Simulizi za Abunuasi...

abunuwas nyumba yake
iliungua moto,akifikiria atafanyaje na
yale majivu ya nyumba yake akapata jibu,akayapakia magunia kibao ya
majivu kwenye punda akafanya safari
ya kwenda nchi ya mbali, kufika kule
alikuwa na gunia moja lililokuwa na
sugari.Akatangazia mji ule kuwa
amekuja na biashara ya sukari nzuri sana...wakuu wa mji ule wakapikiwa
chai yenye sukari wakaipenda
sana.Abunuwas akafanya biashara
nzuri ya kuuza na yale magunia yote
ya majivu nakurejea kijiji kwake
akiwa na ukwasi mkubwa wa fedha.... Wanakijiji wakajiuliza huyu bwana
imekuwaje kaondoka na yale majivu
ya nyumba yake iliyoungua na kurejea
na mihela mingi?!...wakajiongeza
wenyewe kwa kuchoma majumba yao
na miti ili wapate majivu mengi kwenda kufanya biashara alipotokea
Abunuwasi...
kilichotokea huko nitamalizia baadae!
 
Hiyo nakumbuka kwelii
 
Kipo kisa kimoja ambapo bwana mmoja aliota ndoto amemtaliki mkewe,akaenda kwa kadhi na kumsimulia juu ya ndoto yake,yule kadhi akamwambia yule bwana ni sharti amuache mkewe. Yule bwana akamuacha mkewe,baada ya siku si nyingi yule kadhi alimuoa yule mwanamke,yule bwana alisononela sana kwa kua bado alikuwa anampenda mkewe. Hivyo akamueleza kisa chote Abunuwasa,alichokifanya Abunuwasa alikodi watu na kwenda kwenye nyumba ya yule kadhi na kuwaambia wale watu aliowakodi waanze kuvunja ile nyumba. Kazi ya kuvunja ile nyumba ilianza,kadhi na watu walipohoji ni kwa nini Abunuwasa anafanya hivyo,akasema ameota kwamba baba yake alimuwachia hazina ya mali na imchimbiwa sehemu ilipo nyumba ya kadhi,watu walipohoji tangu lini ndoto ikawa kweli? Abunuwasi akawajibu tangu huyu bwana alipoota kuwa amemwacha mkewe na kadhi akasisitiza huyu bwana shurti amuache mkewe,hapo ndipo ndoto inakuwa kweli
 
Raha sana hii kitu weka mbali na watoto
 
Aisee ubungo kuna wale wanaouza magazeti na vitabu vya udaku udaku pale terminal akanionesha kitabu cha hekaya za abunuwasi kukichk hakina hata hadithi nyingi nahisi kuna wajanja wanafanya collection humu na kwa watu wengine na kufyatua vitabu wakati og chenyewe kimesheheni mastory nakumbuka mzee lilikuwa anayukataza kusoma kile kitabu nikamvizia siku nikakiiba sasa wqkati nipo kwenye harakati za kusoma jamaa aliniazma da! Hadi Leo wapi naweza pata og version
 
Mkuu napataje hiki kitabu nilisomaga sikumaliza stori zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…