Sindano ya kutibu U.T.I yadaiwa kumletea madhara mwanamke huyu

Ni sahihi.
Sasa unakutana na case kama hii aliyoleta mtoa mada,huko mitaani mtu akiumwa kiuno anakwambia ni UTI akienda duka la madawa ndo yanaishia haya ya kuchomana sindano bila indications.

Siku hizi kumekua na abuse kubwa sana ya antibiotics na wanaugonjwa mpya unaitwa mchafuko wa damu,tiba yao ni antibiotics
Ni shida kubwa, janga la drug abuse drug resistance.
 
Mwanamke anayejulikana kama Ester Mkombozi mkaazi wa Kimandolu Arusha ameoza sehemu ya vidole vyote vya mkono wa kushoto baada ya kuchomwa sindano katk duka la dawa ktk eneo la Ngulelo jambo ambako limepelekea kukatwa vidole vyote.

Ester ameseme March mwaka huu alienda ktk duka la dawa kwasababu aliambiwa ana tatizo la UTI ndipo akachomwa sindano mkononi na ghafra akaanza kuhisi maumivu makali ya mkono na kupelekea baadae kupata maumivu ya mkono mara kwa mara, mkono kuvimba na vidole kubadilika rangi.

Ester ambaye kwasasa anaendelea na matibabu ktk hospitali ya rufaa ya Mount Meru anasema alifika ktk duka hilo March 20 mwaka huu baada ya kuwa hajisikii vizur na alipofika hapo walimpima na kumwambia ana UTI hivyo anatakiwa kuchoma sindano hiyo ya mkono.

Ester anaendelea kusimulia kwamba kesho yake alirudi kwenye like duka na kukuta wamefunga huku mkono ukiendelea kuvimba na kuuma Hali iliyomlazimu kurudi siku ya tatu yake ambapo walimpa dawa ya kuchua na vidonge vya kumeza ambavyo hata hivyo havikumsaidia Hali iliyomlazimu kwenda kwenye duka la dawa lingine ambapo aliwaonyesha kile kichupa Cha dawa wakamweleza kwamba dawa haina shida ila haikupaswa kuchomwa mkononi bali matakoni.

Anaendelea kusimulia kwamba baada ya kuona mkono inazid kuvimba, maumivu makali na vidole kubadilika rangi aliamua kwenda hospitali ya Rufaa ya Mount Meru ambapo alipelekwa kitengo Cha dharura na madaktar walipomchinguza wakagundua kwamba vidole vyote vya mkono wa kushoto vimeoza hivyo anatakiwa afanyiwe upasuaji wa kuvikata.

Ester anasema kazi yake ilikuwa ni kusuka na ndio ilikuwa inamuendeshea maisha yake na amesikitishwa na mmiliki wa duka hilo la dawa kumkana na kusema hamjui hivyo anaomba asaidiwe kupitia namba 0788618073 kifedha na hata kisheria ili aweze kupata haki yake Kwan ana watoto wawili ambao wanamtegemea.

FUNZO:

Duka la dawa jukumu lake kubwa ni kuuza dawa ulizoandikiwa na Dr na sio kutibu hivyo ukiwa unaumwa hatua ya kwanza nenda hospitali kuepukana na matatizo ya namna hii unaweza Kuta dada wa watu hata hiyo UTI hakuwa nayo ila kwakuwa waliitaka pesa yake wakambambikizia ugonjwa, na siku hizi wafanyakazi kwenye maduka mengi ya dawa ni Vimeo hatari.

Pole sana dada Ester.
 
Aiseee, sindano ya UTI mtu anachomwaje mkononi?? Na hiyo dawa aliyoingiziwa ni dawa ya aina gani??
 
  • Wapo pia walioenda hosptali na kukumbwa na majanga ndg. Nina visa kadhaa vya vifo vilivyotokana na kuchomwa sindano visivyo.
  • Japo pia kuna ajali kazini kutokana na uzembe
  • Ni vyema kuwa na Dr/famasia wako mwenye uzoefu wa huduma. Vijana wengi si wa kuwaamini
 
Wanawake ni watu wa kurahisisha Mambo sana.wengine utakuta wanawabebesha wadada wa kazi kupeleka mtt clinic .pole kwake
 
Vidole vimekuwa vyeusi sana alafu binti kazi yake ni msusi inasikitisha mkono wa kusukia ndiyo unamatatizo.
 
Ukishangaa ya Mussa...sijawahi kujua kama duka la dawa pia kuna mchoma sindano.

