Simulizi za Abunuasi...

Simulizi za Abunuasi...

abunuwas nyumba yake
iliungua moto,akifikiria atafanyaje na
yale majivu ya nyumba yake akapata jibu,akayapakia magunia kibao ya
majivu kwenye punda akafanya safari
ya kwenda nchi ya mbali, kufika kule
alikuwa na gunia moja lililokuwa na
sugari.Akatangazia mji ule kuwa
amekuja na biashara ya sukari nzuri sana...wakuu wa mji ule wakapikiwa
chai yenye sukari wakaipenda
sana.Abunuwas akafanya biashara
nzuri ya kuuza na yale magunia yote
ya majivu nakurejea kijiji kwake
akiwa na ukwasi mkubwa wa fedha.... Wanakijiji wakajiuliza huyu bwana
imekuwaje kaondoka na yale majivu
ya nyumba yake iliyoungua na kurejea
na mihela mingi?!...wakajiongeza
wenyewe kwa kuchoma majumba yao
na miti ili wapate majivu mengi kwenda kufanya biashara alipotokea
Abunuwasi...
kilichotokea huko nitamalizia baadae!
 
Ile kali zaidi ya Abunuwasi ni pale
alipokuwa na shida na Sultani. Kufika
mlangoni kwa sultani wale mlinzi
akakataa kumruhusu aingie kumwona.
Abunuwasi akaomba sana aruhusiwe
kumwona Sultani maana alikuwa na shida kubwa. Mlinzii alijuwa kuwa
abunuwasi akiingia kwa sulatani
atapata anachotaka maana alipendwa
sana na sultani. Mkwara aliompa ni
kwamba aahidi kuwa atakachopata
kwa sultani wagawane nusu kwa nusu na mlinzi wa sultani, abunuwasi
akakubali na akaingia kwa sultani.
Kufika ndani sulatani anamuuliza sema
shida yako abunuwasi maaana leo
unaonyesha una huzuni. Abunawasi
akasema Seyidina wangu naomba unichape viboko mia, Sultani
akashangaa, kwa kosa gani?
Abunuwasi akasema nichape tu
Seyidina wangu na akasisitiza kuwa
haondoki mpaka achapwe. Sulatani
akaamura askari pale kwenye kiti cha enzi amtandike Abunuwasi taratibu
sana viboko mia. Walipomchapa
mpaka viboko hamsini Abunuwasi
akasema vimetosha maana mlinzi wa
pale getini tumekubaliana kuwa
nitakachopata humu ndani kwa sultani lazima na yeye apate nusu
Hiyo nakumbuka kwelii
 
Kipo kisa kimoja ambapo bwana mmoja aliota ndoto amemtaliki mkewe,akaenda kwa kadhi na kumsimulia juu ya ndoto yake,yule kadhi akamwambia yule bwana ni sharti amuache mkewe. Yule bwana akamuacha mkewe,baada ya siku si nyingi yule kadhi alimuoa yule mwanamke,yule bwana alisononela sana kwa kua bado alikuwa anampenda mkewe. Hivyo akamueleza kisa chote Abunuwasa,alichokifanya Abunuwasa alikodi watu na kwenda kwenye nyumba ya yule kadhi na kuwaambia wale watu aliowakodi waanze kuvunja ile nyumba. Kazi ya kuvunja ile nyumba ilianza,kadhi na watu walipohoji ni kwa nini Abunuwasa anafanya hivyo,akasema ameota kwamba baba yake alimuwachia hazina ya mali na imchimbiwa sehemu ilipo nyumba ya kadhi,watu walipohoji tangu lini ndoto ikawa kweli? Abunuwasi akawajibu tangu huyu bwana alipoota kuwa amemwacha mkewe na kadhi akasisitiza huyu bwana shurti amuache mkewe,hapo ndipo ndoto inakuwa kweli
 
Kufwendaaaaa...
Wakuu ni muda wetu na wakati wa kuandaa nyoyo zetu juu ya vichekesho ndani ya Maisha ya Abunuasi kuwa karibu na thred hii.

