Kulikuwa na sherehe
kubwa kwa mfalme na akaalika watu
kibao matajiri, kwenye eneo hilo
kulikuwa na maskini mmoja alikuwa
na njaa sana ila ndio hivyo hakualikwa
kwenye sherehe. Ndani alikuwa na kiporo chake cha wali akakichukua na
kukaa nje akisikilizia harufu ya msosi
toka kwa mfalme, akala kiporo chake
kwa kusindikizia ile harufu nzuri ya
chakula.
Alipomaliza akanywa maji akaenda kwa mfalme kumshukuru kwa kushiba!
mfalme alikasirika sana akamkwida
aeleze ni vipi amekula chakula chake
wakati hakualikwa, kesi ikapelekwa
barazani itolewe hukumu kesho yake.
maskini akaenda kwa abunuwasi kuomba msaada kwani alijua faini
atayopewa hatoweza kulipa,
abunuwasi akamwambia tulia kesho
tutaenda wote. asubuhi wakaenda,
maskini akaambiwa alipe faini,
abunuwasi akaenda mbele ya mfalme akamuuliza 'ulimualika maskini?'
akajibu hapana, sasa alikulaje chakula
chako? akamwambia amekula harufu.
abunuwasi kamjibu sawa, basi ngoja
nikupe faini yako.
Akatoa sarafu kadhaa mfukoni mwake akaziangusha chini zikazagaa kwa
kelele nyingi, zilipotulia akazichukua
na kuzirudisha mfukoni, kisha
akamwambia mfalme' kama maskini
alikula harufu akashiba, basi umelipwa
faini kwa mlio wa sarafu uridhike!'