Sina mashaka na tuhuma dhidi ya TB Joshua

Umenena vema. Sina tatizo na kumnywesha mtu mwenye shida maji ili afunguliwe, au mafunuo ya kutumia chumvi. Tatizo ni pale watumishi kuanza biashara kanisani. Mtumishi ananunua chumvi tsh 500 anakuja kuuza tsh 5000 vivyo na maji pia na mafuta. Huo ni UTAPELI makanisani.
 
Hao wa kununua malighafi ndio tatizo.

Mathayo (Mat) 10:8
Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.

Kwanza Wakristo tumepewa uwezo wa kufanya kazi za Kimungu Bure kabisa.

Tusimame katika Neno la Kristo.
Kuuza maji au mafuta au udongo ni utapeli.
Neno la Kristo halisemi hivyo.

Anayeuza hizo gadgets ni Tapeli kutokana na Neno la Kristo.
Fullstop.
 
Hakumuuzia mtu udongo au kitu chochote kile
 
Hicho unacho sema sivyo kilivyo ...tena umeongea ujinga uliotukuka madhehebu ni kitofauti na hicho ulicho sema ndiyo maana hata eneo moja yanaweza kuwa madhehebu 6 na kila dhehebu lina sera zake na itikadi zake na viongozi wanapokea amri kutoka mkondo wa dhehebu lao tu ...mfano papa majuzi kasema mashoga wabarikiwe kwenye dhehebu katoriki huo mwongozo siyo kwa wasabato wala walokole wala TAG wacha kupayuka usiyo yajua
 
Sawa basi tunakutegemea wewe uongee vizuri.
Karibu sana
 
Bwana Yesu akubariki sana.
 
Nakumbuka maajenti wa kuuza maji ya upako ya TBJ walikuwepo hadi hapa DAR.
Hao maajenti walikuwa Matapeli.
ieleweke hivyo.
Niliwahi fika ofisini kwao pale Mkapa House Posta Mpya.

Walisema wanayauza hayo maji ili kukabiliana na ghalama ya kuyasafirisha na pia kuchelea wasiohusika kuyachukua hayo maji Bure na kuyatumia tofauti na yanavyotakiwa kutumiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…