Pole sana. Hayo ni matokeo ya kufanya uamuzi wa kuacha kazi sehemu na kuchukua kazi mpya bila ya kufanya uchunguzi wa kutosha wa huko unakoenda. Nina uhakika kabisa kama ungefanya uchunguzi zaidi, kwa mfano kwa kuongea na watu kadhaa ambao wako huko TAMISEMI nafasi kama yako, usingefanya uamuzi huo. Kosa hili likufanye ujifunze next time kabla ya kuchukua uamuzi mkubwa kama huu, usiurupuke bali ufanye utafiti wa kutosha.
Kosa limeshafanyika, je nini cha kufanya sasa?
Geuza kosa hilo kuwa ngazi yako: Kaa tafakari kwa umakini mkubwa bila hisia (ondoa kwanza hisia hasi kabla hujatafakari), je nafasi hiyo pamoja na negativity zake, ukiji position kinamna fulani haiwezi kukusukuma mbele zaidi? How? Nitakupa mfano: Kuna nafasi za scholarship za masomo kwenda nje ambazo watumishi wa Serikali ndio huwa wanapewa vipaumbele zaidi. Kama moja ya malengo yako yamekuwa ni kujiendeleza kielimu, unaweza kutumia nafasi hiyo kupata scholarship ya aina hiyo, ukaenda kupiga shule, angalau ukatimiza lengo lako; kisha ukirudi utaangalia cha kufanya kulingana na mazingira yatakavyokuwa. Pia, unaweza kutumia nafasi hiyo kuomba scholarship za nje kama vile Chevening, Commonwealth, nk. Utakuwa na points zaidi za kupata kwa sababu ni rahisi kujinadi kwamba unatumikia wananchi at the grassroot, na unaleta impact nzuri katika huduma za jamii. Hivyo, ukiwa mzuri na mjanja kuandika na kujieleza, inakupa nafasi zaidi ya kuweza kupata kuliko aliye katika private sector.
Mfano katika hili, kuna jamaa yangu alisoma Computer Science, alipomaliza alipata kazi PWC, kisha akakaa kama miaka miwili hivi, akapata kazi bank fulani kubwa ya binafsi nchini; baada ya kama miaka mitatu, nkashangaa jamaa kahamia TANESCO....! Nilishtuka sana, na nikamuuliza kaka vipi, mbona kama unapotea njia? Akaniambia, tulia, nina mpango wangu, utakuja kuelewa baadaye kidogo. After two years, jamaa akapata scholarship fulani hivi ya kupiga masters UK, chuo kimoja maarufu sana duniani. Guess what? Sasa hivi jamaa yuko zake World Bank, Washington DC, USA anapiga kazi. Nilikuja kuongea naye juzi kati, akaniambia kuwa ile kazi yake ya TANESCO, japokuwa mazingira ya kazi yalikuwa mabovu sana, na mshahara sio kivile, ndiyo ilimsaidia sana kupata ile scholarship yake ya UK, ambayo eventually ikamfanya apate kazi World Bank baada ya kumaliza shule. There is no way angeweza kupata ile scholarship akiwa mfanyakazi wa private bank.
Njia ya pili, unaweza kutumia pia nafasi hiyo kukua zaidi, labda baada ya mwaka mmoja au miwili ukajikita katika kupata ujuzi au uzoefu fulani, kisha uombe kazi katika mashirika makubwa ya Kimataifa na ya Kitaifa. Kuna mashirika ukiwa umefanya kazi TAMISEMI na unajua kudeal na government systems, hasa TAMISEMI na wizara zingine za kisekta, unakuwa na advantage sana kupata kazi huko kwa sababu wanatafuta sana watu ambao wanaijua vizuri mifumo na taratibu za serikali, maana wao kazi zao zinategemea sana kukubalika na kupenetrate mifumo ya kiserikali; na kuendelea kwao kufanya kazi nchini na kupata fedha na miradi zaidi kunategemea hilo kwa asilimia kubwa.