harufu ya msosi
toka kwa mfalme, akala kiporo chake
kwa kusindikizia ile harufu nzuri ya
chakula.
Alipomaliza akanywa maji akaenda kwa mfalme kumshukuru kwa kushiba!
mfalme alikasirika sana akamkwida
aeleze ni vipi amekula chakula chake
wakati hakualikwa, kesi ikapelekwa
barazani itolewe hukumu kesho yake.
maskini akaenda kwa abunuwasi kuomba msaada kwani alijua faini
atayopewa hatoweza kulipa,
abunuwasi akamwambia tulia kesho
tutaenda wote. asubuhi wakaenda,
maskini akaambiwa alipe faini,
abunuwasi akaenda mbele ya mfalme akamuuliza 'ulimualika maskini?'
akajibu hapana, sasa alikulaje chakula
chako? akamwambia amekula harufu.
abunuwasi kamjibu sawa, basi ngoja
nikupe faini yako.
Akatoa sarafu kadhaa mfukoni mwake akaziangusha chini zikazagaa kwa
kelele nyingi, zilipotulia akazichukua
na kuzirudisha mfukoni, kisha
akamwambia mfalme' kama maskini
alikula harufu akashiba, basi umelipwa
faini kwa mlio wa sarafu uridhike!'
 
Back
Top Bottom