Taharuki yaibuka mkoani Arusha baada ya mwanamke mmoja Ester ambae ni mzaliwa wa Singida, Baada ya kuvimba na kuoza kwa kwa vidole vyake vya mkononi kudai kwamba sababu ya tatizo lake hilo baada ya kuchomwa sindano ya U.T.I katika moja ya duka la madawa (pharmacy) linalopatikana mkoani hapo.
Akieleza tukio hilo kwa uchungu Ester ameeleza kwamba tatizo hilo linampelekea kupata maumivu makali yanayompelekea kushindwa kulala usiku na mchana.
Aidha aliendelea kueleza kuwa baada ya tatizo hilo alipojaribu kwenda sehemu alipopewa huduma hiyo iliyomletea madhara muhusika alimkana kwamba hamtambui na kuwa hajawahi kumchoma binti huyo sindano.
Chanzo: Global TV Online
Your browser is not able to display this video.
====
UPDATE;
WIZARA ya Afya imeelezea kupokea kwa masikitiko kuhusu taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuanzia Mei 7,2023 kuhusiana na Bi.Esther Mkombozi mkazi wa Mtaa wa Kimandolu mkoani Arusha ambaye ameeleza kuwa, alichomwa sindano katika duka la dawa na kumsababishia madhara katika mkono wake.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Mei 9,2023 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Afya, Bw.Aminiel Buberwa Aligaesha.
"Tunapenda kuufahamisha umma kuwa, ni kosa kisheria kwa duka lolote la dawa nchini kutoa huduma za kitabibu ikiwa ni pamoja na kuchoma sindano, kufanya tohara au vipimo vya kimaabara.
"Kutokana na hilo, Wizara imeelekeza Baraza la Famasia (PC) na Bodi ya Hospitali Binafsi (PHAB) kufuatilia suala hili mara moja ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa wote watakaobainika kukiuka sheria, kanuni, miongozo na taratibu za usimamizi na udhibiti wa utoaji wa huduma za afya nchini.
"Tunampa pole, Bi.Esther kutokana na madhara aliyoyapata. Tunawaomba wananchi kuendelea kuwa watulivu ambapo suala hili linafanyiwa kazi.
"Wizara yya Afya inatoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanapata huduma za afya katika maeneo stahikiu ikiwemo hospitali, vituo vya afya na zahanati ili kuepuka madhara na athari mbalimbali zinazoweza kuwapata ikiwa watakwenda sehemu zisizo rasmi,"imefafanua kwa kina sehemu ya taarifa hiyo.
Tanzania kwenye matibabu inatakiwa uwe makini kweli kweli. Tena wakati mwingine unaweza kuwa makini lakini bado ukapatwa na mkasa mbaya hivyo wakati mwingine ni kuomba tu Mungu asaidie. Haya ni matokeo ya kukosa uongozi bora na nchi kuendeshwa kiholela kama uwanja wa fisi. Kila siku kuna watu wanapata madhara na wengine kufa kwa sababu ya kutibiwa na vilaza.
Tanzania kwenye matibabu inatakiwa uwe makini kweli kweli. Tena wakati mwingine unaweza kuwa makini lakini bado ukapatwa na mkasa mbaya hivyo wakati mwingine ni kuomba tu Mungu asaidie. Haya ni matokeo ya kukosa uongozi bora na nchi kuendeshwa kiholela kama uwanja wa fisi. Kila siku kuna watu wanapata madhara na wengine kufa kwa sababu ya kutibiwa na vilaza.
Taharuki yaibuka mkoani Arusha baada ya mwanamke mmoja Ester ambae ni mzaliwa wa Singida, Baada ya kuvimba na kuoza kwa kwa vidole vyake vya mkononi kudai kwamba sababu ya tatizo lake hilo baada ya kuchomwa sindano ya U.T.I katika moja ya duka la madawa (pharmacy) linalopatikana mkoani hapo.
Hata hospital madhara yanaweza kutokea sikatai. Lakini wahudumu wengi wa pharmacy hawana kibali cha kuchoma watu sindano. Wanafanya nje ya utaratibu.
Angechoma hospitali ingekuwa rahisi kufatilia.
Kama hapo mchoma sindano amemkana na hana ushahidi wowote kama ni kweli alichomwa hapo. Maumivu mara mbili...