Pole kwa dada Esther...Mungu Atamfanyia wepesi katika maisha yake...amin
 
Taharuki yaibuka mkoani Arusha baada ya mwanamke mmoja Ester ambae ni mzaliwa wa Singida, Baada ya kuvimba na kuoza kwa kwa vidole vyake vya mkononi kudai kwamba sababu ya tatizo lake hilo baada ya kuchomwa sindano ya U.T.I katika moja ya duka la madawa (pharmacy) linalopatikana mkoani hapo.

Akieleza tukio hilo kwa uchungu Ester ameeleza kwamba tatizo hilo linampelekea kupata maumivu makali yanayompelekea kushindwa kulala usiku na mchana.

Aidha aliendelea kueleza kuwa baada ya tatizo hilo alipojaribu kwenda sehemu alipopewa huduma hiyo iliyomletea madhara muhusika alimkana kwamba hamtambui na kuwa hajawahi kumchoma binti huyo sindano.

Chanzo: Global TV Online

View attachment 2614383

====

UPDATE;

WIZARA ya Afya imeelezea kupokea kwa masikitiko kuhusu taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuanzia Mei 7,2023 kuhusiana na Bi.Esther Mkombozi mkazi wa Mtaa wa Kimandolu mkoani Arusha ambaye ameeleza kuwa, alichomwa sindano katika duka la dawa na kumsababishia madhara katika mkono wake.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Mei 9,2023 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Afya, Bw.Aminiel Buberwa Aligaesha.

"Tunapenda kuufahamisha umma kuwa, ni kosa kisheria kwa duka lolote la dawa nchini kutoa huduma za kitabibu ikiwa ni pamoja na kuchoma sindano, kufanya tohara au vipimo vya kimaabara.

"Kutokana na hilo, Wizara imeelekeza Baraza la Famasia (PC) na Bodi ya Hospitali Binafsi (PHAB) kufuatilia suala hili mara moja ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa wote watakaobainika kukiuka sheria, kanuni, miongozo na taratibu za usimamizi na udhibiti wa utoaji wa huduma za afya nchini.

"Tunampa pole, Bi.Esther kutokana na madhara aliyoyapata. Tunawaomba wananchi kuendelea kuwa watulivu ambapo suala hili linafanyiwa kazi.

"Wizara yya Afya inatoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanapata huduma za afya katika maeneo stahikiu ikiwemo hospitali, vituo vya afya na zahanati ili kuepuka madhara na athari mbalimbali zinazoweza kuwapata ikiwa watakwenda sehemu zisizo rasmi,"imefafanua kwa kina sehemu ya taarifa hiyo.
Kumbe ilisharipotiwa huku? Kuna wahudumu wa afya chenga sana siku hizi huyo jamaa anatakiwa kuchukuliwa hatua kali sana za kisheria
 
Serikali tilieni mkazo kwenye wahudumu wa afya wawe weledi zaidi hata kama ni pharmacy ila akiwepo mtu sahihi mambo yanaenda ile kozi ya ADO imeishia wapi?
Mi naona suala la kuboresha zaidi mafunzo kwa wahudumu wawe weledi zaidi nimekutana na wahudumu wazuri na wasio waelewa kutoka hospital za Serikali na pharmacy pia katika halmashauri mojawapo hivi karibuni.Nilijaribu kuzunguka kuangalia namna ya huduma zinavyoenda kuna wachache wanaharibu ingawa wengi wanajitahidi ila kuna wahudumu wanafanya vitu wasivyovielewa vizuri au wanakosa kujiamini hili nimeliona Kwa macho yangu.
Nashukuru wizara ya afya kwa kulitolea ufafanuzi.
 
Taharuki yaibuka mkoani Arusha baada ya mwanamke mmoja Ester ambae ni mzaliwa wa Singida, Baada ya kuvimba na kuoza kwa kwa vidole vyake vya mkononi kudai kwamba sababu ya tatizo lake hilo baada ya kuchomwa sindano ya U.T.I katika moja ya duka la madawa (pharmacy) linalopatikana mkoani hapo.

Akieleza tukio hilo kwa uchungu Ester ameeleza kwamba tatizo hilo linampelekea kupata maumivu makali yanayompelekea kushindwa kulala usiku na mchana.

Aidha aliendelea kueleza kuwa baada ya tatizo hilo alipojaribu kwenda sehemu alipopewa huduma hiyo iliyomletea madhara muhusika alimkana kwamba hamtambui na kuwa hajawahi kumchoma binti huyo sindano.

