SINGIDA: Auawa baada ya kufumaniwa na mke wa mtu shambani

SINGIDA: Auawa baada ya kufumaniwa na mke wa mtu shambani

MKAZI wa Kijiji Cha Merya Tarafa ya Ilongero wilayani Singida, Innocent Dube (49), ameuawa kwa kuchomwa kisu mgongoni baada ya kukutwa akifanya ngono na mke wa mtu shambani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Stella Mutabihirwa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo wakati akizungumza na waandishi wa Habari ambapo amesema, tukio hilo limetokea Julai 9, 2023.

Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi linamsaka Simon Mwangi (58) mkazi wa Ghata wilayani Singida anayedaiwa kuhusika na mauaji hayo.

CHANZO: NIPASHE
Aisee
 
Nakumbuka nilifumaniwa karibu na mto malarasi kiukweli sikusubir mie nilijitupia mtoni bora kupambana na mamba mwenye njaa kuliko bin adam niliogelea huku nikifuatilia nyomi la watu wengine wakirusha mawe na vigongo lakini nilifanikiwa kufika ng'ambo kabla yao nikiwa kama nilivyozaliwa nilifukua mbio hata San LG ikasome sikukanyaga kijijini miaka dahali halafu nikadhani nitaacha ndo kwaanza nimenoa panga upya
 
Back
Top Bottom