Singida Black Stars yawabadilisha Uraia wachezaji wanne wa Kigeni na kuwa raia wa Tanzania ili Kukidhi Kanuni

Singida Black Stars yawabadilisha Uraia wachezaji wanne wa Kigeni na kuwa raia wa Tanzania ili Kukidhi Kanuni

Kupewa uraia wa nchi maskini hakuna shida yoyote, waafrika ni ndugu ni jamii moja, ni mipaka ya wazungu ilitutenganisha tu.

Shida itakuja pale wakishuka viwango na kuachwa na timu hiyo wataenda wapi kula ugali na sukari maana hawana ukoo bongo!! Au kwa Shem yule mrembo?
Wachezaji wanalipwa vizuri Sana kupata makazi inawezekana
 
Wachezaji wanalipwa vizuri Sana kupata makazi inawezekana
Kwa mambo haya ya kupewa uraia wachezaji wa kigeni wanapaswa sasa kuanzisha umoja wa wachezaji wa kigeni wasaidiane mmoja akipewa thank you maana hawa ni raia wenzetu bongo haina mwenyewe, ila hawana ukoo bongo, nani atawashika mkono wakifilisika? katibu awe Aziz Ki, Chama m/kiti , Dube mjumbe!! Yule Waziri aliekuwa akicheza wimbo wa Yanga Africa baada ya kushinda tano awe Mlezi wa Chama.
 
Kwa mambo haya ya kupewa uraia wachezaji wa kigeni wanapaswa sasa kuanzisha umoja wa wachezaji wa kigeni wasaidiane mmoja akipewa thank you maana hawa ni raia wenzetu bongo haina mwenyewe, ila hawana ukoo bongo, nani atawashika mkono wakifilisika? katibu awe Aziz Ki, Chama m/kiti , Dube mjumbe!! Yule Waziri aliekuwa akicheza wimbo wa Yanga Africa baada ya kushinda tano awe Mlezi wa Chama.
Kikikiki
 
Singida Black Stars imewabadilisha uraia wachezaji wake wanne wa kigeni na kuwa raia wa Tanzania, Singida imefanya hivyo ili kukidhi kanuni ya kuwa na wachezaji 12 wa kigeni.

Wachezaji hao ambao wamebadili uraia ni Emmanuel Keyekeh, Arthur Bada, Damaro Mohamedi na Golikipa Amas Obasogie.

Josaphat Arthur Bada (22) ni kiungo raia wa Côte d'Ivoire amewahi kuichezea klabu ya ASEC Mimosas na timu ya taifa Ivory Coast chini ya miaka 23

Soma pia: Idara ya uhamiaji yatoa ufafanuzi dhidi ya wachezaji wa kigeni Singida Black Stars, wote ni raia wa Tanzania kwa Tajnisi
Emmanuel Keyekeh (27) kiungo mkabaji raia wa Ghana alijiunga na Singida Big Stars akitokea FC Samartex ya ligi kuu ya nchini kwao.
Pamoja na Mohamed Damaro (22), kiungo mkabaji raia wa Guinea ambaye pia ni mchezaji wazamani wa timu ya taifa chini ya miaka 18.

==

View attachment 3210345
View attachment 3210383
1. Kwa kuwa Sheria hiyo ya Uraia inatamka Wazi kwamba kabla Raia wa Kigeni (Mwombaji wa uraia) hajapatiwa Uraia wa Tanzania, Mwombaji huyo anatakiwa awe ameishi ndani ya nchi hii kwa muda wa angalau minimum miaka saba (7).
Je, hao Wachezaji wa Kigeni waliingia hapa nchini Tanzania lini ili kuishi hapa na ili kutimiza hiyo miaka saba inayotakiwa Kisheria? Lini hasa (tarehe ngapi) ilikuwa siku ya hao Wachezaji waliyotimiza kipindi Cha kuishi hiyo miaka saba wakiwa Wakaazi hapa Tanzania?

Ufafanuzi wa kina kabisa unahitajika kwenye Hoja hizi kwa sababu Uhamiaji ndiyo Taasisi yenye Mamlaka yote kabisa ya kutunza kumbukumbu zote kabisa za Wageni au Wasafiri wote wa Kimataifa ambao wanaoingia na kutoka hapa nchini.

2. Tumekuwa tukiona Matangazo kwenye Magazeti mbalimbali yanayowahusu Raia wa Kigeni ambao wenye nia ya Kuomba Uraia wa Tanzania, Matangazo hayo yamekuwa yakiutaarifu umma wa waTanzania kuwasilisha Mapingamizi yao (endapo kama wanayo) dhidi ya hao Watu wanaoomba Uraia wa Tanzania.
Uhamiaji wanapaswa watueleze, Je, lini hasa hao Wachezaji wa Kigeni waliopatiwa uraia wa Tanzania walitoa Matangazo hayo ili kuutaarifu umma juu ya hilo suala lao la kuomba uraia wa nchi hii? Je, Matangazo hayo yalitolewa lini na yalitolewa kwenye Magazeti gani hasa ya hapa Tanzania?
 
Wakipewa uraia wewe na mimi tunaathirikaje? Na wakinyimwa wewe au mimi tunafaidikaje? Acheni wapewe.

Bukayo saka, sterling, na mifano kibao walipewa uraia kama ambavyo wamepewa hawa..kwani hawakujua kama na wao vipaji.

Tatizo sisi tunaona uraia wa bongo ni Big deal sanaaaa.

Tuna watu kibao hapa kwetu japo ni legal citizens wa Tanzania lakini hawana uhakika wa kula, hawana ajira, hawana huduma muhimu, Je unafikiri hawa wanajivuniaje na huo uraia
 
Karibuni Watanzania wapya,ila tu muwe wazalendo wa kweli na sii wazalendo uchwara.Tanzania ni yetu sote.
Hawajakidhi vigezo vya kupewa uraia, muda walioishi nchini hautoshi, tangazo la kuomba uraia halijachapishwa gazetini nk.
Mwanasheria aisaidie nchi wahuni wanaharibu nchi.
 
Back
Top Bottom