GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
1. Ili wana Simba SC tunaodanganywa kila mara mpaka kutuletea Mchezaji Mhamasishaji, Majeruhiwa, Mwanasiasa ( hasa za Michezo ), Mpiga Kura, Msanii na kufanywa Wapumbavu tuumbuke.
2. Ili Uongozi mbovu na wa Upigaji mwingi ubadilike au uachie ngazi.
3. Itufanye Mashabiki wa Simba SC kuachana na Ushamba wa Kutambia kila mara kufika Robo Fainali ya CAFCL.
4. Imfanye Mwekezaji Mo Dewji ajawe na Hasira na Msimu ujao atusajiie Majembe.
5. Iwafanye Wachezaji wa Simba SC nao waige Fighting Spirit ya Wachezaji wa Yanga ili nao Msimu ujao wafanye vyema zaidi yao.
6. Itasaidia kuinua Soka la Tanzania kwa Vilabu vingi Kusajili vyema, kuongeza Ushindani na Kukaribisha Wafadhili wengine hivyo Kuinogesha Ligi Kuu.
7. Kutazidi kuitangaza zaidi Tanzania hasa Kimataifa, Kuitangaza Ligi Kuu yetu na kuipa Mailage Kubwa Benki ya NBC hivyo Kuwashawishi kwa Msimu ujao Waongeze Dau la Udhamini na Ligi Kuu yetu Inoge na iendelee Kuibua Vipaji vingi ndani na nje ya Tanzania.
GENTAMYCINE nikiwa kama Mwanamichezo na Mdau mkubwa wa Michezo na Mshindi wa Shindano la Kwanza la Mwanachama Bora Jukwaa la Michezo ( Sports ) hapa JamiiForums kwa mwaka Jana ( 2022 ) kwa Moyo Mkunjufu kabisa na hata bila ya chembe ya Unafiki naitakia Kila la Kheri Yanga SC katika Mechi yao ya marudiano na Marumo Gallants FC Keshokutwa ( Jumatano ) tarehe 17 Mei, 2023 ili Watinge Fainali ya CAFCC na Wabebe kabisa na Kombe lenyewe katika Mechi ya Fainali na Inshaallah Mwenyezi Mungu atalifanikisha hili.
Kwa kuonyesha kuwa hili nimelidhamiria na namaanisha nahitaji mwana Yanga SC yoyote mwenye Jezi ya Kijani ya Yanga SC ainunue kisha akampe Mtani wangu na Kaka JamiiForums Founder Maxence Melo na Yeye atajua kwa kunipata na Kunikabidhi hiyo Jezi ya Mabingwa wapya wa CAFCC ili niivae / niitinge hiyo Keshokutwa Jumatano.
Mwisho nitaomba kwa wale JamiiForums Members wana Yanga SC jikusanyeni nyote kisha niambieni hii Mechi mtaiangalizia wapi ili nijumuike nanyi kwani sasa ni rasmi hata kama wana Simba SC tutaumia na Kununa ( kuwa na Usununu ) kwamba hili Jambo la Yanga SC ni la Kitaifa na Kinchi kabisa.
Kila la Kheri Yanga SC na mkashinde.