Sina hamu kabisa ya kuoa na umri unazidi kwenda

Sina hamu kabisa ya kuoa na umri unazidi kwenda

mwanyaluke

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2015
Posts
704
Reaction score
2,435
Mwisho wa mwaka huu, nitakuwa na miaka 35, umri wa uzee, kinachonichanganya sihisi wito kabisa wa kuoa na kuishi na mwanamke, huko nyuma atleast nilikuwa na hiyo hali ya kutamani kuishi na mwanamke kiasi kwamba niliifanikiwa kupata watoto wawili kwa mwanamke mmoja, na nilitoa hadi mahari

Cha ajabu hamu ya kuishi na mwanamke inazidi kupotea huku umri unaenda, na kinachonitisha ni mwili kukata hamu kabisa kwa wanawake, hivi nandika hapa nina miezi miwili sijui uchi wa mwanamke, ratiba yangu imekuwa ni hivi asubuhi nakwenda shule, mchana nikitoka naenda kwenye biashara zangu au mashambani kwangu kuhudumia mimea na mifugo, najikuta tayari ni usiku nikirudi kwangu ni kulala tu

Sikumbuki kuhusu wanawake kabisa, huko nyuma afadhali kila juma tatu nilikuwa nazifumua mbususu lakini saizi hamna hiyo, hata tu kutongoza siwezi, hata hamu mama kwa mama watoto imepotea kabisa , nilipanga niishi naye kuanzia mwaka huu, ila naona akili haisemi chochote, ninachowaza ni pesa pesa basi

Niliamini sana huko nyuma pesa ikiongezeka na shughuli zikiwa kubwa ntaishi na family kwa furaha, yes pesa kibongo bongo ipo kiasi chake yaani zile ndoto za kuwa mtanzania nimetimiza (nyumba, gari n miradi flani ninayo tayar🙂 ada ya wanangu nalipa na take care kwa kumpatia mama yao pesa ya matumizi kila mwezi, mahali nilitoa, shida ni kuishi na mwanamke tu

Nawaza kazi zangu tu, kinachonitesa sana ni wanangu kuwa siishi nao (ni kitu ambacho kinaniumiza sana) imefika wakati naweza toka shule ninapofundisha na kwenda kuwasalimia na huwa natoa hadi machozi nikifikiri why siishi nao, ila linapokuja suala la kuishi na mama yao inaKuwa mtihani, msaada wenu napokea ushauri , napokea pia matusi na kejeli, i'm old enough na maisha ya mtandaoni nayafahamu
 
Nilichogundua mimi. Mwanaume unapozidi kuchelewa kuoa ndipo hamu ya kuoa inazidi kupungua..

Unajua baada ya 35 yrs kwa mwanaume hamu ya tendo na sperm quality inapungua.

Sasa hii ikikukuta bado hujaoa... ndipo unazidi kusita kuoa.. japo uhalisia umri huu unamuhitaji sana mwanamke kama partner
 
Pole mkuu, kama unavoishi ni umepata amani ya moyo na faraja basi ishi tu

Cha msingi uwapatie matunzo wanao na mama yao.
 
Nilichogundua mimi . Mwanaume unapozidi kuchelewa kuoa ndipo hamu ya kuoa inazidi kupungua..

Unajua baada ya 35 yrs kwa mwanaume hamu ya tendo na sperm quality inapungua.

Sasa hii ikikukuta bado hujaoa... ndipo unazidi kusita kuoa.. japo uhalisia umri huu unamuhitaji sana mwanamke kama partner
Ni kweli mzee, akili inawaza pesa pesa tu, kazi zangu tu, najiona sipo kawaida aisee, hata yale maisha yangu ya kila jumatatu lazima nipite bar ninywe, nifurahi na marafiki naona hiyo hali imeisha , sijawhi kujikuta bar au kwenye ukumbi wa mpira zaiadi ya sambili usiku
 
Sio kweli mwanaume hazeeki labda kama hazingatii chakula.

Back
Top Bottom