Simuungi tena mkono Rais Samia kwa haya yanayoendelea na kadhia ya Mafuta

Simuungi tena mkono Rais Samia kwa haya yanayoendelea na kadhia ya Mafuta

Nitaendelea kumuunga mkono mh Rais wetu mpendwa siku zote.Nitakuwa upande wake,nitasimama naye popote alipo na kumtetea popote niwapo, nitasema kwa nguvu zangu zote mazuri yote anayoendelea kuyafanya katika Taifa letu.kila mtu anatambua dhamira njema aliyonayo mh Rais katika Taifa letu. Sote tumeona kazi kubwa aliyoifanya katika secta ya Elimu, Afya, miundombinu,kilimo n.k. Tumeona shule zilijengwa kila eneo,tumeona vyumba vya madarasa zaidi ya elfu 20 vikijengwa,tumeona Elimu ikitolewa bure hadi kidato cha sita,tumeona vituo vya afya vikijengwa kila kona ya Taifa letu.Tumeona leo hii miradi mbalimbali ya maendeleo ikichipua kila sehemu .kwa hakika nitaendelea kuwa pamoja na Rais samia na serikali yake mpaka mwisho.
Nakuchukia we jamaa kuliko hata hao mabwana zako unaowatetea na kama siku kikija kunuka we jamaa kitakachokukuta hautaamini
 
Back
Top Bottom