Singeli, muziki wa ajabu kuwahi kutokea Tanzania

Singeli, muziki wa ajabu kuwahi kutokea Tanzania

"Hiii hiii nikuogopeee eeti nisibambie nikuogope wewee
Hiii hiii akuogopeee eeti asicheze chura akuogope wewee"

Shika chini we dada usiangalie sura tikisa moja moja sijaona ukicheza chura twendeee X2

Hiii hiii nikuogopeee haunilishi haunivishi nikuogopeee wewee
Hiii hiii nikuogopeee sikujui hunijui nikuogopeee wewee

Sina fagio fagio langu la chuma kwanza hatuendani mi mzigua sijui mwenzangu "we nanii"

Sina fagio fagio langu la chuma kwanza hatuendani mi mmakonde sijui mwenzangu "we nanii"

"Jaman ule mchezo wa kususiana sijaona ukisusa hiloooo[emoji527], amekupa amekususia"X2[emoji16][emoji16]

Acha kabisa mkuu likichanganya kuna vibe lake [emoji16][emoji16]
 
- humo hakuna hoja (maudhui) ya maana, ni kuhimiza kuinama na kuonyesha namna unavyochuma tembele na mchicha tu basi!

- juzi kati hapa niliona video moja ya singeli na hatua ya muziki wao waliyoipiga imenistua.......madensa wa kiume wanatwerk, yaani wanainama na kutikisa makalio kama wafanyavyo kina dada.

- yote tisa, kumi nilichokisikia jana; muimbaji anaimba singeli yake kwa kutukana kabisa wazi wazi tusi kubwa la kutaja kiungo cha wazazi wetu wa kike. Ajabu watu walikuwa wanajimwaga tu na kuchekelea.

- kwenye vigodoro vya kupatia mimba wanafunzi muziki ndo mtawala!
Ktk aina ya muziki ambao siupendi hata kidogo ni huu unaita singeli.Sijuwi vigezo vinavyotumika kufungia njimbo.
 
Hata ukiboreshaji kimaudhui, lakini kamwa huo sio mziki labda tuweke kwenye kundi la ngoma za kienyeji. Ukiutest kwenye sifa za muziki haupo, muziki ni lugha iliyokamilika ambayo huongea yenyewe hata bila neno hata moja.

AVOGADRO- PHD in music
Hii kazi producer ndiyo ataelewa nazungumzia nini.
Mziki hauna lugha chief.
 
- humo hakuna hoja (maudhui) ya maana, ni kuhimiza kuinama na kuonyesha namna unavyochuma tembele na mchicha tu basi!

- juzi kati hapa niliona video moja ya singeli na hatua ya muziki wao waliyoipiga imenistua.......madensa wa kiume wanatwerk, yaani wanainama na kutikisa makalio kama wafanyavyo kina dada.

- yote tisa, kumi nilichokisikia jana; muimbaji anaimba singeli yake kwa kutukana kabisa wazi wazi tusi kubwa la kutaja kiungo cha wazazi wetu wa kike. Ajabu watu walikuwa wanajimwaga tu na kuchekelea.

- kwenye vigodoro vya kupatia mimba wanafunzi muziki ndo mtawala!
Mziki mahsusi kwa watu wasiotaka kutumia akili zao,wavivu na wazembe, mana hauna maudhui, unahubiri starehe za grade D yani siwez sema ni starehe ni kahara tu...mtu anamruhusu mke wake akadange na kama akipata boss ampeleke njia isio sahihi...unareflect lazy ass-es reunion kwenye maisha yao...yani mkeo akadange wewe ndio ule [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
hata Hip-hop ilipitia huko, mbona wasanii wakubwa Prof Jay, Harmonize wameimba singeli ktk lugha ya kistaarabu tu... Ni vile WaTz mnapenda kushobokea miziki ya nje na hamjui lolote... Ila cha ajabu singeli ikipigwa kwenye harusi na pub zenu mnasimama kucheza ila huku mtaani mnajifanya hamuupendi...
 
Ila tamu kuiangalia mijimama inavyotikisa wowowo dah. Halafu unasogea unacheza nyuma ya wowowo inayotikisika bila malipo.

Ukiona mtu anamind singeli ujue kazaliwa sijui Rorya, simiyu, kishapu, sijui Ikungi nk. Acheni Singeli lipigwe tu kashindwa Makonda kuzuia ndio mtaweza nyie
 
Humo kwenye huo mziki utakuta kijana wa kiume anabana makalio Kisha anayatingisha mbele ya wavulana wenziee
Mungine vijana wenziee wanamwagia maji makalioni Kisha kijana anaanza kunengua kama kabint flan hivi kwa vivulana vyenzie
Ni aina ya mziki wa kipuuuuzi kabisaaa
 
Mkuu kumbuka msanii Ni kioo cha jamii .
Kwhy meja Kunta na wenzake nao mfano Bora ,,,,,habha aaaaa muziki wa laana sana
Huwa nashangaa sana wanaouita huu upuuzi ni Muziki. Huna quality ya kuitwa muki.
Haya ndio yale mangoma ya kienyeji ya kizaramo yaitwayo mdundiko ambao asilimia 99 ya maneno yake ni matusi ndio watu sasa hivi wanayarekodi studio na kuyabatiza ni muziki wa singeli.

Mbaya zaidi, sisi wote ni watanzania na ni waswahili, Tafsiri na tasfida ya maneno yaliyotumika yapo wazi kabisa na watoto wadogo wanayaimba mitaani na kufanya majaribio ya kile walichokisikia kwenye vyombo vya habari, ni kweli mamlaka zinazohusika huwa zinapitia fafsiri ya maneno yanayotumika kwenye huu utopolo uoitwao singeli ambao hata haujakaa ki melody bali limtu linajitamkia tuuu maneno kwa kufuata mdundo wa ngoma?
 
Mkuu mimi nakumbuka kwa jina la Mchiriku.
Labda wengi hamfahamu chimbuko la mziki huu ila mnabahatisha tu.

Segere ni mziki uliotokana na ngoma ya mdundiko.
Lile goma ambalo likipigwa mitaani wamama wanaunguza m oga na watoto kupotea.

Ila mziki wa Singeli umetokana na mziki wa Mnanda ambao nao uliibia kwa mbali segere wakachanganya na malimba halafu kinanda kikaingizwa.

Mnanda ukaja kuzaa mchiriku ambao wenyewe unahusika na kuimba zaidi.

Mchiriku baada ya miaka mingi ukafifia hivi, Ndio watu wakachukua taarabu wakaanza kughani.

Hapa unawazungumzia watu kama Msaga sumu na wengineo.
Aina hii ya kughani mashairi kwenye vigodoro ndio ikazaa Singeli.

Singeli ni mziki ulioanzia uswahilini na unavhanganya Radha zote za waswahili yaani mule ndani Kuna Mnanda, Mchiriku, Kibao kata, mdundiko, mdumange ila tofauti yake bit ya Singeli inakwenda fasta yaani unakimbizwa kimbizwa hivi.

Aina hii kama Nyerere asinge ipiga marufuku miaka ya 70 basi ndio ungekuwa utambulisho wa Watanzania.

Ukiwakilisha kundi la daraja la watu wa chini kwenye jamii ila niamini Mimi mtu akichukia Sanaa ujue ana shida mahali.
 
Si mziki wa kucheza kwenye hadhara maana mh mh mh,,,nikinoga huwa najilowesha maji na dera langu naanza Sasa kumpa singeli dubwana,,, maisha ndo haya haya
 
Back
Top Bottom