Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Anaenda kukaa mtaani akiwa relax.Jikaze tu, sasa unaacha unaenda wapi.
Umempa ushauri mzuri sana huu, napitia njia hiyo hiyo pia baada ya shule nitaangalia nini cha kufanya. Kuacha kazi sio njia sahihi kwasababu hizi kazi wakati mwingine hazikupi pesa na maisha unayoyataka lakini unaweza zitumia kama channel ya kupata fursa zingine nzuri zaidi ndani ama nje ya nchi na ndoto zako zikatimia.Pole sana. Hayo ni matokeo ya kufanya uamuzi wa kuacha kazi sehemu na kuchukua kazi mpya bila ya kufanya uchunguzi wa kutosha wa huko unakoenda. Nina uhakika kabisa kama ungefanya uchunguzi zaidi, kwa mfano kwa kuongea na watu kadhaa ambao wako huko TAMISEMI nafasi kama yako, usingefanya uamuzi huo. Kosa hili likufanye ujifunze next time kabla ya kuchukua uamuzi mkubwa kama huu, usiurupuke bali ufanye utafiti wa kutosha.
Kosa limeshafanyika, je nini cha kufanya sasa?
Geuza kosa hilo kuwa ngazi yako: Kaa tafakari kwa umakini mkubwa bila hisia (ondoa kwanza hisia hasi kabla hujatafakari), je nafasi hiyo pamoja na negativity zake, ukiji position kinamna fulani haiwezi kukusukuma mbele zaidi? How? Nitakupa mfano: Kuna nafasi za scholarship za masomo kwenda nje ambazo watumishi wa Serikali ndio huwa wanapewa vipaumbele zaidi. Kama moja ya malengo yako yamekuwa ni kujiendeleza kielimu, unaweza kutumia nafasi hiyo kupata scholarship ya aina hiyo, ukaenda kupiga shule, angalau ukatimiza lengo lako; kisha ukirudi utaangalia cha kufanya kulingana na mazingira yatakavyokuwa. Pia, unaweza kutumia nafasi hiyo kuomba scholarship za nje kama vile Chevening, Commonwealth, nk. Utakuwa na points zaidi za kupata kwa sababu ni rahisi kujinadi kwamba unatumikia wananchi at the grassroot, na unaleta impact nzuri katika huduma za jamii. Hivyo, ukiwa mzuri na mjanja kuandika na kujieleza, inakupa nafasi zaidi ya kuweza kupata kuliko aliye katika private sector.
Mfano katika hili, kuna jamaa yangu alisoma Computer Science, alipomaliza alipata kazi PWC, kisha akakaa kama miaka miwili hivi, akapata kazi bank fulani kubwa ya binafsi nchini; baada ya kama miaka mitatu, nkashangaa jamaa kahamia TANESCO....! Nilishtuka sana, na nikamuuliza kaka vipi, mbona kama unapotea njia? Akaniambia, tulia, nina mpango wangu, utakuja kuelewa baadaye kidogo. After two years, jamaa akapata scholarship fulani hivi ya kupiga masters UK, chuo kimoja maarufu sana duniani. Guess what? Sasa hivi jamaa yuko zake World Bank, Washington DC, USA anapiga kazi. Nilikuja kuongea naye juzi kati, akaniambia kuwa ile kazi yake ya TANESCO, japokuwa mazingira ya kazi yalikuwa mabovu sana, na mshahara sio kivile, ndiyo ilimsaidia sana kupata ile scholarship yake ya UK, ambayo eventually ikamfanya apate kazi World Bank baada ya kumaliza shule. There is no way angeweza kupata ile scholarship akiwa mfanyakazi wa private bank.
Njia ya pili, unaweza kutumia pia nafasi hiyo kukua zaidi, labda baada ya mwaka mmoja au miwili ukajikita katika kupata ujuzi au uzoefu fulani, kisha uombe kazi katika mashirika makubwa ya Kimataifa na ya Kitaifa. Kuna mashirika ukiwa umefanya kazi TAMISEMI na unajua kudeal na government systems, hasa TAMISEMI na wizara zingine za kisekta, unakuwa na advantage sana kupata kazi huko kwa sababu wanatafuta sana watu ambao wanaijua vizuri mifumo na taratibu za serikali, maana wao kazi zao zinategemea sana kukubalika na kupenetrate mifumo ya kiserikali; na kuendelea kwao kufanya kazi nchini na kupata fedha na miradi zaidi kunategemea hilo kwa asilimia kubwa.
Watu wanajiongelesha tu huku tamisemi ni zaidi ya kutupwa kwenye maandaki, una pesa hakuna lakini hupati mbususu za kuchakata una hu ya kitimoto lakini hakuna, wanawake wanasura za babu zao kutwa wapo bize na ulanzi tu dah hatari sana.Hukujui huku local gvt weweeee
Waswahili wanasema....acha kazi ....uone kazi .....kupata kaziMkuu husijaribu kuacha kazi wenzio hatuna kazi tunatamani hadi uko uliko
Sio koteeee kwingine wanakula maisha sanaNilishawahi kusema watu serikalini wanapenda kuingia kwa sababu ya ulimbukeni tu na wakiingia tu kinachofuata ni majuto na kufa moyo.
1. Mazingira magumu
2. Marupurupu hakuna
3. Mishahara MIDOGO
4. Exposure zero
5. Connection zero
Kufanya kazi TAMISEMI Nchi hizi za ulimwengu wa tatu ni ishara ya Umaskini tosha.
Huko tamisemi ndio sehemu ilihaa miungu watu, mfanyakazi wa tamisemi huna thamani, kianzia balozi ni boss wako, mwwnyekiti wa kitongoji ni boss wako, mwenyekiti wa kijiji ni boss, mtendaji wa kijiji ni boss, mtendaji wa kata ni boss, mwalimu mkuu ni boss, diwani ni boss, mbunge ni boss, katibu afya ni boss, DMO ni boss, RMO ni boss, bado wa huko wizarani asee....Pole sana jamaa kazi za serikali jau jana sana kila mtu mjuaji plus uchawa kuchukiwa bila sababu.
🤓Mwanzo Mgumu, Badilika Geuza changamoto zako ziwe fursa. alafu achana na motivational speakers kuhusu kutajirika kazini (Mapema) na fikiria zaidi kuisaidia jamii yako.
View attachment 2933161