HEKAYA ZA ABUNUASI.
Part one 1.
Abunuasi Alinunua Punda Ila Hakuwa Na Sufuria Kubwa La
Kumnyweshea Maji Ikabidi Aende Kuazima Kwa Jirani Na
Akapewa Baada Ya Siku 3 Akalirudisha Kwa Mwenyewe
Huku Akiwa Ameweka Sufuria Nyingine Ndogo Ndani
Yake,
Abunuasi Akamwambia Yule Jirani Wakati Anaichukua Ile
Sufuria Ilikuwa Na Mimba Kwahiyo Imezaa Yule Jirani
Akashangaa Na Kufurahi Kusikia Sufuria Imezaa,
Siku Nyingine Abunuasi Akaenda Kuazima Yule Jirani
Akampa Akijua Itarudi Imezaa Lakini Siku Nyingi Zikapita
Bila Sufuria Kurudishwa Ndipo Alipoamua Kumfata
Abunuasi Akamwambia "Samahani Jirani Ile Sufuria
Imefariki Wakati Inajifungua."
Jirani "Haiwezekani Sufuria Haiwezi Kufa."
Abunuasi "Kila Kinachozaa Pia Hufa."
Yule Jirani Alirudi Kwake Bila Sufuria...

Hope of Jf
Cc
Senator jr
Raha sana hii kitu weka mbali na watoto
 
Aisee ubungo kuna wale wanaouza magazeti na vitabu vya udaku udaku pale terminal akanionesha kitabu cha hekaya za abunuwasi kukichk hakina hata hadithi nyingi nahisi kuna wajanja wanafanya collection humu na kwa watu wengine na kufyatua vitabu wakati og chenyewe kimesheheni mastory nakumbuka mzee lilikuwa anayukataza kusoma kile kitabu nikamvizia siku nikakiiba sasa wqkati nipo kwenye harakati za kusoma jamaa aliniazma da! Hadi Leo wapi naweza pata og version
 
Kulikuwa na sherehe
kubwa kwa mfalme na akaalika watu
kibao matajiri, kwenye eneo hilo
kulikuwa na maskini mmoja alikuwa
na njaa sana ila ndio hivyo hakualikwa
kwenye sherehe. Ndani alikuwa na kiporo chake cha wali akakichukua na
kukaa nje akisikilizia harufu ya msosi
toka kwa mfalme, akala kiporo chake
kwa kusindikizia ile harufu nzuri ya
chakula.
Alipomaliza akanywa maji akaenda kwa mfalme kumshukuru kwa kushiba!
mfalme alikasirika sana akamkwida
aeleze ni vipi amekula chakula chake
wakati hakualikwa, kesi ikapelekwa
barazani itolewe hukumu kesho yake.
maskini akaenda kwa abunuwasi kuomba msaada kwani alijua faini
atayopewa hatoweza kulipa,
abunuwasi akamwambia tulia kesho
tutaenda wote. asubuhi wakaenda,
maskini akaambiwa alipe faini,
abunuwasi akaenda mbele ya mfalme akamuuliza 'ulimualika maskini?'
akajibu hapana, sasa alikulaje chakula
chako? akamwambia amekula harufu.
abunuwasi kamjibu sawa, basi ngoja
nikupe faini yako.
Akatoa sarafu kadhaa mfukoni mwake akaziangusha chini zikazagaa kwa
kelele nyingi, zilipotulia akazichukua
na kuzirudisha mfukoni, kisha
akamwambia mfalme' kama maskini
alikula harufu akashiba, basi umelipwa
faini kwa mlio wa sarafu uridhike!'
Mkuu napataje hiki kitabu nilisomaga sikumaliza stori zote
 
Back
Top Bottom