Kwanza, hali hii hutokea na si kitu cha ajabu.
Tunapaswa kujua kuwa mtu ni roho iliyouvaa mwili. Lakini pia mtu anamoyo ambalo ndimo mawazo na hisia na maamuzi hufanyika. Roho zetu huwa kuna kipindi huona kitu na tunapatwa na mabadiliko fulani bila kujua yamekuja vipi, mfano mtu anasema nilichezwa na machale, si kweli kwamba ni machale ila ni namna ambazo roho zetu hupokea taarifa kutoka kwa Mungu wetu kwamba kuna jambo fulani halipo sawa sawa ama kuna shida mahali.
Ukiweza itambua njia na taarifa za rohoni husaidia sana maana hutokana na Manufacturer wetu (Mungu), kututaarifu juu ya mambo ya maisha yetu.
Jambo hili lililokutoea, limemtokea Kaka yangu mwaka 2002. Alikua ametoa mahari, na wameanza kuandaa harusi. Ila ilikuja ghafla tu, akamchukia Mchumba wake, na akasema hawezi kumuoa kwa jinsi alivyomchukia. Binti hakuwa na kasoro yoyote, hakufanya jambo lolote baya, na alikua mlokole huyo binti. Ikabidi Kaka aende kwa mchungaji wake na akamwambia hata mahari yangu sitaki kuichukua ila nakuomba uongee na binti mahusiano yaishe. Na kweli yote yalifanyika.
Mwaka 2003, akapata mke akaoa, hapakuwa na shida. Mpaka leo 2021 wako pamoja, katika mazungumzo yangu na yeye anasema changamoto alizopitia kwenye maisha tangu aoe, yule Mchumba wa kwanza asingeziweza, na njia anayopita ni njia ngumu sana na ananifundisha kuwa angekua na yule asingefika hapo alipo sasa
NB:
Yapo mengi kuhusu kesho yako ambayo huyajui ila Mungu tu, ukijua roho yako haitaki kuoa/kuolewa na fulani usilazimishe maana anaweza kuwa fit kwa muda huo ila hujui baada ya 20 years maisha yatakapo kupeleka, vipi mwenzako ataweza??
Pata muda wa kukaa na kusikiliza ndani yako (roho) kuliko hisia za moyo wako.
Jambo hili ni pana sana, siwezi andika kila kitu. Ukiona ushauri huu waweza kuwa njia na msaada kwako, basi njoo inbox.