Chanzo: Global TV Online

View attachment 2614383

====

UPDATE;

WIZARA ya Afya imeelezea kupokea kwa masikitiko kuhusu taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuanzia Mei 7,2023 kuhusiana na Bi.Esther Mkombozi mkazi wa Mtaa wa Kimandolu mkoani Arusha ambaye ameeleza kuwa, alichomwa sindano katika duka la dawa na kumsababishia madhara katika mkono wake.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Mei 9,2023 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Afya, Bw.Aminiel Buberwa Aligaesha.

"Tunapenda kuufahamisha umma kuwa, ni kosa kisheria kwa duka lolote la dawa nchini kutoa huduma za kitabibu ikiwa ni pamoja na kuchoma sindano, kufanya tohara au vipimo vya kimaabara.

"Kutokana na hilo, Wizara imeelekeza Baraza la Famasia (PC) na Bodi ya Hospitali Binafsi (PHAB) kufuatilia suala hili mara moja ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa wote watakaobainika kukiuka sheria, kanuni, miongozo na taratibu za usimamizi na udhibiti wa utoaji wa huduma za afya nchini.

"Tunampa pole, Bi.Esther kutokana na madhara aliyoyapata. Tunawaomba wananchi kuendelea kuwa watulivu ambapo suala hili linafanyiwa kazi.

"Wizara yya Afya inatoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanapata huduma za afya katika maeneo stahikiu ikiwemo hospitali, vituo vya afya na zahanati ili kuepuka madhara na athari mbalimbali zinazoweza kuwapata ikiwa watakwenda sehemu zisizo rasmi,"imefafanua kwa kina sehemu ya taarifa hiyo.
True kabisa NDUGU yangu aliandikiwa dawa za TEZI DUME hosptri moja kubwa ya serikali ya wilaya hapa mjini dar es salaam
Akaanza kutumia basi bana kesho yake ASUBUHI mkojo hautoki akilazimisha kwa tabu sana
Ikabidi tumkimbize MWANANYAMALA docta kumcheck akamuuliza shida ilianza vipi
Akaanza kueleza kama dalili za U.T.I
akamuuliza mbna hizi dawa za tezi dume je alikupima TEZI DUME ndugu haelewi
dr akamuuliza alichukua vipimo gani akajibu mkojo na damu ya marelia
Dr akaguna akarudia tena kupima mkojo na damu ikaonekana U.T.I dr akamchoma
sindano Ya CEFTRIAXONE akampa na VIDONGE vingine
akamuambia asikikizie siku mbili kama mkojo hutatoka kwa tabu hvyohvyo arudi
Ikawa fresh ila mpk kesho ana KILEMA akikojoa mkojo hauishi wote au wakti mwingine flow inakuwa ndogo
Hizi Hosptari ukienda uombe MUNGU tu lakini hawa MADOCTA sio kabisa hawajali kabisa kuhusu AFAYA ya mtu
 
dah! asee pole yake sana
 
Ila ma Dr jamani, kuna ndugu yangu alikuwa mjamzito ile miezi mitatu akalazwa ili wafunge mfuko wa kizazi, isiku Dr kamiandikia madawa na flagil juu. Kabla ya kumeza akamwambia nesi unajua miye nina mimba hizi flagil vipi? Nesi akamwambia oooh basi usinywe. Asingejua leo angezaa mtoto sijui wa dizaini gani?
 
Ni antibiotic yenye nguvu sana dhidi ya bacteria
Hii powercef(ceftriaxone)nahc kila mtu anaijua kias kwamba mtu akihisi tu dalili ya U.T.I anajua moja kwa moja dawa yake ni powercef hawajui cha first choice,second choice wala nini na mhudumu wa pharmacy anamchoma moja kwa moja ndo maana kuna kipindi kuliibuka ugomvi mkubwa na malalamiko kwa hawa waliosomea Addo na physician sababu ya huu ujinga unaozidi kufanyika
 
Wauza dawa ambao ni product ya addo, ambao hawana taaluma yoyote ya afya, hasa wa miaka kuanzia 10 iliopita, wengi wao ni watupu.
 
Sahihi kabisa mkuu yaani kiujumla wanaidhalilisha kada ya Afya kwanza kabisa hy Addo ni kozi iliyoanzishwa na kikundi flani cha watu wachache ambao mpaka muda huu wenye vyeti vya addo wanahesabika.
 
Back
Top Bottom