Introsagvert
JF-Expert Member
- Sep 9, 2019
- 1,459
- 3,020
Ktk aina ya muziki ambao siupendi hata kidogo ni huu unaita singeli.Sijuwi vigezo vinavyotumika kufungia njimbo.- humo hakuna hoja (maudhui) ya maana, ni kuhimiza kuinama na kuonyesha namna unavyochuma tembele na mchicha tu basi!
- juzi kati hapa niliona video moja ya singeli na hatua ya muziki wao waliyoipiga imenistua.......madensa wa kiume wanatwerk, yaani wanainama na kutikisa makalio kama wafanyavyo kina dada.
- yote tisa, kumi nilichokisikia jana; muimbaji anaimba singeli yake kwa kutukana kabisa wazi wazi tusi kubwa la kutaja kiungo cha wazazi wetu wa kike. Ajabu watu walikuwa wanajimwaga tu na kuchekelea.
- kwenye vigodoro vya kupatia mimba wanafunzi muziki ndo mtawala!
Mnanda mbona uko vizur tu RIP Dogo Simela,Omary Omary .Mnanda nao ndio wale wale
Hii kazi producer ndiyo ataelewa nazungumzia nini.Hata ukiboreshaji kimaudhui, lakini kamwa huo sio mziki labda tuweke kwenye kundi la ngoma za kienyeji. Ukiutest kwenye sifa za muziki haupo, muziki ni lugha iliyokamilika ambayo huongea yenyewe hata bila neno hata moja.
AVOGADRO- PHD in music
Mziki mahsusi kwa watu wasiotaka kutumia akili zao,wavivu na wazembe, mana hauna maudhui, unahubiri starehe za grade D yani siwez sema ni starehe ni kahara tu...mtu anamruhusu mke wake akadange na kama akipata boss ampeleke njia isio sahihi...unareflect lazy ass-es reunion kwenye maisha yao...yani mkeo akadange wewe ndio ule [emoji1787][emoji1787][emoji1787]- humo hakuna hoja (maudhui) ya maana, ni kuhimiza kuinama na kuonyesha namna unavyochuma tembele na mchicha tu basi!
- juzi kati hapa niliona video moja ya singeli na hatua ya muziki wao waliyoipiga imenistua.......madensa wa kiume wanatwerk, yaani wanainama na kutikisa makalio kama wafanyavyo kina dada.
- yote tisa, kumi nilichokisikia jana; muimbaji anaimba singeli yake kwa kutukana kabisa wazi wazi tusi kubwa la kutaja kiungo cha wazazi wetu wa kike. Ajabu watu walikuwa wanajimwaga tu na kuchekelea.
- kwenye vigodoro vya kupatia mimba wanafunzi muziki ndo mtawala!
Huwa nashangaa sana wanaouita huu upuuzi ni Muziki. Huna quality ya kuitwa muki.
Haya ndio yale mangoma ya kienyeji ya kizaramo yaitwayo mdundiko ambao asilimia 99 ya maneno yake ni matusi ndio watu sasa hivi wanayarekodi studio na kuyabatiza ni muziki wa singeli.
Mbaya zaidi, sisi wote ni watanzania na ni waswahili, Tafsiri na tasfida ya maneno yaliyotumika yapo wazi kabisa na watoto wadogo wanayaimba mitaani na kufanya majaribio ya kile walichokisikia kwenye vyombo vya habari, ni kweli mamlaka zinazohusika huwa zinapitia fafsiri ya maneno yanayotumika kwenye huu utopolo uoitwao singeli ambao hata haujakaa ki melody bali limtu linajitamkia tuuu maneno kwa kufuata mdundo wa ngoma?
Labda wengi hamfahamu chimbuko la mziki huu ila mnabahatisha tu.Mkuu mimi nakumbuka kwa jina la Mchiriku.
Na wewe huwa unacheza?Inashawishi kucheza,lakini basi tu.