Sina hamu kabisa ya kuoa na umri unazidi kwenda

Nimewaza tu,vipi kama kuna chemistry mmeshindwa kuijenga na mkeo/mzazi mwenzako?na huo mwanya unaukimbia na kwenda kujificha kwenye 'kichaka' cha kutafuta pesa?
Ni kweli kabisa unaambiwa kila mtu ni mvivu katika Jambo flani,huyu jamaa ni mvivu ktk kuishi na mwenza kwahiyo anatafuta sababu ktk kutafuta pesa,huo ndio ukweli, wangapi wanatafuta pesa na wanaishi na wenza wao, jitafakari Mzee unafeli Sana, unapoteza mapenzi na wanao.
 
Zama zetu hizi kuoa ni kujitafutia matatizo ya kujitakia

Tafuta naman ya kusuuza moyo na mwili. fanya kazi zako ndoa acha nayo........
 
Kutokufanya miezi miwili tu ndo unatuandikia "huwez amini?😳"watu wanafunga miaka tu
 
Hofu tu mkuu unayo.Tupo wengi wenye 35 na kuendelea but hatuna wasiwasi.Hata hivyo zama hizi kupata na kuishi na hawa wenzetu imekuwa ni changamoto sn.

Ukiwa kwenye ndoa miaka hii ni hatariiii sn,kwani kuua ama kufa wewe ni possible sn
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]we jamaa bhn
 
Umeoungukiwa nguvu za kiume ni kawaida ila bora umekubali kutooa maana mke angekutangaza kwa mwanaume anayelala nae kuwa humgongi kabisa na ingekuwa fedhea
 
Kuja mambo mengi

1.Una trauma ambayo hutaki ku admit una historia mbaya na wanawake au mwanamke uliyezaa nae ni km hatoshi kuwa mkeo au una soma taarifa mbaya mbaya kuhusu mahusiano.

2.Una jini mahaba
Mke wangu ameshawahi kuwa na jini mahaba ni balaa sana ni vile tu mimi nina nguvu ya asili kwenye ulimwengu wa roho ila hilo nalo lipo na limewapoteza wengi

3.Wewe unapenda space flani hivi privacy
Binafsi wakati sijaoa nilikuwa na hofu moja kubwa,nitawezaje kukaa na mtu ndani mda mrefu maana mimi nilivyo siwezi kukaa na yeyote yule mda mrefu bila kujitenga mwenyewe kwa mda.Sasa nikawa nawaza itakuwaje hii tabia yangu ya kupenda kukaa mwenyewe tena nyumbani!!!Huwezi amini nilikuwa Nina kila kitu na uwezo wa kuishi na mke ila hofu yangu ilikuwa privacy,itakuwaje nitawezaje??nilivyotoa mali nilikaa na mke wangu chini nikamwambia pamoja na wewe kuniona mi ni charming,social ila siwezi kukaa na mtu mda mrefu hivyo nikikuoa ukiona nipo chumbani mwenyewe au nipo nje na kiti mwenyewe ujue kabisa ndo nilivyo na sijabadilika.

Nikaoa!!!cha ajabu nikajikuta tena siwezi kukaa mbali na mke wangu mda mrefu na hata nikiwa kimya ila nataka yeye awe pembeni tu na ukimya huo huo.

Kuna vitu unaweza kuhisi huviwezi ila ni kwasababu haujawahi jaribu,ukijaribu ni vyepesi sana.

Mke ana raha yake hasa km hukukurupuka kwenye kuoa siku hizi wanaume hatujui kuchagua wanawake tupo busy sana na kuwaza ngono tuna miss wanawake wazuri wa kufanya nao maisha.Utakuwa binti wa Miaka 33 unamuona kabisa mbona huyu binti hana shida ila mume hana sasa hao tunaowaoa sasa[emoji23][emoji23][emoji23]mmmmh
 
Nachoweza kukushauri ni tafuta msaada wa kiroho, kwa dini yako. Tafuta watu wa kiroho na wakusaidie kwenye dua na maombi. Kidunia hali yako inaweza chukuliwa poa tu na ni kawaida, lakini usijidanganyie hapo, siyo kawaida kuishi hivyo. Zingatia hili, mtafute Mungu sana. Sema naye na fungua roho yako kwake. Kupoteza hamu kama hivyo uanzaga taratibu na uendelea hata kwenye maswala mengine, vitu, kazi, watu, hisia yani taratibu utajikuta hamu ya kuishi nayo huna, inaweza kuwa tatizo liko akilini...lakini bado msaada wa haraka hapo ni Mungu maana sidhani kama kibongo bongo unaweza pata cancelling itakayokufaa. Sijui kama tuna wataalamu wa pyschology. Kama wapo basi unaweza pia waona. Hili si jambo la kuzoea ama kupuuza....maisha matamu wewe, ukipoteza hamu sa utafanyaje? Tumeumbwa tuishi....mengineyo anajua muumba.
 
Kaombewe wewe sio mzima
 
I'm in love with this comment [emoji120]
 
Chukua mke wako na watoto wako walete nyumbani kwako, imarisha eneo lako la kiroho, nikiwa nina maana rejesha uhusiano wako na Mungu.
 
Hofu tu mkuu unayo.Tupo wengi wenye 35 na kuendelea but hatuna wasiwasi.Hata hivyo zama hizi kupata na kuishi na hawa wenzetu imekuwa ni changamoto sn.

Ukiwa kwenye ndoa miaka hii ni hatariiii sn,kwani kuua ama kufa wewe ni possible sn
Aiseee vijana mmekata tamaa sana, sijui tatizo nini

Serikali iweke kipengele kwenye Katiba cha kulazimisha vijana waoe.
 
Dalili za mwanamke mwenye jini mahaba ni zipi ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…