Wakuu habari..
Mmebarikiwà sana na Mungu wa Mbinguni hakuna laana.
Aisee Mimi Nina wadogo zangu wawili Mimi nikiwa mtoto wa Kwanza tena wa kiume mdogo wangu wa pili ni wa kike na wa mwisho ni wa kiume.
Cha ajabu toka nikiwa mdogo hata sijaanza chekechea nilikuwa naishi na shangazi yangu ndiye kanilea mpaka najitambua nilikuwa namuita mama mpaka namaliza darasa la Saba nilijua ndiye mama yangu.
Wakati huo mdogo wangu wa kike anayenifuata yeye alikuwa anaishi na Baba mkoa mwingine huko Naye sikuwa namjua wala yeye hakuwa ananijua zaidi ya kujua Tu Nina mdogo wangu yupo mkoa Fulani
Yule dogo wa mwisho yeye ndo alikuwa na mama mzazi sasa maana kumbe Mzee aliachana na mama mara Tu baada ya kumzaa dogo wa mwisho na tetesi zilizopo inasemekana alienda kwao huku nyuma akamuacha beki tatu ambaye shangazi zangu walifanya mapinduzi ili beki tatu awe mama wa familia sa mama aliporudi kwake akakutana na mapinduzi hayo akaamua kusepa Hz ni tetesi Tu huwa naskia na huyo beki tatu ndiye mama wa familia hata sasa akiwa na watoto kadhaa.
Shida imekuja kwamba malezi yangu yote sikuwahi muona mama pale kwa shangazi nakumbuka nilipohitimu darasa la Saba nilisafiri na shangazi kwenda huko alipokuwa mama tulipofka shangazi akawa anaongea na watu fulan akanionyesha njia nipite nitangulie anakuja njiani nikapishana na mama mmoja nikamsalimia tukapishana kumbe aunt aliona si ndo akamstua mama kwamba huyo ndo mtoto wako unayepishana Naye hapo.
Ndo tukafahamiana sasa.
Sasa shida inayonikabili si Mimi Tu hata mdogo wangu wa pili hatuna mapenzi kabisa na mama yetu yaani hamna kabisa mama Naye Kila siku tunasikia anasema Sisi tuna mama zetu wengine mbaya zaidi anarusha mpaka na maneno mazito hata akifa tusiende kwenye msiba yaani hata sielewi kabisa.
Kingine mama anaamini uganga sana anaendaga kwa waganga sjui wampe dawa ya kurudsha uhusiano wake na Sisi lakini wapi imeshindikana.
Wakuu mnanishauri nn aisee maana sielewi siguswi kabisa na uwepo wa mama yangu.
NB: Wazazi hakikisheni mnakaa na watoto wenu hata kama wako mbali mjitahidi watambue uwepo wenu vinginevyo mtalaumu watoto bure Tu na kutupa laana.
Mkuu Kwanza pole Sana kwa changamoto hyo,
Jambo la Kwanza kabisa kabla sijakushauri chochote, jifunzi kuyaweka mambo ya familia Kama Siri, maana hizi familia zinambo mazito mno, ikiwa watu watayatoa nje Ni hatari kubwa na kibaya zaidi huwa hayana solution...
Sasa Basi, naomba nami nitoe ushauri wangu,
Ni vyema kabisa ukiweza ugomvi wa kifamilia hasa wa Baba na mama usije kuuingilia au kuruhusu mtu akakuingiza kwenye ugomvi huo, iwe Ni mama au baba au ndg usiruhusu kabisa hlo Jambo, maana unaweza kuambiwa ukadhani kuwa Ni kwel kumbe wanapandkiza chuki tu Wala hakuna ukwel,
Pili, wapende wazaz wako, cjui Kama unaamini katika dini ipi, ila waombee wasaidie, wajari, tengeneza network nao bila kujal yaliyopita..
Ntakupa mfano wa aliekuwa jaji mkuu wa tz fransis nyalali, fuatilia historia yake, kifupi yy aliamua kuwasaidia wazaz wake wote bila utofauti wao, na kwake ilimpa Amani mno..
Tatu, .mkuu kwenye familia kunasili nyingi mno ambazo huwa Ni aibu na nadra kuzisema hi ni kwa kuwa husalia kuwa Siri za familia, usiruhusu mzaz wako kwa namna yoyot kumwongelea vibaya..
Nmeangalia age yako nmegundua ww ni mwanaume si mvulana, badili mtazamo wako juu ya wazaz wako, nkakuambia siku ukibadili altitude zako ukawaombea wazaza, akamwambia Mungu akufundishe namna Bora ya kuwapenda, utakuja kutoa ushuhuda hapa..
Kila raheri mkuu, Mungu akutangulie, hakuna mzazi mbaya ambae anamchukia mwanae, amka mkuu