Bila kupoteza Muda ngoja nikupe jibu kuna sababu za kisaikolohia na sababu za ki roho, Naaza na za kisaikolojia. Huenda baada ya kufanya process zote za ndoa na unajuabhuyo ndiye unayekuja kuishi nae umeanza kumlinganisha yeye na vi dada vingine kwenye mitandao huko fb, insta nk, au ukaanza kupimishia wadada wa sehemu unapofanya kazi, majirani zako au sehemu za vituo vya daladala town Trust me huku mjini hasa Dsm kuna sehemu unaeza enda ukaona kila mdada unaekutana nae ni mrembo hadi huyo wako unahisi ilikuaje ukanasa kwake hasa huko Posta, Mwenge na Kkoo.
Ila tu hawa kimsingi sio kweli kwamba ni wazuri kuliko wakwako ila tu ni ile hali ya huwajui ki undani na ndio mara ya kwanza unawaona na unawaona wakiwa wamekwosha jipigilia vitu vyao vya mitoko tofauti na wa kwako kwanza umemzoea afu hata yeye wakati mwingine wakati akitaka kukuona hajiandai saaana maana anachukulia kawaida haji kwaajili ya kukuvuta.
Nikupe mfano mdogo kwa wale watu ambao day 1 wameambiwa na ki binti kinakuja gheto kwao huwa wanachakalika haswa kuandaa mazingira mara kupanga hiki na kile na usafi wa kufa mtu, mpaka kupika utapika au kuandaa chakula ambacho huwa huli mara kwa mara, vipi mkisha kuwa wote kwa mwezi ivi au ukiahakutana nae zaidi ya mara 5 akikwambia anakuja kama umelala unaweza usiamke mpaka anafika na huenda usifungue mlango kama upo wazi yeye mwenyewe akafungua na akapakuta gheto palo hivyo hivyo kama palivyokua muda mnaongea kuwa yupo njiani anakuja.
NAKUSHAURI TU ACHA KABISA KUANZA KUMLINGANISHA MCHUMBA WAKO NA PISI KALI ZA MJI UTAFELI UTAMUONA WAKWAKO KAMA ULIPITIWA IVI.
Sasa nakupa sababu ya ki ufundi zaidi, sababu ya Kiroho kuna baadhi ya watu kutokana na kukandamizwa kwao na mapepo au mambo ya mikosi katika familia au ukoo huwa hawaruhusiwi yaani wameshikiliwa kutoolewa, au haolewi kwa ndoa yani ni kuzalishwa tu afu badqe ndo labda asogezwe.
Wengine walichezewa mkono wao kushoto kwenye vidole husika kidole cha kwanza kidogo ni cha Uzuri na mvuto kwa mtu katika uhusiona walozi wakikuchezea hapo hutaonekana uzuri wako wala mvuto wako, kidole kile cha pili kushoto kile cha ndoa hicho nacho wakikiharibu katika swala la ndoa utapata tabu sana kama ni mdada kuolewa kwako itakua bahati nasibu au na utasakamwa na kuumizwa sana kwenye mahusiano.
Hivyo basi kati ya wewe au mwenzi wako mmoja wenu anaweza kuwa muhanga wa hizo sababu za Kiroho. Au wewe unaweza kuwa muhanga wa zile sababu za kisaikolojia za kuanza kumpambanisha mchumba wako na vi pisi kali vya mji.
KAMA UPO SERIOUS KUSAIDIKA NAKUSHAURI UPATE MSAADA WA KIROHO ISIWE KWA WAGANGA HAO WATAKUHARIBU ZAIDI, TAFUTA SEHEMU SAHIHI KWA MTUMISHI WA KWELI WA MUNGU WASIWE WATUMISHI JANJA JANJA.